Wednesday, August 09, 2006

Meli ya M.V. Liemba



Kuna sinema ambayo itatoka hivi karibuni kuhusu meli ya MV Liemba. Hiyo meli iko Ziwa Tanganyika. Nilishangaa sana kusikia kuwa baada ya miaka yote hii bado inafanya kazi. Yaani imefanya kazi karibu miaka 100!

Kumbe ndo meli iliyotumika kwenye sinema ya The African Queen. Kwa hiyo wacheza sinema wa enzi zile Humphrey Bogart na Katherine Hepburn walipanda.

Kwa habari zaidi someni hapa:

http://www.liemba.org/

Mimi sijawahi kufika Ziwa Tanganyika. Kama umewahi kusafiri na hiyo meli tupeni story basi.

5 comments:

boniphace said...

Tunasubiri hii pia ikataliwe kama Darwin Nightmare! Yaani meli imeishi miaka 100 na bado inachapa mzigo? Hili swali linahitaji ufumbuzi gani zaidi ya kusubiri ajali ya kuua watu elfu wanaoipanda sasa? Tuna kazi na mwenye machio haambiwi tazama.

Chemi Che-Mponda said...

Hi Kaka Boniface,

Meli ilijengwa 1914. Bado ni nzima na inachapa kazi. Walitumia utaalamu gani? Lazima ina HISTORIA, nami nangonjea kwa hamu nisikie.

Lazima ilivyojengwa weusi (waafrika)walipigwa marufuku kupanda. Na je, miaka yote hiyo ilimilikiwa na nani? Living history!

Anonymous said...

Chemi, nilishasahau kabisa kuwa kuna meli inaitwa Liemba. Tovuti ya hawa jamaa ina muziki wa jamaa wa Sisi Tambala ambao ninawazimia sana. Wazo hili la kufanya filamu hii sijui walilipata vipi, ngoja nipite kwenye tovuti yao niwafahamu zaidi.

MzeeMzima said...

Chemi,

Asante sana kwa taarifa yako kuhusu MV Liemba. Mwishoni mwa miaka ya sabini na mwanzoni mwa miaka ya themanini wakati nasoma pale Tabora Boys nilikuwa nakwenda Burundi mara kwa mara kufuata mitumba kwa kupitia meli hii hii ya Liemba; kwa kweli ilikuwa inachapa mzigo vizuri tu,utadhani mpya.

Meli hii kama zilivyokuwa mashine nyingi za zamani ilikuwa overdesigned. Mahala pa mzigo wa kilo moja, wahandisi walitumia chuma cha kubeba kilo kama hamsini hivi. Miaka hiyo, wahandisi walikuwa wakitumia vitu vinaitwa slide rule na log table kukokotoa mahesabu ya design, na kama kawaida hii ilikuwa inaweka rounding error kubwa sana ambayo ilikuwa ikisawazisha kwa kuongeza ukubwa wa chuma kinachotakiwa kwa safety factor kama mara hamsini au zaidi. Wakati huo pia kulikuwa hakuna mashindano ya kibishara kwa hiyo watengenezaji wengi wa mashine walikuwa hawafukuzii kupunguza gharama.

Anonymous said...

Karibuni kuangalia makala ya Liemba kwenye Wikipedia ya Kiswahili. Karibu kuongeza picha au habari zaidi!

Kipala