Tuesday, November 13, 2007

Je, Michuzi ni Oprah wa Bongo?
Juzi, nilikuwa naongea na marafiki hapa Boston. Tukawa tunajadili habari za Tanzania kama serikali kuongeza mishahara ya wafanyakazi na madhara yake. Watu wameachishwa kazi shauri ya waajiri kushindwa kulipa mishahara mikubwa. Tuliongea kuhusu wasichana wanaopata mimba shuleni Bongo na kasi ya UKIMWI. Tuliongea kuhusu kuingiza magari Bongo na barabara zilivyojaa magari mpaka yanashindwa kutembea.

Ajabu tulijadili kwa kirefu zaidi kaka Michuzi na blogu yake maarufu ambayo karibu kila MTanzania nje ya nchi ana habari nayo. Tulisema amekuwa kama Oprah hapa Marekani, mtu ambaye watu wanamwamini na wanamtegemea kwa mambo kadhaa. Kuna watu ambao hawana raha mpaka wameona blogu ya Michuzi kama vile watu hawaoni raha mpaka wameona show ya Oprah.

Watu wakitaka habari za Bongo hawaendi kwanza ippmedia.com au site ya Daily News wanakimbilia blogu ya Michuzi. Na sasa kwa vile watu wengi wanasoma blogu ya Michuzi basi watu wanataka habari zao zionekane pale maana wanajua wengi wataziona.

Michuzi akibandika kitu watu wanakimbilia kwenye blogu yake kutoa maoni yao maana wanajua wengi watasoma. Kama kuna msiba watu wanatoa habari pale, pia kama kuna haja ya mchango watu wanatoa habari pale. Juzi tuliona habari ya mtoto mdogo aliyehitaji msaada wa kutengeneza uso. Watu walitoa pesa na ushauri mara moja. Pia Michuzi kaanzisha lugha ya 'Michuzi talk' yaani kuandika kiingereza kwa kiswahili. Wabongo wanaipenda kweli.

Na Michuzi akitoa maoni yake watu wanaona kama ndo sheria. "Michuzi kasema!" Lakini hasa navyoona waBongo wa nje ya nchi wanampenda kwa sababu anatoa picha za nyumbani na kufanya watu wajisikie hawako mbali na nchi yao.

Tulibishana kuhusu habari ya kuwa eti anatoza watu kubandika habari zao kwenye blogu. Ilibidi nimpigie Michuzi kumwuliza. Alisema hiyo habari si kweli. Hatozi hata senti tano kubandika kitu kwenye blogu yake. Alisema wakati mwingine anaweza kupewa kitu kama shukurani lakini hatozi.

Kwa kifupi uhusiano wangu na Michuzi ulianza zamani hata kabla hajawa mpiga picha wa Daily News. Alikuwa ni kijana tu mwenye kamera aliyekuwa anapiga picha za watu wakiwa disko. Msemo wake ulikuwa, " Natafuta michuzi!" Ndo kapewa jina la Michuzi. Tukamshauri awe mpiga picha wa kujitegemea Daily News, yaani freelance. Akawa analeta picha nzuri kuliko hata wapiga picha walioajiriwa pale.

Nakumbuka alivyoajiriwa Daily News mwanzoni wahariri waligoma kumwita Michuzi, wakasema atumie jina la Muhidini Issa. Lakini kila mtu alikuwa anamwita Michuzi na watu wa nje wakawa wanamwita Michuzi, mwisho walikubali aitwe Michuzi. Kwanza ilikuwa kwenye brackets, 'Michuzi'. Mwisho waliachia vizuizi na Michuzi ndo ilikuwa jina lake.

Michuzi ana moyo ya kazi anayofanya. Na kwa wasiojua Michuzi ni mwigizaji mzuri sana.

Karibuni mtoe maoni yenu.

18 comments:

Anonymous said...

HAPANA OPRAH AMESOMA NA HAANDIKI UDAKU!

Anonymous said...

nafikiri ku-post matangazo au maoni kwenye blog ya michuzi ni bure, ila kuna matangazo ya biashara ndio yanaomuingizia "michuzi". Sidhani kama hayo matangazo ya TIGO, TTCL n.k, ambayo yamebandikwa kwenye blog yake ni bure!!

