Showing posts with label Ze Utamu. Show all posts
Showing posts with label Ze Utamu. Show all posts

Monday, June 22, 2009

Habari zaidi za Ze Utamu Kukamatwa

Haya, naona karibu tutasikia rasmi jina la aliyekamatwa. Na kweli huwezi kumchokoza mkuu wa nchi.

***************************************************************
Kutoka ippmedia.com

How `Ze Utamu` host was nabbed

Na Staff writer

21st June 2009

He rose suddenly from the IT World, conquering the corridors of celebrities in Tanzania due to his ability to post damning pictures online with some of these pictures showing celebs and politicians naked, before he was nabbed this week in Essex, UK.

The man behind the reckless website that has highly damaged the reputation of over 6,000 Tanzanians including the head of state was arrested in a well planned move coordinated by the Tanzania intelligence community and their counterparts from UK and Israel, The Guardian on Sunday has learnt.

According to the well placed sources within the Interpol, just a few days after the report that damning cropped pictures purportedly showing the head of state were posted online, the intelligence communities tasked its IT experts to track down the culprit behind the defamatory website.

To nab the host of the website, local IT experts from the intelligence communities contracted their counterparts from Israel who helped tracing the real host and author of the popular website known as ‘www.zeutamu.com’.

After conducting a thorough investigation to various local Internet Service Providers, it was concluded that the server that host the website originated in the United Kingdom.

This, according to sources, was reached after analysing over one hundred posts posted in the website whereby their origins finally showed the country’s code used in hosting internet services.

Following that link, local IT experts from Intelligence Communities contacted their counterparts in UK mainly from MI5, in order to establish the person behind the website.

The investigation within UK was conducted by experts whereby finally the real suspect behind the website was located after his Internet Service Provider was identified.

The ISP provider was interrogated thoroughly and finally the experts established the real identity of the man whose website has defamed and offended a total of 6,080 prominent Tanzanians, including politicians, celebrities and others.

The dramatic move by the local intelligence communities is the first to be done in East Africa in cracking down online crimes, sending an alarming message to the growing number of bloggers inside and outside the country.

Perhaps the most disturbing question is that the man behind this damning website is a highly trained IT expert who was educated by taxpayers’ money and has a link to some of the prominent political figures in the country.

The investigators are still conducting thorough investigations to establish other local suspects who have been collaborating with the blogger to post damning and defamatory pictures online during the past few months.

After concluding their findings, the investigators tipped Interpol as required by international law in order to arrest the suspect.

Interpol working on the tips from intelligence officials raided the home of the suspect early this week in Essex, UK, and arrested the suspect who is a Tanzanian national.

The Tanzanian national aged 39 years old is an expert in IT with strong command in both written and oral English, Chinese and Swahili languages.


When you rattle the snake get prepared for its reactions…You can’t mess around with people including the head of state and expect to walk freely, ” a senior official from the Interpol told The Guardian on Sunday under conditions of anonymity.

CHANZO: GUARDIAN ON SUNDAY

*********************************************
Mmiliki wa ze utamu adaiwa kukamatwa

Kutoka ippmedia.com

20th June 2009

Mtandao wa Ze utamu ambao mmiliki wake anasakwa kwaudi na uvumba.
Kuna habari kwamba Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) wamefanikiwa kumnasa mtu anayedaiwa kumiliki blog ya Ze Utamu ambayo imekuwa ikionyesha picha za kuwadhalilisha watu.

Miongoni mwa udhalilishaji huo ni kuwaonyesha watu wakiwa katika utupu na wengine wakifanya vitendo vya ngono.

Habari ambazo Nipashe ilizipata jana kutoka vyanzo mbalimbali, zilieleza kuwa aliyekamatwa ni raia mmoja wa Uingereza ambaye ana asili ya Tanzania.

Mmiliki huyo anadaiwa kuwa ni mtoto wa kiongozi mwandamizi mstaafu aliyewahi kuitumikia nchi katika nyadhifa kubwa, lakini ana uraia wa Uingereza. Kutokana na sababu za kimaadili hatuwezi kutaja jina lake kwa sasa, hadi vyombo vya usalama vitakapothibitisha.

Kijana huyo anatuhumiwa kwa kuendesha mtandao wa Ze Utamu, ambao umekuwa ukionyesha picha mbalimbali na hasa za watu maarufu, wakiwemo viongozi waandamizi serikalini wakifanya ngono.

Nyingi ya picha hizo na hasa za viongozi zimekuwa zighushiwa (doctored) ili kuwaonyesha kuwa wanafanya vitendo vya aibu kwa nia ya kuwadhalilisha.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, alipoulizwa kukamatwa kwa mtu huyo nchini Uingereza, alisema kuwa ofisi yake haina taarifa kuhusu kukamatwa kwake.

