Nami nakemea vikali hiyo tabia ya wanaume kujisaidia hapa na pale bila hata kujali nani anapita au watoto watacheza hapo!
*******************************************************************************
DC akoromea Wanaosumbua wenzao kwa Mikesha
2008-04-08
Na Abdul Mitumba, Magomeni
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Jijini, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, ameagiza watu wote wanaokesha wakipiga na kucheza muziki wa rusha roho na aina nyingine za muziki kwa sauti ya juu kiasi cha kuwasumbua wengine wakome kufanya hivyo na kwamba kuanzia sasa wawe wakiburuzwa kortini kwani wanavunja sheria za nchi.
Kadhalika, DC Massawe amechukizwa na tabia ya wanaume wengi kujisaidia aja ndogo kila sehemu akisema ni baadhi ya dalili za kuporomoka kwa maadili miongoni mwa jamii. Bw. Massawe ameyasema hayo wakati wa mkutano wake mmoja na wananchi wa Kata ya Ndugumbi hivi karibuni.
Mkuu huyo amesema sheria za namna watu wanavyoweza kufanya sherehe majumbani mwao na hata zile zinazoelezea utaratibu wa shughuli za starehe ziko wazi na kila mmoja anapaswa kuzifuata. Akasema kamwe hairuhusiwi watu kukesha wakicheza muziki usiku kucha, tena kwa sauti ya juu kiasi cha kuwasumbua wengine.
Mbali na hayo, DC Massawe pia alikemea tabia ya baadhi ya watu wanaotiririsha maji machafu na kinyesi katika mifereji ya mvua. ``Matukio yote hayo ni mwanzo wa matatizo katika jamii. Kupiga muziki usiku kucha katika makazi ya watu ni tatizo linalokemewa kila siku na ninasisitiza kuwa sasa sheria zifuatwe... kujisaidia ovyo mitaani ni aibu nyingine ambayo jamii inapaswa kuikemea ili kujenga kuwa na kizazi kilichostaarabika,`` akasema DC Massawe.
Agizo la Kanali Massawe limekuja kufuatia baadhi ya wananchi kutoa kero mkutanoni hapo, ambapo kero iliyotawala mkutano ni tabia ya baadhi ya watu kukesha wakipiga muziki katika makazi ya watu.
SOURCE: Alasiri