Friday, December 31, 2010

Heri ya Mwaka Mpya 2011

Nawatakia wadau wote Heri ya Mwaka Mpya!
Kwa heri Mwaka 2010! Karibu Mwaka 2o11!

Salaams za Mwaka Mpya kutoka Kwa Rais Kikwete



SALAM ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MHESHIMIWA DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA,
TAREHE 31 DESEMBA, 2010

Ndugu Wananchi;
Habari za jioni.
Leo tunauaga Mwaka 2010 na kuukaribisha Mwaka 2011. Kama ilivyo ada, hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, kwa kutujaalia uhai na kutuwezesha kuifikia siku hii adhimu. Wapo ndugu, jamaa na marafiki zetu wengi ambao hawakujaaliwa bahati hii kwa kuwa wametutangulia mbele ya haki. Tuzidi kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awape mapumziko mema.

Ndugu Wananchi;
Kwa namna ya kipekee mimi binafsi, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia uzima na kuniwezesha kuendelea kuitumikia nchi yangu na ninyi wananchi wenzangu. Nawashukuruni sana wananchi wenzangu kwa kuendelea kuniunga mkono mimi na kuiunga mkono Serikali yetu ninayoiongoza. Mmefanya hivyo mwaka huu tunaoumaliza leo na tangu tuingie madarakani miaka mitano iliyopita mpaka sasa. Imani na upendo mliyotuonesha vimetupa faraja na ari ya kuendelea kuwatumikia kwa bidii zaidi. Nawaomba muendelee na moyo huo katika mwaka mpya tunaoukaribisha usiku wa leo. Mimi nawaahidi kuendelea kutumia vipaji vyangu vyote nilivyojaaliwa na Mwenyezi Mungu kuwatumikia wakati wote na kwa hali yoyote kama nilivyofanya mwaka huu tunaoumaliza leo na miaka ya nyuma.

Ndugu wananchi;
Mwaka 2010 ulikuwa na shughuli nyingi na mafanikio mengi licha ya kuwepo changamoto mbalimbali zilizojitokeza. Kwa ajili hiyo tunaingia mwaka 2011 tukiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri zaidi.
Hali ya Usalama Nchini

Ndugu Wananchi;
Hali ya usalama wa nchi yetu ni mzuri, mipaka iko salama na hakuna tishio lolote kutoka mahali popote au watu wowote linalotia mashaka. Uhalifu umeendelea kudhibitiwa na mafanikio yamekuwa yanapatikana. Taarifa ya Jeshi la Polisi ya hivi karibuni inaonyesha kuwa matukio ya uhalifu yamepungua mwaka huu ukilinganisha na mwaka uliopita.

Ndugu Wananchi;
Ni jambo la kujivunia kwamba tumemaliza mchakato wa uchaguzi mkuu kwa amani na salama. Tulikuwa na siku 70 za kampeni, moja ya kupiga kura na siku 6 za kusubiri matokeo bila ya kuwepo matukio ya uvunjifu wa amani yanayostahili kuzungumzwa. Sehemu zetu zote mbili za Muungano kulikuwa salama na Zanzibar ndiko kulikuwa na utulivu mkubwa zaidi kuliko miaka ya nyuma.

Hakika Tanzania tumeendelea kudumisha sifa yetu ya kuwa kisiwa cha amani na utulivu. Naomba sote tujipongeze, lakini tutoe pongezi maalum kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya mwaka huu ya kuhakikisha kuwa nchi yetu na watu wake wako salama.
Demokrasia Inazidi Kuimarika

Ndugu Wananchi, Watanzania Wenzangu;
Mwaka huu tumeshuhudia demokrasia ilivyozidi kuota mizizi, kukomaa, kustawi na kuimarika. Tumefanya Uchaguzi Mkuu wa nne chini ya mfumo wa vyama vingi kwa mafanikio makubwa. Sisi wenyewe ni mashahidi na dunia nzima ni mashahidi wa ukweli huo. Wakati tukitambua na kujipongeza kwa mafanikio haya, hatuna budi kujiwekea dhima ya kufanya mambo yetu vizuri zaidi katika chaguzi zijazo. Tufanye tathmini ya uchaguzi wetu uliopita ili tuimarishe na kudumisha yaliyo mazuri na kurekebisha yenye mapungufu.

Ndugu Wananchi;
Uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa na ushindani mkali na nguvu ya vyama vya upinzani imeongezeka. Hili ni jambo jema kwa utawala bora na uwajibikaji nchini. Bila ya shaka Bunge litachangamka kama tunavyotarajia sote. Nimewakumbusha Mawaziri wajibu wao wa kuwa makini na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi Bungeni. Kwa upande wa Chama tawala hatuna budi kujipanga na kujijenga upya kwa kuzingatia mazingira mapya ya kisiasa nchini.

Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;
Naomba kurudia kukumbusha kuwa uchaguzi ulishaisha Oktoba 31, 2010 na malumbano ya kampeni za uchaguzi yalimalizika wakati ule. Sasa ni wakati wa kuendelea kufanya shughuli zetu za kawaida za kujiletea maendeleo yetu wenyewe na ya nchi yetu. Kuendeleza malumbano na kuendelea kuishi kama vile kampeni za uchaguzi bado zinaendelea siyo sahihi hata kidogo.
Najua wapo baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa ambavyo vimepanga mikakati ya kuendeleza malumbano ya uchaguzi na kutaka Watanzania waishi kama vile nchi ipo kwenye kampeni za uchaguzi. Wamepanga wakati wote kutafuta jambo au hata kuzua jambo ili kuwachochea wananchi waichukie Serikali. Wamepanga kuchochea migomo vyuoni na maandamano ya wananchi mara kwa mara. Kwao wao huo ndiyo mkakati wa kujijenga kisiasa ili kujiandalia ushindi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

Nawatanabaisha ndugu zangu myajue hayo ili msipoteze muda wenu muhimu wa kujiendeleza na kugeuzwa kuwa mbuzi wa kafara kwa ajili ya kuendeleza maslahi ya kisiasa ya watu fulani. Kwa jinsi watu hao walivyokuwa wabinafsi na wasivyokuwa na huruma na wenzao, wako tayari kuchochea ghasia bila kujali madhara yatakayowakuta watu watakaoshiriki. Wao hasa wanachotaka ni ghasia kutokea na vyombo vya dola kuingilia ati waiambie jumuiya ya kimataifa jinsi Serikali yetu ilivyo katili. Nawasihi ndugu zangu msiwasikilize wala kuwafuata wanasiasa hawa.
Nawaomba, wakiwafuata wakumbusheni kuwa wao wanazo fursa nyingi za kusema wayatakayo Bungeni na kwingineko, waache kuwatumia kama chambo au wahanga wa maslahi yao.

Uwajibikaji wa Mawaziri
Ndugu wananchi;
Tunaumaliza mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011 tukiwa na Serikali mpya yenye damu mpya nyingi na changa katika Baraza la Mawaziri. Nimejitahidi kuwapanga Mawaziri hao kwa namna ambayo wanaweza kutumia vyema maarifa yao na uzoefu wao kulisukuma kwa kasi, ari na nguvu zaidi, gurudumu la maendeleo ya nchi yetu. Nimeshakutana na kuzungumza nao wote kuhusu majukumu yao na wajibu wao.

Nimewasisitizia matumaini yangu kwao ya kuwa wachapa kazi hodari na kupiga vita rushwa, uzembe na ubabaishaji bila ya ajizi. Wawe watu waaminifu na waadilifu, watakaochukia maovu na kuyapiga vita kwa nguvu zao zote katika maeneo yao ya kazi. Wawe ni watu wenye moyo wa kuipenda nchi yetu na watu waliotayari kuitumikia kwa moyo na uwezo wao wote. Wawe karibu na watu wawasikilize na wawe wepesi kutatua shida zao. Aidha, nimewakumbusha kutambua kuwa ahadi kubwa ya CCM kwa Watanzania ni Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010, hivyo wahakikishe kuwa malengo ya Ilani kuhusu maeneo yao ya uongozi wanayatambua vizuri na kuyapangia mipango thabiti ya utekelezaji na kufuatilia kwa dhati utekelezaje wake. Nafurahi kwamba Mawaziri tayari wameanza kazi kwa kasi nzuri na wengine kwa kishindo. Naomba tuendelee kuwaunga mkono na kuwasaidia.

