Saturday, August 29, 2015

Anguko la Upinzani Nchini Na Hadithi ya Bora Shetani Nimjuaye Kuliko Malaika Nisiyemjua! - Edward Lowassa

Edward Lowassa, Anguko la Upinzani Nchini Na Hadithi ya Bora Shetani Nimjuaye Kuliko Malaika Nisiyemjua!

Na Dkt. Hamisi Kigwangalla
Raia Mwema. Agosti 26, 2015.

Nimekuwa na siku nyingi kidogo sijaandika. Leo nikiwa Arusha nikitokea msibani Usangi kumzika Mzee wetu na muasisi wa TANU na CCM, Mzee Peter Kisumo, nilikutana na marafiki zangu wa UKAWA na tukataniana kidogo; na hapo nikasikia matumaini waliyokuwa nayo, si ya kushinda uchaguzi bali ya kukidhoofisha chama changu, Chama Cha Mapinduzi, mmojawapo alisema: ‘baada ya Oktoba CCM na uwanja wa siasa hautabaki sawa na leo…CCM haitokuwa imara na salama tena.’

Mazungumzo yale yalinifikirisha. Nikafanya tafakuri tunduizi. Nikaamua kuweka mawazo yangu kwenye rekodi.

Kwa hakika ushindi kwa CCM mwaka 2015 kwenye uchaguzi mkuu kwa nafasi za Urais, wabunge na madiwani uko wazi kabisa. CCM itapata ushindi wa kishindo. Kwa nini? Nitafafanua kwa ufupi tu hapa.

Sababu kubwa za kwa nini CCM itashinda mwaka huu ni zifuatazo; kwanza, CCM ni chama ambacho kimejengwa kwenye misingi na itikadi, na kina wanachama wengi zaidi wanaoamini kwenye itikadi na misingi hiyo kuliko wale wachache wanaokiuka, mfano mzuri ni wale wanaofanana na Ndg. Edward Lowassa ambaye aliondolewa kwenye kinyang’anyiro cha Urais bila maelezo ya kina, japokuwa wengi wa wachambuzi wa mambo ya kisiasa walibaki wakisema kwa kiasi kikubwa inawezekana ni historia yake ya kuhusika kwenye moja ya skendo kubwa kabisa za ufisadi kuwahi kutokea nchini, maarufu kama ‘kashfa ya Richmond’. Kashfa hii ilipelekea kujiuzulu kwake nafasi ya uongozi wa Waziri Mkuu.

Pili, CCM ndicho chama pekee chenye muundo thabiti wa kitaasisi – kutokea kwenye nyaraka mbalimbali zinazoeleweka, muundo wa utumishi, watumishi na ofisi, muundo wa vikao na ratiba zake, sera, itikadi, vifaa na majengo, na vitega uchumi vinavyoendeshwa kwa mfumo unaoeleweka, ukilinganisha na vyama vya upinzani vinavyoendeshwa kwa matukio – ni tukio moja baada ya jingine, hakuna mfumo wa muundo wa kitaasisi uliosimama na unaoeleweka. Vyama vingi vya upinzani vinajaribu kuanza harakati za kuunda mfumo na muundo wa kitaasisi lakini havijafika popote.

Tatu, CCM ni chama chenye wanachama wengi kuliko vyote; kwa mtaji wa wanachama zaidi ya milioni saba, ukiongeza na wapenzi, washabiki na watu wanaoamini tu kwenye uwepo wa dola imara inayotokana na CCM, kwa hakika ushindi kwa CCM ni dhahiri. Namba zina sifa moja kubwa, kuwa huwa hazisemi uongo.

Nne, CCM itashinda mwaka huu sababu imefanya kazi nyingi na zinaonekana. Sintozitaja kwenye makala hii.

Tano, CCM inafanya mabadiliko ya uongozi, sera, mikakati yake ya kuendesha shughuli zake na ina falsafa ya ‘kujikosoa na kukosoana’ na inakubali kujirekebisha ama kurekebishwa. Tofauti na vyama vingi vya upinzani, ambavyo toka vianzishwe, baadhi yavyo, mpaka leo hii havijawahi kufanya mabadiliko kwenye sera, muundo na hata sura za viongozi wake, na badala yake vinaongozwa na familia ama watu wa kanda ama kabila fulani. Ukitaka kubadilisha sura za viongozi utakumbana na hasira za waasisi hao wenye vyama hivyo.

Sita, ngome za CCM hazijatikiswa hata kidogo na haziwezi kuyumba ndani ya miezi hii miwili ya kampeni. Ushindi kwenye serikali za mitaa wa takribani asilimia 80 ni kipimo tosha kuwa bado CCM ni chama kilichojikita mpaka kwenye nyumba kumi za kila mtaa/kitongoji, na kwamba bado kinapendwa na kuaminiwa na watanzania walio wengi.

Saba, kitendo cha UKAWA kuwa tayari kumpokea na kumteua Ndg. Lowassa kuwa mgombea wao ni pigo kubwa kwao; kwanza ni kiongozi mbabe na asiyeshaurika, hawezi kukubali kuendeshwa na taratibu za vyama hivyo – anajiamini yeye ni ‘taasisi’, maarufu na ana timu ya kumfanyia kazi, tayari tunavyoongea amekwisha wakatisha tamaa wenzake aliowakuta huko, baada ya kuvijenga vyama vyao kwa jasho na damu kwa miaka zaidi ya 20, ameingia yeye tu na kateuliwa kuwa mgombea wao, na tayari ameanza kuzitenga timu za kampeni alizozikuta huko na mifumo ya uongozi aliyoikuta huko na kuanza kutumia makundi yake ya Urais aliyotoka nayo anakokujua.

Nane, kuna hiki kitu wataalamu wa mambo ya siasa wanaita ‘incumbency advantage’, yaani ‘faida ya kuwepo madarakani’. Hii peke yake, kisaikolojia, inaiweka CCM juu ya vyama vingine hata kabla hatujaanza kampeni.

Tisa, kwenda kwa Ndg. Lowassa na hatimaye kuteuliwa kupeperusha bendera ya UKAWA kunafanya kambi ya upinzani, iliyoungana, kwa mara ya kwanza kuwa kwenye upande wa kujitetea (defensive side) muda wote, nafasi ambayo hawajazoea kucheza kwenye mechi hizi, badala ya ile ya kushambulia (offensive), ambayo wameizoea. Pia kwenda kwake UKAWA na wao kumkubali kunajenga mazingira ya kuwafanya wapinzani waonekane ni wenye tamaa ya kushika dola kwa nguvu zote hata kama ni kwa kuchukua makapi; kwamba, wanataka kwenda kwenye pepo ya mwenyezi Mungu hata kama ni kwa kupitia kwa shetani!

Maana kumchukua mtu kama Ndg. Edward Lowassa kuwa mgombea wao, ambaye walitumia muda mwingi na nguvu zao zote kumchafua, na ambaye wanapaswa wamshukuru kwa kuwapa umaarufu na heshima nchini – kipindi wakimchafua, kunaondoa imani ya wananchi juu ya nguvu ya kimaadili (moral authority) ya wao kukemea ufisadi, na kunazua maswali ya uhalali wao kisiasa (political legitimacy) na maswali ya thamani yao kiitikadi na kimaadili (ideological values and integrity): kwamba, kama wiki tatu zilizopita alipokuwa akigombea kupitia CCM alikuwa shetani, na leo anagombea kupitia UKAWA amekuwa malaika, kwamba alikuwa shetani kwa miaka 8, na leo amegeuka malaika kwa kuingia UKAWA.

Kumi, Chama Cha Mapinduzi, kimeteua mgombea mzuri wa Urais. Ndg. John Pombe Magufuli anamuacha mbali Ndg. Edward Lowassa kwa sifa za kimaadili, mwonekano wa kiutendaji, imani ya wapiga kura kwenye uwezo wa kutekeleza ahadi atakazotoa, uwezo wa kuhutubia, uwezo wa kiutendaji, na rekodi ya mafanikio katika utendaji, uadilifu, elimu na hata uwezo wa kufanya kampeni na kujieleza.

Kumi na Moja, kwenda kwa Ndg. Edward Lowassa UKAWA kumefanya watu wanaoamini kwenye mabadiliko ya kweli kutokea nje waone kama wamesalitiwa maana Ndg. Lowassa si mwanamabadiliko, ni mtu wa mfumo wa kizamani (status-quo), lakini pia kumefanya wanasiasa walioupa upinzani nguvu na umaarufu kidogo walionao leo, ni kama hawajui la kusema wala la kufanya.

Ndg. Wilibrod Slaa – hatujui kama amejiuzulu wadhifa wake wa Katibu Mkuu wa CHADEMA na kama atarejea kwenye majukwaa kumsafisha Ndg. Lowassa ama ameamua kukaa kimya kabisa – yote ni machungu kwake, amsafishe ili avunje alichokijenga toka mwaka 2007 na astaafu kwa aibu? Na watanzania wamuone ni mtu asiyeamini kwenye chochote kile, ama anyamaze kimya, athibitishe kuwa aliyoyasema kwa kipindi chote hicho ni ya kweli, na kwamba wenzake ni walafi wa madaraka tu.

