Monday, November 19, 2007

Tanganyika Enzi Za Mjerumani 1885-1918

Mjerumani asema "Tulia niwapige picha!"
Tumetoka mbali!


Hospitali ya Tanga 1914.

Tanga kulikuwa na mapigano makali 1914.
Hao wanawake walifungwa kama watumwa. Sikuweza kupata maelezo ya kisa cha wao kunfungwa na mnyororo.

Ocean Road Hospital ilijengwa na Mjerumani 1897.


Zamani ilikuwa kawaida kwa mabibi zetu kutembea vifua wazi. Hii picha ilipigwa maeneo ya Bukoba" WHITE HUNTER" Waindaji wa kizungu waliua wanyama wengi kweli bila huruma!


Mjerumani alivyowakuta waCHAGGA

Kwa habari zaidi someni:


10 comments:

Anonymous said...

Chemi,

Yaani unagusa penyewe. Unafikiri hawa jeremani wamebadilika? Ni wale wale kwani ufikiri na taswira yao bado ni ya baada ya mkutano haramu wa Berlin.

Wakituona watu wenye ngozi nyeusi, ufikiri, dharau, udhalilishaji na dharau inaruudia pale pale walipotutawala.Ukisikia jeremani amini ni jeremani, hafai

Kinachouma zaidi ni jinsi hawa viongozi wetu "majuha" wanawafwata kuwarudisha eti "wawekezaji". Sina ubaguzi wa rangi, lakini ukikaa na jini ndipo utajua machungu na matamu ya ujini wakedrcddzzv

Anonymous said...

Naona kuna watu una utani nao umeamua kuwadhalilisha. Au umepata bwana wa kijeremani anakupiga mdeki hadi umepagawa! Yaani unasifia wabaguzi wakubwa hawa, kwa lipi? Umenichefua kabisa!

Anonymous said...

Kwenye hiyo picha ya watumwa mbona kuna akina mama ambao wanafanana na akina mama fulani naowafahamu Dar! Au bibi zao hao.

Anonymous said...

Huyo wa pili kutoka kushoto anafana na yule Maimuna wa sokoni Tandika!

Anonymous said...

Chemi umenikumbusha kitu kimoja,hasa hiyo ya bukoba.Hivi tunapolalamika leo kuwa akina dada zetu hapa bongo na kwingineko kuwa wanaiga utamaduni wa kigeni wa kutembea nusu uchi yawezekana si kweli,utamaduni wetu halisi kumbe ni wa kutembea uchi na si nusu uchi kumbe hizi nguo tuvaazo ndio utamaduni wa kigeni haswaaaaa.Kwanza twaficha nini mbona huyu binti Koku wa Bk yuko full mtindi nje nje na hakuna anayeshawishika kumbaka?laiti kama ingekua leooooooo sijui!thumb up chemi from L lete na nyingine...........Ludewa hapa

Anonymous said...

Wewe anoy uliandika "Kwenye hiyo picha ya watumwa mbona kuna akina mama ambao wanafanana na akina mama fulani naowafahamu Dar! Au bibi zao hao."
Lazima wafanane na sisi si kwa sababu ni kizazi chetu. Ukiangalia vizuri wanafanana na wewe na mama yako, "ila nyani haoni kundule". Usiwe na mawazo finyu kama mbu!!!!

Anonymous said...

DAAAAH! SALLLALELEE! WACHAGGA WALIKUWA WANATEMBEA UCHI! LOL!

Anonymous said...

hiyo hospital ya tanga inatwa bombo hospital mpaka leo hilo jengo lipo na huo mti mara ya mwisho naondoka tanga 2002 ulikuwepo hapo hapo, duuu kumbe ni mti wa long time

Anonymous said...

Kweli tungeona matiti kila siku tungeona jambo la kawaida. Hata hiyo nyeti tusingeshutuka!

Anonymous said...

jamani naomba niwatoe ujinga watanzania wanaopenda kubwabwaja bila msingi na wala kufikiria!!

kwanza aliye mtukana dada wa watu kua amepata bwana wa kijerumani ndo maana kaamua kuwasifia... alotamka sifa kwa wajerumani hapo nani?mbona dada chem hajaandika neno hata moja kusifia kitu chochote na wala hakukosoa...ameandika tu maelezo ya picha kua hii imepigwa wapi na mwakagani nk.sasa ulojidai umeguswa sana na kutukana vipi?

na mwingine aliyesema wajerumani ndo walivyo kwa ukatili mpaka sasa...si ukweli,si kua nna unga mkono kwa ukoloni wa kisasa bila kwa kutumia kigezo cha uwekezaji, ila haimaanishi kua wajerumani wasiwe wawekezaji kwakua ni makatili. katili anaweza kua mtu yeyote,wajaluo wakurya na wamasai pia ni makatili...
nna ishi ujerumani kwa miaka mitatu sasa na sijawahi kudharauliwa tena ndo wakikuona wanakuchekea na kukusifia....mara jamani nywele zako nzuri mara ngozi nzuri,hakuna kabisa yale wanayosimuliana watu vijiweni kua wajerumani ni makatili, wao pia ni binadamu wenye ubinadamu kama wengine na kama ilivyo kawaida popote pale panaweza kua na wanaopinga chochote kile kwahivyo wako pia watu wanaoandamana kutaka watu wote wasio wajerumani haijalishi ni weusi au wanjano-waondoke nchini kwao,ila ni wale wale tu wanaotaka kupata pesa za bure bila ya kufanya kazi na wanaona kukiwa na wahamiaji wengi basi serikali inapunguza pesa zao kwa kusaidia wahamiaji...maana wao huku wasipokua na kazi wanapata pesa za bure kutoka serikalini!

kwa kifupi na sisi tujifunze kujituma na kuchunguza vizuri ukweli wa mambo sio kuangia kichwa kichwa tu kua ooh ujerumani makatili siendi au sitaki kua na rafiki wa kijerumani... stori zs vijiweni ni kufurahisha genge hakuna ajiaye zaidi ya mwingine ukizibeba hizo juu juu utapotea...