Thursday, November 29, 2007

Mwalimu Mwingereza afungwa Sudan!

Mwalimu Gillian Gibbons


Macho ya waiingereza yamekuwa Sudan tangu jumapili kwa sababu ya mwalimu kutoka Uiingereza anayefundisha katika shule ya International huko. Mwalimu Gillian Gibbons ana miaka 54. Wanafunzi wake wana miaka saba na lazima bado wako kwenye umri wa kupenda toys (vitu vya kuchezea). Walikuwa na mdoli wa darasa. Aliwapa zoezi la darasa kumpa jina. Wengi walichagua jina Mohamed. Kwa kidemokrasia wengi wanashinda. Hao watoto wa miaka 7 ndo waliochagua jina la Mohamed. Majina mengine yaliyopendekezwa ni Hassan na Abdullah.

Huyo mwalimu namhurumiwa sana. Lazima hakuelewa uiislamu vizuri. Hakuna picha ya mtume Mohamed na wala hakuna sanamu yake. Hivyo kumwita huyo mdoli Mohamed ilikuwa tusi kubwa kwa waislamu. Pia kaanza kufundisha Sudani juzi juzi tu. Kwa wazungu kutoa jina kwa midoli ni kawaida. Sasa anashitakiwa kwa kosa la kutukana uislamu.

Sasa nauliza hivi, hao waSudani hawakuweza kumwelezea kuwa kafanya kosa na kumwelimisha. Baadala yake walitishia kumchapa viboko 40 na kufungwa jela.

Leo mahakama huko wameamuru afungwe siku 15 na awe deported akitoka. Tayari waSudani wanaonekana wabaya duniani kwa kuua raia wao wanye asili ya Afrika hasa kabila la Dinka huko Darfur.

Nawauliza wasomaji waislamu, je, walivyofanya waSudani ni sawa au walizidisha kipimo na hii tukio?

Na hao watoto je, waadhibiwe kwa kuchagua hiyo jina au waelimishwe sheria za uisilamu? Lazima wataathirika maishani mwao wakikumbuka mwalimu wao mpendwa alivyonyanyaswa kwa kosa hiyo.

Hii kesi inasisitiza umuhimu wa watu wanaoenda nchi zingine kuelewa mila na desturi na dini za huko!

Kwa habari zaidi someni:

http://www.cnn.com/2007/WORLD/africa/11/29/sudan.bears/index.html

http://www.abcnews.go.com/International/story?id=3931681&page=1

http://www.cfnews13.com/News/International/2007/11/29/briton_convicted_in_sudan_blasphemy_case.html

12 comments:

Anonymous said...

Ukitaka kupata ukweli kama mwalimu huyu kafanya kosa muulize Mtikila.Mnashangaa hii?????Subirini hiyo mahakama sijui ya Kadhi muone balaa lake.Mtikila oyeeeeeeeeeeeeeeeee

Anonymous said...

This is very sad,

Anonymous said...

Hapa Britain watu wanasema waiislam wamezidi na wazungu wanazidi kuona kama ni dini mbaya. Kwa nini hawa Sudanese hawakumsamehe na kumwambia asirudie. Au angefukuzwa kazi! hii ni too much!

Anonymous said...

Unajua wangekuwa wanatoa foundationc course kwa wageni wa nchi yao kwamba nchi yetu ina sheria hizi, hutakiwi kufanya a,b,c na ukifanya na huku unatambua unlofanya ni kosa basi utaadhibiwa. Je kama watoto waliona huyo mdoli labda wamuenzi mohamed kwa mapenzi yao kwa mtume basi na wanaowaita watoto wao mohamed waadhibiwe au nakosea jamani?

Anonymous said...

Hao wasudani wameongezea maumivu kwenye taswira mbaya ambayo tayari uislamu unayo hapa uingereza. Wamesababisha hiyo dini izidi kuonekana kuwa ni kitu kisichofaa katika jamii iliyostaarabika. Mbona kuna watu wengi tu wanaitwa Mohamed, kwa nini waliowaita hivyo wasiadhibiwe kama ni kweli kuwa Mohamed hafananishwi? Na je hiyo toy ingeitwa Hassan au Abdulla, waislamu wangekubali? Mimi siwaelewi hawa jamaa, ni wapenda fujo tu, wako over-sensitive na vitu visivyokuwa na msingi!

Unknown said...

Mimi ni muislamu na ninafikiri yaliyofanyika ni makosa.Ilipaswa aelimishwe tu.isitoshe si yeye aliyependekeza hilo jina.Upande mwingine watu msiwe bias.Steriotyping is not good.Tayari watu wamehushi hili tukio na suala la Kadhi.Ifahamike kuwa Islam is religion and also ideology kama secularism.Interpretation differs when mixed with culture and way of thinking.When secularism brings injustice like USA war in Iraq,people never generalize this failure.When christians fought each other in Ireland people never generalize christianity.But what i always surprise in why whenever a muslim does something in this part of the world...media and even people`s presentation of the matter reflect islam in general.This is very wrong....Da Chemi na wengine you must understand now that islam is more than just a religion based on the way people define religion.It is rather an ideology with a different kind of interest.JUst like Communism,Socialism,Capitalism,Secularism etc..Its just an orientation of the mind..We are now in Capitalism(Secularism),a system which pollutes the atmosphere(Global warming) and put the whole planet in danger,a system which turn back on poor countries even in disaster period,a system full of injusts,corruptions,Bush-ism,prostitution etc...All these are bad and people know it but people never get bad image when they hear that system....Look at islam now,There are bad people doing things.NOw why would people get bad image when they hear islam?Biasness and stereotype.

Anonymous said...

Ni vyema kujua upande mwingine wa shilingi kabla ya kutuhumu, kwani habari tulizo nazo ni za kumtetea mwalimu, ni sawa kwa hilo, kama kweli alikuwa hajui, je na hawo waliomtia hatiani tutapataje habari zao, ili tuweze kutoa maamuzi yaliyo sahihi,(hizi habari zao ni nadra kuzipata kwa ukweli halisi, lazima zitapotoshwa ili ajenda iitikie wito wake, sijui kwanini).
Vitu vya kujiuliza ni Je ni swala la kidini kweli au kuna mambo mengine ya chuki binafsi (huenda ikawa ajenda ya siri)??
Mara nyingi watu hupenda kuzishutumu dini watu wakitenda mambo yao binafsi, ni heri tukaangalia nini dini inasema na je huyu mtu anayetumia dini kama ngao yake amesimamia kweli kwenye dini au la?
Nashangaa sana mtu wa dini fulani akifanya kosa hutajwa kwa dini yake wakati wengine hawafanyiwi hivyo, utasikia `mtu mwenye dini fulani kafanya kosa kadhaa..'

Anonymous said...

huu ni upuuzi tu-yaani Sudani wana matatizo kibao, nafikiri nguvu zao wangeelekeza kwenye vitu vingine na sio mambo ya midoli.
Watu huwa wanaelimishwa mila na desturi, lakini nani angefikiria maswala ya majina ya midoli??

Anonymous said...

Hapo bwana hakuna udini wala nini, kilichofanyika ni siasa tu. Nchi ya Sudan imeamua kufanya hivi kwa maslagi yake ya kisiasa.

Anonymous said...

Waingereza wenyewe na wazungu wengine wanazungumiza intergration, watu waikubali culture yao na ku-intergrate. Hao watoto ndio wanaojua ukweli kwanini mdoli aliitwa hivyo mpaka wazazi wakaamua kushtaki, sio kila siku waislamu hawana akili lazima kutakuwa na kitu tu kama kawaida ya media iko biased na propaganda zao tangu enzi ya ukomunist sasa ni kuushambulia uislamu.

Huyo mwalimu hakuwa sensitive na dini na culture ya huko alikokwenda! Angepaswa kufahamu hayo kwanza ndio akaenda kufanya kazi huko. Yeye hakujua kuhusu uislamu kwanini asingewaambia watoto wale kuwa kuna Jesus na huu mdoli tuuite Jesus christ! Ni wazi asingeweeza kuuita mdoli jesus christ kwa sababu kama ni mkristo na mapenzi yake kwa jesus asingemwita huyo mdoli jina hilo.

Wazungu wanaita midoli na mbwa na paka majina mbona sijasikia kuna mbwa au paka anaitwa jesus!

Camon dont be biased, ukumbuke yeye ni mwalimu na wale ni watoto wadogo, watoto wamwongoze yeye au yeye kama mwalimu awaongoze watoto?

Halafu nao wapunguze kupeleka tamaduni zao kwa watu ndio maana kunatokea cultural clashes.

Kuna wakati wazungu fulani sitaki kuwataja wawapi walimfanyisha mapenzi msichana wa kitanzania na mbwa, watu walipiga kelele kweli nusu wazungu waliwe nyama, kwa sababu kwa culture ya kwetu hicho kitu hakiwezekani lakini pengine mbwa wao alizoea kufanya mapenzi na hookers wa kwao walikotoka hao wazungu.

Tukirudi kwenye mada ya mdoli Dada Chemi jinsi ulivyoiandika hiyo mada haukuwa neutral tayari majibu umeshatoa uko biased hata kuwauliza waislamu ni changa la macho najua unautaalamu wa uandishi wa habari ni yale yale ya media na islamophobia na mnazidi kuwachanganya watu. Usome uuelewe Uislam. Na ukiusoma na kuuelewa hutakuwa biased wala kuhangaishwa na islamophobia!
Sababu usilolijua ni kama usiku wa kiza na litakusumbua. Mwandishi inabidi awe mtafiti, mada sensitive kama za culture na dini za watu unafanya utafiti japo kidogo ili uilewe concept ya hicho unachotaka kukisema, kwa sababu knowledge is power. Mie sikujibu kuwa uislamu unasemaje kuhusu mtu kuuita mdoli jina la mtume lakini nimetumia common sense nimejiuliza maswali hapo juu kwanini mwalimu hakuuita mdoli jesus christ kwa sababu she knows about jesus but she doesnt know about Mohamed!

Anonymous said...

Kwani Jina "Mohamed" lina Copyright? Kiasi kuwa mtu hawezi ita Paka wake Mohamed akitaka?

Jina kama halina Copyright huwezi mshitaki mtu kuita Doli lake au choo chake Mohamed.

Wakitaka walisajili hilo jina liwe na Copyright kuwa huruhusiwi kulitumia isipokuwa kwa matumizi ya kidini kama wanataka.

Vinginevyo waache upuuzi wa kunyanyasa watu.

Wamwachie huyo mwalimu haraka.Ni uvunjaji wa Sheria.

Anonymous said...

wewe anon November 30, 2007 3:55 PM nilivyoelewa mimi watoto walichagua jina si mwalimu,sasa yepi? ya nini kumwadhibu mwalimu,hao watoto wangekuwa wakristu labda wangechagua jina la Jesus ungesemaje.Mwacheni chemi atoe maoni yake hafanyi kazi dailynews siku hizi ,ana haki ya kutoa maoni yake kama wewe, afterall its her blog.Nimegundua hao wenye mablog wanasemwa sana kama hawatimizi matakwa yenu wachache mnawalipa?