Saturday, September 09, 2006

Cynthia Masasi - The Original Tanzanian Pin-Up Girl

Nilipokuwa nasoma Tabora Girls niliwahi kumwambia clasasmate wangu kuwa naona kawa, "Popular " sana. Nilisema hivyo kwa vile niliona kila mtu anampenda kuanzia wasichana wa O level na walimu wavulana wa shule zingine. Basi kusema hivyo aliona kama nimemtukana. Kwa kweli nilisema hivyo kwa nia ya kumsifia na siyo nia ya kumkashifu. Na aliona mbaya mapaka tunamaliza Form 6.

Sasa nasema kuwa Cynthia Masasi amekuwa ‘pin-up’ kwa nia ya kumsifia na siyo kumkashifu. Na sijui kama nimekosea kusema kuwa dada Cynthia Masasi ni pin-up girl wa kwanza Mtanzania. (Site yake ni http://www.cynthiamasasi.com) Kwa sasa anaishi Atlanta, Georgia, USA.

Ngoja niwaeleze maana ya ‘pin-up’ girl. Ni mrembo anayekuwa kwenye poster au calendar na mara nyingi mrembo anakuwa kavaa nguo ya kuogelea, mara nyingi bikini. Picha inaitwa pin-up kwa vile unakuwa chomekwa ukutani. Akina Marilyn Monroe na, Jayne Kennedy (mweusi), walikuwa pin-up girls. Na enzi zao nadhani wanajeshi wengi, vijana wa shule waliweka picha zao ukutani na kwenye locker. Na kila wiki gazeti la ‘Jet’ inatoa pin-up girl wa wiki. Wanawake wengi hawakubali iwekwe kwenye sebule zao. Wanaume ndo watakuwa wanunuzi wakuu. Lakini ndo swimsuit kalenda zilivyo. Unazikuta mfano kwenye maklabu ya wanaume, barbershop, vyuoni kwenye bweni za wavulana.

Kama hamjasikia, Cynthia anatoa kalenda enye picha zake akiwa amevaa swimsuit. Kila mwezi na picha yake. Nimesikiliza interview Cynthia aliyofanya na Kaka Deus Gunza wa Pod Radio Butiama huko Columbus, Ohio.

Cynthia anasema alikuwa na copy 5,000 za kalenda yake na zimeisha. Imebidi agize zingine. Nasema ‘Hongera ‘kwa kupendwa hivyo! Kwanza hapa Marekani model wangapi watauza kalenda nyingi hivyo kama si Supermodel au wana-promote kitu kama pombe na sigara.
Modelling una sehemu nyingi mfano kuna runway model, catalog model, store model, kalenda model. Nampongeza Cynthia kwa kuingia katika fani ya modelling, tena ana model akiwa amevaa bikini. Umezua maneno kwa vile watu wanahushisha na umalaya. Kwa mila na desturi za kiTanzania naweza kusema kavunja miiko maana tumefundishwa kujifunika . Lakini nikiona bikini na picha za wanawake huko Swaziland, tena wanaacha matiti na matako nje, nasema bora ya hiyo bikini. Kwa Marekani si wengi wanaweza kuwa na mwili wa model. Na hao supermodel wanajishindisha njaa na kujikondesha mno.

Kwa wapenzi wa rap na MTV, Cynthia ametokea kwenye music video za Nelie, Bow Wow, na Ludacris akiwa kama mcheza densi. Anasema amekuwa kwenye video 15. Kwa mashindano yaliyoko kapiga hatua, maana kwenye audition wanatokea mamia ya wasichana. Kuchaguliwa wakati mwingine ni kama bahati nasibu. Huenda kuna siku tutamwona kwenye fashion show ya Boateng.

Kwa binti zetu wa kiTanzania nasema, fanyeni kama moyo wenu unavyowatuma. Na kama umebarikiwa na mwili wa kuwa model, na unapenda fania hiyo fuatilia. Si lazima uwe swimsuit model, tunaweza kukuona kwenye mafashion show. Nani atakuwa 'pin-up' girl ijayo?

