Sunday, February 28, 2016

Mipango ya Mazishi - Jessie Chiume

RATIBA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU DADA JESSIE CHIUME KWA SAFARI YAKE YA MILELE TANZANIA. RATIBA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU DADA JESSIE CHIUME KWA SAFARI YAKE YA MILELE TANZANIA.

Ratiba kamili ya kuaga mwili wa mpendwa Da Jessie ni kama ifuatavyo.
 1. Kuanzia Jumatatu tutaendelea kujumuika nyumbani kwa marehemu, 44 Fleetwood Ave, Mt. Vernon, NY, 10552
 2. Jumatano, Machi 2, 2016 Flynn Memorial Home, 1652 Central Park Avenue, Yonkers, NY 10710. Tel: 914-963-5178 Heshima za mwisho (Viewing): 4pm-7pm Ibada (Service): 7pm-8pm Baada ya shughuli kumalizika, tutatoa tangazo la wapi pa kukusanyika usiku huo kwa wale ambao watataka kujumuika na wafiwa.

Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuondoka New York kwenda Dar es Salaam, Tanzania asubuhi ya Alhamisi Machi 3, 2016. Mwenyezi Mungu akipenda Da Jessie atapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele siku ya weekendi mara baada ya kuwasili Dar es Salaam siku ya Ijumaa, Machi 4. Taarifa zaidi zitafuata.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mpendwa wetu Da Jessie Wayasa Mgeni Chiume mahala pema Peponi. Ameen. Link ya kutoa rambirambi ni: http://www.gofundme.com/daMgeni Kwa taarifa zaidi: Michael Chiume: # 6466626999 Chris Litunwa: #6145926231 Nathan Chiume:# 6465526347

Saturday, February 27, 2016

Taarifa Zaidi Kuhusu Msiba wa Dada Jessie Chiume USA

The Late Jessie Chiume (1960-2016)
Jumuiya ya Watanzania New York pamoja na familia ya Marehemu Mzee Kanyama Chiume inasikitika kuwataarifu Msiba wa Dada yetu mpenzi Jessie Wayasa Chiume (maarufu kama Da Mgeni) uliotokea ghafla asubuhi ya Jumatano February 24/2016 kwa ajali ya gari huko Mt. Vernon, NY. 


Jumuiya  ya Watanzania wa New York tunasisitiza ushirikiano katika kufanikisha Msiba huu mzito. Tuungane kuwafariji wanafamilia pamoja na kutoa rambirambi zitakazosaidia gharama za kumpumzisha Dada yetu kama ilivyo desturi yetu. 


Leo hii Ijumaa familia itaendelea kuwapo 44 Fleetwood Ave, Apt 3B, Mt Vernon NY 10552). Kuanzia kesho Jumamosi February 27 msiba utakwenda Poconos, PA nyumbani kwa Kaka mkubwa wa marehemu, Ndugu Michael Kwacha Chiume 
(Address : 359 Saunders Drive,Bushkill,
PA,18324) 
ambako ndipo pia alipo Mama Mzazi wa Marehemu hadi hapo taarifa zaidi za lini na wapi taratibu za mwisho zitakapoelekezwa.


Link ya kutoa rambirambi ni : 


Kwa taarifa zaidi wasiliana na:


Michael Chiume:#  646-662-6999
Chris Lutinwa :# 614-592-6231
Nathan Chiume:#  646-552-6347Dada Jessie atakumbukwa na wengi kwa upole, ukarimu, ucheshi na mapenzi yake kwa Watanzania na wote waliobahatika kumjua. Da Jessie ametuachia pengo kubwa mno. Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema Peponi. AMEEN.
Mungu ametoa, Mungu ametwaa. 

R.I.P Jessica Chiume. We love you, we will miss you.

Wednesday, February 24, 2016

Msiba New York - Jessie Chiume

Jumuiya ya Watanzania New York,  New Jersey na Pennsylvania  (NYTC) imepokea habari za msiba ambazo zimethibitishwa na kuruhusiwa kutangazwa na ndugu Michael Chiume kwa niaba ya familia ya Chiume. Dada yetu mpendwa Jessie Chiume hatunaye duniani. Amefariki leo asubuhi kwa kugongwa na gari  huko Mount Vernon,  NY. Mungu ailaze roho ya dada yetu Jessie mahali pema peponi. Ni wakati mgumu sana kwa familia ya Chiume na sisi wote Watanzania ndugu zake. Habari zaidi za mipango  zitatangazwa na jumuiya au familia ya Chiume kadri  zitakavyopatikana.  Mungu ametoa, Mungu ametwaa.  RIP Jessica Chiume. We love you, we will miss you.

Monday, February 22, 2016

Punguzeni Make-Up msije mkaonekane kama Sanamu!


 Wadau, nimeona hii picha Facebook, watu wakicheka wingi wa Make-up kwenye uso wa huyo dada. Kavaa vizuri lakini kapaka make-up usoni usiolingana na rangi yake.  Hebu mtizame shingoni, unaona rangi yake ya ukweli.  Aliyempaka kakosea hiyo foundation na kumpaka ya ngozi ya kizungu. Matokeo yake dada wa watu anaonekama kama kinyago.

Saturday, February 20, 2016

Rais Magufuli Akutana na Makundi Mbalimbali Ikulu

Transcather - Njia Salama ya Kutibu Tatizo la Moyo Kwa Watoto
DK. C.S Muthukumaran, mtaalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka hospitali za Apollo.

Na Mwandishi Wetu,

Watoto wachanga wanaozaliwa na tatizo la tundu kwenye moyo, linalosababishia kudumaa katika ukuaji wao na hata kuwa na matatizo ya moyo wanashauriwa kupata matibabu ya kuziba tundu hilo kwa njia ya mrija bila kufanyiwa upasuaji. Hayo yamesemwa na DK. C.S Muthukumaran, mtaalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka hospitali za Apollo.

(VSD) ni tundu katika ukuta unaotenganisha ventriko ya upande wa kulia na kushoto katika moyo. Ni tatizo linalotokea mara nyingi wakati wa kuzaliwa kwa mtoto na linaweza tokea lenyewe au kama ugonjwa.
Ni kawaida kwa watoto wote kuzaliwa na tundu dogo katikati ya atria mbili na mara nyingi tundu hilo huziba ndani ya wiki chache. Mara nyingi hakuna tundu kati ya ventiko hizo mbili, ila baadhi ya vichanga huzaliwa na tundu hilo ambalo linakuwa ni chanzo cha magonjwa ya moyo na ndio sababu kubwa  ya watoto wachanga wengi kuonana na wataalamu wa magonjwa ya moyo.

Imezoeleka mara zote kuziba tundu hili kwa upasuaji wa moyo (operesheni), ambao unahusisha kupasua kifua, kupitisha mashine na kuziba tundu hilo. Kwa mujibu wa DK. Muthukumaran kwa miaka 10 iliyopita kumekuwa na maendeleo makubwa ya kutibu tatizo hili ambapo hospitali za Apollo wamegundua njia ya kuziba tundu hilo kwa kutumia njia ya “pini kwenye tundu” (angiogram) bila kovu lolote kifuani. Licha baadhi ya aina za tundu hilo kwenye moyo kama lile lililopo chini ya valvu za moyo ni lazima lizibwe kwa upasuaji. Makala hii inaonyesha jinsi gani tundu hilo katika moyo linaweza kuzibwa bila upasuaji au wowote.

