Received via Email:
Na Mdau Hildegarde Kiwasila
Watu Tanzania hula vibudu anyway wawe wakristu au waislamu. Tunaonaga
kwenye TV na magazeti kuwa baadhi ya kuku wa kizungu au hata wa kienyeji
hufa wanapokuwa wanasafirishwa nao huchinjwa na kuchanganywa na wale
wazima. hata baadhi ya mifugo hufa haitupwi bali utumbo uliooza ndio
hutupwa. Mizoga hiyo huuzwa kwa bei rahisi na ikaingia mahotelini
tukajilamba kuku wa kukaanga, mbuzi etc na supu ya ndizi asubuhi. Wakati
mwingine unaona nyama imebunda inanuka au kuku yupo pink babisa na
harufu mpaka unamwita mtoa huduma na kumrudisha unaona hapana pink
colour na harufu imezidi. Haya-hapa panan udini kweli?
Hawa
watoa huduma wa kupika kwenye sherehe, mahoteli unafikiri vyote
wapikavyo ni vipya halali hakuna haramu? kama ni vipya-haijatokea ukala
ukaharisha? Hebu fika Shoprite na supermarket nyingine ukae nje unapunga
upepo na kuangalia magari na mizifi
Canter na Pickups. utaona ya Hoteli yamekuja kuchukua chakula kilicho
expire kinakwenda kupikwa vyakula vya kisasa mahotelini. Kisa wanunue
ghali wasipate profit. havitupwi hivyo vya supermarket si bongoland hata
Ulaya. Na sote wakristu na waislamu tukiwa ulaya ughaibuni husubiri
mpaka vime-expire muda wake vimeshuka bei sana badala ya $10 kuku kawa $
1 au 0.50 ndio twanunua kwa wingi na anakaa miezi kadhaa january hadi
June katika fridge lako chumbani na unamuangalia kuku daily kwa tabasamu
la kuupiga chenga ukata na umasikini wa kukufanya utembelee wenzako
kudowea kula. Unamla huyo hujui kachinjwaje na ame expire unamuongezea
muda wa kuexpire.
Ukikuta kuku, nyama zilizopita muda wake,
matunda etc wametupa nje ndani ya dustbin la supermarket mnawahi wazungu
na waafrika kuzoa kabla mbwa hazijaja kupindua na kuziharibu. Ombaomba
wa mitaani ndio wanazoa makuku na nyama hizo kichizi. Hata hapa TZ
ukienda maeneo ya kutupa taka-utakuta wachakura
takataka wanaokota nyamba zilizotupwa kule kutoka mazizi ya watu au
machinjioni zinaokotwa na kuingia vilabuni zinapikwa subu. Nyanya
zinaokotwa nan kuingia magengeni.
Ulaya-Wanyama wanachinja kwa
kisu cha umeme kumpa shock mnyama kwanza akazirai kisha kumchinja. Twala
wakristu na waislamu huko vyauzwa supermarket na tupo hai hadi leo. Na
wengi wakimbiao vita vya Boko-haram na vita vinginevyo nchi za kiislamu
(Afghanistan, Iraq, Egypt etc) na nyinginezo zisizo vita wahamiaji
hukimbilia zaidi huko Ulaya na USA kwenye mataifa ambayo ni ya Katiba za
dini za kikristu-mbona hawaogopi kwenda huko kwenye nguruwe na
madhehebu hayo ya kukaba wanyama?
Binadamu wote mahitaji yao
mamoja-Uhuru, Upendo, Amani; kula kushiba, Starehe na haja. Usishangae
kuona kuwa mmewa utoao unga wa kulevya (cocaine) unapandwa na kutumika
na kuuzwa au kupatikana kwa waswalihina sana na wanalinda mashamba yake
kwa mtutu na huku wanasali kwa Mungu wao kila muda
unapofika; wanakosali sana au kusema hivyo kuna maovu kibao ambayo
yatakupa maswali mengi-ubakaji, mauaji ya watu kwa kujilipua; killing
for family honour; mtu wa dini kubaka na kulawiti vichanga au watoto;
kunywa pombe kwa kificho; kubaka watu wazima au wasichana kimtandao na
kuwazika; kuua watoto wako au mwenzi wako ili upate bima etc.
Dini
ni kama OPIUM. Mbona maovu ni mengi tufanyao watu wa dini na wa kusali
sana sasa huko kuchinja ndio kutuletee uzoba mpaka tuuane? Kuna
lililojificha hapa litaonekana tu muda si mrefu!!
Showing posts with label Kuchinja. Show all posts
Showing posts with label Kuchinja. Show all posts
Saturday, April 06, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)