Saturday, November 24, 2007

Bi Kidude ana miaka mingapi?

Hivi Bi Kidude ana miaka mingapi? Sasa anadai kuwa ana mika 113. Lakini anasema hajui alizaliwa lini. Mimi nilimwona Zanzibar mwaka 1993 na wakati huo alisema ana miaka 80. Kwa hiyo nahisi kama ana miaka 94.

Aliolewa kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1930's. Alikuwa mwanafunzi wa marehemu Siti Binti Saad ambaye alifariki 1950.

Ni Kungwi na mwenyewe kwa mafundisho ya Unyago. Huenda ni kweli wazungu wanavyosema, "sex makes you younger" (yaani ngono inakufanya uwe kijana).

Je, umemwona kwenye show zake. Ngoma zikianza kulia anageuka kijana!

GO BI KIDUDE!

6 comments:

Anonymous said...

Mimi nahisi ana miaka kati ya 83 na 97, na kwa wastani miaka 90. Kama aliolewa miaka ya 1930, yawezekana kabisa aliolewa immediately baada ya kuvunja ungo na kuchezwa, labda akiwa na miaka 15 hivi, au kama alisubiri zaidi labda miaka 20. Kwa hiyo kama aliolewa 1930 inawezekana alizaliwa kati ya 1910 na 1915, na kama aliolewa 1939 alizaliwa kati ya 1919 na 1924. So kwa ujumla alizaliwa kati ya 1910 na 1924, kwa hiyo umri wake ni kati ya miaka 83 na 97. Ukichukua wastani wa umri huu yaani (83+97)/2 utapata miaka 90.

Chemi Che-Mponda said...

Bi Kidude anasema aliolewa akiwa na miaka 13.

Anonymous said...

Chemi awali ulisema Bi Kidude hajui alizaliwa lini hivyo yeye kudai aliolewa akiwa ana umri wa miaka 13 hivyo bado haileti mantinki!

Anonymous said...

Kama aliolewa na miaka hiyo 13 na aliolewa miaka ya 1930s (1930-1939), basi alizaliwa kati ya 1917 na 1926, kwa hiyo umri wake ni kati ya miaka 81 na 90. Wastani wake ni miaka 85.

Anonymous said...

bi kidude ana miaka 58 tuu. bibi yangu ana miaka 61, ana alipokuwa darasa la 4, bi kidude alikuwa la kwanza

Anonymous said...

Anonymous wa 6:32am huyo unayemsema atakuwa ni Bi Kidude mwingine. Bi Kidude aliimba na Siti binti Saad ambaye alifariki 1950.