Showing posts with label Indiana Jones. Show all posts
Showing posts with label Indiana Jones. Show all posts

Thursday, October 04, 2007

Steven Spielberg amkomesha Kijana aliyefichua siri ya sinema yake!

Steven Spielberg

Actor/Dancer Tyler Nelson

DOH! Steven Spielberg na George Lucas wana mabilioni ya dola. Lakini walimshitaki kijana wa miaka 24, aliyekuwa extra kwenye sinema yao mpya. Sasa maskini ya mungu huyo Tyler Nelson, atakuwa maskini kupindukia na itabidi aishi kwenye boxi chini ya daraja! Kisa kamwudhi Spielberg. Tyler alikuwa anaigiza kama askari wa kiRusi. Pia anacheza densi.
Spielberg anatengeneza sinema inaitwa, Indiana Jones and the Kingdom of the Crystal Skull . Wafuasi wa sinema za Indiana Jones wanaingojea kwa hamu. Itatoka 2008. Sasa huyo kijana Tyler Nelson, alihojiwa na gazeti la huko kwao, Edmund Oklahoma na kusema alichoona akiwa kwenye seti.

Mkono wa Spielberg ulivyo mrefu na enye vitisho sasa hata hiyo article huwezi kuisoma! Ni hivi kila mtu aliyecahguliwa kuigiza na kufanya kazi kwenye hiyo sinema ilibidi wasaini, "NON-DISCLOSURE Agreement" Yaani wasiseme walichoona. Lakini inaelekea Tyler aliingiwa na Kiwewe na kashindwa kuvumilia maana kuigiza katika sinema ya Hollywood ilikuwa kitu kikubwa mno maishani mwake.

Uko Hollywood kuna watu ambao wanaogopwa na hasa ni hao wenye majina makubwa makubwa. Ukiwa kwenye seti zao ni lazima ufuate masharti waliyoweka. Wakisema "Ukitoka hapa hakuna kusema ulichoona!" ni lazima ufuate waliosema. Navyoona kumshitaki mtu mdogo kama Tyler wanataka iwe fundisho kwa watu wadogo wengine.

Kinchonichukiza ni kuwa Spielberg kasema eti huyo kijana "hata fanya kazi Hollywood tena"
Yaani walishindwa kukata scenes zake au kudai arudishe malipo aliyopata.

Lakini mikosi na hiyo sinema inaendela. Leo wametangaza kuwa vifa akama computer na props zimeibiwa kutoka kwenye set.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.express.co.uk/posts/view/20541/Actor-s-big-mouth-loses-him-his-break-in-Indiana-Jones-IV

http://www.femalefirst.co.uk/entertainment/Steven+Spielberg-41473.html

http://news.scotsman.com/entertainment.cfm?id=1583572007

http://www.digitalspy.co.uk/movies/a76961/indiana-jones-lawsuit-is-settled.html