Thursday, April 29, 2010

Ajali Mbaya Tanga - Wanafunzi 18 Wafariki Dunia

Habari hizi kwa hisani ya Da Subi. Mola alaze roho zao mahala pema peponi. Amina.

Jamani, hizi ajali za kizembe Tanzania zitaisha lini?!


BOFYA HAPA KWENDA KWA DA SUBI:


Wednesday, April 28, 2010

Maangamizi the Ancient One



Wadau hebu mcheki Prof. Amandina Lihamba, Barbara O, Bibi Mwanajuma Ali Hassan, Mimi, Mona Mwakalinga, marehemu Mwalimu Kisaka A. Kisaka, Dada Mhando, Stumai Halili, Mary Chibwana, Waigwa Wachira na wengine katika sinema Maangamizi the Ancient.

Maangamizi the Ancient One ni sinema pekee kutoka Tanzania iliyopelekwa katika mashindano ya Oscars. Sinema iliigwa Bagamoyo, Arusha, na Morogoro mwaka 1994 na 1997.

Tuesday, April 27, 2010

IT Training kwa Vijana

Spread the word

Free IT Training for 18-24 year olds who live in the DC, MD, or VA.
If you know any one with a high school diploma or a GED who are between the ages of 18-24 yrs old and have an interest in IT. Refer them to this site http://www.yearup.org/ to learn more about this free program. This program asks for a 1 year commitment between the hours of 8:30 am and 5:00 pm. They provide the student with a stipend and after six months, internships at companies such as Freddie Mac and AOL to name a few.

Check out the website. http://www.yearup.org/

About Year Up

Year Up is a one-year, intensive training program that provides urban young adults 18-24, with a unique combination of technical and professional skills, college credits, an educational stipend and corporate apprenticeship.

Our success is our graduates -- enabling them to move on to full-time employment and higher education. Year Up is about providing opportunities for urban young adults to demonstrate their true potential.

We have achieved excellent results to date:

100% placement of qualified students into apprenticeships
83% student retention
90% of apprentices meet or exceed apprenticeship partner expectations
87% of graduates placed in full or part-time positions within 4 months of graduation
$15/hr average wage at placement

Friday, April 23, 2010

Tanzanian Marathoners Put Kenyan Runners on the Alert!

(Pichani Josiah Kibira baada ya kukimbia katika Marathon huko Minnesota)

TANZANIAN MARATHONERS PUT KENYAN RUNNERS ON THE ALERT


By Josiah Kibira

If you follow the results of almost any marathon in the United States, you are bound to find one or more Kenyans in the top 10. In most cases, Kenyan runners place in the top three finishers, and, often times win the whole race.

It is no different in Minnesota, where both the Grandma’s Marathon of Duluth, and the Twin Cities Marathon have been dominated by Kenyan runners.

Running a marathon is not an easy proposition to undertake, in fact only 1% of all human beings do participate in this challenging sport. It is often compared to an analogy asking, “Why do you keep hitting yourself with a hammer? Because it feels good when you stop.”

But Kenyan runners have dominated this sport worldwide, a fact that Tanzanian runners find hard to swallow. When confronted by the subject, most will always bring up Filbert Bay, a Tanzanian who was not even a marathon runner, but won a gold medal in the Olympic Games many years ago.

I have been a maratho n runner for over 14 years. I try to run a marathon every year. Last year I was surprised at about mile 15 or so, wondering why can’t I see mile 16 marker on the horizon, when suddenly I heard someone say, ”Vipi, mzee! I looked up, to find a Tanzanian in the middle of the pack of runners.

We exchanged few words, and I should say, I was in worse shape than he was at that point in the race, then I urged him to proceed ahead without me. He did, but then it somehow gave me an immediate surge of energy. Seeing him was like saying, ”Wabongo na sisi tumo”, or “We, the Tanzanians,…got this!”… or so I thought.

I was proud because it was the first time in my fourteen years of running that I actually met a fellow Tanzanian in the race...running.

After the race, I made a po int of getting in touch with the Tanzanian runner so that we could tell the world and put the Kenyan runners on alert for the next marathon! Who knows? We may one day beat them! It could happen!
He surprised me, when he mentioned that there was yet another Tanzanian who was also in that same Twin Cities Marathon that day.

This is about us…the Tanzanian Marathoners and why we run.

Meet Gracious Msuya.

He started running before he ever landed in the United States. He was a student at the University of Dar Es Salaam in Tanzania. You can see his dedication to the sport because Dar can be very hot and it takes a serious commitment to run.

Running is such a personal decision because you have yourself for motivation. Gracious found motivation in the promise he made to his young kids that he would run the marathon once the kids were teenagers. His kids still have years to become teenagers, but the statement itself motivated him to start training instead of waiting so long.

The other motivator for him is his health. It is a proven fact that there are many health benefits from running including reversing the aging process. That’s right, you not only reverse the aging process, and sometimes you can even delay it.

I asked Gracious if there was anyone who inspired him to run, he said when he was in primary school (Elementary School) he saw a man who was in his 30’s who used to run and practice Karate. That was it. Gracious’ actual running would come later in his adult life as a student at a University.

Gracious admits running a marathon has not been easy. To date, he has run about 5 full marathons and a few short races. “It takes time and it is simply hard,” he remarks. But he also admits that the challenges of life do not make this easy. Balancing work and family is difficult enough, and squeezing in training time as well makes life all the more interesting. All in all, the advantages of running far outweigh all the hassles one goes through.

Gracious has high hopes for Tanzanians or any one who wants to take up running. In his words, he says “If you can walk a mile, you can run a mile.” One first mile could be a start to running many miles in the future. He also offers words of encouragement stating not to be afraid to start something new because in the end you may surprise yourself.

So, to all Kenyan runners, look out! Gracious Msuya is coming!

My inspiration to run came to me by accident. After I graduated from college in Kansas, I moved to Minneapolis. It was after the Twin Cities Marathon was completed and I was reading the race results in the paper. As I read at the men’s results list, I saw that there was a 99 year old man who completed the race in 5 hours and 20 minutes. This was enough for me. I thought, if a 99 year old man can complete a full marathon, I should be able to complete one. I have never looked back and I have logged 14 marathons ever since.

I use running as meditation. Most of the movies I have written were conceived as I ran. Right now I have a few movie plots in my head, and as I run, the plots get polished.
I agree with brother Msuya, “If you can walk a mile, you can run a mile.” It is a discipline that has taught me to be in control of my many aspects of life, especially the fact that I don’t quit easily and I don’t sweat the small stuff. I always tell myself that it is only mile 5, with 21 more to go. With this perspective, there are few things that surprise me.

And this is why we run. A sense of accomplishment. A sense of setting a goal and achieving it. A sense of an overwhelming individual success. This can be transferred to any aspect of life, finances, school, career, family. Because really at the end of the day, we are first answerable to ourselves…

And yes, even beating Kenyan runners…it can happen!

So guys and gals – “TWENDE KUKIMBIA….”

Know any Tanzanian runners? Share the story with us!! - Josiah

***********************************************************

Naomba huyo Gracious Msuya aje mwakani akimbie Boston Marathon! Kweli waKenya wame-dominate!

Ngono Uliponza Uchumi wa Marekani?

Jamani, mimi nimeblow kusikia habari hizi. Eti wataalam wa uchumi wa SEC (U.S. Securities and Exchange Commission) walikuwa wanatazama ngono (pono) kwenye mtandao badala ya kulinda uchumi wa Marekani! Hebu someni habari hizi halafu mjadili.

Mbona sehemu nyingi za kazi hapa Marekani huwezi kuangalia pono wala kutumia e-mail kama yahoo/hotmail ukiwa kazini! Tena wameweka vizuizi. Haya makubwa! Ngono uliponza uchumi wa Marekani!

*************************************************************************
Kutoka CNN.com

SEC Staffers Watched Porn as Economy Crashed


(CNN) -- As the country was sinking into its worst financial crisis in more than 70 years, Security and Exchange Commission employees and contractors cruised porn sites and viewed sexually explicit pictures using government computers, according to an agency report obtained by CNN.

"During the past five years, the SEC OIG (Office of Inspector General) substantiated that 33 SEC employees and or contractors violated Commission rules and policies, as well as the government-wide Standards of Ethical Conduct, by viewing pornographic, sexually explicit or sexually suggestive images using government computer resources and official time," said a summary of the investigation by the inspector general's office.

More than half of the workers made between $99,000 and $223,000. All the cases took place over the past five years.

The inspector general's report includes specific examples of misuse by employees.
A regional office staff accountant tried to access pornographic Web sites nearly 1,800 times, using her
SEC laptop during a two-week period. She also had about 600 pornographic images saved on the hard drive of her laptop.

Separately, a senior attorney at SEC headquarters admitted to downloading pornography up to eight hours a day, according to the investigation.

"In fact, this attorney downloaded so much pornography to his government computer that he exhausted the available space on the computer hard drive and downloaded pornography to CDs or DVDs that he accumulated in boxes in his office," the inspector general's report said.

"It is nothing short of disturbing that high-ranking officials within the SEC were spending more time looking at pornography than taking action to help stave off the events that brought our nation's economy to the brink of collapse," said Rep. Darrell Issa. The Republican is a ranking member of the House Committee on Oversight and Government Reform.

"This stunning report should make everyone question the wisdom of moving forward with plans to give regulators like the SEC even more widespread authority," he said. "Inexplicably, rather than exercise its existing regulatory enforcement authority, SEC officials were preoccupied with other distractions."

The investigation came to light on the same day President Obama gave a speech in lower Manhattan, calling for reform in the finance industry.

On Capitol Hill, the Senate is working on a reform bill that would set up regulatory oversight of the financial industry's practices with the goal of preventing another Wall Street meltdown like the one in 2008 that launched the U.S. recession.

The bill includes an "early warning" system intended to spot signs of crisis, as well as a $50 billion liquidation fund created with money from banks and other finance industry corporations to ensure an orderly transition in closing down failing entities. It's approved by the Senate's Banking and Agricultural committees.

The House passed its version of the bill in December.

Wednesday, April 21, 2010

Mshiko Boston - Wanaongea Kifaransa

oCP CASTING IS LOOKING TO CAST:

A non-union, female actress, age 45+, to portray a West African Grandmother with a Francophone African accent, &

non-union, female, 9-11 years old to portray her West African Granddaughter with a Francophone African accent,

for museum video pieces about the African Forest
This is well paid work for 1 day in the near future.
Please sumbit ASAP to:mailto:matt@cpcasting.com

Tuesday, April 20, 2010

Flaviana Matata Na Russell Simmons


Aisei, wiki hii na siku zijazo utasikia Tanzania, na jina la mrembo wetu Flaviana Matata ikitajwa sana huko Hollywood. Habari kutoka Hollywood zinasema kuwa Flaviana Matata yuko kwenye uhusiano na Russell Simmons. Wanasema kuwa wamekuwa pamoja kama miezi mitatu ila wiki hii ndo habari zimekuwa wazi kwa kila mtu kujua.

Hongera Flaviana, wakilisha Tanzania!

Hebu someni habari wanazoandika na badooo.... wengine wamempachika Flaviana jina BALDILOCKS! (Mwenye upara). Wengine wanasema huyo Simmons ni mzee mno kwa Flaviana. Wengine wanasema kuwa Flaviana mrembo na Simmons ana sura mbaya...yaani.

Wengine wanasema kwa vile Kimora Lee Simmons aliamua kuzaa na Djimon Hounsou (Mwafrika) naye Simmons analipiza kisasi kwa kumchukua Mwafrika.....yaani maneno. Kimora na Simmons waliachana mwaka 2006. Simmons ni tajiri aliyewahi kuwa CEO wa kampuni Phat Farm, na pia ana kampuni ya muziki.

Lakini namtakia Flaviana mafanikio mema. Ajiendeleze katika fani ya umodel. Flaviana ana mkataba na kampuni ya Umodel New York. HONGERA! Waonyeshe urembo asili ni nini!

Mapenzi ni mapenzi. Kama wamependana, wamependana. LOVE IS BLIND! Na kumbuka watu watasema, mwisho watachoka!

