

Wadau, kuna habari ya kusikitisha kutoka Illinois. Tena imetokea kwenye makaburi ya weusi huko Alsip, Illinois (nje ya Chicago) kwenye Burr Oak Cemetery. Watu wenye roho ya kikatili wenye uchu wa pesa wamefukua makaburi na kutupa maiti walizokuta na kuzitupa ovyo. Kuna habari pia kuwa maiti zingine zilipondwa pondwa ndani ya makabauri waliozikwa na wengine kuzikwa juu yao! Watu walikuwa wanauziwa plot bila kujua yaliyotokea. Yaani huwezi kuamini.
Aliyekuwa anaongoza huu uharibifu wa makaburi na kutupa maiti ni mwanamke, Carolyn Towns (49) kutoka, Chicago. Waliokuwa wanamsaidia wametajwa kuwa ni: Terrence Nicks (39), Keith Nicks (45) na Maurice S. Dailey (59). Wote wamewekwa ndani ka dhamana kubwa $250,000 kila moja. Wakihukumiwa wanaweza kufungwa miaka sita hadi 30. Naona kila moja atafungwa miaka 30! Huo ni ushenzi wa hali ya juu.
Polisi wanasema wamekuta mifupa ya wafu wakiwemo watoto wadogo kabisa zimezagaa sehemu mbalimbali huko makaburini. Markers/Headstones (misalaba) zimepondwa na kutupwa pia. Wanasema walivyokuwa anafukua makaburi hawakujali kitu, wanachukua bulldoza na kuchimba na kutupa walichopata sehemu yoyote enye nafasi! Rev. Jesse Jackson anasema nafasi zinawangojea hao wanne huko motoni!
Wadau, lazima niseme kuwa nimeona ushenzi kama huo Tanzania! Tabora Mjini! Kuna makaburi fulani kwenye njia ya kwenda Isevya. walikuwa wanafukua maiti na kuzitupa na mtu anajenga nyumba hapo makaburi yalipokuwa. Wewe mpita njia unatukana na mifupa ya binadamu njiani.
Wadau, lazima niseme kuwa nimeona ushenzi kama huo Tanzania! Tabora Mjini! Kuna makaburi fulani kwenye njia ya kwenda Isevya. walikuwa wanafukua maiti na kuzitupa na mtu anajenga nyumba hapo makaburi yalipokuwa. Wewe mpita njia unatukana na mifupa ya binadamu njiani.
Na nina wasiwasi Kinondoni cemetery mchezo huo wa kuzika watu juu ya wengine upo. Hayo makaburi yalijaa zamani lakini bado wanaendelea kuzika watu huko. Na kumbuka miaka ya 70 mwisho walipofungua ule sehemu mpya Kinondoni, na penyewe palishajaa.
Kwa habari zaidi someni:
Mnaweza kuona News Conference hapa: