Showing posts with label Bernard Madoff. Show all posts
Showing posts with label Bernard Madoff. Show all posts

Monday, June 29, 2009

Tapeli Bernard Madoff Afungwa Miaka 150!


Tapeli Mkuu wa Marekani, Bernard Madoff, amehukumiwa kifungo cha miaka 150 jela. Madoff alitapeli matajiri, vyuo vikuu, mahospitali na wengine zaidi ya dola bilioni 70. Waathirika wote ni wayehudi wenzake. Ilikuwa jambo la fahari kuingia kwenye klabu ya Madoff na kufungua akaunti naye. Kumbe hamna lolote. Pesa za waweka hisa wapya alikuwa anawapa waliokaa siku nyingi. (Ponzi Scheme) Jamaa aliwahi kuwa mkuu wa NASDAQ! Walikuwa wanamwamini kweli. KUMBEEEE!

Asante Madoff kuna waliokuwa matajiri ambao sasa ni makamchape kama sisi. Utasikia huyo alipoteza pesa zake na Madoff, sasa anafanya kazi Walmart, au Starbucks kusudi wapate pesa za chakula cha kawaida tu.

Haya story ya Madoff haijaisha, bado tutaendelea kusikia mengine.

Kwa habari zaidi someni: