Showing posts with label Crisps. Show all posts
Showing posts with label Crisps. Show all posts

Wednesday, February 25, 2009

Kiwanda cha Crisps (Potato Chips) Bongo

(Picha na Maelezo na picha kutoka Lukwangule Blog)

Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Getrude Mpaka (anayecheka) akiwa ndani ya kiwanda cha Crispo cha Iringa kinachotengeneza viazi vya kutafuna pamoja na Bodi ya wakurugenzi ya DANIDA iliyofadhili kiwanda hicho kupitia mpango wa B2B . Picha hii ni kwa hisani ya Frank Leonard ambaye ana makazi yake kwa watani zangu wala mnyama.
*********************************************************

Haya wapenzi wa crisps/potato chips mtafaidi sasa. Kiwanda cha kutengeneza snacks tamu kimefunguliwa huko Iringa. Frito Lay na Utz mlie tu.Mlioko huko Bongo hebu tuambie ladhaa ikoje. Nina imani zitakuwa tamu sana na zenye 'quality' safi.
Lakini natumani haitakuwa kama kile kiwanda cha SIHA mikate. Wadau mnaoikumbuka. Ilikuwa lazima itumie unga ngano kutoka Canada tu ndo mkate iwe nzuri. Je, hiki kiwanda cha Iringa kinatumia viazi kutoka wapi?