Monday, June 30, 2008

Kusogoa Chooni - Marudio


Niliposti kwa mara ya kwanza- August 23, 2006

Jamani Marekani watu maofisini wananishangaza sana. Kuna mtindo wa watu kusogoa na kupiga gumzo chooni. Tena kwa muda mrefu. Yaani mtu anajisaidia, huko mwenzake yuko nje anamsemesha. Au unaingia chooni na kukuta watu wamepiga kambi kwenye masinki ya kunawia mikono na kupiga soga, huko watu wanajisadia kwenye stalls. Wanasikia mtu anakojoa, au anadonssha haja kubwa, hao wanaongea bila kujali.

Kwa kweli nashangaa sana. Labda mtu akiwa anajisaidia haja kubwa ndo wakimbie kwa ajili ya mishuzi.Kwa kweli Restrooms/Bathrooms za Marekani maofisini ni safi sana, yaani unakuta toilet bowl cheupe kama vile bado kipya. Zinasafishwa mara kwa mara kwa siku. Nakumbuka Mbongo fulani aliwahi kusema vyoo vingine visafi mpaka unaweza kula huko, (mhhh sijui, mimi siwezi kula huko)! Usafi chooni ni muhimu sana hapa, na hao wanaosafisha wakizembea wanashutukia kazi hawana wanaletwa wengine. Lakini bado sijaona kama chooni ni sehemu ya kupiga gumzo.

Unaingia kwenye stall (kichumba chenye choo), mwenzako yuko nje kaona unaingia anaanza kupiga mastori. Aisei umesikia, hivi na hivi, je, unaonaje hivi na vile. Kwa kweli naona mkojo unataka kwa shida huko unajisaidia, huko unajaribu kuongea.

Lakini kuna kitu niligundua. Kisheria Marekani, mwajiri anarushisiwa kuweka recording devices kila mahala ofisini na Mfanyakazi asijue. Wanaweza kuwa na makamera na ma-audio device na usijue. Ila ni mwiko kuweka hizo devices chooni! Je, ni sababu ya watu kupiga gumzo chooni kwa vile wanajua

hawawezi kunaswa kwa ajili ya kupoteza muda kazini.

Mnaonaje kuhusu suala hii?

Wanenguaji wa Kenya

Picha kwa hisani ya Kazungu Samuel

Wasichana wa Kikenya wanavyozuga jukwaani huko Mombasa.

Tamasha la Kukata na Shoka Pwani nchini KenyaPicha kwa hisani ya mdau, Kazungu Samuel.
Dada Chemi, hivi ndivyo ilivyokuwa katika ukumbi wa Jomo Kenyatta Public Beach viungani mwa jiji la Mombasa wakati wakazi wa pwani walipojitokeza katika tamasha la Family Fun Show ambalo liliandaliwa na stesheni ya Pwani FC pamoja na kampuni ya Kaluworks. Kwa kweli ufuo ulifurika kama unavyoona katika picha hizi. Weka kwa blog wabongo wajue kuwa hata Kenya jamaa hupenda kujirusha.
Kazungu Samuel(Mhimili)

Sunday, June 29, 2008

Humshindi huyo ndege kwa kucheza Ngoma!

Asante Da Subi kwa kuniletea hii kideo.

Cheki ndege anavyocheza kwa 'rhythm' kabisa! Lazima katoka Afrika huyo.

Saturday, June 28, 2008

Makengeza


ANGALIA HII PICHA KWA MAKINI KAMA HUIONI VIZURI UJUWE UNA MAKENGEZA!!!!!!!!
Asante mdau Masoud kwa kuniletea hii picha.

Miss Zimbabwe 2008

Miss Zimbabwe 2008
Asante mdau Masoud kwa kuniletea hii picha.

Friday, June 27, 2008

Picha ya Rais Kikwete

Kassim Mpenda akionyesha picha ya zamani (kulia) na ya sasa (kushoto)

Kutoka Ippmedia.com

Picha ya Rais yabadilishwa 2008-06-27

Na Lucy Lyatuu

Serikali imebadilisha picha rasmi ya Rais Jakaya Kikwete kutokana na kubainishwa kuwa kwa kiwango kikubwa inaonyesha dalili za msongo wa mawazo ya kampeni za uchaguzi mkuu 2005.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Bw. Kassim Mpenda alitoa taarifa hiyo jana jijini Dar es Salaam. Alisema uamuzi wa kubadili picha hiyo umefikiwa kufuatia ushauri wa wataalam kwamba picha ya sasa haifai kuendelea kutumika kwa sababu hizo.

Alisema picha inayotumika hivi sasa ilipigwa baada ya Tume ya Taifa ya uchaguzi kumtangaza Rais Kikwete mshindi wa uchaguzi huo. Aliongeza kuwa makatibu wakuu na maofisa wafawidhi wengine wote wa ofisi za serikali kuu, serikali za mitaa, wakala na asasi nyingine zote za serikali wameshauriwa kuanza kutumia picha mpya ya Rais.

``Kila nakala ya picha hiyo itauzwa sh. 15,000 na zitapatikana mwanzoni mwa Julai katika Idara ya Habari. Wakati huo huo, serikali kupitia wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, imekamilisha uchapishaji wa bango la baraza jipya la mawaziri. Alisema nakala zake haziuzwi zinatolewa bure na ofisi ya Idara ya Habari (MAELEZO) kuanzia jana.

SOURCE: Nipashe

Kumbukumbu - Amina Chifupa


Wadau, ni mwaka moja tangu Mbunge maarufu na chipukizi, Amina Chifupa, atutoke. Sitasahau nilivyopata habari za kifo chake kutoka kwa kaka Michuzi.

Kaka Fadhili amatunga shairi safi ya kumkumbuka.

*********************************************************************************

Bado Tunakukumbuka

Mwaka sasa umepita, bado tunakukumbuka,
Machozi hatujafuta, bado tunahuzunika,
Jina bado twaliita, kumbe ulishatutoka,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.

Ni vigumu kuamini, kuwa ilishatokea,
Machungu tele moyoni,vigumu kuyazowea,
Hupo tena duniani, mbali umeelekea,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.

Ni kama utani vile, ua letu kunyauka,
Nakumbuka siku ile, kichwani haitotoka,
Umekwenda zako kule, mwisho wako ‘lipofika,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.

Amina mpiganaji, mahiri wetu vijana,
Nasi tulikutaraji, ‘ngetusaidia sana,
Mambo yetu kuyahoji, majibu kupatikana,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.

Uliacha changamoto, kwenye timu ya taifa,
Sasa imepamba moto, yacheza kwa maarifa,
Na sasa tunayo ndoto, itat’ongezea sifa,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.

Bunge uliloliacha, sasa kumepambazuka,
Kwa hakika kumekucha, hoja zinajadilika,
Kwa mafisadi kwachacha, kwao moto unawaka,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.

Ila vita ya madawa, bado inasuasua,
Ingawa wanaelewa, moyoni ‘likusumbua,
Dhati kwao haijawa, bado hawajatatua,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.

Amina dada Amina,rafiki yetu wa kweli,
Kama ingewezekana, kulitenda jambo hili,
Basi tungeomba sana, uturejee kimwili,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.

Kimwili haupo nasi, kiroho tupo pamoja,
Ni kweli tunakumiss, tutakwona siku moja,
Familia yakumiss, Mungu aipe faraja,
Bado tunakukumbuka, rafiki yetu Amina.

Naweka kalamu chini, bado sisi twakupenda,
Upumzike kwa amani, mahali ulipokwenda,
Mahala pema peponi, malaika kukulinda,

BADO TUNAKUKUMBUKA, RAFIKI YETU AMINA.

WAPI Zanzibar Juni 29, 2008!

JUMAPILI YA TAREHE 29 JUNI

WAPI ZANZIBAR INAWALETEA:


Lile tamasha la kila mwezi ambalo huwakusanya pamoja wasanii mbalimbali katika kunadi kazi zao. Tamasha hili na nafasi pekee kwa wasanii ambao hawafahamiki sana kuweza kujitangaza na kuthibitisha vipaji vyao.Wasanii husika ni pamoja na Waimbaji, Ma emsii, wachezaji, wachoraji, wabunifu wa mavazi, wafumaji, wachekeshaji washairi, waigizaji na wengine wengi.

KWA MARA YA KWANZA WAPI ZANZIBAR INAWALETE MASHINDANO YA WASANII WA JUKWAANI PAMOJA NA WACHORAJI NA WASHINDI WATAPATIWA NAFASI YA KUSHIRIKI KATIKA TAMASHA LA KIMATAIFA LA NCHI ZA JAHAZI.

Tamasha litafanyika katika ukumbi wa Ngome Kongwe (Old Fort) kuanzia saa 9 Alasiri hadi saa 2 usiku.

KARIBUNI MADA YA MWEZI HUU NI SANAA NI AJIRA "iendeleze ikuwezeshe"

Wednesday, June 25, 2008

Bi Kidude naye ni Supa Modo!
Mwimbaji taarabu mkongwe na Kungwi mkuu wa Tanzania, Bi Kidude ameingia kwenye fani mpya! Umodo! Ameonyesha waTanzania kuwa umodo si kwa vijana tu, hata wazee wamo!
Bi Kidude alionyesha vitu vyake hivi karibuni kwenye fesheni show ya Mustafa Hassanali. Kuona picha zaidi za hiyo show tembelea blogu ya Father Kidevu!
Hongera Bi Kidude! YOU GO GIRL!

Wazimbabwe Wakatwa Mikono na Vidole! - Ushenzi wa Mugabe


Ama kweli raisi Mugabe wa Zimbabwe kawa kichaa mwendawimu. Badala ya kutoka kwenye ofisi ya raisi na heshima zake atatoka kama mnyama!
Leo kuna habari kuwa watu huko Zimbabwe wanakatwa mikono na vidole kusudi wasipige kura. Wengine wamevunjwa mikono na vidole. Pia watu wanapigwa ovyo!

Na mpinzani wake, Morgan Tsvangirai ameomba hifadhi kwenye ubaolizi wa Uholanzi huko Zimbabwe.
Sikutegemea kuwa nitasikia habari za kusikitisha kama hizi kutoka Zimbabwe. Kweli huyo Mzee Mugabe kapatwa na 'senility' (kichaa) ya ajabu. Labda anadhani ataishi daima. Ametawala Zimbabwe kwa miaka 28 na sasa ni nchi enye dhiki.

Kwa habari zaidi someni:


Ruben Studdard Anaoa!


American Idol wa mwaka 2003, Ruben Studdard (29) (Pichani kulia) anaoa. Habari zinasema kuwa Ruben aka. Velvet Teddy Bear, atamwoa, Bi Surata Zuri McCants (30) jumamosi hii inayokuja!
Kama mtakumbuka alivyoshinda Ruben kulitokea maneno ya kibaguzi. Watu walitaka huyo shoga Clay Aiken ashinde kwa vile ni mzungu. Lakini Ruben na sauti yake tamu kama hayati Luther Vandross alifanikiwa kulewesha watu na ndiye aliyeshinda.
Ruben anatoka Birmingham, Alabama, na Bibi arusi anatoka Atlanta, Georgia. Nawatakia maisha mema ya ndoa.
**************************************************************

BIRMINGHAM, Ala. (AP) — He won the affection of millions of people on "American Idol," but this weekend, Ruben Studdard is giving his heart to one woman.

A representative for the former "Idol" confirmed to The Associated Press on Tuesday that Studdard, 29, plans a Saturday wedding. He and Surata Zuri McCants, 30, took out a marriage license on Monday, according to court records.

The Birmingham native, nicknamed the "Velvet Teddy Bear" on the show for his big frame and sonorous voice, has released three albums since his 2003 win, including the platinum CD "Soulful." He is working on a new album.

Tuesday, June 24, 2008

Ajali ya Fung Wah Bus mjini New York

Fung Wah Bus mjini New York, Canal St. ikipakia abiria
Ajali ya Fung Wah Bus 6-23-08 Mjini New York

Wadau wanaosafiri kati ya New York City na Boston wanapenda sana kusafiri na mabasi ya waChina. Bei zao ni nafuu sana. Dola $15 kwenda, dola $15 kurudi. Si mbaya ukilinganisha na Greyhound wanaotaka dola $44 kwenda, na hiyo kurudi.

Mabasi ya waChina yanayopendwa na kujulikana sana ni Lucky Star na Fung Wah Bus. Greyhound na vyombo vya haabri walijaribu sana kuua biashara zao na walikuwa wanasumbuliwa sana na ma state troopers (polisi). Lakini waChina hawakukata tamaa na biashara yao ilizidi kukuwa. Walianza kwa nauli dola $10. Watu walidhani ni utani, lakini habari zilienea na Fung Wah Bus ilikuwa.

Greyhound walilia, maana watu waliunga mkono waChina na kuandamana walipotaka Fung Wah bus kusimamisha huduma ya bei nafuu. Sasa inabidi haya mabasi yaondoke kwenye kituo kikuu cha mabasi ya Boston, South Station. Greyhound sasa wamepunguza nauli kwenye baadhi ya mabasi yao kwenda New York City. Ndo ubepari huo.

Lakini njama ya kuua biashara ya mabasi ya waChina bado upo. Kila wakipata ajali wanasemwa. Wanaonya watu wasipande hayo mabasi ya waChina. Lakini watu bado wanapanda.

Jana huko New York, basi la Fung Wah iligongwa na lori ikiwa inapakia abiria. Mama moja aliyekuwa anavuka barabara alikufa. Ingawa si kosa la Fung Wah bus, utadhani ni kosa lao. Kwenye taarifa ya habari wanaonyesha ajali za nyuma za Fung Wah bus. Duh! Kweli njama za kuua biashara ya Fung Wah bus bado upo.

Lakini hata waseme nini, mimi bado ni mpenzi wa hiyo basi. Ukitaka usafiri wa haraka na wa hakika na ya bei nafuu kati ya New York na Boston ni hiyo! Greyhound mlie tu!

Kwa habari zaidi someni:


Monday, June 23, 2008

Bongoland II itakuwa kwenye DVD hivi Karibuni


BONGOLAND II DVD - An Update

We have been busy getting ready to release BONGOLAND II on DVD. We are getting closer and closer...the date that we have planned to release the DVD is July 15th. More details to come.We are also proud to announce that Bongoland II was officially selected for the Zanzibar International Film Festival and the Black Harvest International Festival this is in Chicago.

Both of these film festivals will take place in the month of July. We are confident that there will be more festivals to come where you can possibly watch Bongoland II.

Please watch the blog to see how you can pre-order your new DVD.

In the meantime, we are working on two new projects. A documentary about the relationships between Africans and African Americans and a love story drama by a cast of mainly actors from Kenya. It is a Kenyan story by all measures.

Sunday, June 22, 2008

Sisi Marafiki Tutapata Mimba Pamoja!Jamani! Kwa kweli kuna habari ya kusikitisha sana kutoka Gloucester, Massachusetts. Wasichana 27 was shule ya sekondari huko Gloucester wamepata mimba. Ajabu ni kuwa hawa wasichana wanasherkea na kuringia mimba zao! Wana miaka 14 hadi 16.

Kama mko Marekani lazima mmesikia habari hizi kwenye TV na kwenye talk shows. Kwanza ni wasichana wengi mno waliopata mimba. Pili sababu ya wao kupata mimba, "eti wanataka kulea watoto wao pamoja na kuwa marafiki daima".

Huko kwenye zahanati ya shule, wasichana walikuwa wanapongezana wakithibitishwa kuwa wana mimba, na kulia wakiambiwa hawana. Si ndo watu walishutuka na kuanza kuchunguza kuna nini. Maana si kawaida kwa wasichana wadogo kutaka mimba, mara nyingi ni za bahati mbaya.

