Showing posts with label Olympics. Show all posts
Showing posts with label Olympics. Show all posts

Saturday, April 19, 2014

WaTanzania Wako Wapi Katika Mbio za Kukimbia Siku Hizi?

Wadau, mnakumbuka majina, Suleiman Nyambui, Juma Ikangaa, Filbert Bayi, Nzael Kyomo,  Walikuwa wanariadha walioshinda katika Marathon na  michezo Olympics.  Walifanya jina la Tanzania ijulikane na isifike! Waliinua jina la Tanzania.  Lakini kwa sasa mbona Tanzania haijawa na mwanariadha anayeweza kushinda  kwa miaka mingi?

Jumatatu kutakuwa na mashindano ya Boston Marathon. Karibu kila mwaka ni MKenya anayeshinda! Kenya ni nchi jirani na sisi, kwa nini Tanzania hatuwezi kushinda? Au tabia ya Party kila wiki na mkao wa kula/bahasha umefanya watu wasijali.

Kwa habari zaidi za KUZOROTA KWA MICHEZO TANZANIA, BOFYA HAPA:

************
Suleiman Nyambui - Alishinda Tuzo ya Fedha (Silver) katika Commonwealth Games huko akiwa amefunga kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhan!  BOFYA HAPA kwa habari zaidi



Suleiman Nyambui akifanya mazoezi Texas, USA
********************

Nzael Kyomo  alishiriki Olympics mwaka 1980 halafu alienda kusoma Marekani.  BOFYA HAPA:


********************

Juma Ikangaa alishinda Marathon nyingi ikiwemo New York Marathon.  Alipata zawadi ya Benzi ambayo serikali ya Tanzania walizuia bandarini kwa zaidi ya mwaka kwa vile Ikangaa hakuweza kuilipia ushuru! Aibu kwa serikali kumnyanyasa shujaa!  BOFYA HAPA:  

Juma Ikangaa katika Boston Marathon 1990

****************************

Filbert Bayi alishinda mashindano ya Olympics na Commonwealth Games.   Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

Filbert Bayi katika mashindano ya Commonwealth 1974

Friday, August 10, 2012

Video za WaTanzania Katika Michezo ya Olimpiki


Hizi linki mbili kuhusu Watanzania  Olimpiki na mataifa mengine hapa London:

Urban Pulse wakishirikiana na Freddy Macha watoa video mbili kuhusiana na michezo ya Olimpiki London 2012. Zote katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza...
1.Ya kwanza inaongelea siku ya kwanza.


2. Ya pili inajaribu kutathmini juma la kwanza; tulivyochemsha na kwa sababu gani:


Habari zaidi tembelea


Friday, August 08, 2008

Timu za Afrika kwenye michezo ya Olympiki

Baadhi ya Timu za Afrika kwenye Ufunguzi wa michezo ya Olympiki, huko Beijing, China leo. TANZANIA
NAMIBIA
IVORY COAST
MISRI


BURUNDI SOUTH AFRICA
SWAZILAND

Kuona picha zaidi: http://sports.yahoo.com/olympics/beijing/gallery

Wednesday, August 06, 2008

Michezo ya Olympiki 2008


Bendera yetu imepandishwa kwenye kijiji cha wanaOlympiki, huko Beijing, China! Mungu Ibariki Tanzania!

Picha kutoka Xinhua News Agency.