Showing posts with label Hair Weave. Show all posts
Showing posts with label Hair Weave. Show all posts

Friday, February 20, 2009

Weave yaokoa Maisha ya Mwanamke Huko Kansas City!

Wadau, kumbe hizi weave za nywele za akina mama zina faida zake! Huko Kansas City, Missouri mwanamke alipigwa risasi kichwani na boyfriend wake. Huyo jamaa alikuwa na hasira kwa vile walikuwa wameachana hivi karibuni!

Bado sijajua jina la huyo mwanamke ila ana miaka 20. Alienda supermarket na huyo jamaa kamfuata huko na kumpiga risasi kichwani. Kwa bahati risasi haikupenya kichwani shauri ya kukumbana na weave!!!! DUH! Ila dada mwenyewe anasema alisikia joto la risasi. Anasema alitumia hela nyingi kuweka hiyo weave kichwani bora imekuwa na faida kwake! Polisi walivyokuja walikuta risasi imenasa ndani ya weave.

Wazungu wamenichekesha kwenye taarifa ya habari leo. Wanauliza hiyo weave ni nini na inatengenezwa na nini! Je, inatumia gundi au chuma?

Kwa habari zaidi na kuona kideo, bofya chini: