Thursday, March 22, 2007

Sinema ya '21'Wapendwa wasomaji, nimepata bahati ya kuwa katika sinema ya '21'. Wahusika wakuu ni Laurence Fishburne na Kevin Spacey. Kwa habari zaidi mnaweza kusoma hapa:

http://www.imdb.com/title/tt0478087/

Naigiza kama mhudumu wa hoteli ya Planet Hollywood. Nitawapa habari zaidi siku nyingine.

7 comments:

ndesanjo said...

Hongera Chemi!

Anonymous said...

Chemi,
hongera sana-sijaona jina lako kwenye hao cast, kwa hiyo nafikiri role yako ni ndogo.
Lakini kwa jinsi ushindani wa kuingia hollywood ulivyo, inabidi tukupongeza kwa role yoyote kubwa na ndogo.

Msalimie sana Kevin Spacey nilipenda sinema yake ya American beuty.

Chemi Che-Mponda said...

Kaka Ndesanao na Anonymous wa 7:15am asanteni sana.

Kwa kweli role yangu ni ndogo na jina itaonekana baadaye kwenye credits za mwisho mimi ni 'extra'.

Anonymous wa 7:15, jana nilikuwa karibu kabisa na huyo Kevin Spacey, ningeweza hata kumgusa, lakini hakunisemesha na tuliamabiwa tusiongee naye unless anaongea na sisi. Eti inaharibu 'moment'. Kama actor Lazima niheshimu hiyo moment. Fishburne alinisalimia lakini siko kwenye scene naye.

Anonymous said...

Dada kemi hongera kwa hatua hii. Siku zote kikubwa huanza na kidogo, ni dalili nzuri hizi. Ongeza juhudi kwa njia zote, lobbying n.k ufike juu zaidi. "The end justifies the means" alisema Niccolo Macchiavelli

Brian Kithuku

Anonymous said...

Hongera sana nadhani huyo director Robert ni yule aliyeongoza sinema ya Monster-In-Law he is good

SIMON KITURURU said...

Hongera!Itafika tu siku role kubwa ndio itakutafuta wewe kama ilivyomdondokea Djimon Hounsou

Anonymous said...

Dada Chemi hongera....u r brave...I remember you while at Warsaw....(Tabora Girls' Secondary School...keep it up....Veronica