Mtoto wa kike wa umri wa miaka 12 amekuwa na tatizo la moyo. Aligundulika akiwa na tundu katika moyo akiwa na umri wa miaka miwili. Madaktari walishauri afanyiwe upasuaji kwa sababu tundu lilikuwa karibu sana na valvu hivyo ingeweza kuharibu valvu ya moyo. Wazazi wake waliogopa suala la binti yao kufanyiwa upasuaji huo ambao ungeweza kusababisha apoteze maisha lakini pia kuwa na kovu kubwa kifuani. Waliahirisha upasuaji huo mpaka pale binti alipofikisha umri wa miaka 14. Kwa umri huo tayari lile tundu lilikuwa limeshaanza kuharibu ile valvu iliyokuwa karibu nalo.

Wazazi walikwenda hospitali ya watoto Apollo kwa ajili ya ushauri mwezi Septemba  2014. Baada ya utafiti wa kwanza madkatari walisema wanashauri tundu lile lizibwe kwa njia ya “pini” bila kufanya upasuaji. Baada ya wazazi kuelewa, walimchukua mtoto kwa ajili ya maandalizi. Hatua za maandalizi zilifanywa mtoto akiwa katika nusu kaputi (local anaesthesia). Hatua hizo zilichukua nusu saa tu. Tundu hilo lilizibwa kwa mafanikio makubwa kwa njia ya pini na katheta na mgonjwa aliruhusiwa kutoka hospitalini siku iliyofuata. Familia ilifurahi sana, kwa jinsi walivyotua mzigo mkubwa wa tatizo hilo la binti yao wa miaka 14.

Wakati wa ufuatiliaji wa maendeleo kwa muda wa mwaka mmoja, binti alikuwa akiendelea vizuri, hakukuwa na uvujaji wowote wala tatizo katika aortic na valvu za upumuaji. Tiba hii ya siku moja imemwezesha binti huyu kuepuka upasuaji katika mfumo wake wa upumuaji, kovu kubwa la maisha yake kifuani na siku 5-6 za kulala hospitali kwa ajili ya upasuaji.

Uzibaji wa tundu katika moyo umekuwa ukifanywa kwa mafanikio kwa muda wa miongo miwili. Ufuatiliaji wa maendeleo  kwa muda mrefu umeonyesha kuwa uzibaji wa tundu katika moyo kwa njia hii mpya ijulikanayo kitaalamu kama ‘Transcatheter’ ni mbadala bora wa kuepuka upasuaji. Kwa kipindi kirefu upasuaji umekua njia pekee ya kuziba tundu katika moyo. Ila ina kuwa hatarishi mara kadhaa hasa moyo kuziba kabisa, baada ya kufanyiwa upasuaji zaidi ya mara moja na hata vifo. Zaidi ya yote, matatizo ya maambukizi, mfumo wa fahamu na mapigo ya moyo kwenda kasi zaidi (tachyarrhythmia). Baada ya kufanyiwa upasuaji, kovu litadumu maisha yote. Hivyo kwa njia ya hii mpya ya kuziba tundu ni bora na salama kwa afya ya baadae.

Dk. C.S Muthukumaran ametoa maoni yake kwamba, kurithi ni moja kati ya sababu kubwa za kusababisha tundu katika moyo. Kwa mfano, mzazi mwenye tatizo la tundu kwenye moyo ana nafasi kubwa ya kupata mtoto mwenye hali hiyo zaidi ya mazazi asiye na tatizo hilo. Watoto wenye maradhi ya kurithi kama utindio wa ubongo mara nyingi huwa na tundu katika moyo. Uvutaji sigara kipindi cha ujauzito kwa mama kumehusishwa pia kama chanzo cha matatizo haya ya tundu katika moyo wa mtoto.