Sina uhakika kama watu wa nyumbani wanamjua michuzi-mfano wale wanoishi mikoani -mikoani kuna mtandao upo lakini sio kila mtu anaweza kusoma blog , sana sana email tu.
Mie nampa hongera Bwana Michuzi kwa kutupa vitu ambavyo magazeti mengine hawawezi kutupa-ZIDUMU FIKRA ZA MICHUZI!!!

Anonymous said...

Mie sitaki kumlinganisha na yeyote maana hata Oprah naye ana matatizo na mapungufu yake kibao. Hata hivyo niseme kuwa michuzi ana tatizo kubwa sana la kuminya maoni ya watu wengi ambao ama watatofautiana naye au watagusa misimamo tofauti na yake au watu ambao wakati fulani anawawakilisha.
Ipo mifano mingi lakini nitaje mmoja tu kuwa Michu aliandika kuwa wana kutwanga na kupepeta eti walinyimwa viza kwenda Rotterdam Holland baada ya onesho lao la UK kumbe baadaye ikaja gundulika kuwa ni ubabe tu wa mwenye bendi Msiilwa alipoona kuwa hakuna masilahi, licha ya matangazo yaliyokuwa yamefanywa na watu wengine wakawa hata wameshajiandaa kutofanya kazi siku hiyo na kusafiri kutoka sehemu mbalimbali kama vile ujerumani na ubelgiji kwenda Uholanzi. Tulipokuwa tunaandika maoni yetu kuomba Msiilwa atoke waziwazi kurekebisha matamshi yake MICHUZI AKAWA ANAKATAA KUCHAPISHA MAONI YETU!!
CHEMI ni bora umheshimu Mwanakijiji kuliko Michuzi hususani katika hali ya kuwa wazi na kuacha hoja ijibiwe kwa hoja!
Pili Michu huwa si makini sana katika kuandika habari. Yaani mara nyingi ama huandika kwa makosa au pasipo kuwa na habari kamili. tunapenda kumwambia kuwa yeye ni mpiga picha bora lakini bado anaendelea kuwa bora mwandishi!

Anonymous said...

Halafu Oprah haiwakilishi CCM. Mie nashangaa kila siku ni Kikwete tu. Kikwete tu as if anafanya kazi nzuri. Jama...yaani watanzania katika mambo tunayohitaji hata hapa Dar ni uwanja wa neshno au kutatua swala na foleni? Mikoani huko tusiseme. Halafu mambo ya BOT huwezi kuyakuta kwa Michuzi. Kama bwana Michu anataka kukomaa, aulize maswali magumu kama hayo. Kupiga picha ni vizuri lakini wakati mwingine unashangaa point ni ipi? Kama siku alipoonyesha mchawi akimla paka - I swear to allah!

Anonymous said...

Michuzi anajitahidi lakini hajamfikia Oprah. Je, amejenga shule wapi? Oprah ana international following Michuzi ana following ya wabongo and wakenya wachache,

Anonymous said...

Nafikiri tukubaliane na Chem kwamba Michuzi ni celebrity kwa wale wanaopenda picha zake, lakini kwa sisi ambao hatumo kwenye huo ushabiki huwezi kutwambia kwamba Michuzi ni celebrity, this applies the same to oprah, kwangu mimi sina time na kipindi cha huyo mama, how are you going to convince me, ofcourse nakubali kwamba ni billionea, I admit on that.

Anonymous said...

Mi naona jamani penye ukweli uongo hujitenga.
Michuzi ametokea kukubalika na walio wengi.
Kazi yake pia inaheshimika.
Alishawahi kufuatilia matatizo ya wizi wa vifurushi au barua posta na posta wakaja kutoa maelezo ya kina. Huyo ni Michuzi wala sio Mkuu wa Mkoa au waziri.
Tukubali tu jamani kuwa mchango wake kijamii unaonekana na kukubalika.

Anonymous said...

Ni kweli anajitahidi kwa mapicha anayopost lakini huwezi kumlinganisha na Oprah. Unachofanya Dada Chemi ni kulinganisha kichuguu na mlima Kilimanjaro! Kama baadhi ya wadau walivyosema Michuzi yuko biased kiasi fulani labda kutokana na kuwa mwajiriwa wa serikali. Nakubali kazi za Mwanakijiji na Mjengwa kwani wanajitahidi kutoa mada 'chokozi'. Michuzi anatakiwa ajirekebishe manake kuna wakati yeye ndo anakuwa center of attraction kwa kupost picha zake kwa wingi badala ya za matukio.

Anonymous said...

Mimi naona kama Michuzi ame REVOLUTINIZE blogu za Tanzania. kuna wabongo kibao wanataka kumwiga.

Anonymous said...

Dada Chemi kama kungekuwa na zawadi ya mwanblogu bora wa Tanzania lazima Michuzi angepata maana yeye ndiye anajulikana sana. Kwa maana hiyo ni sawa kusema yuko sawa na Oprah.

Anonymous said...

Wewe Chemi acha kumtusi Michuzi. Ati wamfananisha na nani?

MICHUZI BLOG said...

Chemi!

U have made me blush. I guess as other contributors have said, to compare me with Oprah is... well, flattering, but frankly speaking I must also admit that I am an anthill against the Oprah mountain. However i thank u and those who have discussed about me which however blunt is a mileage to urs truly. To u and them I say i respect all their suggestions and ideas, but habits die hard and what's good for the goose is bad for the hen. in other words its tough to satisfy all and sundry.

as for urself i admire u both professionally and socially and you are one of my role models in terms of standing up for what u believe in.

lastly, but not least, allow me to say that though i have yet to reach home, but revolutionalising the media in TZ is one of my fundamental resolves. ever since the ICT bug has bitten me i have always strived to send the message home that give the people what they want/need and be fast at it. Gone are the days of waiting to read stale news and i am happy to note that many media houses are edging towards that end

Anonymous said...

We Michuzi mbona huwa unasema kwako English is NOT 'richabo' lakini hapa umetoa ng'enge kama TIME magazine!

Anonymous said...

hey michuzi. Kumbe english is reachable!! safi sana bwana-we chapa mzigo tu , gurudumu la maendeleo unalisogeza polepole.

Anonymous said...

michuzi yupo juu, il akweli hapendi kuandika habari za kiserikali kama haki ngowi, mjengwa yeye kila time anabiga picha zake halafu anaweka kwenye blog ila its ok kwa sababu anatembea sana, ila apige na picha za vijijini sio kila siku za town tuuu, na huwezi kufananisha michuzi na oprah, oprah ana show na michuzi yeye ni mpiga picha tuuu sema blog yakendo imekubalika sana na watu wengi walio nje ya bongo ila wabongo wengi tuuu hajui hii blog hata mimi wakati nipo bongo nilikua sijui hii blog mpaka nilipotoka bongo, nilikua namjua michuzi kaama mpiga picha wa magazeti na pale golini kwake photo point my fair plaza basi

Anonymous said...

We Chem unasubutu kumlinganisha Michuzi Na Oprah? Kifo na usingizi! Safari hii umakosa cha kuandika.

Anonymous said...

michuzi anapenda sana sifa bila mpangilio anapenda kujionyesha sana pia yani kuwa anajua mambo mengi na anapenda sana kujiongelea yeye mwenyewe kwenye blog yake ili watu wamuone babkubwa.Pia michuzi anaboa sana kwa mfano juzi wakati anamhoji richard big bro2 na kulazimisha eti aongelee mambo yake personal na mkewe,yaani nilitamani nimpige jiwe mpaka rich akamshushua,Eti anasema amefanya tresearch ya ndoa ya rch na mkewe kuwa eti walioana haraka bila kujuana sana HIVI HAYO YANAMHUSU NINI???Yeye na Petty Msechu wameishia wapi?????boring ......

Anonymous said...

who is Oprah!! wat is bilionea!!
Chemi mimi niko shinyanga.Hapa kijijini maganzo watu wengi wanatembea na milioni hadi mia mbili kila siku kutokana na shughuli zao za almasi.Lexxus ni nyingi maganzo kuliko dar!!