Showing posts with label Ibada. Show all posts
Showing posts with label Ibada. Show all posts

Sunday, November 01, 2015

Ibada ya Kumbukumbu ya Marehemu Godfrey Mngodo

Pr. Mwakabonga akiongoza ibada ya kumbukumbu ya marehemu Godfrey Mbiu Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini Marekani na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo wafanyakazi wa kituo cha utangazaji Sauti ya Amerika idhaa ya Kiswahili (VOA). Marehemu Godfrey Mbiu Mngodo aliaga Dunia Tarehe 11 Septemba, 2015 Dar es Salaam na kuzikwa Tanga. Godfrey Mbiu Mngodo amefanya kazi katika sehemu mbalimbali kama Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Voice of America, wizarani na kituo cha Channel Ten ameacha watoto 10 na wajukuu 14. PICHA NA KWANZA PRODUCTION/VIJIMAMBO
Mmoja ya mtoto wa marehemu Michael Mngodo akiwa na mwanae Alvin wakifuatilia ibada ya kumbukumbu ya mpendwa baba yake marehemu Godfrey Mbiu Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini Marekani.
Familia ya Mngodo ikifuatilia Ibada.
Pr. Mwakaboma akifanya maombi kwa wanafamilia.
Michael Mngodo akisoma wasifu wa mpendwa baba yake. Kulia ni mtoto wake Alvin.
Ndugu, jamaa na marafiki wakifuatilia ibada. Kwa Picha zaidi bofya HAPA

Wednesday, October 22, 2014

Ibada ya Kiswahili Ottawa - Ottawa Swahili Fellowship

Wadau, Pastor Edith Mwita, wa Ottawa, Canada anafurahi kuwatangazia kuwa kutakuwa na Ibada ya Kiswahili jumapili hii Oktoba 26th, kuanzia saa 11 hadi saa 1 jioni (5:00pm to 7:00pm) mjini Ottawa.

Anwani ni 36 Bentley Avenue, Ottawa.

Pia, Ibada ya Kiswahili itafanyika kila jumapili ya mwisho wa mwezi.

Wote Mnakaribishwa!