Profesa Ibrahim Lipumba, aliyeamua kujiuzuru wadhifa wake wa Mwenyekiti wa CUF kufuatia ujio wa Ndg. Lowassa amesema hakubaliani na uamuzi huu wa UKAWA.

Kwa hakika kuna makundi makubwa yaliyodumu kwenye ufuasi wa wanamageuzi hawa wakongwe kwa muda mrefu watakubaliana nao na hawatounga mkono UKAWA.

Kumi na Mbili, watanzania watachagua CCM kwa sababu, kwa wale wanamabadiliko walioamini kwenye mabadiliko kutokea nje ya mfumo hawatoona jipya linalokuja na UKAWA, wataona hakuna tofauti kati ya CCM na UKAWA na kwamba wataona bora hata ya CCM imekataa kwa vitendo, pamoja na vitisho vya ‘mafuriko ya kuigiza ya Ndg. Lowassa’, kwa kumkata jina na hatimaye kumuondoa kwenye mbio za Urais, kwa tuhuma za ufisadi uliokubuhu. CCM wamefanya hivyo bila kupepesa macho. Wametoa uongozi kwa nchi, wameonesha kuwa kuna mambo wanayoamini na wanayasimamia. Upinzani wamempokea na kumpa bendera yao apeperushe. Wapiga kura wataona hawa wanasiasa wote ni mashetani tu (kama kipimo cha wanasiasa ni ushetani), na watachagua bora shetani waliyemzoea kuliko malaika wasiyemjua na ambaye ameanza safari kuelekea kwenye dola kwa kusajili shetani mkubwa kuliko wote na kumwita ‘malaika’. UKAWA wamemomonyoka kimaadili (moral decay) zaidi ya CCM kwa kumpa bendera yao Ndg. Lowassa.

Kumi na Tatu, lugha ya CCM kwenye kampeni itakuwa rahisi sana kutokana na kuwa na mgombea wa upinzani wanayemjua vizuri, na lugha ya kuwasambaratisha wasemaji wote wa UKAWA itakuwa rahisi sana, maana CCM itakuwa na kauli zao wakimchafua Ndg. Lowassa alipokuwa CCM na watawakumbusha tu wananchi.

Kumi na Nne, uwezo wa kifedha wa Ndg. Lowassa utaathirika kwa sasa akiwa mgombea wa UKAWA kwa maana atahofia kutumia pesa zake nyingi kwenye kutafuta Urais kupitia upinzani hali ya kuwa anajua hana nafasi ya kushinda, pia marafiki zake waliokuwa wakimchangia kipindi akiwania Urais ndani ya CCM wamebaki CCM ama wanahofia kutengwa na CCM mara atakaposhindwa na hawana imani kuwa atashinda Urais kutokea nje ya CCM, na UKAWA hawana ruzuku ama vitega uchumi vya kulingana ama kuishinda CCM, hivyo vifaa vya kampeni (branding materials) ya CCM na uwezo wa kujitangaza utampoteza mgombea huyu mtata wa UKAWA mara moja kampeni zitakapoanza.

Kumi na Tano, UKAWA hawana sera ambayo itamuunganisha mgombea wao na kumuuza kwa wananchi sababu UKAWA siyo chama cha siasa, na hivyo mbali na kumsafisha mgombea wao, hawatokuwa na jipya la kutoa kwa umma ukilinganisha na CCM ambao watakuwa na ilani ya kueleweka na ambayo wataiuza kwa wananchi bila shaka.

Je, wataweza kumsafisha Ndg. Lowassa ndani ya siku 64 za kampeni na watanzania wakawaelewa? Ni maswali watakayopaswa kuyatafakari na kuyajibu, pengine wakati wanayapatia majibu, muda wa kampeni utakuwa umeishakwisha na watakuwa wameishashindwa uchaguzi.

Kwa vyovyote vile malengo ya Ndg. Lowassa, kudhoofisha CCM, hayatotimia na huu utakuwa ni mwisho wake kisiasa, na hatoanguka peke yake, ataanguka na vyama vyote vya upinzani vinavyounda UKAWA. Baada ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, siyo CCM itakayokuwa inarudi kwenye meza kujipanga upya, bali ni vyama vitakavyosambaratika kutoka UKAWA vitakavyorudi kujiuliza vilipoangukia na kuanza upya safari ya kujijenga, na hii ni kama hata kutakuwa na mabaki ya vyama hivyo.

Tuesday, August 25, 2015

Sauti za Busara 2016 is Cancelled

Sauti za Busara 2016 is Cancelled
 
Due to shortage of funds, Busara Promotions reluctantly announces Sauti za Busara 2016 is cancelled.
Yusuf Mahmoud, CEO of Busara Promotions, said today “This decision was not taken lightly. We set ourselves the target to raise US$200,000 before July, when we hoped to announce dates for Sauti za Busara 2016. After meetings with various stakeholders, we extended the fundraising deadline to Aug 20. The amount of support we were finally able to raise was well short, so we were unable to continue preparations. The pressure was on further, as we were receiving enquiries from all over the world from people needing to know the dates, to make arrangements for their own flights and hotel bookings. Selling tickets for Sauti za Busara was never a problem, but these only cover 30% of festival costs”.
Yusuf continued, “Since 2004, we had no financial support from the government in Zanzibar, the United Republic of Tanzania or the East African Community. Despite tireless efforts, support from donors, embassies and commercial sponsors has reached an all-time low. Busara Promotions is an NGO; the festival is non-profit. Friends of Busara suggested we try crowd-funding. However, to be more sustainable, before the 2017 edition our priority is to develop long-term partnerships with donors and sponsors who share our vision. If anyone reading this is interested to help keep Sauti za Busara alive, generating employment locally, whilst shining the spotlight on our rich musical traditions and promoting cultural tourism for Zanzibar and Tanzania, please contact Busara Promotions.”
Annually in February over the past twelve years, Busara attracted thousands of visitors from all corners of the world to Zanzibar, at a time which used to be low season. Even conservative estimates suggest since 2004 Sauti za Busara generated USD 70 million in revenues for the island. Meanwhile, BBC World Service hailed Sauti za Busara as one of “Africa's best and most respected music events”. It is also included in CNN's “7 African music festivals you really have to see” and tops Afro-Tourism's list of “Best Music Festivals”.

Yusuf Mahmoud said finally “Sometimes it’s necessary to take one step back, before continuing to move forwards. Busara Board and management shall be working hard over the coming months, to ensure the festival resumes stronger than ever from 2017. Possibly this will mean moving location, or making it a biennial event. Certainly our priorities will be to keep the event accessible for the local population, whilst seeking to build longer-term partnerships, with the public and private sectors”.
Whilst the festival takes a break, Busara Promotions continues with its regular activities to promote African music, strengthen local know-how and build livelihood in the regional music sector. Throughout the year, Busara ensures East African artists are invited to other international events and facilitates skills-building for local artists and festival crews, through exchanges and training in arts management, marketing, media and technical skills. This work, as generously supported by the Royal Norwegian Embassy in Dar es Salaam, is unaffected by the decision to cancel Sauti za Busara 2016.

With thanks to Royal Norwegian Embassy, Dar es Salaam

Saturday, August 22, 2015

Prof. Henry Kadete Thirty Year Wedding Anniversary!
It was 30 years ago tomorrow 8/24/85, that I said "I Do" to Prof. Henry Kadete, (pronounced KAH-DEH-TEH) in Dar es Salaam, Tanzania at St. Alban's Anglican Church. It was the wedding of the year in Dar. Both my grandfathers were in attendance (my grandmothers had both passed). My grandpa flew from USA to attend and always talked about it until his death. Sadly Prof. Kadete, was taken from us ten years later in 1995 leaving me with two beautiful children. May he continue to rest in eternal peace. Amen. Tanzania and the African continent lost a genius of Electrical Engineering. For those who don't know, Prof. Kadete did the groundwork for bringing LUKU (prepaid) Electricity to Tanzania. At the time of his death, he was the Head of the Electrical Engineering Department at the University of Dar es Salaam. Only God, knows why some die so young. Prof. Kadete may be gone, but he is not forgotten.

Sunday, August 09, 2015

Star wa Bongoland 'Mukama Morandi' Afunga Pingu za Maisha!

Stelingi (Star) wa sinema Bongoland, Mukama 'Jimmy' Morandi, amefunga ndoa mjini Minneapolis, Minnesota, jana na mpenzi wake Priscilla.  Mukama ni mcheza sinema na mwanamuziki pia.

Tunawatakia maisha mema ya ndoa!

Director wa sinema Bongoland, Bongolan II na Tusamehe, Josiah Kibira, (katikati) na Mukama na Priscilla.

Mukama na mke wake nje ya Kanisa, Minneapolis
 


Mnaweza kupata habari za Kibira Films kwa kuBOFYA HAPA:

Mnaweza kuona kanda ya Mukama, You Tube

TURN BACK TIME


Facebook Giving out Cashouts - Utapeli

 Wadau, hao matapeli hawachoki!  Facebook hawatoi hela! Msikubali kutapeliwa!

****************************************

Facebook Corporate Office & Headquarters
INTERNATIONAL PROMOTIONS/PRIZE AWARD.
CATEGORY: 2ND
 

You have been approved to receive an Award of $150,000 from Facebook Corporate Office viaATM.

Your winnings can be access by issuing an ATM card.
Award Reference code: FB/575061725
File number:77801209/N
ATM Code : ATM822
To collect Card ,contact and reconfirm your details to Lloyds Bank which has been mandated to give you cash outs with below details ASAP:
==============================================================
Customer Care
st93828 @yahoo.com.hk
angssst1 @gmail.com
==============================================================
1 Your Full Names:
2 Your Tel/Mobile Number:
3 Your Nationality:
4 Current Country:
5 Your contact Address:
6 Occupation:
==============================================================

Once again: CONGRATULATIONS!!!
Regards,
Facebook Management.
Promo Coordinator.
Lam Thanh Tu

Tuombe Wenye Ugonjwa wa Saratani Wapone!


Wadau, tuombe wenye ugonjwa wa saratani wapone.  Baba yangu mzazi, Dr. Aleck Che-Mponda alifariki mwezi Machi kwa ugonjwa wa Prostate Cancer (saratani).  Mfanyakazi mwenzangu hapa USA alikufa kwa kansa ya tumbo, mwingine kwa kansa ya mapafu mwaka huu.  

Tuombe haya makampuni ya madawa yanayotumia hela KUZUIA utafiti ya tiba ya saratani wabadilishe mioyo yao. Wamezidi uchu ya ya pesa! Waende Motoni wote!  Tiba ingeshapatikana lakini wanazuia kwa vile wanaogopa watashindwa kuuzwa madawa yao!

Saturday, August 08, 2015

Shopping while black? Ubaguzi Boston

Shopping while black?     Jamani, hata wasomi weusi wanaonewa Boston!

Dr. Ben Carson Mgombea Rais Upande wa Republican ni Mnafiki


Wadau, Dr. Ben Carson ni mweusi pekee mgombea urais wa Marekani upande wa Republican safari hii.  Ni daktari wa Ubongo (Neurosurgeon),  Kazi yake kuponda weusi, huko akisahau kuwa yeye ni mweusi, mwam ayake alimlea bila baba na alikuwa kwa foods stamp na kutibiwa na serikali bure kwenye Medicaid! hebu aache Unafiki! Kazi kulamba mikundu ya wazungu!

Mkutano Bandia - Msikubali Kutapeliwa!

Wadau, watu wengi wamepokea huo mwaliko bandia!  Msikubali kutapeliwa.  Uataambiwa utume hela ya hoteli halafu utaridushiwa.  Ni mbinu ya hao matapeli wa Nigeria. Futeni hizo email, mtalizwa.

 ************************************************
For registration information you are to contact the conference Registrar: {hrha registrar@ gmail.com}.

Dear Colleagues,

  I am pleased to invite you to participate on the forth - coming World Conference on Human Rights and HIV/AIDS treatment (HRHA) against Women, Youth & Children.

The International Human Rights and HIV/AIDS treatment (HRHA) against Women, Youth & Children, is scheduled to take place from October 19th – 23th 2015, New York, United States and from October 26th - 30th 2015 in Dakar-Senegal, and other benevolent donors worldwide.

The sponsors of the event will cover the cost of your round-trip air tickets on a direct flight at the most economical fare and we shall provide assistance for your visa arrangement, and your ground transportation from the airport to the conference venue. Hotel accommodation booking costs will be your own responsibility in Dakar Senegal. Please contact the conference secretariat office for more information and registration for participation :{ hrha registrar@ gmail.com}.

Please share the information with your colleagues.

Sincerely

Mrs. Violet Williams,
M.D Human Rights and HIV/AIDS.
Activities Coordinator.

Saturday, August 01, 2015

Ujue Ukubwa wa Shaq!

Shaq O'Neill  na Kelly Ripa
Wadau, mcheza Basketball (mpira wa kikapu) Shaq O'Neal kweli ni jitu!  Ana urfeu wa futi 7. Duh, hapa pichani amesimama  na Kelly Ripa ambaye ni mtangazaji maarufu hapa Marekani.