





Hizi ni picha nilizopiga leo asubuhi wakati polisi wanafanya uchunguzi kuhusu hiyo ajali mbaya Central Square iliyomtoa roho mwanafunzi wa chuo kikuu cha Harvard. Alikata roho saa 6 na dakika ishirini mchana. Marehemu ametambulika kama Isaac Meyers, mwenye miaka 28. Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.
Kuna watu ambao wanadai kuwa marehemu alikuwa anasikiliza Ipod yake ajali ilipotokea. Mwingine anasema alikuwa anatazama kuelekea MIT na hakuwa natazama mbele ndo maana alizolewa na matairi ya nyuma ya lori. Dereva wa lori hajafunguliwa mashitaka.
Wadau, hapo jamaa lipogongwa ni pa hatari sana, maana wenye magari mara nyingi hawaheshimu waenda kwa miguu! Dawa wasimamishe magari ndo watu waruhusiwe kupita!
Kwa habari zaidi someni: