Tuesday, November 27, 2007

Obama - Nimevuta bangi na kutumia unga!

Mgombea nafasi ya rais wa Marekani kutoka chama cha Democrats, Senator Barack Obama, amekiri kuwa alitumia madawa ya kulevya akiwa kijana.

Akiongea na vijana wa NewHampshire alisema kuwa akiwa anasoma shule ya sekondari alitumia unga aina ya Cocaine na pia alivuta bangi. Alisema kipindi hicho hakufanya vizuri shule na ni sababu ya hayo maovu. Anasema kuwa ana majuto na kipindi kile. Anasema alivyoacha alianza kufanya vizuri shuleni mpaka aliweza kusomea sheria chuo kikuu cha Harvard na kuwa mhariri wa Harvard Law Review.

Si mara ya kwanza kusema kuwa alitumia madawa ya kulevya. Akigombea uSenator alisema, na pia kwenye kitabu chake, ' Dreams from my Father, A story or Race and Inheritance' anasema pia.

Obama si mgombea wa kwanza kukiri kuwa walitumia madawa ya kulevya. Rais Bill Clinton alisema kuwa alijaribu kuvuta bangi, na rais Bush wa sasa anasema alikuwa mlevi wa pombe (bado ni mlevi)! Pia kuna watu ambao wanadai kuwa Bush alitumia unga.

Navyoona Obama aliamua kusema alifanya nini akiwa kijana maana kuna watu wangemwumbua. Aliona ni bora aseme mwenyewe kulikoni aonekane kama alijaribu kuficha. Sasa kuna watu ambao wanadai kuwa Obama si mfano mzuri kwa vijana maana wao wataona kuwa ni sawa kutumia madawa ya kulevya maana baadaye wataweza kugombea urais! Haya!

Hapa Marekani, ukiwa mgombea nafasi ya siasaa hasa hizi kubwa kubwa uwe msafi! Maana yangu si msafi wa nguo au mwili. Uwe msafi kabisa na usiwe na kitu cha kuficha. Viongozi wengi wameabikia baada ya kugundulika walikuwa na vimada pembeni au walitembea na malaya! Usiwe umezaa nje ya ndoa yako! Usiwe unatumia madawa ya kulevya au mlevi.

Watu kama Newt Gingrinch, Henry Hyde, Gary Hart, waliaibika baada ya siri zao na kuwa na vimada kugundulika! Na lazima unakumbuka kuwa Rais Clinton karibu avuliwe urais shauri ya kunyonywa ume wake na Monica Lewinsky ofisini kwake!

Kwa habari zaidi someni:

http://www.cnn.com/2007/POLITICS/11/27/costello.drug.use/index.html

http://www.iht.com/articles/2006/10/24/news/dems.php

http://www.washingtonpost.com/wp-dyn/content/article/2007/01/02/AR2007010201359_pf.html


1 comment:

Anonymous said...

obama looks tired and worn, it seems to the proffesional observer,he is still a junkie