ASANTE SANA RAIS WETU MPENDWA JAKAYA KIKWETE!
*************************************************
Kutoka ippmedia.com
Serikali yaondoa ushuru wa Kamera
Na Mwandishi wetu
12th June 2009
Serikali imeondoa ushuru wa forodha kwenye kamera maalum za kupiga picha za filamu ili kuhamasisha sekta ya filamu kwa nia ya kuongeza ajira na kipato kwa vijana hapa nchini.
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustapha Mkullo wakati akisoma bungeni mjini Dodoma bajeti ya mwaka 2008 na 2009. Kwa mujibu wa Mkullo, kamera hizo zilizofutiwa ushuru ni zile maalum za kupiga picha za filamu zinazotambuliwa chini ya HS Codes 8525.80.00.
Hatua hiyo ya Serikali ya kuondoa ushuru imekuja baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Mrisho Kikwete kukutana na watengenezaji na wacheza filamu wa Hollywood wakati alipotembelea Marekani kwa ziara ya kikazi.
Sekta ya filamu hapa nchini imekuwa ikipanda chati kwa haraka sana, ambapo vijana wengi wamekuwa wakijihusisha na shughuli za uchezaji na utengenezaji wa filamu mbalimbali.
Hatua hiyo ya Serikali itasaidia wawekezaji kuja nchini kuwekeza katika sekta hiyo kama sekta nyingine na kuinua fani hiyo ambayo ilikuwa chini sana.
Showing posts with label Ushuru. Show all posts
Showing posts with label Ushuru. Show all posts
Friday, June 12, 2009
Subscribe to:
Posts (Atom)