Saturday, February 26, 2022

Agnes Trip Killing Brings Awareness to Domestic Violence and Sexual Abuse in Kenya



                       AGNES TIROP 1995-2021

By MUTWIRI MUTUOTA and GERALD IMRAY

Associated Press ELDORET, Kenya (AP) -  The brutal killing of Olympic runner Agnes Tirop last year shows signs of being a turning point for Kenya in finally confronting a scourge of abuse and violence against female athletes. It hasn't been spoken about or even acknowledged until now. The 25-year-old Tirop was stabbed to death at her home last October. Her partner has been charged with murder in her killing. Her death provoked a deep reckoning in Kenya and prompted current and former athletes to finally speak out and put pressure on authorities. They say young female athletes have been abused by partners, coaches and others for years and their stories have gone untold or been ignored.


Sunday, February 13, 2022

Tanzia - Professor Samahani Kejeri

Mwanahistoria na Mtembeza Watalii maarufu, "Professor" Samahani Kejeri, amefariki dunia, leo Februari 13, 2022, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Alikuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu ya kansa.

Binti yake, Furaha Kejeri amethibitisha  habari hiyo, Mazishi yatafanyika kesho, Jumatatu, Februari 14, 2022 nyumbani kwa marehemu, Magomeni, Bagamoyo. (Siyo Magomeni ya Dar es Salaam)

Prof. Kejeri alipewa jina la "Professor" kutokana na ufahamu wake wa Historia ya Bagamoyo.  Alikuwa anatunza vitabu, "friend books" ambazo zimesainiwa na watu ambao aliwatembeza Bagamoyo.  Mimi mwenyewe nilikutana naye mara la kwanza mwaka 1988, nikiwa mwanafunzi wa Tanzani School of Journalism.  Tulienda Bagamoyo kwenye Field Trip na alitutembeza na kutoonyesha sehemu muhimu za kihistoria ya Bagamoyo ikiwemo "hanging tree" ambako wajerumani walikuwa wananyonga weusi.  

Prof. Kejeri pia aliigiza katika sinema Maangamizi the Ancient One kama Mganga Simba Mbili.  Sinema hiyo ilikuwa ya kwanza kutoka Tanzania kuwa katika mashindano ya Academy Awards (Oscars) Hollywood.

Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Amin



Prof. Samahani Kejeri, Prof. Amandina Lihamba na Msanii Barbara O katika sinema Maangamizi the Ancient One

Prof. Samahani Kejeri Explains History of His Name - YouTube



Friday, February 11, 2022

SAHIHISHO - CORRECTION Pichani siyo Mh. Anna Makinda

 Kuna mtu ameposti hii picha mtandaoni akidai aliyesimama ni Mh. Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania, Mrs. Anna Makinda. Si kweli, aliyesimama ni Mama yangu mzazi Mrs. Rita Che-Mponda.  Picha ilipigwa mwaka 1965, Biti Titi alivyokuja Marekani kwenye mkutano wa akina Mama.  Baba alimwalika nyumbani, Washington D.C. kwa ajili ya chakula na mahojiano.  




CORRECTING THE RECORD - SAHIHISHO!!

Since last night, there has been a photo of my Mom with the Late Pioneer Female Leader of Tanzania, Bibi Titi Mohamed. My Mom is identified as a young Former Speak of the Tanzania Parliament, Mama Anna Makinda.
I'd like people to see the original photo that was cropped by someone. The young lady standing is my mother, Mrs. Rita Che-Mponda and NOT Mh. Mama Anna Makinda.
The photo was taken in 1965, Bibi Titi was in the USA for a Women's Meeting. My father was an Announcer at the Voice of America - Swahili Service at the time, He invited Bibi Titi to the house and interviewed. I originally published in my 'Swahili Time Blog' in 2010.

Thursday, February 10, 2022

Tanzia - Dr. MweleNtuli Malecela

 



Dr.  Mwele Ntuli Malecela  1963-2022

Nimepokea kwa huzuni na masikitiko habari ya kifo cha dada yangu wa Ubatizo Dr. Mwele Ntuli Malecela.  Amefariki Geneva, Switzerland jana.  Alikuwa na sumbuliwa na ugonjwa wa Kansa tangu mwaka 2019.   Kwa maneno yake mwenyewe..kansa iligundulika ikiwa tayari imekwisha sambaa mwilini.

Wakati wa kifo chake, Dr. Malecela, alikuwa anafanya kazi World Health Organization, kama Mkurugenzi wa Udhibiti wa  Magonjwa ya Yasiopewa Kipaumbele.  Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti za Kiafya Tanzania (NIMRI). 

Tanzania na Africa kwa ujumla imepata hasara. Tumempoteza mtaalamu aliyeboboea katika fani yake.

Poleni sana familia ya Malecela.  Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.


Kwa  habari zaidi BOFYA HAPA