Cynthia atakuwa na Calendar party Chicago, Illinois, September 30th. Atazindua Calendar yake ya 2007.

8 comments:

Anonymous said...

Big up cynthia kaza buti kazi ni nzuri.

Anonymous said...

Yeah ya"ll welcome kwenye uzinduzi wa calender ya cynthia in chicago September 30th...

Chemi Che-Mponda said...

trio kaka,

Ni kweli kabisa kuwa Oprah amekataa hao rappers kuwa kwenye show yake kwa vile anaona kama wananyanyasa wanawake kijinsia. Mimi mwenyewe nimeangalia rap videos chache sana kwa vile naona nyingi zinanyanyasa wanawake na pia wanatumia lugha chafu kwa wanawake. Sikiliza lyrics (meneno ya wimbo). Pia wana - advocate violence against women!

Kwa nini hao rappers waite wanawake b-tch, ho, na maneno mengine machafu? Halafu wanasema watawapiga na hata kuwaua kwenye muziki, huko unaona msichana nusu uchi ana cheza akifurahia.

Je hao rap models wanagegoma kucheza kwenye video hao rappers wangeimba nyimbo chafu?

Anyway, Cynthia amechagua kuingia katika fani hiyo, ni mapenzi yake.
Na hiyo idea yake ya kutoa swimsuit calendar ni 'unique'. Hasa kwa vile market ni wabongo.

Maisha said...

yani macho bado yanauma baada ya kusoma yale maoni kule kwa michuzi.yale matusi jamani sasa ule ndio utamaduni wa kitanzania?tumefundishwa kutukania wenzetu mama zao na kutaja sehemu za watu za siri kama njugumawe?ish!

enewei,mimi kwa mtazamo wangu huyu dada anaweza akafanya chochote anachotaka.hasira za watu wanaomtukana nafikiri ziko misplaced tu.wamepata upenyo wa kutoa chuki zao kwake.basi.wnatumia kigezo cha kutuaibisha watanzania kimakosa kabosa.mangapi tunayaona hapa ya ajabu kupita upeo?ndio maana nimeposti kule nikasema mambo yaliyoko hapa tanzania sasa hivi cynthia ataonekana kama malaika!

kinachonikera mimi ni kauli yake ya kumpelekea rais hiyo calendar.hata kama watanzania sisi wote wachafu kuna sura fulani lazima ziwe in place and mtu yeyote awaye haruhusiwi kutemper nazo.rais ni sura ya nchi.utamaduni halisi wa kitanzania (haijalishi sisi tumeukiuka kiasi gani) unajulikana.kumhusisha rais wa muungano na hizo takataka zake si sawa.

otherwise,cynthia anachukua njia ya kawaida kabisa ambayo aspiring celeb yeyote atachukua.kujipublicize na kujitangaza kwa sababu in that industry ndio jinsi pekee ya kujiweka sambamba na maendeleo ya hiyo sekta.no sin in that!

kwa kifupi im o nobdy's side i guess.ila kila mtu katoa maoni mazuri sana.

once again,nice blog chemi...:)

Maisha said...

trio kaka,mbona hatuwezi kuview blog yako?

Chemi Che-Mponda said...

trio kaka,

I also was wondering about that.

Why don't you post something about yourself in there. It would be nice for people to know a little something about you.

Maisha said...

trio is one of the shy ones...hehehehehehehe!come on now,dont be shy....heh...

Maisha said...

you should.my blog is all about me actually (pat my fro).lol.thats cause i cannot share my everyday mundane things with anybody.so i have found a place to dump them.i also have issues that eat me up that i cant talk abt.it is nice to have strange people i do not know give their honest opinions abt matters that i post.

i like your individual style though.that you registered just to comment.that too is good.you are heard.

so drop by my blog and help fix my dysfunctional mind sometime...:)