Showing posts with label Twilight. Show all posts
Showing posts with label Twilight. Show all posts

Thursday, March 26, 2009

Jamaa Ananuka!


Robert Pattinson

Jamani, leo asubuhi nimeshangaa sana nilipofunga TV na kusikia watangazaji wakisema kuwa, mcheza sinema, Robert Pattinson' ananuka! Tena walisisitiza kuwa jamaa ananuka vibaya sana. Wanasema haogi na haoshi nywele zake. Je, anapiga mswaki? Pattinson anaigiza kama mnyonya damu (vampire) kwenye sinema, Twilight. Yaani wakawa wanamsema vibaya na hata kumwita 'skunk' (mnyama ananuka huyo). Yaani kunuka kwa mtu ni habari! Kweli ilikuwa slow news day.

Halafu cha kuchekesha huyo Pattinson aliwahi kulalamika kuwa alivyokuwa Marekani alishindwa kumpata bibi ingawa ni mzuri na anaongea na lahaja ya Uingereza. Labda angekuwa msafi angefanikiwa. Anavyopendwa na wasichana hapa Marekani ni balaa. Ila wakiisikiahiyo harufu mapenzi yatapungua. Unasikia kwenye TV msichana anasema, "nikikutana na jamaa na ananuka....kwa heri!"

Waliosoma historia wanajua kuwa hapo zamani za kale wazungu walikuwa na tabia mbaya ya kutokuoga. Walishangaa walipoenda sehemu mbalimbali duniani na kukuta watu wanaoga mara kwa mara. Inadaiwa kuwa Malkia Elizabeth wa kwanza alikuwa anaoga mara moja kwa mwezi na hivyo walimwona msafi mno. Walisema kuwa kunuka ni jambo la kawaida na kuwa na uchafu mwilini ni vizuri maana ni kinga dhidi ya magonjwa, huko waafrika wanajitahidi kuoga kila siku. Nani mshenzi?

Kwa kweli hapa Marekani, kuwa na (Body odor/B.O.) ni mwiko. Or course watu kuna watu ambao wananuka, na mtu unaweza kufukuzwa kazi ukienda na kikwapa. Watakuambia hizo deodorants, shampoo na sabuni zina kazi gani! Hebu tumia! Matokeo yake pua zetu hapa Marekani zimekoshwa (sanitized). Yaani ukisikia kikwapa unaona balaa. Mara nyingi unakuta ni hao ombaomba na wasio na makazi (homeless) ndo wanakuwa wachafu.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.trendhunter.com/slideshow/robert-pattisons-body-odor-problem

http://www.mtv.com/news/articles/1607791/20090326/story.jhtml

http://www.suntimes.com/entertainment/zwecker/1496176,CST-FTR-zp26.article