Showing posts with label Nguo ya kuogelea. Show all posts
Showing posts with label Nguo ya kuogelea. Show all posts

Saturday, December 14, 2013

Mimi Katika Sinema American Hustle

Mcheza sinama wa Hollywood, Amy Adams akionyesha nguo yake ya kuogogelea ya kuvutia. Mimi niko nyuma yake.
Wadau, sinema America Hustle inatoka wiki hii. Kama utaenda kuiona hebu tazama hiyo scene inayotokea kwenye party kwenye nyumba ya matajiri enye bwawa ya kuogelea. Mimi niko katika scene hiyo tena nimevaa nguo ya kuogelea. Tulipiga hiyo scene mwezi wa pili kukiwa na theluji na barafu nje!

Waigizaji wenzangu wa hapa Boston tumefurahi sana maana wengi tumepata nafasi kuwa katika hiyo sinema, na wengine hata kubahatika kupata nafai ya kuongea.  Kweli waigizaji wa Boston tunapiga htaua.

Wednesday, July 31, 2013

Mimi Katika Sinema American Hustle

Wadau, mnaweza kuniona nyuma ya mcheza sinema maarufu, Amy Adams katika trela ya sinema mpya American Hustle.  Inatoka mwezi Desemba.  Niliigiza mwezi wa pili mwaka huu. Waliomba wacheza sinema wasio na miili ya stars kujitokeza kwa ajili ya hii scene ya party.  Nilituma picha nimevaa nguo ya kuogelea na wakanichagua. Awali ilikuwa nivae bikini lakini kutokana na urithi wa bibi (matiti makubwa) walishindwa kunipatia nguo iliyofaa.  Sehemu ya chini  ilikaa viuri lakini juu ziilikuwa ndogo hadi matiti yanamwagika!  Basi, wakanipatia hiyo one piece nyeusi na ndo nilivaa.  Ajabu siku tulivopiga sinema nilidhani kuwa sitaonekana hata kidogo.  Pia ilikuwa winter na kulikuwa na theluji na barufu nje!  Leo asubuhi, nilishangaa watu walipoanza kunipigia simu na kunitumia text kuwa wameniona.  Kumbe hiyo sehemu imeongelewa na kuonyeshwa sana kwa vile Amy Adams kavaa nguo ya kuogelea ilitengenezwa kwa mkono kwa mtindo wa macrame.  Katika sinema hiyo naonekana katika scene hii moja tu kwenye bwawa ya kuogelea kwenye nyumba ya tajiri fulani hapa Boston.  Waigizaji wote tulizuiliwa kusema kitu, yaani tumefanya nini na tumeona nini.  Tulisaini agreement za usiri.  Sasa tunaweza kusema.