Kama tatizo hilo la tundu katika moyo lisipopatiwa matibabu huwa linaweza kusababisha matatizo ya moyo, anasema Dk. Muthukumaran. Ukuaji wa tundu hilo katika moyo inaweza kusababisha moyo kushindwa kuendelea kusukuma damu, au kuwa na mapigo yasiyo sahihi, kudumaa kwa mwili hasa kwa watoto wachanga. Mtoto anashindwa kula sawa sawa na hivyo kuathiri ukuaji wake. Na matokeao yake mtoto anapungua uzito au asikue kabisa.
Katika hospitali ya watoto ya Apollo uzibaji wa tundu katika moyo kwa njia ya Transcatheter  umefanywa kwa zaidi ya watoto 300 kwa miaka 5 iliyopita kwa kutokuwa na matatizo yoyote makubwa. Zaidi ya 50% ya matatizo ya tundu la saizi ndogo mpaka yale ya wastani yamezibwa kwa njia hiyo kuingiza katheta. Ujuzi mkubwa wa madaktari, uchaguzi sahihi wa wagonjwa, mipango sawia ndio ufunguo wa mafanikio katika njia hii ya kisasa.Kuhusu Hospitali ya Apollo

Hospitali za Apollo ni za kwanza katika eneo Asia Pacific kutoa huduma za upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa Robot, ambayo ni aina ya upasuaji isiyokuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji kutumia Robot iliyopo hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa. Taasisi ina wataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika utoaji wa huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu bora kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya Da Vinci inayotumika katika upasuaji.
Mfumo huu wa upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya wanawake (Gynaecology), moyo, utumbo, na magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa mgongo


Sunday, February 14, 2016

Happy Valentine's Day - Sikukuu ya Wapenzi


Nawatakia wadau wote sikukuu njema ya Wapenzi (Valentine's Day).  Mkumbuke mnaowapenda.   Na msisahau kufanya mapenzi wa usalama leo.

Maandamano Burundi Dhidi ya Rwanda

 

Warundi wakiandamana leo
BUJUMBURA, Burundi` (AP) - Thousands of Burundians on Saturday participated in government-sanctioned demonstrations against neighboring Rwanda whom it accuses of supporting a rebellion to topple Burundi's president.

   The demonstrations highlight the souring of relations between the Central African neighbors since Burundi President Pierre Nkurunziza was re-elected for a disputed third term.

   Burundi was rocked by violent street protests for months after Nkurunziza's April announcement that he would seek another term. At least 400 people have died since then in violent street protests, assassinations, attacks by a rebel group and a failed coup attempt. More than 200,000 Burundians have fled to neighboring countries, mostly to Rwanda. Burundi is accusing Rwanda of training and arming rebels in the refugee population.

   Rwanda on Friday said it plans to relocate 75,000 Burundian refugees to other countries following the accusations.

   Burundi's Interior Minister Pascal Barandagiye, in a radio broadcast urging people to participate in the demonstrations, accused the Rwandan government of trying to topple Burundi's government through military means.

   Demonstrators camped at Rwanda's embassy in Bujumbura Saturday morning, singing songs against Rwanda President Paul Kagame.

   The songs described Kagame as an enemy whom Burundians are going to "kumesa." The Kirundi word kumesa means wash. During Burundi's civil war a decade ago, "to wash someone up" was a euphemism for killing people perceived to be enemies.

   A U.N. panel of experts has made similar allegations against Rwanda, saying in a new report that refugees from Burundi received training from Rwandan military personnel last year with the goal of removing Nkurunziza from power. The experts spoke to 18 Burundian combatants who said they had been recruited at the Mahama refugee camp in eastern Rwanda in May and June 2015 and that their numbers total four companies of 100 recruits each.

Saturday, February 13, 2016

Nyie Warembo wa Leo ni Wazee wa Kesho!


Hospitali ya Rufaa ya Mbeya yapewa siku 60 Kununua Mashine ya CT- Scan

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla amefanya ziara, Februari 12, 2016 katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini- Mbeya, na kutoa maagizo mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa mashine CT-Scan ndani ya siku 60 huku akibainisha kuwa endapo watazembea basi watawachukulia hatua kali na kuwajibishwa watendaji na uongozi wa Hospitali hiyo.

Dk. Kigwangalla alifika hospitalini hapo majira ya saa tisa alasiri na kutembelea idara mbalimbali za hospitali hiyo kuona jinsi ya ufanyaji kazi ambapo ndipo alipobaini ukosefu wa mashine hiyo ya CT-Scan pamoja na vifaa vingine muhimu ambavyo alibainisha kuwa hata uongozi wa Hospitali hiyo walikuwa na uwezo wa kuvinunua bila kutegemea Serikali.

Baadhi ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla alitembelea ni pamoja na kitengo cha kutolea huduma kwa wagonjwa (OPD), Kitengo cha upasuaji, wodi ya upasuaji, duka la dawa la hospitali hiyo, wodi ya wanawake, wodi ya wanaume, watoto na kitengo cha Maabara ambapo kisha alipata kuongea na wafanyakazi pamoja na uongozi mzima wa Hospitali.

Dk.Kigwangalla alitoa wasaha mwingi kusikiliza kero za wafanyakazi hao kuongea lile linalowakabili bila kuogopa ili aweze kujua matatizo na changamoto zinazowakabili.

"Hospitali kubwa kama hii hapa Mbeya na wataalam wote mlionao mnashindwa kufanya biashara!, Mnategemea tu Serikali? lini mtakuwa na CT-scan kwa upande wenu? wakati mnaingiza Milioni 500 kwa mwezi?" alihoji Dk. Kigwangalla.

Dk.Kigwangalla aliwaambia uongozi wa hospitali hiyo ina fursa na uwezo wa kufanya jambo kubwa kwani pia ina uwezo hata wa kukopa fedha kutoka mashirika ya bima ya afya.

Aidha, Dk Kigwangalla amewataka uongozi wa Hospitali hiyo kuwa wabunifu katika uendeshaji wao ikiwemo kutengeneza jengo la kisasa la matibabu ya kulipia, kujenga nyumba za wafanyakazi ambapo amewapa mikakati hiyo imeanza na pindi atakaporejea tena hospitali hiyo.

Imeandaliwa na Andrew Chale, modewjiblog, Mbeya

DSC_3499

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akisisitiza suala la Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini- Mbeya kununua mashine ya CT-scan ndani ya siku 60, huku akiahidi kuwachukulia hatua kali ya kuwawajibisha watendaji watakaozembea katika hilo.

kigwangalambeya2

Baadhi ya wafanyakazi na madaktari wa hospitali hiyo wakifuatilia mkutano huo wakati Naibu Waziri Dk.Kigwangalla (hayupo pichani) wakati wa alipofanya ziara Februari 12,2016. Wafanyakazi hao waliweza kutoa maoni yao mbalimbali ikiwemo suala la motisha na uboreshaji wa mishahara pamoja na ukosefu wa vitendea kazi ikiwemo kitengo cha maabara.

kigwangala mbeya

Mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo ya rufaa Mbeya akiuliza akitoa maoni yake kwa Naibu Waziri Dk.Kigwangalla.

kigwazz

Kaimu Mkurugenzi wa hospitali ya Kanda ya rufaa Mbeya, Thomas Isidori akitoa fursa kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla (kulia) kuzungumza na wafanyakazi katika mkutano wake huo.

kigwangala2

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipita katika moja ya maeneo ya hospitali hiyo ya Kanda ya rufaa Mbeya sambamba na wenyeji wake...

kigwaz

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akitazama moja ya kipimo cha mgonjwa ambacho hata hivyo ilieleza kuwa kilipimwa nje ya Hospitali hiyo na kuletwa hapo ambapo alipotaka kujua kwa nini imekuwa hivyo kwa hospitali kubwa kama hiyo alielezwa kuwa hawana mashine ya CT-Scan ndipo alipoutaka uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha mashine hiyo inapatikana ndani ya siku 60 kuanzia hiyo Februari 12.

kigwangala mbeya6

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipata maelezo ya moja ya mashine ndani ya maabara ya hospitali hiyo ya Kanda ya rufaa Mbeya. Hata hivyo ameelezwa mashine hiyo ni ya zamani sana hivyo ufanisi wake ni mdogo huku wakimweleza kuwa inatakiwa wapatiwe mpya ilikuendana na kasi.

