Showing posts with label Food Prices. Show all posts
Showing posts with label Food Prices. Show all posts

Tuesday, August 16, 2011

Unakumbuka SUPA-GHEE?





Wadau, hapo zamani za kale kulikuwa na mafuta ya kupikia Tanzania maarufu yanaitwa SUPA GHEE. Yalikuwa mazuri sana, lakini miaka ya sabini hasa baada ya Vita Vya Kagera, quality ilishuka vibaya mno. Hata hivyo ilikuwa mali kweli kupata SUPA GHEE! Watu walikuwa wanapanga foleni ndefu za makilomita (siyo utani) kuipata. Nyumba zilikuwa zinavunjwa na SUPA GHEE inaibiwa. Supa Ghee ni moja ya bidhaa ambayo wenye uwezo walikuwa wanaunua na mwisho yalikuwa yanuzwa magendo! Mama Mwenye nyumba anatoa kijiko kimoja kwa ajili ya kukaangia mboga halafu yaliyobaki yanafichwa chumbani! Tumetoka mbali wadau. (Picha ya SUPA GHEE kwa hisani ya mdau S.K.)

Thursday, April 24, 2008

Mchele umekuwa Adimu Marekani!


LOH! Haya sasa ni makubwa! Mchele umekuwa adimu Marekani, mpaka maduka yana weka 'limit' ya kiasi ambacho unaweza kununua. Nilikuwa nimesika fununu wiki iliyopita lakini sikutaka kuamini.

Mchele hasa ambao sasa umekuwa haba ni zile Basmati (pishori) na Jasmine (ya kunukia). Sehemu zenye wahindi wengi ndo wanaumia. Hebu fikiria watu wapenda madishi ya wali kama sisi waafrika na wahindi tukianza kukosa! Si itakuwa balaa! haya tuanze kuzoea pasta (spaghetti). Utakuwa kama enzi za mwalimu na miezi 18 (miaka 18). Sidhani kama hali unaweza kuwa mbaya kiasi hicho lakini.

Kwa kweli ni jambo la kushangaza sana kusikia uhaba wa chakula. Hata hivyo ni watu ambao wali ni chakula chao kikuu ndo wanaanza kuona uchungu. Bei umepanda mno. Hata hivyo bei ya vyakula kwa ujumla umepanda.

Yaani nikienda supermarket siku hizi nasikia hata wazungu wanalamika kuhusu bei ya chakula. Bei ya cereals, mikate, mayai, maziwa, nyama umepanda. Pia bei ya petroli umepanda mno . Na mimi nasema ukisikia mzungu analalamika basi unajua kweli hali umekuwa mbaya!

Hayo matatizo ni Asante Bush na vita yake isiyo na maana!

Naomba Obama achaguliwe kuwa raisi!

**********************************************************

Skyrocketing rice prices has Sam's Club limiting sales
4-24-08

(CNN) -- Retail chain Sam's Club will limit the sale of large quantities of rice amid a dramatic increase in the global price of rice.

Sam's Club will limit customers to four 20-lb. bags of jasmine, basmati and long-grain white rice.

The store will limit customers to four 20-lb. bags of jasmine, basmati and long-grain white rice, the company said in a statement. Its restriction mainly will affect businesses that buy rice in bulk, but the company said "a typical Sam's Club Business Member does not buy more than 80 pounds of rice in one visit."

"We currently have plenty of rice for Sam's Club members," the statement said. "This temporary restriction does not apply to retail-sized rice for sale in Sam's or elsewhere at Wal-Mart stores."

The restriction does not apply in Idaho and New Mexico.

Sam's Club -- a division of Wal-Mart Stores Inc. -- has 593 wholesale locations in the United States and more than 100 abroad, in countries such as Brazil, Canada, China and Mexico.
Food prices have soared worldwide in recent months, leading to violence in some developing countries.

"In just two months," World Bank President Robert Zoellick said this month, "rice prices have skyrocketed to near historical levels, rising by around 75 percent globally and more in some markets, with more likely to come."