Kuelekea kwenye set ya filamu huko Burlington, Massachusetts. Hayo mabango ya njano ya kuelekeza pa kwenda.
Baadhi ya Extras wakisubiri kuitwa kwenye set. Huyo dada alicheza kama karani kwenye ofisi ya Uhamiaji
Hao akina dada nilikaa nao meza moja. Hao wawili weusi ni mamodo (models).
Baada ya kusibiri muda mrefu watu wanaanza kuwa Bored.
Hivi huyo caterer kakosea njia maana Burlington siyo Hollywood na huyo ni caterer wa Hollywood. Ni hivi kwa sasa sinema nyingi zinapigwa Boston hivyo wanaita watu kutoka majimbo mengine kusaidia.
Huyo ni mcheza sinema na mwimbaji Doug Weeks, aliwahi kucheza kama Pilato (Pontius Pilate) kwenye Jesus Christ Superstar ilivyokluwa Broadway.**************************************
Wadau, leo nilibahatika kucheza kama mhamiaji wa kiafrika katika sinema, The Proposal. Stelingi wake ni Sandra Bullock. Bahati mbaya sikumwona kwenye set. Scene ilikuwa kwenye ofisi ya uhamiaji. Nilibahatika kuambiwa niongee kiswahili. Sasa huyo mama ambaye nilikuwa naongea naye alikuwa hajui hata neno moja la kiswahili ilikuwa kichekesho.