Kwa habari zaidi someni:

http://juicycelebgossip.wordpress.com/2010/04/19/russell-simmons-is-in-a-new-relationship-with-a-former-miss-tanzania/

http://www.honeymag.com/2010/honeymag/who-is-russell-simmons-new-boo/

http://bossip.com/238971/who-is-choppin-this-thang-down/

http://fashionjunkii.onsugar.com/Flaviana-Matata-Face-Forward-Nylon-mag-April-2010-8031036

http://blog.mtviggy.com/2010/04/19/flaviana-matata-the-original-hottest-bald-model/

Monday, April 19, 2010

Sinema ya Aina Yake kutoka Kenya




Wadau,

Kuna sinema inayotoka Kenya ambayo ni tofauti na sinema zingine. Hadithi yake ni aina ya Science Fiction (Sci-Fi). Ni ya kwanza kutoka Kenya. Inaitwa PUMZI na inahusu miaka baada ya Vita Kuu ya dunia ya Tatu (World War III). Dada fulani kutaka Afrika Mashariki anakuwa mkombozi wa dunia. Iliononyeshwa kwenye Sundance Film Festival. Hii trailer safi sana.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.wired.com/underwire/2010/01/pumzi/

Washindi wa Boston Marathon 2010

WASHINDI WA BOSTON MARATHON 2010

WANAUME

1. Robert Cheruiyot (KEN), 2:05:52 (CR) $150,000 + $25,000 kwa ajili ya kuvunja rekodi.

2. Tekeste Kebede (ETH) 2:07:23 $75,000

3. Deribe Merga (ETH) 2:08:39 $40,000

4. Ryan Hall (USA) 2:08:41 $25,000

5. Mebrahtom Keflezighi (USA) 2:09:26 $15,000


****************************************************

Wanawake

1. Teyba Erkesso (ETH) 2:26:11 $150,000

2. Tatyana Pushkareva (RUS) 2:26:14 $75,000

3. Salina Kosgei (KEN) 2:28:35 $40,000

4. Waynishet Girma (ETH) 2:28:36 $25,000

5. Bruna Genovese (ITA) 2:29:12 $15,000

6. Lidiya Grigoryeva (RUS) 2:30:31 $12,000

7. Yurika Nakamura (JPN) 2:30:40 $9000

8. Weiwei Sun (CHN) 2:31:14 $7400

9. Nailya Yulamanova (RUS) 2:31:48 $5700

Kwa habari zaidi tembelea....

http://www.bostonmarathon.org/

Boston Marathon Leo

Boston Marathon imeanza kama dakika tano zilizopita. Na kama kawaida tunategemea mKenya ahsinde!

Mnaweza kufuatilia hapa:

http://www.bostonmarathon.org/bostonmarathon/114thmarathon.asp

HAKUNA MTANZANIA ANAYEKIMBIA MWAKA HUU!!!!!

Hivi mbona Tanzania tumezorota katika riadha siku hizi?????

Saturday, April 17, 2010

Gavana Deval Patrick Akutana na Waafrika wa Massachusetts

Leo, Gavana wa Massachusetts, Bwana Deval Patrick, aliongea na waafrika waishio Massachusetts. Mkutano huo uliitwa African Town Hall. Ilifanyika Tobin Comunity Center mjini Boston.

Waafrika walitokea kutoka nchi nyingi za Afrika, hasa waafrika kutoka Magharibi walikuwa wengi. Wakutoka Afrika Mashariki tulikuwa wengi pia, hasa waGanda. Lakini kama nilivyotabiri, hao wa Magharibi walijaribu sana kuiteka mkutano. Ila nashangaa watu wengine hawaelewi kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya serikali ya Mkoa (State Government), na serikali kuu ya nchi (Federal Government) ambayo inaongozwa na Rais Obama. Wengine hawakuewelewa kuwa mambo mengine yanahusu serikali ya mji wanaokaa na si mkoa.

Masuala makuu yaliongolewa, ni elimu kwa wahamiaji, bima ya afya, na umuhimu wa census hasa. Kuna waafrika walisema kuna wana majina ya kiislamu na walihofia kuwa wakijaza fomu watanyanyaswa. Wengine walisema kuwa hawana makatarasi na walihofia kukamatwa wakirudisha fomu. Wasaidizi wa Gavana pia walijaribu kuelimisha watu kuhusu umuhimu wa fomu hizo na kuwa haziendi uhamiaji. Kwenye bima ya afya alisema kuwa baada ya mwezi Agosti itakuwa rahisi zaidi kuipata. Pia alisema kuwa wanajitahidi kuruhusu wanafunzi wasio na makaratasi wanaokaa Massachusetts waweze kulipa ada ya 'In State' kama wakisoma katika State Colleges.


Gavana Patrick aliwaomba waafrika wampigie kura katika uchaguzi ujao na waombe ndugu na marafiki wampigie pia.

****************************************************************************


Wasichana wa KiGanda wakicheza ngoma ya asili kumwingiza Gavana kwenye Ukumbi. Gavana yuko nyyuma yao anasalimiana na watu.
Gavana Patrick akielezea hatua alizochukua kama Gavana ilikusaidia wahamiaji wanaokaa Massachusetts.

Gavana Patrick aliwahimiza waafrika wajaze fomu za Census. Aliwaambia watu wasijali kama wana makaratasi au hawana, maana si fomu ya uhamiaji bali fomu ya kujua kuna watu wangapi katika eneo fulani serikali iweze kuwapa huduma ya kutosha, kama shule, hospitali,polisi.

Hao waGanda walipiga ngoma wakati Gavana anaiingia ukumbini. Gavana alifurahi sana.

Huyo MKameroon, alichekesha watu pamoja na Gavana alipoomba waafrika wasinyangywe chakula chao cha asili wakitua katika uwanja wa ndege (Logan Airport) Boston. Gavana alimjibu kuwa ana imani kuwa chakula hicho ni kizuri, lakini hizo ni sheria za serikali kuu ya nchi (Federal) na yeye mwenyewe hawezi kuvunja sheria.

Viongozi wa kidini wa waafrika Massachusetts wakipiga picha na Gavana baada ya shughuli. Huyo mama Mngieria aliyeshika simu alikuwa alijaribu kuleta fujo wakati wa maswali na majibu. Dume MNigeria mwenzake kamkalisha chini!

Shughuli iliisha kwa fujo! Ilibidi walinzi wa Gavana wamzunguke na kumtoa kwenye mlango wa pembeni. Kisa, kila mtu alitaka kupiga picha naye. Jamani, Gavana alisukumwa!!!!! Ila lazima niseme sisi waTanzania ni wastaarabu sana. Sikumwona MTanzania akifanya fujo mle wala kushiri katika kundi la waliomsukuma na kumsakama ili apige picha naye. Shughuli ilianza vizuri, lakini iliisha vibaya!

Ndoa ya Makaratasi Yamponza Mcheza Sinema

Mcheza sinema Fernanda Romero anashikiliwa na polisi wa uhamiaji huko California baada ya kugundulika kuwa na ndoa ya makaratasi. Mume wake feki amekamatwa pia.

Bi Romero anatoka Mexico. Alilmlipa Kent Ross afunge ndoa naye. Hawajawahi kukaa pamoja, Baada ya ndoa hiyo ya makaratasi, Bi Romero aliaanza na uhusiano na dume mwingine, Markus Klinko. Walivyoaachana na Klinko ndo kaenda kusema huko uhamiaji kuwa Bi Romero alifunga ndoa ya makaratasi na Ross. Jamani, ni wivu, uchungu au shetani iliyompeleka kwa polisi wa uhamiaji.

Bi Romero na Ross wako hatarini kufungwa miaka mitano!

***********************************************************************

LOS ANGELES (AP) - Mexican-born actress Fernanda Romero has had bit parts in such movies as the horror film "Drag Me to Hell," but federal prosecutors say her biggest act was pretending to be a bride.

The 28-year-old actress and husband were arrested Friday at their separate Los Angeles homes and charged with marriage fraud, the U.S. attorney's office said. They contend Romero paid Kent Ross, 28, to marry her in 2005 so that she could become a U.S. resident.

Authorities said the two never lived together and Romero, whose full name is Maria Fernanda Romero Martinez, submitted phony documents with her residency application.

An investigation began after Romero's ex-boyfriend, fashion photographer Markus Klinko, told immigration authorities her marriage was a sham. The couple started dating after Romero and Ross were married.

If convicted, Romero and Ross could be sentenced to up to five years in federal prison.
Romero has had roles in several small films and is moderately well known in Mexico, where she appeared in the TV Azteca soap "Eternamente Tuya." She has also appeared on the Spanish-language channels Univision and Telemundo in the shows "Control" and "La Ley del Silencio," respectively.

According to her website, she has appeared in television and print ads for several U.S. companies, as well as a music video. She moved to Los Angeles when she was 18 to study fashion design, according to her site.

Messages to her publicist were not returned Friday.

A phone message left for Ross' attorney, Mike Shannon, also was not returned.
Romero and Ross were both released after initial court appearances Friday. However, a judge restricted Romero's travel to certain Southern California counties and said she could not leave the country.

Special Assistant U.S. Attorney James M. Left, said immigration officials began investigating in 2007 after Klinko mentioned the marriage during a lawsuit he filed in New York.
Left says a marriage ceremony was performed on June 12, 2005, but the couple never lived together.

He said immigration marriage fraud cases may be brought in either criminal or immigration courts. The case against Romero was pursued because of "the overwhelming amount of evidence" and repeated misstatements by the actress, Left said.

"Immigration benefit fraud is a serious crime," said Miguel Unzueta, an Immigration and Customs Enforcement special agent in charge in Los Angeles. "Not only does it potentially rob deserving immigrants of benefits they rightfully deserve, it also undermines the integrity of our nation's legal immigration system."

OffSide Trick Feat Mzee Yusuf - Bata

Friday, April 16, 2010

Mume Mzuri!


A guy woke up in the morning with a terrible hangover. Next to the bed was a couple of aspirins, a glass of water, and a note from his wife ? ?Honey, there's a hot breakfast waiting for you in the kitchen. Love, your wife?. He looks around the room and sees that it is in perfect order, spotlessly clean. So is the rest of the house.

He stumbles into the bathroom and notices a huge black eye. After shaving, he goes to the kitchen, and sees that the hall mirror is broken too.

His son is in the kitchen and as he's eating his huge breakfast the guy asks the son what all this is about.

Well, last night you came home drunk off your ass, stumbled into the mirror and hit your head on the doorknob. Mom helped you to bed, and as she's trying to get your pants off you kicked her away and said get off me lady, I'm married?.

If you really enjoyed this story please forward to friend. Or reply and let us know. You might make someone's day!

Reminder

TOMORROW!

Saturday, April 17th, 2:15pm

the

1st African Town Hall Meeting
with
Governor Deval Patrick

at

TOBIN COMMUNITY CENTER
1481 Tremont St, Roxbury Crossing 02120

Be A Part of Strengthening the African Voice in Massachusetts!
Let us Strongly Showcase the African Presence : Invite your friends and Spread the Word!

Please arrive on time. Governor is scheduled to speak at 3pm.

--
The Governor's African Council (GAC) is an independent community initiative that aims to strengthen the African Voice in Massachusetts through political and civic engagement. GAC's objective is to unify and increase the participation of the African community in the Massachusetts political processes and build a voice that can advocate for the community's needs.

If you are interested in learning more or being a part of building the GAC, please email us at gaccampaign@gmail.com or call us at 617-5447- GAC.

Nani Huyo?




Tuesday, April 13, 2010

African Town Meeting Massachusetts


All Tanzanians who live in Massachusetts are invited
to the

1st African Town Hall Meeting
with
Governor Deval Patrick
Saturday, April 17th, 2:15pm
Tobin Community Center, 1481 Tremont St., Roxbury Crossing, MA. 02120

~
AGENDA

We Are Here :
Showcase the African presence in Massachusetts

We Are Speaking Out:
Issues & Concerns of the African Community

We Want To Be Heard:
Q & A Session With Governor Deval Patrick

We Are Moving Forward:
Strengthening the African voice

~
RSVP & Parking Information

If you have not yet done so, kindly RSVP for the event.

Parking is available across the street ( 1460 Tremont St.) from the event venue but is limited and priority will be given to those who RSVP and will have car pooled.

Volunteers Needed!

Kindly indicate whether you are available to volunteer during the event. Please click here to sign up and for more information.

THANK YOU & CONTINUE TO SPREAD THE WORD!
--
The Governor's African Council (GAC) is an independent community initiative that aims to strengthen the African Voice in Massachusetts through political and civic engagement. GAC's objective is to unify and increase the participation of the African community in the Massachusetts political processes and build a voice that can advocate for the community's needs.
If you are interested in learning more or being a part of building the GAC, please email us at gaccampaign@gmail.com or call us at 617-5447- GAC.

Midume Mkome - Yaliyompata Todd!

Todd's Funeral.....Burial of a Husband Liar..

Todd works hard at the office but spends two nights each week bowling,
and plays golf every Saturday.

His wife thinks he's pushing himself too hard, so for his birthday she
takes him to a local strip club.

The doorman at the club greets them and says, 'Hey, Todd! How ya doin?'

His wife is puzzled and asks if he's been to this club before.

'Oh no,' says Todd.. 'He's in my bowling league.

When they are seated, a waitress asks Todd if he'd like his usual and
brings over a Budweiser.

His wife is becoming increasingly uncomfortable and says, 'How did she
know that you drink Budweiser?'

'I recognize her; she's the waitress from the golf club.

I always have a Bud at the end of the 1st nine, honey.'

A stripper then comes over to their table, throws her arms around
Todd, starts to rub herself all over him and says, ‘Hi Toddie. Want
your usual table dance, big boy?'

Todd's wife, now furious, grabs her purse and storms out of the club...

Todd follows and spots her getting into a taxi.

Before she can slam the door, he jumps in beside her.

Todd tries desperately to explain how the stripper must have mistaken
him for someone else, but his wife is having none of it.

She is screaming at him at the top of her lungs, calling him every 4
letter word in the book.

The cabby turns around and says,

'Geez Todd, you picked up a real bitch this time.'

Todd's funeral will be on Saturday.

Mshiko Boston - WanaRiadha

Boston Casting Seeks Experienced Runners for a Saucony Television Commercial


We are looking for the following. Please respond only if you fit the description we're looking for:

Male and Females, 18 - 25 years old, all ethnicities, NON-UNION only
Must run at least 15 - 20 miles per week
Must be in excellent physical condition
Must be available ALL DAY without conflict on Tuesday, April 20 and Wednesday, April 21(rain date) for the shoot. Job will only shoot one day.

Auditions will be held by appointment on Thursday, April 15.

Please e-mail current photo of you, (preferably in athletic gear) and phone number to BostonCastingRunners@gmail.com by 2 pm Wednesday, April 14 to be considered.

If you are chosen for an audition, you will be contacted directly with more information. If cast, job will pay $500 plus free Saucony gear.

Due to heavy phone call volume, please refrain from calling into the office.
Thank you!

Monday, April 12, 2010

Dk. F. Mghanga Akumbuka IlivyokuwaTanzia ya Mh. Edward Sokoine

Asante Da Subi kwa kuleta habari hizi:

Dk. F. Mghanga AKUMBUKA ILIVYOKUWA TANZIA YA EDWARD MORINGE SOKOINE


Pichani -Edward Moringe Sokoine (1938 - 1984)


Ni miaka ishirini na sita iliyopita. Siku ya Alhamisi, majira ya jioni kama saa kumi na moja. Anga la jiji la Dar es Salaam lilikuwa jeusi likihanikizwa na mawingu madogo madogo yaliyojikusanya kuashiria kamvua kalikokuwa kametawala siku hiyo. Hizi ni nyakati za masika katika sehemu kubwa ya nchi.

Ndo kwanza nimerudi toka shule, tayari nimeshajipakia ugali wangu wa njano (Yanga) na maharage ya Iringa.

Nipo mtaani nikicheza na wenzangu chandimu. Hatuna viatu, tupo pekupeku lakini hatujali kitu. Maisha yalikuwa mazuri bila kujua adha na masumbufu ambayo wazazi walikuwa wanayapitia ili kutufanya watoto wao tuweze kwenda chooni.

Nikiangalia pembeni, akina mama walikuwa wamekaa wakisukana na wengine walikuwa kwenye vibustani vyao wakipalilia matuta ya viazi vitamu. Hakika hatukujua lililokuwa limetokea masaa machache yaliyopita hapa nchini kwetu.

Lakini ghafla redio zikaanza kupiga wimbo wa taifa. Si aghalabu kusikia wimbo wa taifa mida kama ile tena kipindi kile kisichokuwa na sikukuu wala mgeni yeyote wa kitaifa. Haiyumkiniki kuna jambo kuu limetkea. Katika utoto wangu, ghafla nikaacha kucheza, akina mama waliokuwa wakisogoa nao wakapigwa na ubaridi wa ghafla. Katika mshawasha wangu wa kitoto nikaijongelea redio kutaka kujua kilichojiri jioni hiyo ya Alhamisi nyeusi. Dakika kadhaa zilipita kabla ya wimbo wa taifa kuisha.

Sauti iliyojaa huzuni ikasikika. Hata katika utoto wangu, naweza kusema kwa hakika kuwa sauti ile ilikuwa katika huzuni na majonzi na ilionesha ni ya mtu aliyekuwa katika kilio muda si mrefu uliopita. Naam, ilikuwa ni sauti ya hayati baba wa Taifa. Nayakumbuka maneno yake mpaka sasa. Hivi ndivyo alivyosema:

"Ndugu wananchi, leo mnamo majira ya saba mchana, ndugu yetu, mwenzetu, Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais, Edward Moringe Sokoine amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea huko Morogoro wakati akilejea Dar es Salaam kutoka Dodoma kwenye mkutano wa Bunge"

Naam, hiyo ndiyo sababu ya kupigwa kwa wimbo wa Taifa jioni ile. Utando mweusi ukatanda. Simanzi ikatawala. Vilio vikasikika, furaha ikatoweka. Giza la mawingu meusi likaongezea upotevu wa furaha. Nikausikia ukelele mkuu kutoka kwa mama mmoja aliyekuwa ameshika jembe akipalilia bustani yake "Mama wee mkombozi wetu amekufa, nani atatutetea sisi wanyonge?" Hakika ndivyo aliomboleza mama yule.

Huzuni kuu ikaniingia ghafla. Nikajiwazia "Sokoine kafa? Hapana, amekufa?" Nafsi ilikataa kuamini, akili ya utoto ikaniambia haiwezekani. Ghafla machozi yakaanza kunitiririka. Naam nililia. Nilimlilia mzalendo wa kweli. Wazazi walilia, wananchi walilia, hata Nyerere alilia tena hadharani, hakulia kiunafiki alilia kweli.

Watanzania wapenda haki tulilia, tulimlilia mpenda haki mwenzetu. Sokione mzalendo wa kweli. Mwana wa Kitanzania asilia, mtetezi wa kweli wa wanyonge, mchapakazi, mpigania mema ya nchi.

Naam, yawezekana kwa wengine ameshafutika lakini kwa wapenda haki, Sokoine atabaki kuwa kioo chetu daima. Huyu ndiye mtu aliyekuwa na sifa nilizozitaja wakati ule kwenye ile ndoto yangu ya "Namuona mtu huyu". Yawezekana alikuwa na kasoro zake kama mwanadamu na hata kiutendaji lakini daima nia yake njema kwa watu wake iliyafunika makosa yake hayo. Alipendwa na wanyonge na kuchukiwa na wezi, wabadhiifu wa mali ya umma na wahujumu uchumi (leo tunawaita mafisadi). Huyu ndiye aina ya mtu tuliyemuhitaji Tanzania ya leo.

Nimemkumbuka Sokoine, mtanzania mzalendo mwana mpenda nchi aliyenifanya nihisi msiba wake kuwa unanihusu kwa ukaribu mno. Naam, wajamaa kama kina Subi lazima watamkumbuka mtu huyu na kumuomboleza daima.Mungu alipenda kumchukua ingawa tuliona amemchukua mapema mno.

Pumzika kwa amani Baba Sokoine, mtanzania na mzalendo wa kweli.

Amina!
Dk. F. Mghanga, MD

*************************************************************************

Na mimi naongezea. Siku hiyo nilikuwa kwenye zamu ya ulinzi wa usiku JKT Masange. Tulijiandaa kwenda zamu, lakini wote kambini tuliambiwa tukusanyike mbele ya ofisi kuu wa kambi. Kwenda huko, tukambiwa kuhusu msiba wa Waziri Mkuu Edward Morine Sokoine. Nadhani kila mtu alipigwa na butwaa kusikia habari hizo huko wengine walisema habari hiyo si kweli.

Wakati huo Masange JKT pori, hata simu hakuna. Kuna afande fulani alikuwa na redio ndo tukathibitisha kuwa habari hiyo ni kweli. Niliendelea na zamu ya ulinzi na wenzangu kama kawaida. Mambo kambini kwa ujumla yaliendelea kama kawaida. Waliobahtika kupata pasi kwenda uraini ndo walisema kulikuwa na vilio kibao. Nawaambia gazeti enye habari hizo zilikuwa kama almasi. Nakumbuka kuona picha ya Mama Gertude Mongella akilia kweli. Wakati huo alikwa Katibu Mkuu katika ofisi ya Waziri Mkuu.

Watu walikuwa wanasema kuwa ajali ya Sokoine haikuwa ajali, bali yule MSoweto alilipwa amwue. Wengine walisema alipigwa risasi na ajali ilikuwa kama cover-up. Eti kuna watu walikchukia kwa vile ilionekana atakuwa rais baada ya Mwalimu, wengine walisema eti kuna watu walichukia maendeleo alikuwa anajaribu kuleta. Lakini nakumbuka Mwalimu na viongozi wengine walisisitiza kuwa ilikuwa ni ajali! - Chemi

Ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi Nchini Algeria:

Kutoka kulia ni watendaji wa wizara mzee Rajabu, mama Kibaya, mh: mkurugenzi wa elimu prof. Abel, mh: Katibu mkuu Alhaji Hamis Dihenga, mkurugenzi mkuu mtendaji wa bodi ya mikopo mh: Nyatega na afisa ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Walipokutana na wanafunzi University of Blida.


Imeandikwa na ndau Mdurban the King - Algiers, Algeria.


Ujumbe mzito wa wizara ya elimu na ufundi ukiongozwa na mheshimiwa katibu mkuu wa wizara hiyo mh. Alhaji, professor Hamisi Dihenga akiambatana na mkurugenzi mkuu wa elimu ya juu prof. Abel, mkurugenzi mtendaji mkuu wa bodi mh.Nyatega, maafisa watendaji wakuu wa wizara Mama Kibaya na mzee Rajabu na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa mh. Flavian Komba.

Ziara hio ya siku7, ya kutembelea na kujua matatizo na maendeleo ya kielimu ya wanafunzi wakitanzania wanaosoma Algeria. Ujumbe huo uliweza kutembelea vyuo mbalimbali na pia kukutana na wanafunzi hao.

Wanafunzi hao walionesha furaha na shukrani kwa serikali ya Tanzania kwa kuonesha kuwajali raia wake kwani Algeria inatoa scholarship kwa bara zima la Africa na baadhi ya nchi za Ulaya na Asia, lkn haikuwahi kutokea kwa serikali zao kuwatembelea wanafunzi wao. Hivyo ilitoa picha nzuri kwa Tanzania.

Pia ujumbe huo uliweza kukutana na waziri wa elimu ya juu, Sayansi na technologia, wizara ya Utalii na Mazingira. Katibu mkuu alifurahishwa na mapokezi mazuri aliyoyapata kutoka kwa serikali ya Algeria na wanafunzi hao. Serikali kwa ujumla imeridhika na ubora wa elimu ya juu inayotolewa nchini Algeria.

Katibu mkuu aliweza kuchangia chama cha wanafunzi hao (ATSA) dollar 1500 na mkurugenzi mkuu mtendaji wa bodi ya mikopo naye alitoa binafsi dollar 1000 kwa chama hicho, hapo awali chama kilipokea dollar 2000 kutoka kwa mh. Membe waziri wa mambo ya nje pindi alivyo tembelea nchi hiyo hivi karibuni.Ujumbe huo mzito umerejea nchini tarehe 10/04/2010

Saturday, April 10, 2010

Afariki Baada ya Kubikiriwa na Kulawitiwa na Mume Wake!


Jamani, kwa kweli nimesikitika sana baada ya kusoma habari hii. Huko Yemen, kuna binti wa miaka 13, ambaye aliozwa na wazazi wake kwa kijana mwenye miaka 23. Siku ya ndoa, mume wake alimfunga kamba, alimtoa ubikira , kamnajisi na pia kamlawiti! Hospitali walisema kuwa uke na mkundu ulikuwa umechanika! Jamani! Jamani!

Mola aipokee roho ya binti na kumweka mahala pema peponi. AMIN.


********************************************************

SHUEBA, Yemen (AP) - A 13-year-old Yemeni child bride who died shortly after marriage was tied down and raped by her husband, her mother said.

Nijma Ahmed, 50, told the Associated Press late Friday that just before her daughter lost consciousness she described how her 23-year-old husband had tied her up and forced himself on her. She bled to death hours later.

Elham Assi died April 2, four days after she was married. A forensic report said her vagina and rectum were deeply ripped, causing her to hemorrhage.

The practice of marrying young girls is widespread in impoverished Yemen. Traditional families prefer young brides and poor families can be lured with hundreds of dollars in gifts.

The UN child agency, UNICEF, says one of three girls in Yemen is married before the age of 18.
"Early marriage places girls at increased risk of dropping out of school, being exposed to violence, abuse and exploitation, and even losing their lives from pregnancy, childbirth and other complications," said regional director Sigrid Kaag, in a statement Wednesday condemning the death.

Tribal custom also plays a role, including the belief that a young bride can be shaped into an obedient wife, bear more children and be kept away from temptation.
Last month, a group of the country's highest Islamic authorities declared those supporting a ban on child marriages to be apostates.

A February 2009 law set the minimum age for marriage at 17, but it was repealed and sent back to parliament's constitutional committee for review after some lawmakers called it un-Islamic. The committee is expected to make a final decision on the legislation this month.
The issue of Yemen's child brides got widespread attention three years ago when an 8-year-old girl boldly went by herself to a courtroom and demanded a judge dissolve her marriage to a man in his 30s. She eventually won a divorce, and legislators began looking at ways to curb the practice.

In September, a 12-year-old Yemeni child-bride died after struggling for three days in labor to give birth, a local human rights organization said.

Mshiko Boston!

Wadau, kazi ya siku moja hii. Mfuate description... Pia muwe na makaratasi ya kufanya kazi Marekani.

****************************************************************
There are several talent that will be hired. The shoot will be either a
half day ($750) or a full day ($1500). Usage is for the client company's
library, unlimited time, print media. No TV/Video and No Outdoor.

Shoot dates are TBA, but somewhere in the 24 - 30th range of April.

The client is looking for the talent types listed below. No appointment is necessary.

The casting is confirmed for this Sunday April 11th at Viewfinder Productions

423 West Broadway Suite 403A
Boston MA 02127

Times:

10:30 AM - 1:30 PM (last acceptance time will be 1:15)
or
2:30 PM - 7 PM (last acceptance time will be 6:45)

Dress should be business/business casual.

No headshots or composite cards are necessary.

We will be asking for talents' REAL age.

Seeking:
- Male, Caucasian, mid to late 40s
- Male, Middle Eastern, early 30s
- Male, early 30s, African American
- Male, Caucasian, late 20s
- Woman, Latino, late 20s, early 30s
- Woman, Caucasian, mid 20s
- Woman, Caucasian, late 30s
- Woman, mid 20s, African American
- Woman, late 20s, Asian
- Man and Woman, early to mid 30s, dark hair, could
be Middle Eastern, Latin, Southern European or Indian.
- Woman, African American, 70s
__._,_.___

Kitabu kuhusu Mwalimu Nyerere




Dear Reader/Mpenzi Msomaji,

MDAHALO KUHUSU KITABU CHA UKOMBOZI WA AFRIKA NA MCHANGO WA MWALIMU NYERERE/ PANEL DISCUSSION AROUND A NEW BOOK TITLED: AFRICAN LIBERATION: THE LEGACY OF NYERERE.

Tembelea Bongo4ever [B4E] katika: http://bongo4ever.ning.com/?xg_source=msg_mes_network

Owino Apata Shahada ya Uzamili wa Sheria za Kimataifa

Natoa Pongezi kwa Kaka Maina Ang'iela Owino, Dada Shose Susa Katende na Rujama Chisumo, waliopata Shadaha zao katika fani mbalimbali kutoka chuo Kikuu cha Oxford Brookes huko U.K. . Kaka Owino ni mwenyekiti wa CCM huko U.K.



Kati ya wahitimu wa sheria za kimataifa Oxford Brookes University siku ya Ijumaa 4/9/10....Maina Ang'iela Owino ( Mwenyekiti wa CCM UK) - LLM International Trade and Commercial Laws Shose Susa Katende (Advocate) -LLM International Human Rights Laws Rujama Chisumo (Mwanasheria Wizara ya Fedha TZ) -LLM International Economic Laws.

Misiba

Askofu Abel Muzorewa wa Zimbabwe amefariki dunia. Habari zinasema Askofu Muzorewa amefariki dunia mjini Harare jana Ijumaa. Alikuwa na miaka 85. Askofu Muzorewa alikuwa anaitwa 'puppet' (kibaraka) wa wazungu kwa vile alijaribu kupooza waafrika wasitake uhuru Zimbabwe. Alikuwa waziri mkuu katika utawala wa mbaguzi Ian Smith.

Kwa habari zaidi someni:
Rais wa Poland, Lech Kaczynski na mke wake wamefariki katika ajali ya ndege usiku wa kuamkia leo. Ndege hiyo ya raisiilikuwa inajaribu kutua huko Urusi wakati wa ajali. Habari zinasema kwa kulikuwa na viongozi wengine wakuu na wakuu wa jeshi kwenye hiyo ndege. Watu 132 wamefariki katika ajali hiyo.

Kwa habari zaidi soma:

Aliyewahi kuwa Chifu wa wahindi wekundu, kabila ya Cherokee, hapa Marekani, Chifu Wilma Mankiller amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa kansa. Chifu Mankiller alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza kabila la Cherokee.

Kama mnafahamu historia ya Marekani, wazungu waliwakuta hao wahindi wekundu hapa. Waliwaua kwa njia mbalimbali....kuwapiga risasi, kuwapa sumu, kuwaambukiza magonjwa kama smallpox kwa makusidi kusudi wafe. Nia yao ilikuwa kuiba ardhi ya na wazungu walifanikiwa kufanya hivyo!

Mnaweza kusoma habari zaidi hapa:

http://www.google.com/hostednews/ap/article/ALeqM5jmKy3_vtUk06fgt2_rFw9nSis-EwD9F028NG0


*********************************************
Kwa wenye watoto Marekani wataijua sinema ya The Wizard of Oz. Meinhardt Raabe ambaye aliigiza kama 'coroner' katika hiyo sinema amefariki dunia. alikuwa na miaka 95. Sinema the Wizard of Oz ilitoka mwaka 1939. Raabe alikuwa katika ile scene dorothy anapotua na nyumba yake 'Munchkinland' Nyumba inamwua mchawi mwenye roho mbaya wa magharibi.

Meinhardt Raabe, who played the Munchkin coroner in "The Wizard of Oz" and proclaimed in the movie that the Wicked Witch of the East was "really most sincerely dead," has died. He was 94.

His caregiver, Cindy Bosnyak, said Raabe - pronounced RAH'-bee - died Friday morning at a hospital in Orange Park, Fla. He was one of the few surviving Munchkins from the 1939 film.
Bosnyak said he complained of a sore throat at his retirement community before collapsing and going into cardiac arrest. He was taken to Orange Park Medical Center, where he later died, she said.

Kwa habari zaidi soma:

http://www.myfoxla.com/dpp/entertainment/celebrity_news/meinhardt-raabe-oz-munchkin-dies-at-94-20100409

Wednesday, April 07, 2010

Kutozwa Mapesa Kwenye Ndege Inazidi... Sasa Hata Kutumia Choo!

Haya, leo tumesikia kuwa tutatozwa hela kwa ajili ya 'carry on' bag kwenye Spirit Airlines. Mjue na airlines zingine zitaiga! Haya sasa Ryan Air wanasema utatozwa hela kutumia choo kwenye ndege! Jamani, sasa kama mtu kambanwa, ndo akae nayo mpaka ndege itue! Hii sasa ni uchu wa pesa!

Kaa habari zaidi:

http://www.cnn.com/2010/TRAVEL/04/07/ryanair.lavatory.fee/index.html?hpt=T2

http://www.latimes.com/business/la-fi-spirit7-2010apr07,0,5945292.story?track=rss

Tuesday, April 06, 2010

Mbaguzi Eugene Terreblanche Ameuwawa!

Wadau, sijui tusherekee au tuwe na majonzi. Mbaguzi Eugene Terreblanche ameuwawa huko Afrika Kusini na wafanyakazi wake wawili. Waliomwua ni vijana wenye miaka 21 na 16. Wamejisalimisha kwa polisi.

Huyo Terreblanche alikuwa ni mshenzi kupindukia, alikuwa hapendi uhuru kwa weusi, na alikuwa anaongoza kikundi cha wazungu wenye sias kali huko. Mikutano waliyokuwa anongoza ilikuwa inajaa wazungu wenye chuki dhidi ya weusi. Alikuwa na mtindo wa kutuma mbwa wake ku'gata watu weusi, na pia alijaribu kumwua mlinzi wake mweusi. Alitega mabomu zaidi ya 20 kabla ya uchaguzi wa kihistoria wa mwaka 1994 huko Afrika Kusini.

Kuna watakaosherekea kifo chake na watakaolia.

Mnaweza kusoma habari zaidi:

http://www.cnn.com/2010/WORLD/africa/04/04/south.africa.terreblanche/index.html?hpt=Sbin

Monday, April 05, 2010

Ona Mambo ya Wahindi Cleveland, Ohio

Wadau hebu cheki wahindi wanavyokuza utamaduni wao huko Cleveland, Ohio. Wamefungua Bustani - Indian Cultural Garden. Wahindi wana sauti Cleveland, ns sisi waafrika tukiwa na umoja tunaweza kuwa na Sauti hapa Massachusetts. Umoja muhimu! Halafu eti hapa Boston tunasemwa na waafrika wenzetu kwa ajili ya kutaka kukutana na Gavana!


http://www.clevelandseniors.com/family/asian-indians.htm

Mapambano Katika Vita Dhidi ya UKIMWI

Wadau, inaelekea kuna maendeleo katika harakati ya kutafuta chanjo dhidi ya UKIMWI:

************************************************************

TUSTIN, Calif., April 5 /PRNewswire-FirstCall/ -- Peregrine Pharmaceuticals, Inc. (Nasdaq:PPHM - News) today announced the publication of data showing phosphatidylserine (PS)-targeting antibodies can block one of the key ways the AIDS virus gains entry into certain blood cells. The data were generated by scientists at Duke University as part of their ongoing AIDS vaccine research. The article titled "Anti-Phospholipid Human Monoclonal Antibodies Inhibit CCR5-Tropic HIV-1 and Induces Beta-Chemokines" is available online today and will be published in the April 12, 2010 edition of the Journal of Experimental Medicine. Peregrine's PS-targeting antibodies are currently in clinical development for the treatment of cancer and HCV infections.

Mnaweza kusoma Article nzima Hapa:

http://finance.yahoo.com/news/Peregrine-Pharmaceuticals-prnews-595526903.html?x=0&.v=1&.pf=banking-budgeting&mod=pf-banking-budgeting

Sunday, April 04, 2010

Heri ya Pasaka! Happy Easter!



Wadau, waKristo duniani pote leo wanasherekea siku ya kufufuka Bwana Yesu Kristo (Pasaka). Pia kwa hapa Marekani, ni siku ambayo Sungura wa Pasaka (Easter Bunny) anapita na kugaia watoto mayai yaliochemeshwa na kupakwa rangi, na pia mayai ya chocolate.

Pasaka Njema! Happy Easter!

Saturday, April 03, 2010

Asante kwa Salamu za Birthday!

Pichani- Mimi mwaka 1965 nikiwa na miezi 14

Wadau, asanteni sana kwa walionitumia salamu za birthday. Tangu juzi napokea simu, text message, kadi na e-mails kutoka kwa watu mbalimbali na nchi kadhaa. Birthday yangu ni leo, April 3rd.

Asante sana kwa moyo huo wa upendo. Sikutegemea! Mungu awabariki nyote.

Friday, April 02, 2010

Kazi Washington D.C. kwa Mwanasheria

Asante Da Subi kwa kuleta habari hizi:

Naona hii kazi ipo maeneo ya kwenu huko. Kama unamfahamu Mtanzania au Mswahili yeyote anayeweza kufanya hii basi tafadhali mpasie.
Subi|www.wavuti.com
***********************************************************************

Hire Counsel is seeking attorney candidates who are fluent in Swahili for document review projects in the Washington D.C. area.

You MUST be licensed to practice in a US jurisdiction.

To be considered for this opportunity, please email your resume as a Word document to dclanguagejobs@hirecounsel.com.

Hire Counsel offers one of the industry’s most generous benefits packages including medical, dental and disability insurance, 401(k) plan, and holiday, and bonus pay. All resumes are held in strict confidence. We NEVER forward your resume anywhere without obtaining your authorization first. At Hire Counsel we take great pride in the professional, courteous and congenial manner in which we work with all of our employees. We recognize our success is due to the efforts of our talented pool of hardworking temporary employees. Hire Counsel is a national legal staffing organization dedicated to providing our clients with the finest candidates available. We keep this promise by offering our candidates an industry-leading benefits package and by hiring smart, experienced staff, all of whom are attorneys and paralegals committed to responsive, active service.

Refer a friend and receive a bonus.
For more details please visit www.hirecounsel.com/employee-referral-bonus-program

For other Attorney opportunities visit www.hirecounsel.com