Showing posts with label The New York Post. Show all posts
Showing posts with label The New York Post. Show all posts

Thursday, February 19, 2009

Katuni ya Kibaguzi?


Wadau naomba maoni yenu. Hii katuni ilitoka jana kwenye gazeti la The New York Post. Imechorwa na msanii Sean Delonas. Viongozi wa weusi Marekani wanasema kuwa hii katuni ni ya kibaguzi na kuwa jamaa anataka Rais Obama auliwe! Bwana Delonas anakataa tena anacheka huko akisema kuwa alikuwa na maana ya kesi ya yule nyani aliyeuawawa huko Connecticut juzi.
Nampinga kwa sababu, polisi anasema "itabidi wamtafute mtu mwingine kuandika stimulus bill". Aliyeandika stimulus bill ya sasa ni Rais Obama na siyo nyani. Hapa Marekani tangu zamani watu weusi wanafananishwa na manyani. Hata kwenye kampeni wabaguzi walikuwa na sanamu za nyani na kusema ni Obama. Na yule nyani wa Connecticut alihusika nini na stimulus bill?
Wadau, Marekani ina rais mweusi lakini ubaguzi bado upo!
Soma maoni ya Roland Martin wa CNN juu ya hii katuni HAPA: