Showing posts with label Urinals. Show all posts
Showing posts with label Urinals. Show all posts

Tuesday, July 01, 2008

Akamatwa kwa kunywa mikojo ya vijana!


Kweli kuna watu wenye ugonjwa wa akili duniani. Kuna habari kutoka Dublin, Ohio kuwa baba fulani wa kizungu amekamatwa kwa kosa la kukinga na kunywa mikojo ya vijana. Alan Patton (56) anadai kuwa eti akinywa mikojo ya vijana anaona raha na inafanya ajiskie kijana!

Alikuwa na tabia ya kwenda kwenye vyoo na kufunga urinals (Vyoo maalum vya kukojolea wanaume) halafu anaomba vijana wakojoe ndani ya vikombe vya plastiki au ndoo halafu anaenda kunywa.

Polisi wanasema kuwa wakati mwingine alikuwa anakusanya mkojo kutoka watu 15 kwa siku! kwa sasa yuko nje kwa dhamana. Kesi yake itasikilizwa huko Ohio, Julai 15.

Mnaweza kuona kideo hapa:

http://www.cnn.com/video/#/video/us/2008/07/01/landers.ohio.urine.collector.wbns?iref=mpvideosview

Kwa habari zaidi someni:

http://www.local6.com/news/16757994/detail.html

http://www.10tv.com/live/content/local/stories/2008/06/30/patton.html?sid=102