Baada ya uchunguzi waligundua kuwa hao wasichana wanatoka kwenye nyumba zilizovunjika, yaani mzazi au wazazi hawapo. Au hali ya maisha nyumabni kwako ni mbaya. Baada ya kuulizwa walisema kuwa "Nataka mtu ambaye atanipenda" (Mtoto).
Aliyemtia mimba msichana fulani ni jamaa wa mitaani ambaye hana pa kukaa mwenye miaka 24. Hapa Marekani ki kosa la jinai kwa mwanaume mwenye miaka 21 au zaidi kutembea na msichana chini ya miaka 17. Of course inatokea, lakini ole wao wakamatwe.
Na pia watu wanalaumu hiyo shule kwa ku-glorify (kusifia) uzazi na umri mdogo. Kuna day care safi sana (Nursery) kwa ajili ya watoto wa wanafunzi. Tena wanasema nzuri kweli. Wanafunzi wanapishana na wanafunzi waliozaa wakisukuma wanao kwenye baby stroller. Mmh!
Huko Gloucester, uchumi ni mbaya maana ni mji wa wavuvi. Kwa sasa kuna vikwazo vingi kwa wavuvi na ni shida wao kuvua samaki bila kuvunja sheria zilizowekwa. Na pia samaki wempungua baharini. Hali ya maisha umekuwa mbaya huko. Wengi wa wale wasichana na wanao wataishia kwenye 'welfare' (yaani kulelewa na serikali).
Tanzania nakumbuka wenzangu na ndugu zangu walifukuzwa shule baada ya kupata mimba. Je, wangekuwa wanafukuza wasichana hapa wangetaka kupata mimba kweli? Zamani hapa ilikuwa msichana akipata mimba, basi anatolewa kwenye hiyo shule na kupelekwa shule maalum.
Mnaonaje hii suala?

Kwa habari zaidi someni:

75th Anniversary Screen Actors Guild Celebration - Boston

Jana nilikuwa kwenye sherehe ya kusherekea miaka 75 ya Screen Actors Guild (SAG) hapa Boston. Party ilifanyika katika hoteli ya Ritz Carlton, mjini Boston. SAG ni chama kinachowakilisha actors wote wa Hollywood. Mimi ni mwanachama na tawi letu hapa ni Boston Branch. Nilibahatika kupata mwaliko wa kujiunga na SAG baada ya kuigiza katika sinema mbalimbali. Nilijiunga mwaka huu. Bado nangojea 'break', yaani nafasi ya kupata role kubwa katika sinema ya Hollywood.

SAG ilianzishwa mwaka 1933 kutetea haki za waigizaji wa sinema za Hollywood. Kabla ya hapo walikuwa wanateswa na wakati mwingine kuwa kama watumwa wa studios. Mnaweza kusoma historia ya SAG hapa. Bofya hapa.

Hapa niko na baadhi ya marafiki zangu ambao ni actors wa hapa Boston. Katikati ni rafiki yangu, Ellen Becker-Gray (gauni nyekundu) Kutoka Kushoto, Ron Murphy, Rob Gray, Paul, mimi, Doug Weeks na Maria.


Thursday, June 19, 2008

Hongera Boston Celtics


Timu ya Basketball ya Boston Celtics ni washindi mwaka huu wa NBA. Waliwatwanga, timu ya L.A. Lakers 131-92.

Ni mara ya kwanza tangu 1986, kwa timu ya Celtics kutwaa ubingwa.

Leo kuna shere kubwa sana hapa Boston. Barabara nyingi zimefungwa downtown. Zaidi ya watu milioni moja wamejitokeza kusherekea ushindi wa Celtics.

Sasa watu wa New England tunaweza kujivunia kweli. Red Sox ni washindi wa baseball, Patriots ni washindi wa Football na sasa Celtics ni washindi wa Basketball.
Kwa habari zaidi someni:

Nafasi ya Kushinda Dola $200 - Mlioko Bongo

I had sent out a survey that I was hoping to get a lot of responses to but haven't. It is a survey for people living in South Africa Kenya Tanzania and Uganda. The response from Tanzanians has been particularly low actually. SO am asking everyone I know if they can possibly help by either contacting their friends, family and asking them to do the same, by filling out the survey.

The survey is really short and takes about 2mins and they can be entered for a chance to win 200 bucks!!!

Please send it to as many people in those countries listed above and ask them to:

1) do the survey and

2) forward it to as many people as possible. Be sure to beg/plead/grovel on my behalf since am so desperate and really need A LOT of help and responses in this. Thank you in advance.

The link to the survey is: http://www.polldaddy.com/s/95308B1FD21947E9/

From Georgina Waweru

Wednesday, June 18, 2008

Ubongo wa ShogaWatafiti wamechunguza ubongo wa mashoga na wasenge 90 ma wamegundua kitu fulani.

Wamekuta kuwa ubongo wa mwanaume mpenda jinsia moja ni sawa na ubongo wa mwanamke wa kawaida ambaye anampenda mwanaume. Wanasema kuwa huyo mwanaume mwenye ubongo wa hivyo anaweza kuwa na kila kitu cha kiume, shepu ya dume, nyeti za dume, mavuzi na sauti ya dume nk. Kasoro ni muumbo wa ubongo.

Na pia wamekuta kuwa ubongo wa mwanamke mpenda jinsia moja (lesbo) ni sawa na ya mwanaume wa kawaida ambaye anampenda mwanamke. Naye anaweza kuwa na kila kitu cha kike kasoro muumbo wa ubongo. Kwa hiyo huyo mwanamke mwenye ubongo wa hivyo akimtazama mwanamke mwenzake ni sawa na mwanume kumwangalia mwanamke.

Haya! Hivi ina maana ni kweli mtu akisema kazaliwa shoga anasema ukweli kumbe?
Ukitaka kusoma ripoti nzima, BOFYA HAPA:

Umeme Umerudi Zanzibar!

Habari kutoka BBC zinasema kuwa umeme umerudi Zanzibar leo. Sehemu ambazo bado hazijapata umeme ni zile ambazo nyaya za umeme ziliibiwa. Wanasema ni kama sikukuu huko leo kwa jinsi watu walivyo na furaha!

http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/7461995.stm

Sakata la Ukosefu wa Umeme Zanzibar

Picha imepigwa na Peter Bennett

Wadau, mambo ni mazito huko Zanzibar. Tangu May 21, kisiwa chote cha Zanzibar kimekosa umeme shauri ya kuharibika kwa ile bomba linalopeleka umeme kutoka TZ bara.

Imebidi watu wakumbuke enzi za mabibi na mababu zao na kununua vibatari, majiko ya mkaa/mchina, mishumaa, nk. Imebidi wakumbuke jinsi ya kuhifadhi vyakula kama nyama kwa kukausha na kuichoma. Wenye majenereta wana nafuu lakini wasio na uwezo wa kuwa na jenereta wanaumia.


Huo ukosefu wa umeme unaathiri uchumi wa Zanzibar. Biashara nyingi ziko karibu kufa hasa zilizotegemea friji na air condition! Hoteli za kitalii zinashindwa kutoa huduma nzuri, na kampuni ya umeme Zanzibar inasema inakosa kipatao cha shs. milioni 30 kwa siku. Hospitali hazina umeme, wanahitaji matibabu wanaathirika. Maji safi ni shida. Jamani!

Lakini cha kushangaza ni kwamba tangu ule bomba uunganishwe miaka 28 iliyopita, haikufanyiwa service. Kwanza ni ajabu kitu kama hicho kudumu miaka 28 bila matatizo. Lazima walioijenga walikuwa ni mafundi hasa. Tena inatembea chini ya bahari kwa km 38! Ni bahati kweli haikuharibika kabla ya May 2008.

Na kwa nini katika muda huo hakuna Zanzibar power generating station? Huo umeme kutoka bara ungekuwa wa ziada tu.

Wataalamu walitoka Norway kusaidia kuitengeneza. Na walikuwa wameagiza spea kutoka Afrika kusini. Lakini bado haijarekebishwa. Wataalamu wanasema kuwa huenda watakosa umeme mpaka mwezi wa tisa yaani Septemba!

Wadau mnaonaje hiyo tatitzo?
Kwa habari zaidi someni:
http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2008/06/16/116583.html
*****************************************************************

Zanzibar without power for another 4 weeks - media

Thu 5 Jun 2008,

By William Sakala

ZANZIBAR (Reuters) - A power cut that hit the Zanzibar archipelago last month will continue for at least another four weeks until an undersea cable is fixed, an engineer working on the repairs was quoted as saying on Wednesday.

The cable linking Zanzibar to mainland Tanzania broke on May 21. It was damaged by a surge at a power station in Zanzibar following a blackout. Norway built the power station, which receives electricity from mainland Tanzania.

Local media quoted Hakon Hamre, an engineer with Norwegian firm Nexans, telling the semi-autonomous islands' deputy chief minister, Ali Juma Shamhuna, that Zanzibar should expect at least a month more without electricity.

"I cannot confirm when power will be restored, but we anticipate the repair works could last ... at least four weeks as the problem is unique," Hakon Hamre, an engineer with Norwegian firm Nexans, was quoted as saying by a privately owned daily newspaper, the Citizen.

Hamre is in the country to help engineers from the state-run utilities Zanzibar Electricity Company and Tanzania Electric Supply Company to fix the cable.

The outage has hurt the economy of Zanzibar, which relies largely on tourism. Businesses have had to resort to expensive diesel-powered generators and airlines now avoid night travel.
"We can not run a 100-room facility on generators for weeks," one hotel owner north of Zanzibar told Reuters.


Zanzibar has been receiving electricity for the last 28 years through the 38 km marine cable, which is reported never to have been serviced.

The lack of power has had a big impact on water supply and hospitals, while Zanzibar Electric Company says it is losing 30 million shillings a day in revenue.

The islands get their electricity from Tanzania's Kidatu hydro power plant, using an average of 40 Megawatts at any given time for its population of about 1 million.

They are the only Indian Ocean islands that fully depend on electricity supplied from the African continent and critics say they were unprepared for this blackout.
"This has been the mistake ... We have had many signals that an alternative source was needed but the government has not taken any action," opposition Civic United Front shadow energy minister, Hamad Masoud, told a news conference

Shughuli Washington D.C. Jumamosi 6-21-08

Taarifa ya shughuli Washington DC Jumamosi

Jumuia ya waislam wa Washington D.C inawaalika watu wote kwenye hitma ya pamoja siku ya jumamosi hii Juni 21, 2008 saa tisa jioni. Tunanatarajia kuwa na hitma ya kuwarehemu marehemu na kuongelea mambo na mipango ya kufanya wakati wa mfungo mtukufu wa Ramadhani hapa D.C

Anuani ni:
North four corners local park,
211 south wood avenue,
silver spring, md, 20901.

Wote mnakaribishwa kutakuwa na soda kwa wingi, juisi nyama choma na mapochopocho ya kila aina. Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na:

IDDY SANDALY -3016135165,
MGANGA MUHOMBOLAJE -2023740988,
SALEH LONDA -2402738871,
MAYOR MLIMA-3018068467
ZAINAB (ZAINA) BUZOHERA-2404132359, ASHURA (BONTO)-2404217017,
NURU MWAMENDE-2406039364.

Tuesday, June 17, 2008

Mr. Sulu anaoa!


George Takei na Mchumba wake Brad Altman

Wapenzi wa Star Trek, hatimaye mcheza sinema, George Takei, (71) maarufu kwa kuigiza kama Mr. Sulu anaoa...bibi arusi ni mwanaume mwenzake! Anamwoa mpenzi wake wa siku nyingi Brad Altman (54).

Kama hamkujua Takei alijitokeza mwaka juzi na kusema yeye ni shoga. Tangu leo asubuhi huko California ni ruksa kwa wapenda jinsia moja (wasenge na mashoga) kufunga ndoa. Wanasema yeye alikuwa wa kwanza kuchukua kibali kwenye mji anayokaa, West Hollywood.

Jimbo la California sasa ni la pili nyuma ya Massachusetts nchini Marekeni kuruhusu mashoga kufunga ndoa.
Kwa habari zaidi someni:
http://www.eonline.com/uberblog/b143090_george_takei_licensed_wed.html

Wazee Waja Juu! - Kuugua kwa Dr. Harrison Mwakyembe


Huko kwetu kusini, kuna imani kubwa sana na mambo ya uchawi, si uongo. Wadau, sasa naona hii story ya Dr. Mwakyembe, itakuwa sinema kiboko hapo baadaye. Alivyowaumbua mafisadi na baada ya hapo kuugua ghafla na wazee wa kijijini kutokea kumsaidia.

***************************************************************

Kutoka ippmedia.com

Kuugua Dk. Mwakyembe: Wazee waja juu...!

2008-06-17

Siku chache tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kyela, Mhe. Dk. Harrison Mwakyembe kuugua ghafla wakati akiwa bungeni na kukimbiziwa kwenye zahanati ya ukumbi huo mjini Dodoma, limeibuka jopo la wazee mbalimbali maarufu mjini Kyela lililokuja juu na kudai kuwa kuumwa kwa mbunge wao huyo si bure na kwamba sasa wanajipanga katika kuhakikisha kuwa hadhuriwi na mambo ya kiuchawi.

Na kwa kuanzia, wazee hao wamesema tayari wameshaunda kamati ya wenzao kumi, ambao wamepiga kambi katika Kijiji cha Nduka kilichopo wilayani Kyela kwa ajili ya kupeana mbinu kali za kiulinzi kabla ya kufunga safari ya kuelekea Dodoma, ili hatimaye wakaonanane na mbunge wao huyo kipenzi na kumueleza kusudio lao la kumpa ulinzi kijadi.

Wakizungumza na PST mjini Kyela, wazee hao waliokataa kuandikwa majina yao gazetini kwa sababu walizodai kuwa ni za \'kiufundi\', wamesema kamati yao hiyo ya wazee kumi mahiri wa mambo ya kijadi, itaanza kwa kufuatilia kiundani ili kujihakikishia kile wanachoamini kuwa kweli, kuugua ghafla kwa mbunge wao huyo ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumetokana na kulogwa.

``Baada ya hapo, kama itabainika kuwa ugonjwa uliompata (Dk. Mwakyembe) umetokana na mikono ya watu wanaokwazika na kazi yake ya kututetea sisi na Watanzania wengine, kitakachofuata ni kumganga na kisha kumtengenezea ulinzi imara ili asidhuriwe tena,`` akasema mmoja wa wazee hao.

Wakasema wamepata wasiwasi mkubwa juu ya kuugua ghafla kwa mbunge wao huyo, hasa baada ya kusikia habari za kuwepo kwa hofu ya vitendo vya kishirikina kufanyika ndani ya Jengo la Bunge.

``Tunajua kuwa siku zote Serikali haiamini mambo haya... na hata mheshimiwa si mfuasi wa mambo haya. Lakini yeye ni mtu wetu muhimu sana. Tukigundua kuwa alichezewa, sisi tutamlinda kwa namna tunayoijua hata kama mwenyewe akikataa,`` mzee mwingine akaongeza.

Alasiri ilipojaribu kuwasiliana na Dk. Mwakyembe ili kupata maoni yake kuhusiana na kikosi cha wazee hao kinachodai kutaka kumpa ulinzi maalum, hakuweza kupatikana kwenye simu yake ya mkononi. Hata hivyo, kuna taarifa kuwa sasa Dk. Mwakyembe yuko buheri wa afya na jana alirejea tena Bungeni kwa ajili ya kuungana na wenzie katika kuijadili bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha wa 2008/09.

Dk. Mwakyembe amejijengea heshima kubwa baada ya Kamati yake iliyotumwa na Bunge kufuatilia mkataba tata baina ya Serikali na Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Richmond kuibua udhaifu mwingi, ambao mwishowe ulimfanya Waziri Mkuu Edward Lowassa na mawaziri wengine watatu kujiuzulu.

Aidha, umahiri wake ulimfanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Jakaya Kikwete amteue kuwa mmoja wa wajumbe waliounda Tume ya Jaji Bomani iliyopitia mikataba ya Madini na kuwasilisha mapendekezo yake (kwa Rais) hivi karibuni.

SOURCE: Alasiri

Ujumbe wa Leo


Monday, June 16, 2008

WaBunge Waogopa Kukalia Viti Vyao! Vina uchawi!


Ilibidi nicheke baada ya kusoma hii habari hasa nikifikiria wabunge kwenye ukumbi wa bunge wakichunguza viti vyao. Hivi kweli unaweza kufuta uchawi/juju hivi hivi?

*******************************************************************

Ndumba Bungeni: Wabunge wahofia viti vyao
2008-06-16
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Ikiwa leo ni siku ya kwanza kwa wabunge kuingia tena ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya kuwapo kwa uvumi wa kunyunyizwa vitu vinavyodhaniwa kuwa ni vya kichawi kwenye viti vyao, baadhi ya wabunge wameonekana leo asubuhi wakiwa bado wanahofia siti zao na hivyo kulazimika kuangalia na wengine kuvipangusa na leso zaidi ya mara moja kabla ya kuketi.
Tukio hilo la wabunge kudaiwa kuwekewa vitu vya kichawi kwenye siti zao, limedaiwa kutokea katikati ya wiki iliyopita na kuzua hofu kubwa, hivyo kuilazimu ofisi ya Bunge, kupitia kwa Kaimu Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashilillah kutoa taarifa kuwa ukumbi uko shwari na hakuna tishio lolote la usalama kwa waheshimiwa wabunge.
Hata hivyo, licha ya kuhakikishiwa kuwa hakuna hofu yoyote bungeni humo, bado baadhi ya wabunge walionekana wakiwa na hofu na kuchunguza sana viti vyao kabla ya kukaa.
Hata hivyo, hofu ya wabunge hao waliokuwa bado wamejawa na hisia kuwa pengine wamefanyiwa kitu mbaya kwa kuwekewa vitu vya kudhuru, iliondolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Samwel Sitta, ambaye alitoa ufafanuzi wa kina kuhusiana na sakata lenyewe kabla ya kuwataka wasiwe na hofu na badala yake waendelee na majukumu yao bungeni humo kama kawaida kwani ukumbi ni salama.
Akizungumza wakati wa kikao cha asubuhi ya leo, Spika Sitta amesema vyombo vya usalama, ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa, vimefanya uchunguzi ukumbini humo na kumhakikishia kuwa hauna hatari yoyote.
Akizungumzia sakata lenyewe, Spika Sitta akasema lilianza kwa kuonekana watu wawili wakitangatanga bungeni humo siku ya Jumanne iliyopita, mishale ya saa 2:00 usiku. Akasema taarifa za kuwapo kwa tukio hilo, alizipata siku ya Alhamisi baada ya kuambiwa na Katibu wa Bunge kuwa kamera za usalama ndani ya ukumbi wa Bunge, zimenasa watu wawili wakitangatanga Bungeni.
Akasema picha hizo zikamuonyesha mtu mmoja kati yao akiwa na vitu mkononi ambavyo alikuwa akivinyunyiza sehemu mbalimbali.
Spika Sitta akasema siku hiyo baada ya kupewa taarifa wakati kikao cha Bunge kikiendelea, akatumiwa kimemo na Mbunge Victor Mwambalaswa, akimjulisha kuwa Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe alikuwa ameugua ghafla ndani ya ukumbi huo.
Akasema alipohusianisha matukio hayo, alihisi huwenda vitu vilivyoonekaka vikirushwa na mtu aliyenaswa na kamera za usalama ilikuwa ni sumu ya kisasa. Akasema hapo ndipo akachukua hatua ya kulikabidhi suala hilo kwa Polisi na Usalama wa Taifa ili kulifanyia uchunguzi wa kina.
Akasema Jumamosi ya juzi, Polisi na maofisa wa Usalama wa Taifa walimpatia ripoti ya uchunguzi, wakimhakikishia kuwa ukumbi huo ni salama. Akasema hata hivyo, suala la kuwabaini watu walionaswa na kamera wakitangatanga ndani ya ukumbi wa bunge, bado linaendelea kuchunguzwa na kuwa litachukua muda mrefu kidogo.
Akasema kuwa suala hilo linahitaji muda kwa vile uchunguzi wake unahitaji kurejea kwenye matukio ya nyuma kwa zaidi ya saa 72 ili kujua kilichotokea siku hiyo. Baada ya ufafanuzi huo, Bunge liliendelea na kikao chake kama kawaida, ambapo mjadala kuhusu bajeti ulianza na hadi tukienda mitamboni, wabunge 56 walishajiorodhesha kwa ajili ya kuchangia mjadala huo.

Bi Kizee Muaji

Betty Johnson Neumar

Mtazame vizuri huyo bi kizee pichani. Huyo ni Betty Johnson Neumar (76). Amekamatwa na polisi huko Charlotte, North Corolina kwa tuhuma za kumkodi mtu kumwua mume wake.

Huyo bibi aliolewa mara tano, na wanaume wake wote watano wamekufa. Moja kafa kwa kupigwa risasi (walisema alijipiga mwenyewe) miaka ya 1950's. Mwingine naye alikufa kwa kupigwa risas mwaka 1986. Mwingine kafa baada ya kupata infection ambato sasa wanadhani kuwa alilishwa sumu.

Watu wanasema kuwa alikuwa anasimulia hadithi za ajabu akiulizwa kuhusu vifo vya wanaume hao. Sasa polisi wanamchukuza kwa makini. Mbona miaka mingi imepita hivyo?

Kwa habari zaidi someni:

http://www.cnn.com/2008/CRIME/06/16/cold.cases.ap/index.html

http://ap.google.com/article/ALeqM5gHG3MzunhA7wcxcqqxhtTf4tUfzQD91B85IGJ

http://www.mirror.co.uk/news/topstories/2008/06/14/black-widow-betty-89520-20606477/

Seti la - The Surrogates huko Taunton, MA

Extras wakingojea kuitwa kwenye set. Kabla ya kwenda tulipanga foleni na kukaguliwa costume/nguo zetu na mwongoza sinema, Jonathan Mostow. Ilinikumbusha enzi za Tabora Girls, na JKT. Kama nywele nguo au viatu havikumfaa unatolewa na kupelekwa wardrobe/make-up. Hatukuruhusiwa kuvaa make-up. Kulikuwa na watu wenye makrimu za kufuta make-up kwenye uso za watu ukikamatwa umevaa. Pia ukionekana msafi, mtu alikuwa anapita na kutupaka make-up ya uchafu. Moja wa majengo kwenye set.

Moja wa kondoo waliotumika kwenye shoot.
Huyo nguruwe naye ni mwigizaji.


Wazazi wa watoto waliokuwa extra waliangalia shoot. Ona nyaya za umeme. Ilibidi watumie magenerata kwa vile hakuna umeme hapo.Hao kuku nao ni waigizaji! ASPCA (Chama cha Kulind ahaki za wanyama) walikuwepo kuhakikisha usalama wa wanyama wote kwenye seti.
Siku hiyo kulikuwa na extras 300! Hapa tumemaliza siku na tunangojea check-out....kupata receipts zetu.Wadau, kwanza samahani kwa kuchelewa kuposti hii habari ya seti. Nilikuwa na matatizo ya komputya.


Hii ni costume niliyovaa siku ya kwanza kwenye set ya The Surrogates. Nilikuwa mpita njia na nilimpita Bruce Willis kama mara kumi na tano. Alikuwa anatembea na kushangaa mji wetu wa Dreads. Siku ya pili sikupiga picha ndo ilikuwa scene ya kuchoma moto maiti.

Kibao kinatueleza sehemu ya kusubiri mpaka kuitwa kwenda kwenye seti. Kampuni ambayo inatengeneza hii sinema ni Walt Disney. Walikodi mabasi ya kutupeleka huko, na haikuwa mbali.

Seti enyewe ilikuwa Paul Devers School, ambayo zamani ilikuwa shule maalum kwa ajili ya watoto wenye magonjwa ya akili. Kuna majengo kibao. Ni kama ghost town, maana majengo yote ni abandoned. Walituweka nje kwenye mahema, kwa vile walisema majengo hayako salama kwa vile zina asbestos ndani.

Saturday, June 14, 2008

MKenya abaka mvulana huko Philadelphia

Fred Magondu akisindikizwa kortini na polisi


Asante mdau Subi kwa habari hizi.

Huko Philadelphia, nesi wa kiume ambaye alikuwa anaangalia vijana wenye upungufu wa akili , alimbaka moja wao. Kijana mwenyewe ana miaka 14. Wanasema mtoto ni kipofu, na hajiwezi.

Nesi ametambulika kama MKenya, Fred Magondu, 36. Kwanza nilidhani wamemsingizia lakini wana ushahidi wa DNA. Walipima shahawa zilizokuwa kwa yule kijana. Magondu mwenyewe ana mke na watoto! Jamani! Aibu kweli kwa familia yake.

***************************************************************************

Mwenye kujifunza na ajifunze, mwenye kutoa onyo kwa wengine na atoe.
Subi

Male nurse charged with raping boy

By MATT COUGHLIN Bucks County Courier Times


A nurse caring for a physically and mentally impaired 14-year-old Bucks County boy is accused of raping the teen in April, according to police.

Fred Magondu, 36, a Kenyan national living on King Arthur Road in Philadelphia, was taken into custody at a Philadelphia nursing home Thursday afternoon and later arraigned on charges of molesting a child who was in his care.

Police said they learned of the rape April 30. The boy receives 24-hour nursing care because he is mentally and physically impaired, unable to speak and blind, police said. According to court records, another individual care nurse, who has been caring for the boy for about nine years, discovered injuries to the boy when she attempted to change his diaper after he arrived at school April 30.

The boy was first examined at St. Mary Medical Center in Middletown and then transferred to The Children's Hospital of Philadelphia. Doctors at both hospitals told police the boy was bleeding and bruised.

Police learned that Magondu, a Harleysville Pediatrics employee who has been caring for the boy for several months, was working at the victim's home from April 29 to 30. Magondu was allegedly alone with the boy from 5 a.m. to 7:40 a.m. before putting him on the bus to school, police said.

Investigators interviewed Magondu in early May at an unnamed Philadelphia nursing home where he works, according to court records. Magondu said that on April 30 the boy had been bleeding but the nurse believed it was a physical problem and had changed a set of soiled linens. Police collected a sample of Magondu's DNA and the boy's bed linens and sent them to National Medical Services for analysis.

In a report to police June 6, the laboratory said the linens tested positive for semen that matched Magondu's DNA and that the possibility of it being from another unrelated person was 1 in 7 trillion, according to court records.

Magondu was arraigned on multiple charges of rape, involuntary deviate sexual intercourse, indecent assault, corruption of minors and unlawful contact with minors and sent to Bucks County prison on $250,000 bail. If he is released, the judge ordered that Magondu have no contact with the child and surrender his passport to authorities.

Magondu has been a practical nurse since June 2006 and had renewed his license earlier this month, according to Department of State records. Those records list no prior disciplinary action. He also has an expired graduate permit that lists a prior address in Falls. During his arraignment Magondu told the judge he moved to Philadelphia from Fairless Hills with his wife and three children in January. He has no prior criminal record in Pennsylvania, according to state records.
The newspaper is withholding information about the teen to protect his identity.

Matt Coughlin can be reached at 215-949-4172 or mcoughlin@phillyBurbs.com.

June 13, 2008

Fabulous Lady!


Hello FABULOUS Ladies! You have been hit. You have been considered one of the 10 MOST FABULOUS ladies with warm loving hearts on my friends list. Once you have been hit, you have to hit 10 FABULOUS ladies. If you get hit again you know you're really FABULOUS.