kigwangaz

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akimjulia hali Mtoto Edger Emmanuel (2) anayepatiwa matibabu ya mguu wake katika wodi hiyo ya watoto kitengo cha upasuaji.

kigwaz11

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla na Kaimu Mkurugenzi, Thomas Isidori wakimjulia hali Mzee Lazaro Mwakapunga aliyelazwa hospitalini hapo.

kigwanga1

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipatiwa maelezo namna ya mfuko wa malipo wa ki-elektroniki unaotumiwa hospitalini hapo na Kaimu Mkurugenzi, Thomas Isidori. Hospiatli hiyo inatumia mfumo huo ambapo imeweza kufanikiwa katika ukusanyaji wake wa mapato.

kigwangala

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akipokelewa na Katibu wa Hospitali hiyo, Maryam Msalale wakati wa kuwasili katika ziara hiyo. (Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog, Mbeya).

Fahamu Jinsi Radiotherapy Inavyoweza kuokoa Maisha

Dk. Mahadev, mshauri mwandamizi wa radiotherapia kutoka Hospitali za Apollo.


Na Mwandishi wetu,
Matibabu ya kawaida ya saratani huwa yanahusisha upasuaji, radiotherapia na kemotherapia. Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa kwenye tiba kwa njia hizo mbili. Katika hatua za mwanzo, saratani huwa ni ugonjwa unaotibika kwa dozi moja mahususi lakini saratani iliyosambaa au kukomaa inahitaji dozi zaidi ya moja katika kuitibu. Radiotherapia, ni tiba iliyopo katika mfumo maalumu unaoleta matokeo katika mwili mzima.
Dk. Mahadev , mshauri mwandamizi wa tiba ya uvimbe kwa mionzi kutoka hospitali za Apollo anaeleza kwamba radiotherapia inahusisha chembe chembe ndogo za mionzi ya gamma au X-rays katika kutibu saratani na hata matatizo ambayo sio ya saratani pia. Mionzi hii imegawanyika katika ile mionzi ya mbali (external radiotherapy) ambayo chanzo cha mionzi kinakuwa mbali na mwili na ile mionzi ya karibu ambayo mionzi inawekwa karibu ili kuchoma sehemu yenye uvimbe peke yake.

Mionzi ya karibu ni aina nzuri ya kutibu saratani ila kwa uvimbe unaoonekana kirahisi na unaofikika. Hivyo saratani iliyopo mdomoni, saratani ya tezi dume, saratani ya kizazi zote zinaweza kutibiwa kwa mionzi ya karibu peke yake. Faida kubwa ya mionzi ya karibu ukilinganisha na mionzi ya mbali ni kwamba mionzi ya karibu inahusisha uponyaji ndani ya muda mfupi (siku 3-5) wakati mionzi ya mbali inachukua hadi wiki 7 hadi 8. Uvimbe wowote uliokomaa unahitaji mionzi ya mbali.

Lengo kubwa la matumizi ya radiotherapia ni kuchoma sehemu pekee yenye uvimbe na kuepuka kuchoma sehemu nyingine za pembeni katika mwili. Mionzi ya mbali inahistoria ndefu kutoka enzi za cobalt kwenda kwenye hali ya teknolojia ya juu ya kutoa tiba ya mionzi kwa moduli ya hali ya juu (IMRT), mionzi kwa kuongozwa na picha (IGRT), upasuaji kwa njia ya sterio (SRS) na njia ya sterio kwa mionzi mwilini (SBRT). Mashine yenye program maalumu kwa ajili ya upasuaji (Cyberknife robotic radiosurgery ) ni njia bora zaidi katika kufanya SRS na SBRT, aliongeza Dk. Mahadev  kuwa teknolojia hizi zinapatikana katika hospitali za Apollo.

Umuhimu pekee wa kutumia mashine yenye program maalumu kwa ajili ya upasuaji ni kukata milimeta sahihi na uponyaji katika siku chache. Ni tiba ya mgonjwa bila kulazwa na hahihitaji nusu kaputi katika kufanyika. Hivyo saratani ya mapafu na tezi dume inaweza kutibika ndani ya siku 3 hadi 5, wakati muda wake kawaida huchukua wiki 7-8 kwa uangalizi wa karibu. Mashine yenye program maalumu kwa ajili ya upasuaji ni muhimu katika kutibu uvimbe, ambao hauwezekani kufanyiwa operesheni kwa sababu ya eneo ilipo aidha katika ubongo au uti wa mgongo. Inatumika kutibu magonjwa kama meningiomas, uvimbe katika pituitary, mishipa ya ateri iliyodhofika (AVM) na madhara kutokana na saratani katika ubongo, mapafu na ini.

Dk. Mahadev  anaelezea njia bora ya kutumia radiotherapia ni kwa protoni. Faida kubwa ya protoni ukilinganisha na njia ya kawaida ni katika kutoa mionzi kwa umakini zaidi hasa kuchoma sehemu yenye uvimbe peke yake. Hiyo inapelekea matokeo mazuri na madhaifu machache. Kutokana na kutokuwa na dozi zaidi katika kutibu uvimbe, ni vyema kudhibiti uvimbe ukiwa katika hatua za mwanzo ambapo huwa tunaogopaga madhara ya kutumia mionzi. Matumizi ya protoni ni mapinduzi katika tiba ya saratani. Saratani ya kichwa na shingo, mapafu na tezi dume huwa zinatibika kirahisi kabisa kwa mionzi hii ya protoni.

Baadhi ya saratani zinazotibika kwa upasuaji, inaweza kutibika kirahisi kwa radiotherapia tu. Ikiwa hatua ya mwanzo, saratani ya mdomoni, mfumo wa chakula, tezi dume, zaweza tibiwa kwa mionzi peke yake. Faida katika kutibu aina hizi za saratani ni kuwa zipo sehemu zinazofikika. Mgonjwa anaweza kuwa na ogani inayofanya kazi vizuri hivyo kuona ubora wa maisha. Saratani nyingi zilizokomaa huwa zinahitaji kwa pamoja upasuaji, radiotherapia na kemotherapia katika kuitibu ambazo zote zinapatikana katika teknolojia ya juu kutoka hospitali za Apollo.

Tumetoka kwenye enzi za kufanya operesheni kubwa na kuingia kwenye utunzaji wa ogani zetu kwa msaada wa teknolojia ya mionzi bora na dawa mpya na bora za tiba kwa kemotherapia. Kwa mfano saratani ya matiti ndio saratani inayoongoza kwa wanawake duniani. Hapo kabla, titi lote lilikuwa linakatwa. Ila kwa sasa wagonjwa wengi wanabaki na matiti yao salama kwa upasuaji mdogo tu unaofanywa.

Tiba hiyo ndogo katika tiba inawasaidia wanawake kuwa na saikolojia chanya inayowafanya wapone haraka pia. Kichwa na shingo, mfumo wa chakula, saratani ya tezi dume na sehemu nyingine ambazo huwa kutokuondoa ogani ni kitu cha muhimu katika tiba.
Radiotherapia ni mbadaka zuri kuepuka upasuaji au kemotherapia katika kupambana na saratani. Mabadiliko makubwa katika teknolojia na matumizi ya kompyuta yamewezesha utoaji bora wa huduma ya tiba ya mionzi kwa madhara kidogo sana.Kuhusu Hospitali ya Apollo

Hospitali za Apollo ni za kwanza katika eneo Asia Pacific kutoa huduma za upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa Robot, ambayo ni aina ya upasuaji isiyokuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji kutumia Robot iliyopo hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Taasisi ina wataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika utoaji wa huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu bora kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya Da Vinci inayotumika katika upasuaji.

Mfumo huu wa upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya wanawake (Gynaecology), moyo, utumbo, na magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa mgongo.
--