Nidhamu ya Matumizi
Ndugu Wananchi;
Miongoni mwa mambo ambayo nimesisitiza kwa Mawaziri ni kuhakikisha kuwa wanasimamia vizuri ukusanyaji wa mapato ya Serikali na hasa nidhamu ya matumizi ya fedha na mali za umma. Tunapata mafanikio ya kutia moyo kwa upande wa ukusanya mapato. Ndugu zetu wa TRA wanastahili pongezi zetu kwa kazi waifanyayo. Pamoja na hayo hatuna budi kuongeza mapato ya Serikali maradufu juhudi zetu za kukusanya mapato, kwani mahitaji yanazidi kuongezeka wakati uwezo wa mapato hauongezeki kwa kasi hiyo hiyo.

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa nidhamu ya matumizi bado hatujapiga hatua ya kunifanya nipoe moyo, ingawaje kuna mafanikio yanayoendelea kupatikana. Niliwakumbusha Mawaziri kuhusu kuwepo Kamati za Matumizi ya Fedha katika kila Wizara, Idara za Serikali na Halmashauri za Wilaya na Miji ambazo niliagiza ziundwe miaka mitatu iliyopita. Niliwakumbusha kuwa, wakuu wa taasisi hizo ndio wanaoongoza Kamati hizo na hivyo wao ndiyo wanaoongoza Kamati za Wizara zao. Nimewataka wahakikishe kuwa Kamati hizo zinatekeleza ipasavyo majukumu yake ili rasilimali za taifa zifanye kazi iliyokusudiwa. Halikadhalika, niliwataka wahakikishe kuwa Kamati za Idara na Mashirika chini ya Wizara zao zinafanya kazi kwa ukamilifu.

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa Halmashauri za Wilaya na Miji, mwaka huu tuliendelea kuziimarisha Idara za Uhasibu na Ukaguzi wa Ndani. Tutaendelea kuhakikisha kuwa kila Halmashauri ina Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani wenye ujuzi na sifa zinazostahili za kitaaluma, uaminifu na uadilifu.

Siku za nyuma tulishafanya uamuzi wa kumfanya Mhasibu Mkuu wa Serikali kuwa na mamlaka ya kuangalia utendaji wa shughuli za fedha katika Halmashauri za Wilaya na Miji kama aliyonayo kwa Wizara na Idara za Serikali Kuu. Mwaka huu tumeamua kuwaunganisha Wakaguzi wote wa Ndani wa Wizara na Idara za Serikali chini ya Uongozi mmoja. Aidha, tumeunda nafasi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani ambaye Wakaguzi wa Ndani wote wa Wizara na Idara za Serikali watakuwa chini yake na kuwajibika kwake. Yeye atahusika na uteuzi wao na kuwapangia vituo. Tumeamua, pia, kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani atakuwa na mamlaka kwa Wakaguzi wa Ndani wa Halmashauri za Wilaya na Miji. Bila ya shaka hatua hii itasaidia kuimarisha uwajibikaji, nidhamu na uaminifu katika matumizi ya pesa na mali za umma.

Hali ya Uchumi
Ndugu Wananchi;
Tunaumaliza mwaka 2010 hali ya uchumi wa nchi ikiwa ni ya kuridhisha. Inaelekea athari za miaka mitatu iliyopita zilizosababishwa na misukosuko mbalimbali ya uchumi wa dunia sasa zinanza kutoweka. Tunatarajia kuwa mwaka huu uchumi utakua kwa asilimia 7 ukilinganisha na asilimia 6 ya mwaka 2009. Matumaini yetu ni kuwa mwaka 2011 uchumi utakua kwa asilimia 7.2 kama mambo yatakwenda kama tunavyotarajia.

Mfumuko wa bei nao umeshuka sana kutoka wastani wa asilimia 12.1 mwaka 2009 hadi asilimia 5.5 Novemba, 2010. Ni dhamira yetu na matarajio yetu kuwa mfumuko wa bei utaendelea kuwa chini ya hapo. Kwa ajili hiyo hatuna budi kuhakikisha kuwa hali ya ipatikanaji wa chakula nchini inaendelea kuwa nzuri.

Kilimo na Chakula
Ndugu wananchi;
Hali ya upatikanaji wa chakula nchini ilikuwa nzuri katika mwaka 2010 lakini hatuna hakika hali itakuwaje katika mwaka 2011. Tunazo sababu za kutia shaka kwa sababu ya hali ya mvua kutokuwa nzuri katika maeneo mengi hapa nchini. Maeneo mengi yanayopata mvua za vuli katika mikoa ya Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara hali ilikuwa mbaya. Mvua zimekuwa pungufu sana na wakulima wengi hawakudiriki hata kupanda mazao. Kwa mikoa hii matumaini yetu tunayaweka kwa mvua za masika zinazotarajiwa kuanza kunyesha mwezi Machi. Tuombe kwa Mola mvua zipatikane za kutosha tunusurike na baa la njaa.

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa Mikoa ya Kusini Nyanda za Juu na mingineyo inayopata mvua moja kuanzia mwezi Novemba au Desemba, mvua zilichelewa kuanza kunyesha. Hivi sasa zimeanza na zinaendelea vizuri. Tuzidi kumuomba Mungu ziendelee vizuri ili taifa liwe na hakika ya akiba ya kutosha ya chakula ambayo huchangiwa kwa zaidi ya asilimia 85 na mikoa ya ukanda huu.
Wataalamu wetu wa Idara ya Hali ya Hewa wametahadharisha kuwa hata maeneo haya huenda yakapata mvua chini ya kiwango cha kawaida. Kwa ajili hiyo, niwaombe ndugu zangu wa mikoa ya Iringa, Ruvuma, Mbeya na Rukwa kuhakikisha kuwa wanazitumia vizuri mvua zinazonyesha sasa. Tukifanya hivyo athari za upungufu wa mvua tutazipunguza. Na, kwa wananchi wote kwa jumla nawaomba tuwe waangalifu katika matumizi ya akiba yetu ya chakula tuliyonayo. Wahenga walisema “tahadhari kabla ya hatari”. Tuzingatie maneno hayo ya hekima.

Hifadhi ya Chakula
Ndugu Wananchi;
Mwaka 2010 tumeamua kuongeza akiba yetu ya chakula katika Hifadhi ya Taifa ili ifikie tani 400,000 ifikapo mwaka 2015. Tumeanza safari hiyo kwa dhati. Mwaka huu tumenunua tani 200,000 na kuzihifadhi. Kwa sababu hiyo tuliongeza fedha za kununulia chakula kutoka shilingi bilioni 18.2 hadi shilingi bilioni 60.26. Tutaendelea kukuza uwezo huo mpaka tufikie lengo letu.

Pembejeo za Kilimo
Ndugu Wananchi;
Mwaka huu tumeongeza mbolea ya ruzuku na wakulima wengi zaidi watapata mbolea hiyo. Tutaendelea kufanya hivyo katika miaka ijayo kwa lengo la kuwafikia wakulima milioni 3.5 mpaka 4 miaka mitano ijayo. Aidha, tutaendelea kufuatilia na kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya upatikanaji na hasa usambazaji wa pembejeo kwa wakulima na wafugaji. Nasikitishwa sana na taarifa za vitendo vya wizi na udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya mawakala wa mbolea, mbegu na dawa za kilimo na mifugo wakishirikiana na baadhi ya watumishi wa umma wa ngazi mbalimbali.

Nimewataka Mawaziri husika na hasa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya na vyombo vya dola yaani Polisi na TAKUKURU kufuatilia mwenendo mzima wa usambazaji na upatikanaji wa mbolea, mbegu na dawa za ruzuku kwa wakulima na wafugaji. Wawatafute na kuwabaini wale wote wanaofanya vitendo viovu kinyume na taratibu zilizowekwa na kuwachukulia hatua za kisheria na kinidhamu. Watu hawa ni wahujumu wa uchumi, ni adui wa wakulima, wafugaji na taifa zima kwa jumla. Hawastahili na wala wasionewe huruma hata chembe.

Ndugu wananchi;
Pamoja na mikakati tuliyojiwekea ya kuboresha kilimo, tutaendelea kuwekeza na kuhamasisha uwekezaji katika sekta nyingine ambazo tunazitegemea zisaidie kukuza uchumi na kupunguza umaskini kama vile viwanda, utalii, biashara, miundombinu ya barabara, reli, bandari, umeme, maji n.k. Kwa upande wa huduma ya fedha, Serikali itaendelea kuongeza mtaji kwenye Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) ili irudie kuwa benki ya maendeleo na kutoa mikopo ya muda wa kati na mrefu kwa wawekezaji wetu. Ni dhamira yetu kuwa mwaka 2011 tuongeze kasi ya kuanzisha Benki ya Kilimo ili ikiwezekana ianze au matayarisho yafikie hatua nzuri ya kuweza kuanza mwaka unaofuata.

Matatizo ya Umeme
Ndugu wananchi;
Mwaka 2010 haukuwa na utulivu wa kutosha kwa upatikanaji wa umeme. Mara kadhaa kumekuwepo na matukio ya kukatika na mgao wa umeme kutokana na uharibifu wa mitambo ya kuzalisha umeme hasa katika kituo cha Songas na vituo vya TANESCO. Pamoja na hayo tatizo la msingi ni uwezo wa uzalishaji wa umeme kuwa mdogo kuliko mahitaji. Hivyo basi, hitilafu katika mtambo mmoja au kituo kimoja cha kuzalisha umeme huzua tatizo kubwa la upatikanaji wa umeme kwa nchi nzima.

Ndugu Wananchi;
Katika kukabiliana na tatizo hilo miaka mitano iliyopita, TANESCO kwa msaada wa Serikali, imeongeza uwezo wa kuzalisha umeme kwa MW 145 (MW 100 Ubungo na MW 45 Tegeta) kwa kutumia gesi asilia. Bahati mbaya mpango wa kuzalisha MW 300 kule Mtwara kwa kushirikiana na sekta binafsi, haukufanikiwa baada ya mwekezaji kushindwa kupata fedha kwa sababu ya mgogoro wa masoko ya fedha ya kimataifa. Kama tatizo hilo lisingekuwepo umeme huo ungekuwa unakamilika au kukaribia kutumika hivi sasa.

Kwa sasa TANESCO ina mipango kadhaa inayoendelea nayo ya kuongeza uzalishaji wa umeme nchini. Kwa msaada wa Serikali ndani ya miezi 12 ijayo, TANESCO itaongeza uzalishaji wa umeme kwa MW 160, (MW 100 Ubungo kwa kutumia gesi asilia na MW 60 Mwanza kwa kutumia dizeli nzito). Kwa kushirikiana na sekta binafsi pia, ndani ya miezi 36 ijayo TANESCO wanatarajia kukamilisha ujenzi wa vituo vya umeme huko Kinyerezi (MW 240) Somanga Fungu (MW 230) na Mtwara (MW 300). Inatarajiwa pia kwamba katika kipindi hicho mradi wa kuzalisha MW 200 pale Kiwira utakamilika.

Bei ya Umeme
Ndugu Wananchi;
Natambua kuwepo kwa mazungumzo, katika jamii kuhusu uamuzi wa EWURA wa kukubali ombi la Shirika la Umeme (TANESCO) kuongeza bei ya umeme. Wakati mwingine mazungumzo yamekuwa na hisia kali na hata jazba kutawala. Wizara, TANESCO na EWURA wameeleza kwa ufasaha misingi iliyotumika mpaka kufikia uamuzi huo. Sina maelezo mazuri zaidi ya hayo. Ninachotaka kusema mimi ni kuwaomba Watanzania wenzangu kutokukubali suala hili la kibiashara na kiuchumi kugeuzwa kuwa la kisiasa na kutafutiwa majawabu ya kisiasa.

Naomba tuamini na kukubali maelezo ya TANESCO na EWURA kwamba katika miaka minne hii gharama za uendeshaji, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme zimepanda kama zilivyopanda katika shughuli nyingine. Hivyo basi, kutaka bei ya umeme ibaki kama ilivyokuwa miaka minne iliyopita hautokuwa uamuzi sahihi kiuchumi na kibiashara kwa TANESCO. EWURA imefanya kazi nzuri ya kuchambua maombi ya TANESCO na kuyakubali yanayostahili na kuyakataa yasiyostahili kuwa sehemu ya bei. Kwa kufanya hivyo, watumiaji wa umeme wamelindwa wasibebeshwe mzigo usiostahili na Shirila la Umeme limewezeshwa ili lisiendeshe shughuli zake kwa hasara.

Mahusiano ya Kimataifa
Ndugu Wananchi;
Katika mwaka 2010 Serikali iliendelea na jitihada za kupigania na kuendeleza maslahi ya Tanzania miongoni mwa mataifa duniani na mashirika ya kimataifa na kikanda. Kazi hiyo tumeifanya kwa mafanikio na faida zake tunaziona. Tumeshuhudia kuongezeka kwa misaada ya maendeleo, kupatiwa misamaha ya madeni, kuongezeka kwa wawekezaji na mitaji kutoka nje na kuzidi kuongezeka kwa watalii. Aidha, mauzo yetu nje pamoja na mapato na akiba yetu ya fedha za kigeni navyo vimeendelea kuongezeka.

Jina la nchi yetu limeendelea kung’ara katika medani za kimataifa. Tanzania imeendelea kushirikishwa katika masuala muhimu ya kikanda na kimataifa. Kwa mfano, Rais Mstaafu, Mheshimiwa Benjamin W. Mkapa aliteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuongoza Tume ya kuangalia mchakato wa kura ya maoni ya Sudan ya Kusini itakayofanyika tarehe 9 Januari, 2011.

Katika kura hiyo, wananchi wa Sudan ya Kusini wataamua iwapo wawe taifa huru au waendelee kuwa sehemu ya Sudan kama ilivyo sasa na Wananchi wa Jimbo la Abyei watapiga kura ya kuamua wawe upande upi: Sudan Kusini au Sudan Kaskazini. Tunamtakia heri Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ili akamilishe jukumu hilo kwa mafanikio. Wakati huo huo tunawatakia wananchi wa Sudan ya Kusini na Sudan, kwa jumla, kuendesha zoezi hilo kwa amani na salama ili watu wapate fursa ya kuamua matakwa yao kwa uhuru.

Ndugu Wananchi;
Katika mwaka huu tunaoumaliza leo Umoja wa Mataifa umetupatia heshima nyingine kubwa. Shirika la Afya Duniani limeniteua mimi na Waziri Mkuu wa Canada Mheshimiwa Stephen Harper kuwa Wenyeviti Wenza wa kuongoza Tume ya Kimataifa kuhusu Afya ya Akina Mama na Watoto. Lengo kuu la Tume hiyo ni kuzisaidia nchi zinazoendelea ziweze kutekeleza Malengo ya Milenia kuhusu kupunguza vifo vya akina mama na watoto.

Tume yetu ina kazi ya kupendekeza mfumo wa kutoa taarifa juu ya maendeleo ya afya za akina mama na watoto na kufuatilia utekelezaji wa ahadi za nchi tajiri kuzisaidia nchi masikini kukabiliana na changamoto za afya za akina mama na watoto. Aidha, tunalo jukumu la kupendekeza mfumo wa kufuatilia jinsi fedha zinazotolewa, zinavyotumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Tunatarajia kuanza kazi Januari 2011 na kuwasilisha Ripoti yetu kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kunako Mei 2011.

Michezo
Ndugu Wananchi;
Nafurahi kama tunavyofurahi wote kuwa kwa upande wa michezo, mwaka huu tumeumaliza vizuri. Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, imefanikiwa kushinda Kombe la Challenge kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati baada ya kufanya hivyo mara ya mwisho miaka 16 iliyopita yaani mwaka 1993.

Timu yetu ya Soka ya Wanawake, Twiga Stars, nayo kwa mara ya kwanza, iliweza kufikia fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake.
Hatuna budi kuyatambua na kuyaenzi mafanikio hayo tuliyoyapata. Wakati huo huo tuwatake wanamichezo wetu kuwa na ari ya kufanya vizuri zaidi. Nimetoa changamoto kwa TFF na timu yetu ya taifa kujiwekea lengo la kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2012. Wakiamua hivyo, itabidi waanze sasa kufikiria na kufanya maandalizi ya namna ya kufanikisha lengo hilo.

Napenda kutumia nafasi hii kuwahakikishia wanamichezo wote na Watanzania wenzangu, kuwa nitaendelea kuziunga mkono kwa hali na mali timu zetu zinazoshiriki michezo mbali mbali. Mwaka huu nitakuwa na mazungumzo na viongozi wa riadha ili tuelewane kuhusu namna ya kufufua michezo hiyo ambayo miaka ya nyuma ilililetea taifa letu sifa kubwa.

Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru
Ndugu Wananchi;
Mwaka mpya tunaouanza usiku wa leo una umuhimu wa kipekee katika uhai na historia ya nchi yetu. Tarehe 9 Desemba 2011 nchi yetu itatimiza miaka hamsini ya Uhuru wa Tanzania Bara. Haya si mafanikio madogo hata kidogo. Ni mafanikio makubwa sana ambayo hatuna budi kuyafurahia na kuyasherekea kwa uzito unaostahili.

Katika miaka 50 ya Uhuru wetu tumefanya mambo mengi mazuri ya kujivunia katika nyanja mbalimbali. Tumedumisha uhuru na umoja wa nchi yetu. Kwa hakika hali yetu ilivyo leo kisiasa, kiutamaduni, kiuchumi, kijamii, kiusalama na kimaendeleo kwa jumla, ni tofauti sana na hali ilivyokuwa wakati Tanzania Bara inapata uhuru wake tarehe 9 Desemba, 1961. Natambua pia kwamba katika miaka 50 hii, nchi yetu na watu wake wamekumbana na kukabili changamoto nyingi. Zipo nyingi tulizoziweza na zipo ambazo tunaendelea kuzikabili na tunayo mipango thabiti ya kuhakikisha tunafanikiwa.

