Saturday, April 13, 2019

Wehu Wavunja Kaburi ya Marehemu na Kubaka Maiti!

Imani ya Ushirikina (Uchawi) umezidi Tanzania!  Watu wanafukua maiti halafu wanaibaka!  Wana uchu ya pesa na mengine kuweza kufanya hivyo au ni wagonjwa wa akili?  Upumbavu! Mary Mkwaya Malamo alikuwa miaka 35. Alifariki mwanzoni mwa wiki.

*********************************************************************
The Late Mary Mkwaya Malamo

Mwili wa aliyekuwa Afisa wa Wizara ya Nishati Mery Mkwaya Maramo aliyefariki mwanzoni mwa wiki hii na kuzikwa jana katika Makaburi ya Pugu Mwakanga jijini Dar es Salaam, Usiku wa kuamkia leo (Ijumaa) watu wasiojulikana wameufukua na kuutoa nje ya jeneza kisha kuuvua nguo .
Kaka wa Marehemu Mary, Deogratius Maramo amesema inasemekana mwili wa marehemu uliingiliwa kimwili lakini bado wanasubiri ripoti ya Polisi ili wajue kilichomtokea ndugu yao.

Kaka huyo wa marehemu amesema kuwa hakuna kitu chochote kilichoibiwa kaburini humo.!


Kaburi la Marehemu Mary Mkwaya Malamo baada ya kuvunjwa na wachawi


Mnaweza kuangalia Video HAPA:

Maelezo ya Fundi aliyegundua Kaburi Imevunjwa. HAPA

No comments: