Kutoka Mzee wa Sumo Blog:
Jamani wabongo wezi yaani mshikaji amekaa na laptop anasubiri chinga anayeuza CD anatoa sh 500 anakopy miziki na movies! Kweli kwa jinsi hii wasanii wetu watafika?
*********************************************************
Wadua, hapa Marekani ukikutwa unafanya piracy unapigwa faini ya maelfu ya dola! Wasanii wanatakwa walipwe na kuna sheria za kuwalinda. Bongo bado, wamepiga hatua lakini bado! Naona akina Dr. Remmy wamelipwa residuals, je, wajukuu wao watarithi haki ya kupokea?