Showing posts with label Plastic Surgery. Show all posts
Showing posts with label Plastic Surgery. Show all posts

Saturday, June 27, 2015

Onyo - Sindano Za Kuongeza Saizi ya Makalio!

Wadau, nimewaambia mpende Mwenyezi Mungu alivyowaumba. Acheni huo mtindo wa kujichubua na kutaka matako yako yawe makubwa sana!  Kuna mtindo Afrika sasa ya kutaka  kuongeza saizi ya matako kwa kuchoma sindano.  Sindano zingine na nyingi ni feki na zina sumu kama Fix a Flat ambayo inatumika kama tairi ya gari ikipata pancha. Sasa unalipa hela yako, wahuni wanakuchoma hiyo sindano, siku mbili tatu unatamba na matako yako waliyovimba kama puto halafu baada ya wiki unaona matakao yako yanaoza.  Hebu ona yaliyompata mwenzenu.


Saturday, October 11, 2014

Athari ya Kuchoma Sindano za Kukuza Matako!

Oh hooo, shauri zenu nyie mnaochoma sindano ile matako na matiti yenu yawe makubwa! Mpende Mwenyezi Mungu aliyokuumba!  Ona yaliyompata mwenzenu aliyeenda kuchoma sindano ili matako yake kama maputo! 


Monday, November 12, 2007

Mama yake mzazi Kanye West Amefariki


Kanye West na mama yake, Dr. Donda West

Kuna habari ya kusikitisha na ya kushangaza....mama yake mzazi, mwimba rap, Kanye West, amefariki dunia ghafla siku ya jumamosi.

Mama yake, Dr. Donda West, alikuwa na miaka 58. Habari za kuaminikia zinasema alikufa baada ya kufanyiwa opresheni ya urembo, lakini hawakusema ilikuwa ni opresheni ya aina gani.

Huenda ilikuwa ya kupunguza matiti, matako, uso, liposuction (kupunguza mafuta).

Mama yake alikuwa meneja wake. Alistaafu kazi ya kufundisha kiingereza Chuo Kikuu cha Chicago kusudi awe na mwanae.
Mungu amlaze mahali pema mbinguni. AMEN.

Kwa habari zaidi someni: