Wednesday, May 31, 2017

Mama Bishanga Amlilia Ivan X - Mume wa Zari

Pichani ni Mama Bishanga  aka Mrs. Marolen
MAMA BISHANGA AMLILIA IVAN X HUSBAND WA ZARI
Nimesikitishwa sana na kifo cha Ivan, ni mapema sana kwa yeye kuondoka duniani kuacha watoto wadogo sana, wanahitaji sana uwepo wa baba na mama, lakini Mungu ni Mwema amependezwa nae kuwa karibu yake mbinguni.
Zari binti yetu pole sana kwa pigo hili kubwa lisilozibika kwa wepesi, Mungu akutie nguvu. Wewe ni mmoja kati ya mabinti wachache walio na msimamo imara kimaisha, wasioyumba, wanaojitegemea zaidi kimaisha kwa kufanya biashara na shughuli mbalimbali kujipatia kipato, usieyumbishwa na mapito ya maisha ya dunia kirahisi. Naweza kusema nimekufahamu baada ya kuwa na mpenzi wako Diamond, umeonyesha msimamo na uimara wako ambao ni ushahidi mzuri kuwa utawatunza wanao watatu ambao sasa wako mikononi mwako forever. Usikate tamaa wengi tumepitia uliyopitia, kuvunjika kwa ndoa na kufiwa na wenzetu na kubakia na watoto, yalinikuta mimi binafsi hayo sikujua ada, nauli, kusomesha watoto  hadi mwenzangu alipofariki mwaka 1994 nikiwa Idara ya elimu ya juu na mshahara wa ualimu, na watoto kurudi kwangu, hapo ndio niliona jinsi Mungu huongeza baraka zake, na jinsi ukoo wa Kamota ulivyosimama nami kulea watoto. Nawewe daima muweke Mungu mbele mambo yatakuwa mazuri, hasa ukizingatia ulishajiimarisha na baba watoto wako amewaacha vizuri, Mungu atakuongezea na kukutia furaha ya maisha ya familia yako, na bila kusahau kuwa Diamond yuko pemebeni yako, tabasamu lake linatosha kukuongezea amani na nguvu ya maisha na kilo za uzito wa mwili confidence! Diamond amelelewa vizuri sana na mama yake na yuko wazi katika penzi lenu, sasa ni wakati wa kushikamana kikamilfu kupeana raha na amani na kuijenga familia yenu .
Kila la heri Zari, huenda tukaonana JHB maana sehemu ya maisha yangu ni JHB kwa mume wangu Orange Grove na Alexander township!
GOD BLESS YOU AND YOUR FAMILY ZARI
MAMA BISHANGA / MRS MAROLEN
CLEVELAND. OHIO

Saturday, May 27, 2017

Ramadhan Kareem


 

Mkutano Mkuu wa Vijana Kimataifa Kufanyika Arusha

Mkutano Mkuu wa Vijana Kimataifa Kufanyika Arusha kwa Siku 7 [caption id="attachment_79335" align="aligncenter" width="800"] Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa Vijana Tanzania, Tajiel Urioh akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kuzungumzia Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa unaokutanisha vijana utakaofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi Mei, 2017 mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Arafat B. Lesheoe.[/caption]   AKIZUNGUMZA na waandishi wa habari Mratibu wa Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa, Tajiel Urioh alisema mkutano huo ni maigizo ya vitendo ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa ambapo vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 30 kutoka sehemu mbalimbali wanapata fursa ya kujifunza Diplomasia, Uongozi na namna Umoja Wa Mataifa unavyofanya kazi. Bw. Tajiel Urioh alisema kuwa, Mkutano huo unaojulikana kama kongamano kubwa kabisa la vijana nchini linalowaleta pamoja vijana wadogo kutoka nchi mbalimbali tangu mwaka 1997. Aidha aliongeza kuwa Mkutano huo Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa utafanyika mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi wa Mei mwaka 2017, ambapo vijana takribani 200 kutoka katika nchi mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria kujadili masuala yanayohusiana na Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango, Demokrasia na Amani katika nchi zinazoendelea, Kuhama kuelekea kwenye Nishati safi na ya teknolojia mbadala na Elimu kwa Maendeleo Endelevu. Aliongeza kuwa majadiliano ya mwaka huu yatajikita katika mada kuu: “Kuwawezesha Vijana katika Diplomasia na Uongozi”. Mada hii inalenga kuwezesha ushiriki wa vijana na kuwajengea uwezo kwenye masuala ya Diplomasia na Uongozi kwa kuwapa mafunzo ya vitendo katika mada ngumu ambazo zitawaongezea ujuzi wa majadiliano na kufikia muafaka wa masuala mtambuka yanayogusa maslahi ya mataifa. "Tunaishi katika ulimwengu ambao diplomasia yenye ujasiri na uongozi vinahitajika sana hivyo basi kuwakuza vijana katika uwanja huu itachangia kukua kwa mataifa yenye watu wenye uwezo wa kuamua mambo yao. Katika mkutano wa mwaka huu wajumbe watakuja na maazimio mbalimbali ambayo kwa namna moja hama nyingine yatakuwa na manufaa katika maisha yao ya kila siku na watu wanaowazunguka katika jamii zao," alisema Bw. Urioh.   [caption id="attachment_79334" align="aligncenter" width="800"] Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa Vijana Tanzania, Tajiel Urioh akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kuzungumzia Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa unaokutanisha vijana utakaofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi Mei, 2017 mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Kushoto ni Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akiwa katika mkutano huo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Arafat B. Lesheoe.[/caption]   “Ni matarajio yangu makubwa kwamba mtakuwa tayari kujifunza kuendana na mada kuu ya ‛ Kuwawezesha Vijana katika Diplomasia na Uongozi′ lakini pia kubadilishana mawazo na wajumbe wengine na kutengeneza mtandao wa vijana wenye fikra mnazoendana nazo,” aliongeza Tajiel Urioh, Mratibu wa Kitaifa wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2017. Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo alisema kongamano kama hilo la vijana lina umuhimu mkubwa kwa vijana kwani huwajenga vijana kupitia Club za UN. Aliwataja miongoni mwa vijana ambao ni matunda ya Club za UN ni pamoja na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Benedict Kikove, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi, Mbunge wa Kibamba (Chadema), John John Mnyika na wengine wengi.

Ucheleweshaji wa Pembejeo Umetajkwa Kuporomosha Kilimo Mkoani Geita

UCHELEWESHAJI WA PEMBEJEO UMETAJWA KUPOROMOSHA KILIMO CHA PAMBA WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA


Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbogwe, (kulia), Elias Kayandabila, akizungumza  na waandishi wa habari, walioongozana na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) pamoja na Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) waliopo mkoani Geita kwa ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani.

Saturday, May 13, 2017

Tanzia - Mh, Said Thabith Mwambungu

 
The late Regional Commissioner Said Thabith Mwambungu
 
Kutoka kwa mwandishi mahili  Nickson Mkilanya 
 
 KWAHERI YA KUONANA RC SAID THABITH MWAMBUNGU
 
Amefariki leo katika hospitali ya taifa ya muhimbili,hatunaye tena, Said Thabith Mwambungu mkuu wa mkoa mstaaf na miongoni mwa wanasiasa wabobezi na wakongwe katika zama hizi.
Ameripotiwa kusumbuliwa na ugonjwa wa figo kwa siku kadhaa hata akapelekwa kutibiwa nchini India na kurejea na nafuu ambayo pia haikupata kumrejesha katika majukwaa ya siasa na hata hadharani.
 
Kuugua huko pasipo kutajwa kuwa ndiyo sababu iliyopelekea rais Magufuli kumhamishia ofisi ya waziri mkuu na kuahidi kumpangia kazi zingine toka juni 26 mwaka jana lakini nafsi yangu yakiri kuwa pengine hiyo ndiyo sababu kuu.
 
Alilitamka kwa ufasaha jina lake la said said thabith mwangu enzi za uhai wake hasa pale nilipofanyakazi naye mimi nikiwa kama mwanahabari wa luninga,radio na hata magazeti, ni mzaliwa wa Malinyi mkoani Morogoro ambaye kwangu mimi ni miongoni mwa wanasiasa bora,baba Bora na kielelezo cha watu wema na wastaarabu niliopata kukutana nao.

Miongoni mwa mambo aliyoyaacha km funzo kwangu ni uvumilivu na upendo. Wakati mmoja akiwa mkuu wa wilaya kuna kiongozi mmoja alimfanyia figisu figisu nyingi ambazo hata wanahabari tuliona na kugundua akionewa dhahiri! Lakini tulipoongea naye jibu lake alijibu kuwa mwacheni tu huyo, hayo ni yakupita, hajui siasa, vumilieni yataisha na kweli huyo mtu alikuja ondolewa ktk nafasi na kumwacha mwambungu akitamba na siku chache baadae kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa ruvuma.
 
Jambo lingine alijua kuthamini watu na kuwaonesha upendo wa dhati hata wale ambao kwa tabia za kibaguzi wasingepaswa kumsogelea lkn bado aliwapa nafasi sawa na wale ambao kimtazamo walikuwa na sifa ya kumsogelea. Nakumbuka wakati mmoja aliniambia nick mwanangu fanya mpango uoe nikufanyie sherehe kabla sijaondoka na hapa alimaanisha kabla hajahamishwa kituo cha kazi nami nilicheka na kuahidi kufanya hivyo lkn leo hatunae tena ameondoka mwambungu pasipo kushughudia harusi yangu.
 
Amini mungu ni mwema wanae wakiongozwa na hamidu mwambungu watashughudia harusi yangu kwa niaba yake inshallah.
 
Wakati wa uhai wake alipata kuwa kada mwandamizi katika ccm, katibu wa chama cha mampinduzi mkoa,  mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa achilia mbali nafasi zingine nyeti ndani ya nchi hii, Na ameacha watoto watatu, hamidu said said thabith mwambungu, Khalid na Abiba S. S Thabith mwambungu na mjane.
 
 Mtoto mkubwa wa marehemu  aitwae Hamidu Mwambungu anasema haijaamuliwa bado kama baba yao atazikwa morogoro au kwingineko.
 
Tangulia mtu mwema Said Said Thabith Mwambungu.

Saturday, May 06, 2017

Buriani Mwanahabari Revocatus Bulizya

Marehemu Revocatus Bulizya enzi za uhai wake
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mwanahabari Revocatus Bulizya wakati ukiingizwa katika Kanisa la Katoliki Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya ibada ya kuuaga kabla ya kwenda kwenye mazishi yaliyofanyika Mwandege Kongowe Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.