"Ndugu mwandishi, suala la kushikiliwa mtu huyo ofisi yangu haina taarifa hizo, na pia habari kuhusu mtandao huo sizijui kabisa," alisema Manumba.

Mwishoni mwa Aprili, mwaka huu, Manumba alitangaza kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa wanaendesha msako mkali dhidi ya wamiliki na watu wanaoendesha mtandao wa Ze Utamu.

Na ilipofika Mei 5, mwaka huu, Manumba alimwambia mwandishi wa Nipashe kuwa uchunguzi wa kuwanasa watu hao umefikia patamu.

Nipashe ilipowasiliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, ili kuthibitisha taarifa za kukamatwa kwa mmiliki huyo, askari mmoja aliyejitambulisha kuwa ni msaidizi wake, Joshua Mwangasa, alipokea simu ya IGP Mwema na kueleza kuwa yupo kwenye kikao, lakini akasema kuwa taarifa kuhusu blog ya Ze Utamu itatolewa wakati wo wote kama zipo.

Alipotakiwa kueleza taarifa hizo zitatolewa lini, Mwangasa alishindwa kuweka bayana suala hilo. Hata hivyo, alipoulizwa kama ni kweli wanamshikilia mmiliki huyo, Mwangasa alisema hana jibu hilo na akamtaka Mwandishi Wetu awasiliane na DCI Manumba.

Mwandishi alipomueleza kuwa tayari alishampiga simu DCI Manumba na majibu aliyotoa, Mwangasa alisema kama taarifa hizo kama zipo zitatolewa.

"Mwandishi kama taarifa hizo zipo, zitatolewa wakati wowote ila siwezi kudhibitisha kama anashikiliwa au zitatolewa lini," alisema.

Habari zilizopatikana kuhusu mmiliki huyo, zinaeleza kwamba ni mtaalamu wa kompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza, Kiswahili na Kichina na ana makazi katika mji wa Essex nchini Uingereza.

Taarifa zilieleza kuwa wataalamu wa Idara ya Upelelezi kutoka Tanzania wakishirikiana na wenzao wa Uingereza, walifanikiwa kuonana na mmiliki wa blog hiyo na kupata ushahidi wa kutosha kwamba ndiye alikuwa mmiliki wake.

Habari hiyo ilidai kuwa Idara ya Upelelezi na Polisi wa Uingereza wameutaarifu Ubalozi wa Tanzania mjini London kuhusu suala hilo, ambapo baadhi ya maofisa wa ubalozi huo, Clement Kiondo na Amos Msanjila wanadaiwa kwenye taarifa zilizozagaa kwamba walifahamishwa kuhusu mmiliki huyo.

Nipashe pia ilifanya jitihada za kuwasiliana na ofisi ya ubalozi Tanzania London, Uingereza, ambako ofisa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Kombo akidai ni Katibu wa Balozi wa Tanzania nchini humo, Mwanaidi Sinare Maajar, alisema ubalozi huo hauna taarifa ya kukamatwa kwa mmiliki huyo.

Kondo alisema Balozi Maajar alikuwa akihudhuria mkutano na maafisa wengine, lakini alithibitisha kwamba hakuna taarifa za kukamatwa kwa mmiliki huyo ambaye anadaiwa kwamba tayari amekwisharejeshwa nchini ili kujibu tuhuma za kuendesha mtandao unaowadhalilidha watu.

Imefahamika kwamba kuna malalamiko 6,850 yaliyoandikishwa juu udhalilishwaji wa watu uliokuwa ukifanywa na mtandao huo.

Mtandao huo ulisimamishwa mwanzoni mwa Februari, mwaka huu kwa maombi ya serikali ya Tanzania baada ya kutoa picha ya kumdhalilisha kiongozi mmoja mwandamizi wa serikali.

Ufuatiliaji uliofanywa baada ya picha hiyo ndio unaosemekana kufanikisha kukamatwa kwa mmiliki huyo.

Taarifa zaidi zinasema kwamba Polisi wa upelelezi wamewahojiWatanzania wengine wawili katika miji ya Wichita na San Diego nchini Marekani, ambao pia wanahusishwa na mtandao huo.

Friday, June 19, 2009

Tanzanian Blogger Faces Jail Term

Wadau, nitarudisha ile posti ya Ze Utamu Blogger kudakwa, mara ikithibitishwa kuwa ni kweli. Kama nilivyosema, nilitumiwa hiyo habari kwenye e-mail. Baada ya kuitazama vizuri zikuona 'accredited source'. Kwa sasa hebu ona macho yalivyo kwetu na hiyo suala ya Ze Utamu.

Ila kama ni kweli kuwa jamaa wa Ze Utamu wamekamatwa basi lazima niseme, serikali wamefanya kazi. Ila nachosikitika ni kuwa ilibidi wakubwa wadhalilishwe ndo hatua ichukuliwe. Inanikumbusha kesi ya Mzee Punch, huko UDSM mwaka 1987. Punch alizimwa baada ya kumchora Mzee Ruksa na Mzee Kawawa!

Mnaweza kusoma habari na maoni zaidi Jamii Forums:

http://www.jamiiforums.com/habari-hoja-mchanganyiko/31691-ze-utamu-blogger-under-arrest.html

***************************************************************
Tanzanian blogger faces jail term over manipulated photographic images

posted by J. Nambiza Tungaraza on Jun 04, 2009 categories:

The Nairobi Chronicle reports that a Tanzanian blogger faces jail after publishing manipulated photographic images depicting Tanzania’s President Jakaya Kikwete engaging in lewd sex acts.
According to Habari Leo , a Tanzanian newspaper[sw] the country’s police are seeking help from Interpol in tracing the owners and publishers of the blog.

Ze utamu (www.zeutamu.com), probably Tanzania's most controversial blog, came to the limelight by publishing a mixture of Tanzanian Diaspora gossip, nude and sex photographs of well known people as well as name-and-shaming articles. While it attracted many readers, the blog has also attracted criticism.

Some bloggers are of the opinion that the authorities did not care when posts about ordinary citizens were posted at ze utamu. A comment from a blog post at Watanzania Oslo blog that posted the Habari Leo article about the police hunt for ze utamu blog owners says:

Mtandao huu wa ze utamu umkuwepo kwa muda mrefu sana na watu wengi wasio na hatia (raia wa kawaida) wamedhalilishwa sana kupitia mtandao huo kwa picha zao kuwekwa bila ridhaa yao. nyingi ya hizo picha ni za utupu na hata zile ambazo siyo za utupu ziliwekwa bila ridhaa ya wahusika. hivi kuwekwa picha ya rais Kikwete ndo kile chombo kinachojifanya cha usalama kinakurupuka kuwasaka wenye mtandao? […]unafiki mkubwa na ufisadi aina nyingine huu. kudhalilishwa ni kudhalilishwa, ama iwe ni raia tu, kiongozi wa kawaida na hata rais.

Ze utamu has been around for a long time and many innocent people (average/normal citizens) have been shamed through this site when their photographs were posted without their consent. Most of them are nude photographs and even those that are not were posted without consent. Is it true that only by posting the president’s photos has prompted that institution that claims to be the security and regulatory body to jump and pretend to search for the site owners? […] this is hypocrisy, degrading people means degrading people, be they ordinary citizens, leaders or even the president.

That point was also raised by Happy Katabazi :
… wiki hii katika mtandao wa www.zeutamu.com mtandao ambao umejipambanua kwa ajili ya kupachika picha za utupu za watu wa kada zote na wanaotembelea mtandao huo huchangia mawazo yanayohusu maisha binafsi ya faragha za watu…Na wakati mtandao huo ukiendelea kujipambanua mamlaka husika zimekuwa zikiukenulia meno mtandao huu hadi wiki hii ulipotundika picha ya kumdhalilisha rais wetu, ndipo mtandao huo umedhibitiwa kwani hivi sasa hata ukiufungua haufunguki.

… www.zeutamu.com site, a blog that has become popular by posting nude pictures of people from all walks of life while those who visit the site give opinions about people's private lives…And while the site became more popular, authorities [have been done little] until this week when they posted a degrading photograph of our president, and now the site is under control, even when you click the page won't open.

During the heyday of ze utamu some bloggers started campaigns to stop the blog, like the Anti-utamu [sw].

As the police search continues and despite having many readers before its disappearance, bloggers and readers who have openly come out to support Ze Utamu owners can hardly be found - at least at the time of writing this post.

http://advocacy.globalvoicesonline.org/2009/06/04/tanzanian-blogger-faces-jail-term-over-manipulated-photographic-images/

Thursday, June 18, 2009

Ze Utamu Umetufundisha Nini?

Dr. Masangu Matondo Nzuzullima


ZE UTAMU IMETUFUNDISHA NINI?

Dkt. Masangu Matondo Nzuzullima

Alhamisi tarehe 23/4/2009 rafiki yangu mmoja kutoka Dar es salaam alinitumia barua pepe ya kushangaza. Alikuwa analalamika kuhusu tovuti moja iliyokuwa ikiitwa Ze Utamu. Alisema kwamba tovuti hiyo mashuhuri sana ilikuwa ni tovuti ya hatari na ilikuwa imesababisha madhara makubwa katika jamii. Katika barua pepe hiyo alisema kwamba watu Dar es salaam walikuwa hawalali kwani hawakujua kama kesho yake wangejikuta wametamuishwa (kutundikwa katika Ze utamu) ama la. Kwa ujumla mambo hayakuwa shwari. Aliendelea kushangaa ni kwa nini serikali ilikuwa imeiachia tovuti kama hiyo kuendelea kuchafua amani na utangamano wa wanajamii.

Siku hiyo hiyo, gazeti la Majira lilikuwa na makala yenye kichwa cha habari "Waendesha mtandao Ze Utamu wasakwa, Ni baada ya kuwadhalilisha viongozi". Habari hizi pacha zilinitatanisha na kuniachia maswali mengi. Je, hii Ze Utamu ilikuwa ni tovuti ya aina gani na ilikuwa inaandika habari zipi mpaka kulisukuma jeshi la polisi kuacha shughuli zake muhimu za ulinzi wa raia na kuanza kuwasaka wamiliki wake? Niliikumbuka Jambo Forum ambayo nayo katika kilele chake ilileta kizaazaa mpaka wamiliki wake wakakamatwa na jeshi la polisi. Bila kupoteza muda nilikimbilia kwenye google na baada ya sekunde chache tu niliweza kuipata hiyo Ze Utamu. Nilichokiona kilinishangaza kwani sikujua kama Tanzania tulikuwa tumepiga hatua kubwa namna ile katika uhuru wa vyombo vya habari. Japo mitandao ya udaku imezoeleka sana katika nchi za Magharibi ambako kusema kweli hakuna mtu anayeshangazwa nayo tena, Ze Utamu kidogo ilikuwa tofauti. Hata huku kwa wazungu, sijawahi kuona mtandao ambao lengo lake ni kutukanana na kuchafuliana majina na hadhi. Kinyume na mitandao iliyotangulia kama vile Jambo Forum ambayo ilijikita zaidi kushambulia tabaka fulani la watu katika jamii, Ze Utamu yeye alikuwa hachagui tabaka la mtu wala nafasi na hadhi yake katika jamii – si matajiri, si masikini, si wanawake, si wanaume, si wazee, si vijana, si viongozi, si waongozwaji, si mafisadi, si wasafi – kila mtu alikuwa sawa mbele yake. Kinyume na nchi za Kimagharibi, mitandao na magazeti ya udaku huwa hayatiliwi maanani sana na wasomaji; na mara nyingi hakuna anayejihangaisha na kutaka kuthibitisha habari yanayoziandika. Gazeti la udaku la Globe kwa mfano limekuwa likiandika mara kwa mara habari zinazodai kwamba Obama ni shoga na kwamba aliwahi kuwa na mpenzi mwanamme wakati akiwa bado seneta (tazama www.matondo.blogspot.com). Kila mtu anajua kwamba habari hizi ni za uwongo na hakuna anayezijali wala kuzitilia maanani hapa Marekani. Hii ndiyo tofauti kubwa na nyumbani ambako watu bado wanadhani kwamba kila kitu kinachoandikwa katika magazeti au katika mtandao basi ni cha ukweli. Kama hili lingeeleweka, tovuti kama Ze Utamu isingeweza kuwa mashuhuri na kufikia hatua ya kuwanyima watu usingizi.

Ze Utamu ilikuwa nini?

Kimsingi, inavyoonekana Ze Utamu ilikuwa ni tovuti ambayo (kama walivyodai waendeshaji wake) ilikuwa na lengo la kurekebisha tabia za wanajamii wote bila kujali nafasi zao. Lengo lake kuu lilikuwa ni kupambana na ufisadi - ukiwemo ule wa ngono - na matendo yote machafu yaliyoonekana kukiuka maadili ya jamii yanayotendwa na mtu ye yote katika jamii bila kujali tabaka lake.

Kama tovuti hii ingemakinikia lengo lake hili, kwa hakika ingekuwa chombo makini na cha muhimu sana ambacho kingetoa mchango mkubwa katika kutetea maadili ya jamii ya Kitanzania wakati huu ambapo utandawazi unameza kila kitu kilicho chetu tena kwa kasi ya kutisha. Mitandao na magazeti ya aina hii wakati mwingine yamechangia kuibua kashfa nzito nzito za viongozi katika sehemu mbalimbali duniani. Kwa mfano, John Edwards - mgombea mwenza wa uraisi wa Marekani mwaka 2004 na mgombea uraisi mwaka 2008 kupitia chama cha Democrat alikumbwa na kashfa ya ngono ambayo iliibuliwa kwa mara ya kwanza na mtandao wa gazeti la udaku la National Enquirer. Mwaka juzi waziri mmoja kule Afrika ya Magharibi ilibidi ajiuzulu baada ya picha zake za ngono kuwekwa katika mtandao wa kurekebisha tabia kama Ze Utamu. Mifano hii inaonyesha kwamba mitandao kama hii inaweza kuwa na mchango fulani chanya katika jamii japo kusema kweli faida zake zinakinzwa na uhasi na migongano ambayo mitandao hii inaweza kusababisha katika jamii kama yetu ambako watu bado wanafikiri kwamba kila kitu kinachoandikwa katika mitandao au magazeti ni cha kweli.

Hata hivyo, Ze Utamu ilikuwa imeshalitelekeza jukumu la kurekebisha tabia za wanajamii, na badala yake iligeuka kuwa chuo kikuu cha matusi, majungu, fitina, udaku na husuda. Kama mtu ulimtongoza akakukataa, kama mtu ana maisha mazuri kukuzidi, kama mwenzio alikuzidi kete na kumchukua binti au mvulana uliyekuwa ukimtaka kwa muda mrefu, kama mtu anapendwa na watu kuliko wewe, kama .....basi ulichotakiwa kufanya ni kuitafuta picha yake (hata bila picha ni sawa tu) na kuituma kwa Ze Utamu. Fomyula ilikuwa rahisi sana: sema kwamba ni fisadi (wa ngono), anatembea na watu wengi kwa kujirahisi (unaweza kutaja majina machache), ana UKIMWI na anausambaza tena kwa makusudi, anachukua waume/wake za watu, anapenda vya bure (mteremko), anajiona sana kumbe hana lolote n.k. Halafu waombe "wadau" wamwage data. Na kweli data zingemwagwa na mara nyingi yalikuwa ni matusi ya kutisha ambayo yangeweza kukufanya ufiche uso wako kwa soni. Mara moja moja wadau wangeweza kusimama kidete na kumtetea huyo aliyetamuishwa wakidai kuwa kaonewa, ni mwanajamii makini asiye na ubaya na mtu n.k. Sifa moja ya Ze Utamu hata hivyo ilikuwa ni kwamba mtu ukishatamuishwa basi ulikuwa huachiwi hata utetewe/ujitetee vipi.

Kwa vile hakuna utafiti ambao umekwishafanywa na wanasosholojia au wanasaikolojia kujua hasa madhara ya kutamuishwa katika mitandao ya aina hii si ajabu mtandao huu tayari ulikuwa umeshaleta misukosuko ya kifamilia na kisaikolojia kwa wale ambao walishatamuishwa. Kutokana na matusi mazito yanayoporomoshwa hapo, bila kujali nafasi na tabaka la mtu aliyetamuishwa, watu wengi walianza kuhoji ulikokwenda undugu, umoja, amani, upendo na Utanzania wetu ambao Mwalimu Nyerere alituachia. Wengine walihoji ni kwa nini serikali ilikuwa imeufumbia macho mtandao wa aina hii kwa karibu miaka miwili mizima. Swali la msingi ambalo linaweza kuulizwa hapa ni hili: tumefikaje katika hatua hii ya kutamuishana – sisi Watanzania na Utanzania wetu? Jibu ni rahisi sana - UTANDAWAZI!

Utandawazi na Lengo Lake

Utandawazi ni joka la mdimu lenye vichwa vingi angamizi – vichwa vyenye kazi tofauti tofauti ambavyo lengo lake kuu la jumla hasa ni kuuangamiza utamaduni wetu na hivyo kutufanya tujidharau, tujidogoshe, tusijitambue na hatimaye tuweze kuendelea kutawalika, kunyonyeka na kudhulumika kirahisi zaidi.
Ni lazima ikumbukwe kwamba tapo la utandawazi tunalolishuhudia kwa sasa ni mojawapo tu ya matapo mengi ya utandawazi yaliyotangulia, matapo ambayo yalitukutanisha na wageni kutoka Ulaya na kwingineko. Mahusiano yetu na ulimwengu wa wageni hawa kutoka nje tangu mwanzo yamekuwa ya kihasama, kiunyonyaji na dhuluma – kuanzia enzi za biashara ya utumwa mpaka wakati huu tulio nao. Uzalendo, utu na Uafrika wetu ulikunguwazwa na kufishwa wakati wa biashara ya utumwa “tulipokubali” kugeuzwa bidhaa na kuuzwa kama nyanya au vitunguu sokoni. Ni wakati huu ambapo tulipondwapondwa kisaikolojia na kuaminishwa kwamba tulikuwa binadamu wa tabaka la chini ambao kamwe tusingeweza kuwekwa katika daraja moja na “mabwana” kutoka Ulaya na Uarabuni. Vita hivi vya kisaikolojia vilivyopiganwa kwa ujanja sana kupitia dini, sera za lugha na elimu dhidi yetu vilipiganwa kwa nguvu zaidi na “mabwana” wakati wa ukoloni. Ni wakati huu ambapo bara letu liliitwa bara la giza na tamaduni zetu zilizotukuza, kutulea huku zikishabihiana vyema na mazingira yetu ya asili zilibatizwa kuwa za kishenzi na kinyama. Ukoloni ulitazamwa na hata kutambulishwa kama mkakati wa “kutustaarabisha” na kututoa katika giza nene la kuabudu dini za “kishenzi”, kuongea lugha za kishamba na kukumbatia tamaduni zetu za kiwango cha chini. Lugha zetu ambazo kupitia kwazo fikra zetu na mtazamo wetu pamoja na nafasi yetu katika dunia hii vimefinyangwa ziliitwa duni, zikadumazwa na kunyimwa nafasi za matumizi katika sekta rasmi. Matokeo yake lugha zetu ambazo ndizo zinaamua sisi ni nani, nafasi yetu ni ipi katika ulimwengu huu na tunahusianaje na wengine katika mazingira yetu zilinyimwa “meno” na tangu hapo zimebakia kuwa lugha zisizo na mwelekeo wala matumaini. Kulingana na Ngugi wa Thiong’o, ukoloni na utumwa wetu wa kisaikolojia ulikamilika pale tulipokubali lugha zetu kuvishwa sanda na kutengwa na ulimwengu na mazingira yetu. Kuanzia hapo, tulikoma kuwa sisi na kuanzia wakati ule, sisi si sisi tena, hatujijui na hatujui kwamba hatujijui kuwa sisi ndisi. Tumekuwa watumwa wa fikra!
Japo kupatikana kwa uhuru wa bendera kuliwasha moto wa matumaini katika mioyo ya Waafrika, sasa ni wazi kwamba matumaini hayo yalikuwa yametiwa mubaalagha na ahadi za “kuutafuta kwanza uhuru wa kisiasa na uhuru mwingine ungefuata” tulizopewa na akina Kwame Nkrumah wetu zimeshindwa kutekelezeka. Lakini utumwa mbaya kabisa ni ule utumwa wa kisaikolojia - utumwa wa kimawazo uliomdogosha Mwafrika na kumfanya ajione kuwa yeye ni binadamu wa daraja la pili na utamaduni wake kuwa wa kizamani, usioendana na wakati na wa kishenzi. Mkakati mama ulioanzishwa na watawala wetu wakati wa biashara ya utumwa na kuendelezwa (wakati mwingine kwa nguvu) wakati wa ukoloni bado unaimarika siku hadi siku na bado umejikita barabara katika fikra zetu. Na baada ya miaka sitini ya uhuru bado tunaamini kwamba utamaduni wetu na hata lugha zetu ni za kishamba na hazifai kutumiwa katika sekta rasmi kama elimu na vyombo vya habari. Matokeo yake lugha zetu za jadi zimegeuka kuwa lugha za kuonewa haya na kizazi kipya hakitaki tena kuzizungumza. Ati bila lugha na utamaduni wetu wenyewe, sisi ni/tumekuwa/tutakuwa nani?
Kutokana na kutawaliwa kwetu kitamaduni, leo tunakazana sana kuiga utamaduni wa “mabwana” zetu wazungu. Kinashosikitisha zaidi ni ukweli kwamba mara nyingi uigaji wetu umegeuka kuwa mashindano ya kujidharau na tunaiga mpaka kuwazidi hao tunaojaribu kuwaiga. Mifano ni mingi kuthibitisha dai hili (mfano mashindano ya urembo yaliyozagaa kila mkoa, wilaya, mji, tarafa, kata, vitongoji na muda si mrefu pengine yataingia katika familia). Naona hata katika Ze Utamu tulifuata ruwaza (pattern) ile ile – kuiga mpaka kuwazidi tunaojaribu kuwaiga. Nadhani hata wazungu, pamoja na uhuru wao wa habari usio na kikomo, wanayo heshima kidogo kwa viongozi wao na hawawezi kuwa na tovuti mashuhuri ya kizushi ambayo inaweka picha za uongo (zilizofanyiwa photoshop) za viongozi wao wakiwa uchi na watu kuanza kuporomosha matusi mazito. Pamoja na kuishi Marekani kwa karibu miaka 10 sasa jambo hili lilinishangaza na kunisikitisha. Hata kama tovuti za aina hiyo zingekuwepo (au zipo), wenzetu hawa, kinyume na sisi ambao tunaparamia na kuiga mambo kwa pupa, wanajua kwamba huu ni upuuzi tu na hakuna mtu anauyetilia maanani.
“Kiinimacho” cha usawa, Undugu na Umoja
Swali kubwa nililojiuliza baada ya kuiona Ze Utamu ni hili: Moyo wa upendo, umoja, usawa, undugu na mshikamano ambao muasisi wa taifa letu Mwalimu Nyerere alijitahidi sana kuupandikiza mioyoni mwetu ulikuwa wapi? Chuki, uhasama na hasira ya “wadau” katika Ze Utamu ilikuwa ya kutisha na ilikuwa ni vigumu kuamini kwamba hawa walikuwa ni Watanzania waliobahatika kuwa na kiongozi mwanafalsafa, msomi na mwenye welewa mpana aliyepigana kufa na kupona kuangamiza ukabila, matabaka na kuhakikisha kwamba kila mtoto anapatiwa nafasi sawa ya elimu ambayo ndiyo mkakati mama wa ukombozi katika jamii. Je, upendo, usawa, amani, undugu na mshikamano vilivyokuwa vikihubiriwa sana miaka michache tu iliyopita vilikuwa vya kweli au vilikuwa kiinimacho tu kwa Watanzania? Hasira hii ya “wadau” – ambayo ilionekana waziwazi hasa kama mtu aliyetamuishwa alikuwa ni kiongozi, “fisadi” au mtu mashuhuri katika jamii – imetoka wapi? Inawezekana usawa, undugu na umoja vilivyokuwa vikihubiriwa sana vilikuwa ni viinimacho tu? Ati, hali halisi ikoje katika jamii? Ahadi zile za MwanaTANU na baadaye mwanaCCM bado zina ukweli wo wote? Ni kweli kwamba binadamu wote ni sawa au (kama wanyama wanavyogundua katika riwaya mashuhuri ya George Orwell ya Shamba la Wanyama) binadamu wote ni sawa lakini binadamu wengine ni sawa zaidi ya wengine?

