Showing posts with label Bruce Willis. Show all posts
Showing posts with label Bruce Willis. Show all posts

Thursday, June 12, 2008

Sinema - The Surrogates

Huyo farasi naye yumo kwenye sinema
Kwa mbali unaweza kuona maiti (mdoli) juu ya vijiti maalum kabla ya kuchomwa. Nilikuwa kwenye basi nilivyopiga hii picha. Crew walikuwa kwenye mapumziko. Haturuhusiwi kupiga picha kwenye seti. Kwa mbali unaweza kuona makaburi feki.

Wadau, samahani kwa ukimya. Nilikuwa Taunton, MA kwenye shooting ya sinema, The Surrogates. Stelingi wake ni Bruce Willis na Ving Rhames. Mimi niliigiza mle kama Dread yaani binadamu wasiopenda Usurrogate. Ilikuwa poa sana, nilimpita Bruce Willia mara kadhaa kama mpita njia. Kumwona kwa karibu ni mrefu, mwembamba. Ving Rhames si mrefu kama nilivyotegemea lakini ni kibonge. Alicheza kama nabii wa Dreads.

Leo tuliangalia maiti inachomwa. Lakini haikuwa maiti ilukwa mdoli. Lakini ukiona utasema ni mtu huyo. Nakuambia kuna wataalamu wa special effects. Mdoli alichomwa kama wahindi wanavyochoma moto maiti. Walikuwa na zimamoto wa Taunton Fire Department pale kuzima baada ya wao kumaliza kuipiga picha. Nakuambia mdoli alitengenezwa kifundi kiasi kwamba walivyosima moto tuliona fuvu na mifupa!

Nadhani The Surrogates itakuwa sinema kubwa ya summer 2009.

Wednesday, March 12, 2008

Audition yangu leo


Leo nimefanya audition kwa ajili ya sinema mpya, The Surrogates. Stelingi wake ni Bruce Willis. Hadithi yake ni ya Science Fiction.

Role niliofanyia audition ni mama moja mwenye hasira ambaye anamwua character wa Bruce Willis kwa kumpiga risasi kichwani. Ila siye mwenyewe ni kloni yake.
Ilibidi nifanye 'pantomine', yaani kuigiza bila kifaa. Sasa waliniambia nijifanye nimeshika bunduki na naifyatua baada ya kusema line. Hapo ilibidi nikumbuke mazeozi ya SAR (semi-automatic rifle) ya enzi za JKT.
Ilikuwa audition safi sana kwa vile niliambiwa kuchangaya action na maneno. Haya sisi actors tunaambiwa ukifanya audition tegemea hapo ndo mwisho, ukiitwa tena ni bahati wakikuchagua ni kama kushinda bahati nasibu! Haya tuone mambo yatakavyokuwa.

Ila nilifurahi sana kuona waigizaji wengi weusi waliitwa kufanya audition.

Kwa habari zaidi ya sinema, The Surrogates bofya HAPA: