Ningependa kuona siku ambao wanawake wa UWT wanasimama imara bila hizi bifu za ajabu ajabu. Mnakumbuka zile bifu za marehemu Sofia Kawawa, Bernadette Kunambi, Mary Kabigi na Esha Stima na wengine. Haziishi na hii ni kizazi kingine!
**************************************************************
Kutoka ippmedia.com
Bifu la Janeth v Sofia: JK kazi anayo!
2008-09-16
Na Job Ndomba, Jijini
Lile bifu kali lililodaiwa kujidhihiri wazi wakati wa kikao kimoja cha chama Jijini Dar baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM mkoani Dar es Salaam, Bi. Janeth Kahama, limeelezewa kuwa ni zito na kwamba linaweza kuwapa kazi ya ziada viongozi wa juu wa chama hicho katika kulimaliza, akiwemo Mwenyekiti wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Jakaya Kikwete.
Kibarua hicho cha ziada katika kutumia busara za uongozi na hatimaye kumaliza kuhasimiana baina ya akina mama hao ambao wana heshima kubwa ndani ya chama, imeelezwa kuwa inatokana na hatua ya mmoja wao kudai kuwa ni lazima atalifikisha suala hilo kwa Mwenyekiti wao wa chama, Rais Jakaya Kikwete.
Wawili hao, wote wamechukua fomu za kuwania uenyekiti wa UWT Taifa.
``Vigogo hawa wa chama ambao wote wanawania uenyekiti wa UWT taifa wanasikitisha sana... kitendo chao cha kugombana waziwazi kitampa kibarua kigumu mwenyekiti na pengine kumpotezea muda wake katika kushughulikia masuala mengine muhimu zaidi ya kukijenga chama na kuliletea maendeleo taifa,`` akasema mmoja wa wajumbe wa UWT aliyekataa kujitaja jina lake.
``Wangeweka kando tofauti zao na kuacha kanuni na taratibu za chama zitwae nafasi badala ya kutaka kuwatwisha mzigo wa kazi ya ziada viongozi wetu... kwakweli akina mama hawa wenye majina makubwa ndani ya chama wanafanya makosa makubwa, kuhasimiana na migogoro ya dhahiri si sehemu ya sifa za kiongozi bora ndani ya CCM,`` amesema mwanachama mwingine wa UWT Jijini.
Bi. Sofia Simba na Bi. Janeth Kahama ambao pia, wote ni wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wameripotiwa wakitupiana maneno makali katika kikao kimoja hivi karibuni na kuzua kasheshe kubwa, huku mmoja akidai kutwangwa na mwenzake hadi kupepesukia kando akitaka kupiga mwereka.
Hata hivyo, wakati soo lao likionekana kuwa kubwa na pengine kuwagawa baadhi ya wanachama wenzao ndani ya UWT, mmoja wao ambaye ni Bi. Janeth Kahama, ameiambia Alasiri leo asubuhi kuwa yeye, anaacha mambo yote kwenye vikao vya juu vya chama.
Bi. Janeth amesema kuwa ugomvi wake na Bi.Simba utapatiwa jibu muafaka ndani ya vikao vya CCM kwakuwa huko, hakuna ambacho huwa kinaharibika.
``Bi. Sofia ni kiongozi mkubwa sana na tunamheshimu, hivyo suala hili (la kudaiwa kupigwa naye) sijaenda kuliripoti polisi, bali nimeufikisha ugomvi huo katika vikao vya chama changu kwa kufuata taratibu na kanuni zilizopo... ninaamini huko kutatolewa maamuzi sahihi,`` akasema Bi. Janeth.
Aidha, licha ya kutokea kadhia hiyo, Bi. Janeth amesema kuwa hivi sasa, chama kiko mbioni kuteua wagombea na hivyo hana haja ya kutoa maelezo kuwa mwenzie Bi. Sophia anafaa kuwa kiongozi au la, na kwamba yeye anamtanguliza mungu kwa kila jambo.
``Mimi siwezi kukomenti kama anafaa au hafai, kwani baraza pekee linaweza kutambua hilo... hivi sasa, karibu baraza linafanya uteuzi wa wagombea,`` akaongeza.
Mwandishi alipojaribu kumsaka Bi. Sofia kwa njia ya simu leo asubuhi hakufanikiwa, lakini amenukuliwa leo hii akisema kuwa naye, yuko tayari kuachia mambo yote kwa viongozi wa juu wa chama kwa ajili ya maamuzi kuhusiana na mgogoro baina yake na Bi. Janeth.
SOURCE: Alasiri