Ndugu Wananchi;
Kwa kutambua umuhimu wa aina yake wa maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba, 2011, tumekubaliana na viongozi wenzangu Serikalini kuwa tusherehekee siku hiyo kwa uzito unaostahili.

Ndugu Wananchi;
Tumekubaliana pia, tufanye mambo manne muhimu katika maadhimisho hayo. Kwanza, nautangaza mwaka 2011 kuwa ni Mwaka wa Maadhimisho ya Miaka Hamsini ya Uhuru wa Tanzania Bara. Kilele chake kitakuwa tarehe 9 Desemba, 2011 ambapo kutafanyika sherehe kubwa na za aina yake nchi nzima ambapo wananchi watashirikishwa kwa ukamilifu.

Pili, tufanye tathmini ya kina ya mafanikio tuliyoyapata, katika juhudi zetu za kujiletea maendeleo katika miaka hamsini hii. Kila Wizara, idara na taasisi za Serikali na hata sekta binafsi zifanye tathmini ya eneo lake. Tathmini hizo ziandikwe katika vitabu ili kuhifadhi kumbukumbu hizo muhimu kwetu na kwa vizazi vijavyo. Vitabu na nyaraka hizo vitakuwa kumbukumbu zenye manufaa makubwa kwa wenzetu watakaokuwepo mwaka 2061 wakati wa kusherehekea miaka 100 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Itarahisisha kazi yao ya kufanya tathmini wakati huo.

Tatu, kwamba yafanyike maonyesho maalum katika Uwanja wa Maonyesho wa Julius Nyerere hapa Dar es Salaam na kote mikoani kwenye viwanja vya maonyesho, kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali katika miaka 50 tangu Uhuru wa Tanzania Bara.

Ndugu Wananchi;
Jambo la nne ambalo tulilokubaliana kufanya ni kuanzisha mchakato wa kuitazama upya Katiba ya Nchi yetu kwa lengo la kuihuisha ili hatimaye tuwe na Katiba inayoendana na taifa lenye umri wa nusu karne. Katiba yetu ya sasa tuliyoachiwa na waasisi wa taifa letu, imeifanyia nchi yetu mambo mengi mazuri na kuifikisha Tanzania na Watanzania hapa tulipo. Tunayo nchi moja huru, ya kidemokrasia na inayoendesha mambo yake kwa kuzingatia utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na mgawanyo wa madaraka miongoni mwa mihimili mikuu ya dola. Nchi yenye amani, utulivu na watu wake ni wamoja, wanaopendana na kushirikiana na maendeleo yanazidi kupatikana.

Pamoja na hayo, mwaka 2011, nchi yetu inatimiza miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, miaka 47 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar na miaka 47 ya Muungano wa nchi zetu mbili. Yapo mabadiliko mengi yaliyotokea katika nyanja mbalimbali za maisha ya nchi yetu na watu wake katika kipindi hiki. Kwa ajili hiyo ni vyema kuwa na Katiba inayoendana na mabadiliko na matakwa na hali ya sasa. Katiba ambayo italipeleka taifa letu miaka 50 ijayo kwa salama, amani, umoja na kuwepo maendeleo makubwa zaidi.

Ndugu Wananchi;
Ndiyo maana tukaamua kuanzisha mchakato huu na kwa ajili hiyo, nimeamua kuunda Tume maalum ya Katiba, yaani Constitutional Review Commission. Tume hiyo itakayoongozwa na Mwanasheria aliyebobea, itakuwa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali katika jamii yetu kutoka pande zetu mbili za Muungano. Jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaowashirikisha wananchi wote bila kubagua, vyama vya siasa, wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbalimbali ya watu wa nchi yetu kote nchini, katika kutoa maoni yao juu ya wayatakayo kuhusu Katiba ya nchi yao.

Baada ya kukamilisha kukusanya maoni, Tume itatoa mapendekezo yake yatakayofikishwa kwenye vyombo stahiki vya Kikatiba kwa kufanyiwa maamuzi. Baada ya makubaliano kufikiwa, taifa letu litapata Katiba mpya kwa siku itakayoamuliwa ianze kutumika.

Ndugu Wananchi;
Ni matumaini yangu kuwa mchakato huo utaendeshwa vizuri, kwa amani na utulivu kama ilivyo sifa ya nchi yetu na mazoea yetu ya kujadiliana bila kugombana. Wananchi watapewa fursa ya kutosha ya kutoa maoni yao kwa uhuru na pawepo kuvumiliana kwa hali ya juu pale watu wanapotufautiana kwa mawazo. Pasiwepo kutukanana, kudharauliana, kushutumiana, kubezana, kuzomeana wala kushinikizana. Naomba washiriki waongozwe kwa hoja badala ya jazba. Tukiwa na jazba, hasira na kushinikizana kamwe hatutaweza kutengeneza jambo jema. Na inapohusu Katiba ya Nchi itakuwa hasara tupu. Haitakuwa endelevu na kulazimika kufanyiwa marekebisho mengi mwanzoni tu baada ya kutungwa.

Nawaomba Watanzania wenzangu wenye maoni yao wajiandae kushiriki kwa ukamilifu katika mchakato huu. Katoeni maoni yenu mazuri yatakayowezesha nchi yetu kuwa na Katiba itakayokidhi matakwa yetu ya sasa na ya miaka 50 ijayo.

Hitimisho
Ndugu Wananchi, Watanzania Wenzangu;
Napenda kumalizia salamu zangu za Mwaka mpya kwa kumshukuru tena Mwenyezi Mungu kwa rehema zake alizotujaalia mwaka 2010. Tuendelee kumuomba atujaalie baraka tele katika Mwaka ujao wa 2011: Tumuombe nchi yetu iendelee kuwa ya amani na utulivu, watu wake waendelee kuwa wamoja, wanaopenda na kushirikiana, uchumi wetu uendelee kustawi, tupate mvua za kutosha na neema ziwe tele kila mahali.

Kwa furaha na matumaini makubwa nawatakia heri na fanaka katika mwaka mpya 2011. Namtakia kila mmoja wetu mafanikio mema katika shughuli zake za kujiletea maendeleo na kuendeleza hali yake ya maisha.
Mwisho, kabisa nawaomba tuukaribishe na kuusherehekea Mwaka mpya kwa usalama na amani. Heri ya Mwaka Mpya!! Happy New Year!!

Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Ahsanteni kwa kunisikiliza.

Thursday, December 30, 2010

Tanzia - Bobby Farrell wa Boney M

Bobby Farrell 1949 -2010


REST IN PEACE DEAR BROTHER, Your Music lives on!
"I'm Crazy like a fool! Watch out Daddy Cool!"

Bobby Farrell, frontman of the 1970s pop group Boney M, was found dead in his hotel bed in St. Petersburg on Thursday while on tour in Russia. He was 61.

Farrell was discovered by hotel staff after he failed to respond to a wakeup call. He had given a concert in St. Petersburg on Wednesday evening.

His agent, John Seine, said he had complained of breathing problems, but the cause of death has yet to be determined.

Boney M was put together by German singer and songwriter Frank Farian in 1974, and had a huge following in Europe, including the Soviet Union, in the 1970s.

Farrell, who was more a dancer and showman than a singer, was the male face of the group, which included three other West Indian session singers — Marcia Barrett, Liz Mitchell and Maizie Williams.

Farian had a hit with Baby Do You Wanna Bump? and created Boney M to support the song.

The group went on to have hits such as Daddy Cool, Sunny, By the Rivers of Babylon and a favourite in North America, Rasputin'.

Boney M had 38 top-10 hits, including 15 that hit No. 1 in Germany, where they were then based, including Brown Girl in the Ring and Mary's Boychild.

Farrell was born Alphonso Farrell on Oct. 6, 1949, in Aruba. He left home at 15 as a sailor, then worked as a DJ in Germany before being picked by Farian to front Boney M.

In 1978, Boney M was the first Western music group to perform in the Soviet Union. They sang for an audience of 2,700 Russians in Red Square after being invited by Soviet leader Leonid Brezhnev.

The original group broke up in 1986. Williams is also touring with a group referred to as Boney M.

Farrell had been performing as Bobby Farrell of Boney M with three female backup singers. He continued to perform Boney M hits, and a mixture of calypso and disco songs.

Farrell, who made his home in Amsterdam, had been scheduled to perform a New Year's Eve concert in Rome.

Read more: http://www.cbc.ca/arts/music/story/2010/12/30/bobby-farrell-obit.html#ixzz19bzeEOhu

Wednesday, December 29, 2010

Mwandishi wa Habari Apigwa Kahama

Natoa pole kwa Kaka Ali Lityawi. Hao polisi wanastahili kuadhibiwa. Kutokana na maelezo sioni kama Ali alifanya kosa. Hao polisi wangefurahi kuwa wanapigwa picha wakiwa wanafanya kazi yao kama ilivyotakiwa.

******************************************************

Kahama Police Beat Up Journalist, Seize His Camera
By The guardian reporter
29th December 2010

A group of police officers whose identities and force numbers could not be immediately established last weekend beat up Tanzania Daima newspaper journalist Ali Lityawi, and seized his camera allegedly for taking pictures without permission.

The police said the newsman was 'punished' for taking pictures of a police officer on duty while chasing a prisoner, who had apparently escaped from custody.

The incident took place on Sunday at Lumelezi near Magai hospital, where the journalist, who was on the beat looking for news, found a police officer running after a prisoner.

According to Lityawi, the police officers saw him taking pictures of his colleague, whereupon they attacked him before seizing his camera.

Later, he was taken to the central police station where he was remanded in custody by Kahama Officer Commanding District George Simba on allegation of taking photographs of a police officer and a suspect without a permit.

“The district police chief ordered that the photos in my camera be deleted and ordered his assistants to remove from the camera the smartcard used to store pictures,” he said.

When reached for comment about the incident, Shinyanga regional police commander Diwani Athumani condemned the action by the police officers and ordered repair of the camera, which the journalist claimed was damaged in the fracas.

“It is a police force’s policy to collaborate with journalists to educate the public on public safety and security. If they (police officers) thought the pictures were not good enough, they should have advised the reporter not to use them instead of beating him up and deleting them,” he said.

Saturday, December 25, 2010

Heri ya Krismasi ! Merry Christmas 2010!

Nawatakia wadau wote Krismasi Njema!
Merry Christmas to All!

Wednesday, December 22, 2010

Monday, December 20, 2010

Mr. Tanzania - Christopher Maganga Malecha




Huyu ni Bwana Christopher Maganga Malecha wa Tenki Bovu, Mbezi Beach, Dar es Salaam. Anasema anataka kutangaza Tanzania kwa dunia. Anapenda sana kuvaa nguo za Khanga amabazo anashona mwenyewe. Asili yake ni MNyamwezi kutoka Tabora. Anapatikana sehemu za Chai Bora njia ya kwenda Goba.

KUMBUKUMBU ZA REMMY ONGALA


Pichani : Marehemu Remmy Ongala (1947-2010)


KUMBUKUMBU ZA REMMY ONGALA

Na Freddy Macha

Miaka yake ya mwisho ya Remmy Ongala alikuwa Mlokole, tuseme akimsifu Yesu Kikristo. Kutokana na hali hiyo huenda baadhi ya vijana waliozaliwa karibuni wakashindwa kumjua vizuri. Mbali na kubadili dini marehemu alikata nywele zake ndefu na kuacha kuimba nyimbo maarufu tulizozoea mathalan Siku ya Kufa, Nalilia Mwana, Samaki na Mambo Kwa Soksi.

Mwaka 1997 televisheni ya Channel Four, Uingereza ilitoa kipindi (documentary) kilichotayarishwa na Mswidi, Jan Roed, kuhusu Remmy Ongala. Picha na mahojiano zilimwonyesha jijini Dar es Salaam, akifanya shoo zake sehemu kadhaa, akiongea na wananchi, vile vile akielezea dini yake asilia, Kibatala.

Nilifurahishwa sana na maelezo yake Mwanamuziki Ramazani Mtoro Ongala kuhusu imani zetu za jadi kabla ya kuja Wazungu. Leo ni wasanii au viongozi wachache sana bara Afrika wanaothubutu kusema hadharani Uislamu na Ukristo vililetwa na wageni. Mwanamuziki mwingine ni Fela Kuti wa Nigeria aliyekuwa akitambika na kusali kupitia imani za kabila lake la Kiyoruba. Fela Kuti alifariki mwaka 1997 ( kwa UKIMWI) pasina kugeuza imani zake za kijadi; kama alivyofanya marehemu Ongala.

Kimaudhui Waafrika hawa wawili mashuhuri wanatukumbusha kwamba iko haja ya kujichunguza zaidi tunatoka wapi, sisi ni nani na tunakwenda wapi, kiutamaduni.

Nilikuwa na mazoea ya karibu na mwanamuziki Remmy ambaye jina lake Ramazani lina maana “mizimu iko nami” toka nikiwa mwandishi wa habari Uhuru (1976-78). Wakati huo alipiga na bendi ya Mzee Makassy iliyokuwa ikiwika Afrika Mashariki nzima.

Remmy alianza kuitwa Dokta na waandishi wa habari wa Uhuru kutokana na alivyokuwa akivaa kama mchawi. Aliitwa pia mvuta bangi, kichaa hata muhuni. Mwaka 1983 nilianza kumwandika na kumhoji nikiwa na safu yangu ya Utamaduni (Cultural Images) gazeti la Sunday News, baada ya kuchoshwa na dharau kwa msanii huyu aliyekuwa akifungua uwanja mpya wa muziki Tanzania. Mathalan alioanisha muziki wa jadi na wa kisasa (pop) akishirikiana na wacheza ngoma wa Muungano wakiongozwa na Norbert Chenga, manju aliyecheza ngoma ya nyoka na Bugobogobo ya Kisukuma.

Ushirikiano huu ulifikia kilele wakati Remmy alipoanza kuunganisha ngoma maarufu ya “Mdundiko” (ya wenyeji asilia wa Dar es Salaam) na ile Sokous aliyoiimba kwa Kilingala, Kifaransa na Kiswahili. Nilitoa kitabu kuhusu maisha yake kilichochapishwa nikishirikiana na marehemu Stanley Mhando, mwaka 1985.

Kitabu cha Remmy kilifuatiliwa na msururu wa vitabu vingine kimojawapo cha hayati Ben Mtobwa aliyemlinganisha na Bob Marley.

Mwaka 1988 kuna Mzungu (Simon) aliyeituma kanda yake (Nalilia Mwana) kwa kampuni ya “Real World” iliyosajili na kuanza kutoa albam zake Uingereza. Awali Dk Remmy (kama wanamuziki wengine) alitolewa tu Redio Tanzania; hapakuwa na runinga au studio kama leo.

Kati ya 1988 hadi 1998 Remmy aliwaka dunia nzima. Alizunguka na Super Matimila akiimba nyimbo zilizoangalia maisha ya walala hoi, wasifu wa Mwalimu Nyerere (kwa kuondoa ukabila Tanzania) na kuchangia vita dhidi ya Ukimwi (“Mambo kwa Soksi”).

Mara kwa mara niliongea, nikamhoji na kumhoji Remmy alipokuja Uingereza.

Mara ya mwisho alipofanya shoo yake London mwisho wa mwaka wa 1996 katika klabu ya Mean Fiddler alinidokeza anao ugonjwa wa kisukari na kwamba waganga wamemweleza apunguze unene, aache pombe na sigara.

Tulizungumzia pia kuandika kitabu chake kipya katika lugha ya Kiingereza. Mara ya mwisho kuongea naye ilikuwa Oktoba 1997 nyumbani kwake. Wanawe niliowaacha wakiwa wadogo ( Kali, Jessica, Aziza) na Shema (aliyezaliwa karibuni) sasa walikuwa vijana wakakamavu. Mkewe Toni bado aliishi Bongo, akisema Kiswahili fasaha. Na nyumbani kwake palikuwa sasa “Kwa Remmy”, kituo cha basi.

Kifupi alinipa taswira ya mtu aliyeshajijenga; aliyechangia muziki wetu na kutukuza utamaduni wa Bongo ingawa hakuzaliwa hapa. Miaka yote alinisisitizia kuwa yeye ni Mwafrika na kwamba popote alipoishi au kutembea barani palikuwa nyumbani kwake. Mungu ailaze roho yake pema peponi, Amina.

http://www.freddymacha.com/

Sunday, December 19, 2010

WikiLeaks na Tanzania

DUH!

Kutoka:

http://www.guardian.co.uk/world/2010/dec/19/wikileaks-cables-tanzania-bae-fears

******************************************************************

WikiLeaks cables: Tanzania official investigating BAE 'fears for his life'

Prosecutor Edward Hoseah voiced safety fears over inquiry into 'dirty deal' involving sale of radar system to government

Sunday 19 December 2010 21.30 GMT

    President Jakaya Kikwete, pictured with George Bush in 2008

    President Jakaya Kikwete, pictured with George Bush in 2008, had his commitment to fighting corruption questioned, according to the cables. Photograph: Jim Watson/AFP/Getty Images

    The Tanzanian prosecutor investigating worldwide misconduct by BAE, Britain's biggest arms company, confided to US diplomats that "his life may be in danger" and senior politicians in his small African country were "untouchable".

    A leaked account of what the head of Tanzania's anti-corruption bureau, Edward Hoseah, termed the "dirty deal" by BAE to sell Tanzania an overpriced radar system, is revealed in the US embassy cables.

    BAE is to appear in court in London tomorrow, when their system of making secret payments to secure arms contracts, exposed by the Guardian, will be officially detailed for the first time.

    Every individual involved in the BAE scandal in Britain and Tanzania has escaped prosecution.

    But the arms giant agreed with the UK Serious Fraud Office (SFO) to pay £30m in corporate reparations and fines, provided the word "corruption" did not appear on the indictment. A corruption conviction would debar the company from EU contracts.

    The former overseas development secretary, Clare Short, said at the time: "It was always obvious that this useless project was corrupt."

    Hoseah met a US diplomat, Purnell Delly, in Dar es Salaam in July 2007, and claimed (unrealistically it turned out) he would be able to prosecute guilty individuals in the BAE case. The US cable reports: "He called the deal 'dirty' and said it involved officials from the Ministry of Defence and at least one or two senior level military officers."

    Hoseah spoke gloomily about the prospects for Tanzania's anti-corruption struggle and his original hopes to prosecute the "big fish" of corruption.

    "He told us point blank ... that cases against the prime minister or the president were off the table ..." The cable then details allegations against former leaders and their inner circles, saying they would be "untouchable".

    "He noted that President Kikwete does not appear comfortable letting the law handle corruption cases which might implicate top-level officials." The cable then says Kwitke "does not want to set a precedent" by going after any of his predecessors.

    There were "widespread rumours of corruption within the Bank of Tanzania", Hoseah said, and the island region of Zanzibar was also "rife with corruption".

    The diplomat noted: "Hoseah reiterated concern for his personal security ... saying he believed his life may be in danger ... He had received threatening text messages and letters and was reminded every day that he was fighting the 'rich and powerful'."

    He might have to flee the country. He warned: "He said quietly: 'If you attend meetings of the inner-circle, people want you to feel as if they have put you there. If they see that you are uncompromising, there is a risk.' "

    The US embassy noted in a "cynical" aside, that probably the only reason Hoseah felt obliged to attempt a BAE prosecution was because the SFO had presented him with "a fully developed case file, brimming with detailed evidence".

    Today's court appearance by BAE is the culmination of lengthy attempts to bring the company to justice since the Guardian exposed its worldwide secret payment system.

    The prime minister at the time, Tony Blair, intervened in 2006 to halt an SFO investigation into payments to members of the Saudi royal family.

    The US department of justice has had more success than the SFO, forcing BAE to pay $400m (£260m) in penalties under the US Foreign Corrupt Practices Act.

    £28m radar deal 'stank'

    Tanzania, on Africa's east coast, is one of the poorest states in the world, formerly controlled in turn by Arab slavers, German colonists and the British.

    At the time of the radar deal, life expectancy was 45.

    Tanzania was forced to apply for debt relief from the west and was heavily dependent on aid. It is ravaged by HIV/Aids and its GDP per head is just $723 (£465).

    President Benjamin Mkapa, whose regime did the deal, was succeeded in 2004 by his political colleague Jakaya Kikwete.

    Tanzania, which has no air force, bought the military air defence radar from BAE in 2001 for £28m.

    It was claimed the Commander system, which was portable and festooned with anti-jamming devices, could also be used for civilian air traffic control.

    The country borrowed the cost from Barclays, adding to its debt burden. Both the World Bank and the International Civil Aviation Organisation called the purchase unnecessary and overpriced.

    In London, the then development secretary, Clare Short, temporarily blocked aid payments in protest. "It stank," she now says of the sale.

    She urged an export licence be withheld, but was overruled by Tony Blair himself. Robin Cook, then foreign secretary, recorded bitterly in his diary that Dick Evans [of BAE] seemed to have "the key to the garden door of No 10 [Downing St]".

    In January 2007 the Guardian disclosed that BAE had used an offshore front company, Red Diamond, to secretly pay £8.4m, 30% of the radar's ostensible price, into a Swiss account.

    The account was controlled by Tanzanian middleman Sailesh Vithlani. His "consultancy" agreement was, it is alleged, formally signed off in London by Evans.

Msiba California - Juliana Senya

Ndugu Wana-Jumuiya,
-
I am very sad to inform you that our beloved sister Juliana Senya past away last night at UCLA Harbor Medical Center. The family of the late Juliana Senya have requested us to transport her body to Tanzania. Currently the total cost of transporting the deceased to Tanzania is estimated at:
· $ 6,700.00 Transportation to Tanzania, this is high due to the holiday season
· $ 2,100.00 Casket
· $ 4,112.95 Funeral Home Services
---------------
$12912.95 Total
-
This Saturday December 18, 2010 at 6 pm we will have an emergency meeting to plan and raise funds to cover the costs of transporting our beloved sister to Tanzania, please come to extend your sympathy and support at the following address location:
14006 Doty Avenue Apt# 17
Hawthorne, CA 90250
-
Dada Juliana Senya had the love of her life who is our brother Ndugu George Mutafungwa, please make every effort to call and encourage him during this difficult time. You can reach him at (323)984-0617 cell or georgemutafungwa@yahoo.com email.
-
For those who won’t be able to make it this Saturday, please make every effort to extend your financial contribution (rambirambi) so that we can honor the request of her family to transport the body of our beloved sister to Tanzania. The details below are for the newly opened account to facilitate all contributions toward transporting the body of our beloved sister to Tanzania...
-
Bank Name: Bank of America
Name on Account: Khalipha Majid
Account Number: 2153171397
Routing Number: 122000661
NOTE: This account will be closed as soon as the body of Juliana Senya is transported to Tanzania, we will also provide the financial reporting at that time.
-
Our support is needed during this difficult time, please pray for the family of the late Juliana Senya and all those all those who are emotionally attached to her passing away.
-
For any additional information please feel free to contact:
· Khalipha Majid, Treasure of the Tanzanian Community in Southern California at khaliphaa@yahoo.com email or (213)841-1994 cell
· Iddy Mtango, Chairman of the Tanzanian Community in Southern California at iddymtango@yahoo.com email or (323)496-4920 cell
-
May God rest the soul of our beloved sister in peace, Amina.
-
Mwenzenu,
Iddy Mtango

Friday, December 17, 2010

Muhimbili Moments

Baba akisoma nakala ya Daily News. Nilikuwa Cover story kwenye Woman section.
Baba akipelekwa Theatre kwa ajili ya Upasuaji.

Njia panda kwenda Block za Sewa Haji na Kibasila


Wagonjwa wakisubiri kuingia Muhimbili Orthopedic Institute

Father Fidelis wa R. C. akipita kusalimia wagonjwa


Roundabout

Magoroja yanjengwa Upanga!


Mafuriko Jangwani - View from Mwaisela Block


Kaka Michuzi na Mke wake nao walipita kutoa salamu za pole kwa Baba.

Mwaisela Block Muhimbili

Mwaisela Block Mwaisela Annex

Ward Number 8 Upande unaotazamana na Orthopedic Institute


Wheelchair Mbovu Ward 8, Watu wanaitumia kukalia tu

Mimi Mwaisela Ward 8

Kunguru

Mwaisela Annex


Mwaisela Ward 8 Emergency Exit


Mwaisela Ward 8 Emergency Exit -lakini mbona hutaweza kupita ikitokea kasheshe?

Panya aliyekamatwa Mwaisela Ward 8 na Mgonjwa

Mdudu aina ya Preying Mantis

Mwaisela Ward 8 upande uinaotazamana na Jangwani

Muhimbili Garden

Pale Garden Muhimbili unaweza kupata vinywaji kama chai, soda, juisi bia. Pia kuna chakula kizuri tu. Asubuhi unaweza kupata supu, maandazi, sambusa, egg chop, mayai etc. Mchana, pilau, wali, ndizi, etc. Bei siyo mbaya. Watu wanamimiminika pale kule. Unaweza kupata phone card pia.



Mwembe Mkubwa Pale Garden
Huo Mwembe una miaka mingapi?
Pilau Nyama Bei 1500/-, Juisi 500/-

Tido Mhando Atemwa TBC

DUH! Mbona watu walisema alifanya kazi nzuri sana pale TBC. Hii habari ya kutisha!


17 December 2010

Tido Mhando atemwa TBC

Sadick Mtulya na Patricia Kimelemeta

BAADA ya kufanya kazi nzuri ya kuboresha matangazo na uendeshaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), serikali imeamua kuachana na mkurugenzi wa chombo hicho, Tido Mhando baada ya mkataba wake kuisha, lakini mtangazaji huyo maarufu ameielezea uamuzi huo kuwa kuwa ni wa utata.

Kuenguliwa kwake kumefanyika takriban miezi miwili baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambao TBC iliripoti kwa kina na bila kupendelea chama chochote na hivyo kujivunia sifa kemkem kutoka kwa watazamaji wa TBC1 na wasikilizaji wa redio hiyo ya umma.

“Hatua hii imenishtua kidogo na hata hivi ninapoongea na wewe wafanyakazi wengi wamepata mshtuko na wengine wanalia," alisema Tido alipoongea na Mwananchi jana. "Ni juzi (Jumatatu) ndio niliandikiwa barua na serikali ya kutakiwa kuondoka.... ilikuwa kinyume kabisa na uratatibu wa serikali.

“Barua ya kutakiwa kuondoka niliipata mara baada ya kukutana na kuzungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Vijana , Seti Kamwanda.’’

Tido, ambaye kabla ya kujiunga na TBC alikuwa mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Habari la Uingereza (BBC), alisema kwa mujibu wa taratibu mfanyakazi anayemaliza mkataba wake anatakiwa kujulishwa suala hilo miezi sita kabla.

"Kimsingi (barua) hukumbusha kwamba mkataba unamalizika na kama serikali inakusudia kuuendeleza au la. Sasa hilo halikufanyika kwangu," alisema.

Kwa mujibu wa Tido, hatua hiyo inaweza kutafsiriwa tofauti na wananchi hasa ikizingatiwa kwamba imefikiwa miezi miwili tu tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

Wafanyakazi walipata taarifa ya kuondolewa kwa Mhando jana baada ya mkurugenzi huyo kubandika tangazo la kuwataarifu kuwa anaondoka na kwamba ametakiwa akabidhi ofisi kwa Joe Rugabaramu.

"Tangazo linasema kuwa amefanya kazi na sisi kwa miaka minne na sasa mktaba wake umeisha na kwamba ametakiwa akabidhi ofisi kwa Rugarabamu," alisema mmoja wa wafanyakazi wa TBC.
"Baadaye alitushukuru kwa ushirikiano wetu kazini na akatuambia tusubiri hadi hapo mkurugenzi mpya atakapotangazwa."

Mfanyakazi mwingine alisema kuwa walitarajia kuwa Mhando angetimuliwa mapema kabla ya uchaguzi kwa kuwa wanadai kuja kwake nchini kulitokana na uhusiano wake na kigogo mmoja wa CCM ambaye kwa sasa hayuko madarakani.

"Angetimuliwa hata kabla ya Desemba 15, lakini ikaonekana kuwa isingekuwa sahihi," alisema mfanyakazi huyo ambaye alieleza kuwa Mhando aliwasiliana pia kwa simu na mfanyakazi mmoja mmoja kumuelezea uamuzi huo wa serikali.

Habari za Tido kuondoka TBC zilianza kuvuma wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wakati iliposemekana kuwa alikuwa akipigana vijembe vya chinichini na vigogo wa CCM kutokana na vyombo hivyo vya umma kutangaza habari bila ya upendeleo.

Baadhi ya mambo yaliyoibua hisia kuwa mtendaji huyo wa shirika la umma angeondolewa ni msimamo wake wa kuendelea kurusha hewani kipindi cha "Jimbo kwa Jimbo" ambacho kilikutanisha wagombea ubunge wa vyama mbalimbali vya siasa kwenye mdahalo kuhusu maendeleo ya eneo lao.

Kipindi hicho kilichorushwa kwa wakati mmoja na vituo vya televisheni na redio kilianza kwa kushirikisha wagombea wote wa ubunge kwenye jimbo, lakini katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akaandika waraka wa kuzuia wagombea wa CCM kushiriki kwenye mdahalo huo akidai kuwa chama hicho tawala kina njia zake za kufanya kampeni.

Pamoja na CCM kujitoa, TBC iliendelea kurusha vipindi hivyo hadi kumalizika kwa uchaguzi ambao uliisha kwa CCM kupoteza viti vingi Tanzania Bara, ikiwa ni mara ya kwanza tangu serikali iruhusu mfumo wa vyama vingi.

"Ilikuwa aondoke kabla kampeni hazijaanza ingawa mkataba wake ulikuwa umalizike Desemba 15. Lakini serikali ilikuwa inarekebisha mambo yake na kumtafuta mtu anayeweza kurithi nafasi yake," chanzo cha habari cha ndani serikalini kilidokeza.

Chanzo kingine alisema: "Kuna watu wanaajiriwa pale TBC ambao malipo yao yanayotokana na Saccos ya shirika hilo, kitu ambacho ni kinyume na taratibu za serikali zinazotaka mwajiriwa alipwe na Hazina."
Jitihada za gazeti hili kumpata katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Seti Kamhanda hazikuzaa matunda.

Alipoulizwa endapo atakubali kurejee kwenye wadhifa huo ikitokea serikali ikamwita tena, Mhando alijibu: "Nitalazimika kuchukua muda zaidi kutafakari hilo kwa kina.

“Nitafanya maamuzi ya kazi ya kufanya kulingana na wakati utakavyokuwa, lakini itanichukua muda kidogo kutafakari hilo kwa kuwa nimefanya kazi mfululizo.’

Kuhusu utendaji wa shirika hilo, Tido alisema amefarijika kwa kiasi kikubwa na mafanikio ya kiutendaji yaliyofikiwa.
“Nilikuwa na mipango mikakati mingi ya kuendeleza shirika hili hususani kulifanya lijiendeshe kwa kujitegemea bila ya kuhitaji ruzuku serikalini," alisema na kuendelea:

“Lakini nimefarijika vya kutosha na utendaji wangu na mafanikio yaliyofikiwa na TBC hadi wananchi kukiamini chombo hiki na ‘reaction’ imekuwa nzuri kutoka kwao na kwa vyama vya siasa.’’

Mbali na kurusha taarifa za kampeni katika njia iliyoonekana kuwa si ya upendeleo hata kwa chama tawala, TBC ilifanikiwa sana katika urushaji wa moja kwa moja wa matangazo ya mechi za mpira wa miguu na matukio makubwa ya kisiasa na kijamii.

Mechi za michuano mbalimbali ya kimataifa na ya ndani, urushaji wa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge, urushaji wa moja kwa moja wa matukio makubwa na staili ya utangazaji ulilifanya shirika hilo kuwa na mvuto mpya na hivyo kuweza kupambana na vituo vingine vya redio na televisheni vya kampuni binafsi.

Wednesday, December 15, 2010

Rest in Peace Dr. Remmy Ongalla

Baadhi ya walombolezaji nje ya nyumba ya Dr. Remmy Sinza
Mama Yangu mzazi Rita Che-Mponda akimpa pole Mama Ongalla

Kali Ongalla akicheza na kasuku wao

Mjane wa Dr. Remmy, Toni Ongalla, wanae Tom na Kali masaa machache kabla Dr. Remmy kufariki dunia.


Wadau, siku ya jumapili 12/12/10, nilialikwa nyumbani kwa Dr. Remmy na mke wake Toni. Tunafahamiana na famila ya Ongalla tangu mwaka 1978. Hivi karibuni walikuwa wamehamia kwa muda nyumba huko maeneo ya Africana kwa vile nyumba ya Sinza inakarabatiwa.

Basi, nilifika huko kwenye saa 7 na nusu. Toni alinipeleka chumabni kumsalimia Dr. Remmy. Dr. Remmy alikuwa amelala kwenye kitanda na mwanae Tom. Mke wake alisema, "Chemi amekuja kukusalimia, unamkumbuka Chemi?"

Dr. Remmy aliwaambia anataka kwenda sebuleni kukaa. Walivyotoka kwenda kumchukua kiti cha kumsukuma kwenda huko (walikuwa wanatumia viwili vya palstiki kwa vile hawakuwa na wheelchair, Dr. Remmy aliinuka mwenyewe kitandani na nguvu zake. Alikaa akanitazama sana, ila hakusema kitu. Nilimwambia pole kwa kuumwa lakini atapata nafuu. Walileta kiti halafu walimpeleka sebuleni kwenye meza ya kulia chakula.

Chakula kililetwa na nilikula na familia huko natazamana na Dr. Remmy. Mara kadhaa alishika mke wake mkono kama vile anamwambia asiwe na wasiwasi mambo yote yatakuwa sawa. Dr. Remmy hakuweza kula lakini alikunywa soda kidogo na supu. Wanae Kali na Tom walimsihi baba yao ale chakula ili apate nguvu. Baada ya muda aliomba arudishwe chumbani, wanae walimpeleka.

Mimi na Toni tuliongea sana maana Dr. Remmy alikuwa na matatizo ya mafigo na marehemu mume wangu Rev. Whitlow alifariki kutokana na maradhi ya figo. Toni alisema kuwa Dr. Remmy alipata Stroke (kiharusi) tangu mwaka 2000. Toni aliniuliza kama ingekuwa vizuri awaite wanae walio nje kuja kumwona baba yao. Nikamshauri awaiite mara moja, maana niliona hali ya Dr. Remmy ilikuwa ya kutisha, lakini sikutegemea kama angefariki siku ile. Alikuwa bado ana mwili. Tuliaagana na familia ya Ongalla, halafu nilienda zangu.

Kesho yake nilitoka Muhimbili baba yangu alikolazwa kwenye saa nne na nusu kwenda kupanda daladala kwenda Kariakoo kwenye stendi pale Muhimbili. Nikiwa nimekaa kwenye basi walitangaza kwwenye redio kuwa Dr. Remmy amefariki dunia. Nilianza kupiga mayowe na kushgangaa kuwa mtu niliyemwona akiwa haia masaa machache kabla alikuwa amefariki. Si watu walinizunguka kusikia kuhusu ile last supper na Dr. Remmy.
Sikumpiga picha maana ningependa ktumukumbuke kama alivyokuwa. Mungu awape familia nguvu katika kipindi hiki kigumu.
REST IN PEACE DR. REMMY!

Zilipendwa Dr. Remmy Ongalla - Siku ya Kifo




REST IN ETERNAL PEACE DR. REMMY

Mifugo Wodini Mwaisela



Wadau, nilikuwa pale Mwaisela Ward namba 8, majuzi ghafla nikasikia watu wanapiga kelele kwenye wodi ya vitanda vitano (viko vitanda tisa). Halafu nikasikia wagonjwa wakisema kuwa kuna mifugo wodini. Kumbe walimwua panya!
Watu walienda kuangalia ni nini? Mgonjwa huyo alisema aliwua kwa kumpiga na kiatu. Manesi walisema kweli panaya wapo wanapanda kwenye mabomba ya vyoo.

Pichani ni mgonjwa aliyemwua huyo panya akienda kumtupa kwenye takataka za Biohazard.

Nimerudi Boston

Mashine ya Fluoroscopy juzi kabla haijatengenezwa na fundi.

Mimi na baba jana nyumbani mara kabla ya mimi kuondoka kurudi Boston.


Wadau, nimerejea Boston kutoka Dar leo.

Baba alifanyiwa X-ray aliyohitaji baada ya mashine ile ya Fluoroscopy kupona. Alikuwa discharged juzi, lakini tulimrudisha Muhimbili jana kwa ajili ya hiyo X-ray. Yuko nyumbani Tenki Bovu sasa anaendelea vizuri. Hiyo X-ray tulilipa 80,000/- wiki tatu zilizopita lakini ndo alipata jana. Nilikuwa nimeanza mpango wa kumpeleka private kwa ajili ya hiyo x-ray lakini nilipigiwa simu kuwa mashine imepona na angeweza kufanyiwa. Ingawa ilifanya kazi jana huenda mashine hiyo imekwishaharibika tena. Niliambiwa ilishawahi kufa kwa miezi mitatu! Sasa wale wagonjwa wasio na uwezo wa kwenda private walifanya nini?
Wanaofanya kazi pale wako frustrated kwa vile wanshindwa kufanya kazi yao vizuri kutokana na mashine mbovu. Ilivyoharibika, wafanayakazi waliondoka kwa vile hawakuwa na kazi ya kufanya. Ilikuwa kila nikienda kucheki kama mashine imepona, hakuna mtu! Wana frustration ya hali ya juu.

Kwa kweli lazima niseme huduma Muhimbili ilikuwa nzuri kwa ujumla. Siyo Best lakini nzuri, tofauti na miaka ya nyuma. Baba alikuwa Semi private Ward huko Mwaisela.

Ila jamani tulikuwa tunafika pale Muhimbili kila siku saa 12 asubuhi, halafu unasikia vilio, mtu kaja kamkuta mgonjwa wake ameaga dunia usiku.
Picha tele za Muhimbili zinakuja. Safari hii sijaweza kwenda popote maana kila siku ilikuwa safari ya hospitali.

Friday, December 10, 2010

Muhimbili Wanahitaji Fluoroscopy X-Ray Machine

Ofisi ya X-Ray Fluoroscopy huko Muhimbili National Hospital

Wadau, nimehangaika na baba yangu hapa Muhimbili siku kadhaa sasa ili afanyiwe Cystourethrography. Bado hajafanyikiwa, mashine inaharibika kila saa. Kuna backlog ya wagonjwa wanaohitaji kufayiwa x-ray na hiyo mashine lakini haijawezekana.

Jana ilikuwa sikukuu hivyo walikuwa wamefunga. Ile juzi tulimtoa baba wodini Mwaisela na kumpeleka kwenye X-ray. Kakaa masaa kadhaa ndo wakasema mashine imeharibika na fundi anitengeneza.

Alitokea Acting Head wa Idara, Dr. Flora Lwakatare, alisema kuwa wana mashine mbili za fluoroscopy. Moja ndo mbovu kabisa na nyingine ndo hiyo inayoleta matatizo mara kwa mara. Alisema wametarifu Waziri kuhusu tatizo lao lakini bado hawajapata mashine mpya.

Haya leo, tumemtoa baba wodini kumpeleka huko kwenye x-ray. Mashine ikaleta matatizo. hivi sasa wanasema fundi anakuja kutengeneza. Isipowekezekana leo basi mapaka juamatatu. Tunaomba mungu kuwa watafanikwa kutengeneza mshine na itaweza kufanya kazi.

Na si zaidi ya saa moja iliyopita, babu ambaye alitolewa wodi nyingine kwa ajili ya vipimo alizimia (fainting) na kuanguka hadi kwenye sakafu! Nesi aliyemsindikiza baba yangu kamhudumia yule mzee mara moja. Wamerudisha wodini. Inasikitisha kweli kuona wagonjwa wamelundikana pale x-ray.

Kwa kweli huduma hapa Muhimbili umekuwa mzuri, ila ndo tumekwama kwenye hiyo x-ray. Je, serikali inampano wa kuleta mashine hiyo, maana wagonjwa wanateseka.

Sunday, December 05, 2010

JERUSALEM - Shairi

JERUSALEM

Imejengwa kinadhifu, waislamu tujivunie
Mji huu mtukufu, Illaahi tubarikie
Amani ni fursa adhim, jerusalem tuililie

Wakati umewadia, jerusalem itun'garie
Rehma kutufikia, na mema tujifanyie
Tuwache yenye udhia, umoja tujivunie
Amani ni fursa, adhim jerusalem tuililie

Masjid al-aqsa, ziara tujifanyie
Mola ameitakasa, Wajibu tujivunie
Al-quds ya sasa, twende tukajionee
Amani ni fursa, adhim jerusalem tuililie

Kwenye Kisa cha miraj, sote tukifatilie
Ardhi na mbigu siraj, Alipita Rasulie
Baada ya ile hajj, Jerusalem tukatembee
Amani ni fursa adhim, jerusalem tuililie

Tawhid na imani, sote tujihimizie
Kamba yaa ikhwan, wajib tushikilie
Hii itajenga imani, umoja itupatie
Amani ni fursa adhim, jerusalem tuililie

Jamii palestina, ya rabi wajaalie
Subra nayo neema, dhambi uwaghufurie
Uwapatie Rehma, amani uwatandie
Amani fursa adhim, jerusalem tuililie

Shairi si fani yangu, wajibu munikosoe
Hili ni la kwanza langu, hivyo munisaidie
Nakiri makosa yangu, ya illahi nighurufie
Amani ni fursa adhim, jerusalem tuililie

Imetungwa na:

Dr. Amur Abdullah Amur

Safarini Tanzania

Hi Wadau Wapendwa,

Niko Dar es Salaam, Tanzania. Nilifunga safari haraka haraka kuja. Baba yangu mzazi, Dr. Aleck Che-Mponda amelazwa Muhimbili, Mwaisela Room 309. Yuko pale zaidi ya wiki mbili sasa akisumbuliwa na maradhi kadhaa ikiwemo Prostate.

Dar ni joto sana sasa hivi. Pia kuna vumbi sana hasa sehemu ambazo hakuna barabara ya lami. Foleni kwenda mjini and kurudi ni balaa.

Mengine baadaye.