Tuesday, October 18, 2005

Acheni Ushamba

Acheni Ushamba!

Jamani, jamani, jamani! Siku hizi nikiona vijana waBongo hapa mitaani Boston nakimbia! Hao vijana siyo wale wa miaka ya nyuma waliokuwa tayari kufanya kazi mbili/tatu ili waweze kuishi vizuri na kupeleka zawadi nyumbani. Hapana vijana wa siku hizi wanataka vya dezo! Wamekuja Marekani wakidhania maisha USA ni kama vile kwenye video za Rap. Hapana vijana, maisha siyo hivyo kabisa.

Hapa USA kama hukuja na hela zako basi uwe tayari kuchapa hizo kazi mbili/tatu, utafanikiwa!

Lakini kinacho niudhi hasa ni hao vijana wanaoenda madukani na kuiba, yaani shoplifting! Yaani mtu anaingia dukani anasomba vitu, tia ma-cap kichwani halafu wanatoka nje ya duka. Wanakamatwa halafu unaombwa uwawekee dhamana! Si waliiba wao wacha wakome huko jela! Tena jela za Boston ni nzuri kuliko kupelekwa Keko!
Nasema hao vijana ni washamba maana ukiwauliza kwa nini waliiba, watasema, “Oh, sikujua kama wananiona!” Hawakuoni???? Heh!

Mjue mkifika kwenye mall tena parking lot, mnaanza kuchgunguzwa na makamera yaliofichawa kila mahala isipokuwa chooni! Yale mapambo na magololi yanayoing’inia si urembo tu, bali ni masecurity camera. Hivyo huwezi kusema, “Oh sikuiba!” huko store detective anakutolea kanda ya video ambacho wewe ndo star! Wanaona kwa vile mlango huko wazi hakuna security, au watu wengi basi ni free for all.

Kitu kingine hao vijana,utasikia wanaongea, sijui vitu gani, wakidhania English! Wanajaribu kuiga ma-slang wanaosikia kwenye movies. Nyie! Watu hawaongei hivyo! Ukitaka kazi ya maana ujfinze kuongea English! Yaani inatisha maana huwezi hata kuelewa ansemaje na Slang zake zenye Bongo accent!

Na acheni kuvaa kama gangsta! Kwanza ukikosea rangi utapigwa risasi na ma-gang au utasumbuliwa na polisi wakidhania wewe ni gang banga! Ngojea niishie hapo… maana!

9 comments:

Ndesanjo Macha said...

Ndio dada yetu. Tuelimishane. Karibu.

Mija Shija Sayi said...

Jamani! yaani siku zoooote ambazo nimekuwa nikimsikia Chemi che Mponda akili yangu ilikuwa ikiniambia ni mwanaume, hii ni ya pili, ya kwanza tulikuwa tukibishana juu ya Idya Nkya. Na hii ndio raha ya majina ya kiafrika, si rahisi kwa gaidi kukukamata kirahisi rahisi kwa kutumia Jinsia au dini.

Karibu dadangu.

Chemi Che-Mponda said...

Hi mija shija sayi,

Asante sana kwa kunikaribisha. Ndiyo mimi ni mwanamke. Nakumbuka hata Tanzania watu walikuwa wanashangaa kusikia kuwa ni mwanamke!

Majina ya kiafrika oyee!

Ndesanjo Macha said...

Nakuunga mkono hapo kwenye "Oyeee" ya majina yetu. Tunaweza kuwa masikini kama Benki ya Dunia inavyodai lakini umasikini ni mbaya kiasi hata cha kukosa majina yetu wenyewe?

Innocent Kasyate said...

Magonjwa tunasikia tu kwenye redio.Hapa Uganda serikali imetangaza watu wajiadhari lakini haijachukua hatua yeyote ya maana ambayo inaonekana.
Walaji wa kuku wameambiwa wajihadhari kununua kuku wanaotoka nje.
Yaani Afrika tumekwisha, tuombe Mungu.

Innocent Kasyate said...

Hii mbona inanichekesha, yaani wanatudanganya huku wanaenda soma kumbe wanatutia aibu.
Nafikiri yote hii ni kufeli kwa familia.Wazazi wana kazi ya ziada.

Indya Nkya said...

Chemi Kazi nzuri ongeza kasi tupe visa.

Fikrathabiti said...

Unajua chemi,mimi nawalinganisha na wale watu wanaoamini kutimia kwa usemi wa KIPOFU KAONA MWEZI! show za nini kwa watu??? wakati ndugu zao wanapigika huku bongo land?????

Tunawaonaga pia wakija huku wao ni matanuzi tu kwa kwenda mbele huku wakibofoa american slang kwenye night clubs bila kutafakari ya kesho ni yapi na yatahitaji nini. Kaza buti dada yetu uwatoe kimasomaso na pia utembelee kwenye fikra zangu.BE BLESSED

Anonymous said...

dadangu kiswahili chaku mufti kaabisa ebu waambie matako makubwa oyyyyyyyye waafrika wamebaarikiwa na vitaku vizuri hat ukvaaaaaaa jeans vinapendeza wazungu hawa nikama televishoni ya flatron lg au sio ,,tena maisha ya hapa amerika ni ngumu kama hauna tuhela kwa hivyooo wacheni ushamba ya chokora mimi nafurahia sana article zako im proud of my language kwa maana watu wakija amerikani hujifanya eti hawaelewi lugha sallllaaallle endele hivyo hivyo kiswahili ktukuzwe