Ze Utamu Imetufundisha nini? Tufanye nini?

Mbali na kuionyesha vyema tabia yetu tatanishi na ya kijinga ya kuiga mambo hadi kuwazidi hao tunaojaribu kuwaiga (na hivyo kuthibitisha zaidi utumwa wetu wa kisaikolojia na kitamaduni), Ze Utamu imetufundisha kwamba mambo si shwari katika jamii yetu na watu wana hasira; na kwamba upendo, amani, umoja na mshikamano uliokuwa ukihubiriwa sana ama vilikuwa ni kiinimacho tu au watu wameshtushwa na mfumuko wa matabaka na sasa wamechoka. Niliangalia maoni yaliyokuwa yakiwekwa na “wadau” baada ya mtu mashuhuri, kiongozi au “fisadi” kutamuishwa na niliweza kuiona hasira ya watu ikiwaka moto. Pengine matabaka ambayo tumeyaachia kufumuka kwa kasi ya risasi - ambapo tumewaruhusu watu wachache wajikusanyie “vijisenti” vyote na kuwaacha walio wengi wakiwa hawana kitu yameshatia sumu katika mioyo ya Watanzania na hasira kali inafukuta mumo kwa mumo kama volkeno iliyolala. Tusije tukaiachia volkeno hii iendelee kufukuta mumo kwa mumo kwani siku itakayoripuka Tanzania yetu itakuwa matatani.
Ze Utamu pia imetuonyesha tabia nyingine ambayo tunayo sisi Watanzania. Tunapenda sana kuongea na kupiga porojo na Mswahili hata kama hana hoja au mchango wa maana katika mjadala ni lazima achangie. Tazama kwa mfano mada mbalimbali makini katika blogu mashuhuri ya michuzi na utaona ninachokisema. Hata kama mada iliyoanzishwa ni nzuri, yenye manufaa na inayotaka mjadala hasa na hoja komavu, badala ya kutoa hoja na kujadili kwa heshima na hatimaye kukubali kutokubaliana kiungwana utakuta mara nyingi watu wataanza kubeza, kudharau na kumponda mtoa mada. Mfano mmoja ni mada ya hivi karibuni ya Profesa Mbele kuhusu safari za nje za Raisi Kikwete. Profesa Mbele kama vile Mtanzania ye yote anayo haki ya kutoa maoni yake na kwa vile hii ni topiki ya muhimu basi mtu ungetegemea hoja madhubuti za kuunga mkono ama kupinga. Badala yake hoja hutaziona na mahali pake ni mashambulizi na mengine ni yale wenyewe wanaita “personal attacks” Tabia hii inayokera na ambayo inaashiria uzembe wa kufikiri, kutafakari mambo kwa kina, kujenga hoja madhubuti na kuzitetea, kwa kiasi fulani inaakisi yale yaliyokuwa yakitokea kwenye Ze Utamu – kushambuliana na kudhalilishana. Kwa sisi Watanzania, tabia hii inatatanisha kwani kutokana na malezi yetu na falsafa yetu ya kitaifa tungetegemewa kuwa watu wenye upendo na masikilizano. Kuna chuki mioyoni mwetu na sijui kiini chake hasa ni nini!

Ninapoandika makala haya Ze Utamu haipo tena. Tusije basi tukakaa kitako, tukabweteka na kukenua meno tukidhani kwamba tumeshinda vita. Vita ndiyo tu kwanza vimeanza kwani inawezekana kabisa Ze Utamu wengine na pengine wabaya zaidi watazaliwa. Kwa vile sisi tunaiga kuzidi hao tuwaigao, tusubiri siku vipindi kama Jerry Springer, Maury na Cheaters vitakapofika kwetu. Sijui vitakuwa na sura gani. Tusije tukasahau kwamba adui yetu hasa ni utandawazi na hao “mabwana” zetu wanaotamani kututawala katika nyanja zote za maisha yetu milele na milele. Tufanyeje basi ili kuuokoa Utanzania, Uafrika na utu wetu? Kusema kweli si jambo rahisi na hakuna njia ya mkato. Kutokomeza utumwa wa kisaikolojia na kasumba ya kujidharau sisi pamoja na utamaduni wetu, kasumba iliyopandikizwa akilini mwetu kijanja kwa karne nyingi, kasumba inayotufanya tujione kuwa binadamu wa daraja la pili si kazi rahisi. Inabidi tuwe na mkakati mama wa kufufua utamaduni wetu na mahali pazuri pa kuanzia ni katika lugha zetu za kienyeji kwani kama asemavyo Ngugi wa Thiong’o katika kitabu chake cha Decolonizing the Mind lugha zetu ndizo nguzo hasa za utamaduni wetu na hatuwezi kuwa huru bila kuziheshimu lugha zetu na hivyo kuulinda utamaduni wetu. Wakati sasa umefika wa kuandaa sera makini inayotekelezeka kuhusu uhimizaji na uboreshaji wa lugha zetu - sera ambayo itazipa nafasi lugha zetu za kienyeji kutumika katika sekta rasmi kila inapowezekana. Mfumo wetu wa elimu urekebishwe na elimu tunayowapa vijana wetu ihusiane na mazingira yao. Ni lazima pia tupunguze tofauti za kitabaka kati ya wenye “vijisenti” na masikini walio wengi wanaoshindia mlo mmoja. Afya na mustakabali wa taifa letu unategemea ni kwa jinsi gani tutakavyofanikiwa katika kupunguza pengo kati ya matabaka haya kinzani. Si budi pia tuangalie upya dhana nzima ya maendeleo. Ati, tunaposema maendeleo tunamaanisha nini hasa? Ni lazima tuvumbue dhana mpya ya maendeleo – dhana yetu wenyewe kulingana na mazingira yetu. Yote kwa yote tukumbuke kwamba hivi ni vita vya kisaikolojia. Tukiweza kuwaaminisha vijana wetu kwamba kuongea Kisukuma, Kihaya au Kichaga kwa ufasaha ni jambo la kujivunia, kwamba siyo lazima kuvaa mitepesho kuashiria usasa, kwamba siyo lazima kujikondesha mpaka mbavu zichomoze kuwa mrembo, kwamba rangi nyeusi haina tofauti na rangi zingine na kamwe Mwafrika siyo kiumbe wa daraja la pili basi tutakuwa tumeanza kupiga hatua (japo za kitoto) katika safari yetu ndefu na ngumu ya kujitafuta na kujifahamu upya sisi ni nani na nafasi yetu katika dunia hii ya sasa ni ipi. Kizazi hiki cha dot com ni lazima kiandaliwe mkakati wa kuanza kukirudisha katika kiini cha Uafrika na Utanzania wake.

Waswahili wana msemo unaosema kwamba zimwi likujualo halikuli likakumaliza. Utandawazi ni zimwi lisilotujua – zimwi lililotuparura vibaya sana wakati wa utumwa, likafinyangafinyanga fikra zetu wakati wa ukoloni na sasa, baada ya miaka zaidi ya sitini ya uhuru, linatishia kuumeza kabisa utamaduni na usisi wetu. Kila siku tunapoamka ni lazima tujisaili: Utandawazi ambalo ni zimwi lisilotujua, linaweza kweli kutula lisitumalize? Je, tufanye nini?