Saturday, December 03, 2005

Wapenzi wa Matako Makubwa

Wapenzi wasomaji, leo nimeamua kuzungumzia suala ya matako makubwa. Tafadhali msione kama ni matusi lakini hapa USA ni issue kubwa, maana watu wanayachukia! Nimeona nizungumzie suala ya matako makubwa kwa vile jana kazini, mzungu aliyekondeana mno kasema ni mnene na akila keki eti yote itaenda matakoni. Nilishangaa na kusikitika sana.

Uzuri kwa wazungu ni kuwa na matako fleti kama vile yamepigwa pasi. Sijui kwa nini. Mtu anashepu ya mbao, mwanamke hana hips kakaa kama dume vile eti ndo uzuri. Kumbe ni kwa sababu hao models na wacheza sinema wako hivyo! Basi wasichana ana akina mama wanajinyima chakula kusudi wakonde na eti wapendeze. Ndo maana magonjwa kama Bulimia na Anorexia zimeshamiri hapa. Lakini ukitazama sinema za miaka ya nyuma kama za 1930's na 1940's, wanawake walikuwa na shepu na walikuwa wamejaa na hata wanaume wa kizungu walikuwa wanasifia. Mpaka 1950's kulikuwa na mcheza sinema Marilyn Monroe, alikuwa na zinga la figure 8, na wanaume wote walikuwa wanampapatikia. Ama kweli mambo yanabadilika. Hivi sasa wanasema eti walikuwa ni obese yaani wanene!

Mbona mimi naona matako fleti kama chapati ni mabaya na hayapendezi? Au ni kwa sababu nimekulia Africa? Brothas (waMarekani Weusi) wanapenda mwanamke awe na matako ya maana! Akipita mwanamke mwenye mbarikio utasikia brothas wakisifia, "umm, umm umm!" Kuna siku nilisikia wanaume wa kizungu wakijadili sababu ya wanaume weusi kupenda matako makubwa, walisema ni "cultural thing". Kwa kweli ni culture yaani utamaduni! Kama umekulia katika mazingara ya kupenda kitu utakipenda. Na ndo maana kuna weusi USA wanataka kuwa na shepu iliyokondeana kama mzungu kumbe haiko katika 'genes' zake. Wajitahidi kupunguza mzigo lakini wapi, iko pale pale.

Sisi wanawake wenye asili ya Afrika tumebarikiwa huko nyuma. Yaani boxi, siha, wowowo, booty, na nasikia waGhana wanaita yokohama, matako makubwa yana majina mengi. Waafrika tunaona kama ni urembo, lakini wazungu na waliokulia uzunguni wanaona kinyaa. Wanasema eti ni dalili ya ulafi na uvivu! Lakini kama ni dalili ya ulafi mbona hata mwanamke mwembamba mwafrika anaweza kuwa na kamzigo huko nyuma? Ubaya mwenye matako makubwa anaweza kubaguliwa kwa vile bosi anaweza kuona kuwa ni 'ugly' na mwenye nacho anachafua mazingira ya ofisi. Kweli kabisa!

Hayo matako makubwa ni 'genes' za sisi waafrika. Lakini ajabu kuna siku nilisikia wazungu wakisema eti waafrika tuna matako makubwa kwa sababu ya utumwa. Eti mabibi zetu walinyimwa chakula hivyo matako ndo ilikuwa godown ya mafuta ya akiba. Nadhani ni uzushi kama ile ya ngamia kuweka maji kwenye nundu zake!

Mimi mara nyingi nimeambiwa nina matako makubwa, niyapunguze kwa kwenda gym kufanya mazoezi. Hayo mazoezi haisadii kitu ni makubwa vile vile! Lakini msione kama naona haya, wala! Mtu akiniambia nina matako makubwa namwambia mbona kama ni madogo, na ningependa yawe makubwa zaidi! Wanabakia kushangaa hasa nikiwaambia kuwa Afrika, matako makubwa ni uzuri.

Na amini usiamini kuna opresheni ya kuyapunguza inaitwa Liposuction. Wanawake wengi weusi na wazungu wamefanya hiyo liposuction ya matako, akiwemo mwimbaji Janet Jackson. Ubaya, ni kuwa ukishafanya hiyo liposuction, mafuta yataenda kwingine mwilini, hivyo utakuwa na shepu ya ajabu!

Sisi waafrika tunapenda kuringia huo mbarikio wa matako makubwa. Nilipokuwa nacheza ngoma shuleni na jeshini, tulikuwa tunatia nguo ndani ya bukta kusudi tuonekana na matako makubwa kweli kweli! Lakini, mara nyingi mitaani hapa USA, nimesikia akina dada wakifokewa, "You got a big a-s!" Kuna siku nilikuwa kwenye kituo cha Subway hapa Boston, kapita mama fualni Mganda, aisei alikuwa amejaliwa kweli huko nyuma, mpaka nikaona wivu. Basi ungeona wazungu walivyokuwa wanamtazama kwa mshangao ungecheka. Ila nilishuhudia baba fulani Mmarekani Mweusi akimtazama kwa furaha na kawa kama vile anamezea mate.

Nampenda sana mecheza sinema, Whoopi Goldberg. Nilikuwa nasoma jinsi akienda kwenye audition au akiwa kwenye movie shoot, wazungu wanamwambia kuwa ana matako makubwa au avae nguo ya kuzificha. Yeye alichoka, na mwishowe kusema, " Mimi ni mwanamke mweusi, nina matako makubwa niache kama nilivyo!" Wanawake wote tungedai heshima kama Whoopi nashani wazungu wangeheshimu matako yetu makubwa.

Tatizo linigine la kuwa na matako makubwa USA ni kupata nguo. Ukienda kununua sketi au gauni uanweza kukuta mbele refu nyuma umepanda. Au unavaa hiyo nguo lakini kwenye hips na matako haipiti! Hii ni kwa sababu nguo imeshonwa kwa ajili ya wazungu wenye matako fleti. Na kupata Jeans inayofiti ni vigumu. Mtu ambaye atatengeneza nguo 'molded for the black woman' atapata wateja kweli kweli, maana tunalilia nguo kama hizo.

Pamoja na yote haya sasa wazungu wameibuka na staili ya kuwa ka ka-butt. Yaani jeans inakuwa na pedi ndani kusudi mtu aonekana ana matako. Loh! Watu hawaridhiki! Sijui tuseme asante J-Lo (mwimbaji Jennfier Lopez) au nini. Kwanza walikuwa wanamcheka J-Lo na matako yake makubwa lakini naona watu wanaanza kuyapenda. Mpaka kuna opresheni sasa ya kuongeza matako. Wacha wafanye haitapendeza kama matako natural tulytozaliwa nayo waafrika.

Matako Makubwa Oyee!

35 comments:

mwandani said...

Oyee!

Mija Shija Sayi said...

Labilalasuli tena! Chemi hujatulia. Sasa uje utuandikie juu ya matiti makubwa.

Chemi Che-Mponda said...

Hey mija shija sayi,

Labilasuli manake nini? Maana sielewi Kisukuma.

Topiki ya Matiti Makubwa iko njiani!

Mija Shija Sayi said...

Si kisukuma, ni neno la kiarabu rafiki yangu mmoja ndio neno lake pale anapoapia. Tatizo sijui kuliandika kwa kiarabu.

Innocent said...

Oh Chemi,
Kwanza nimecheka, manake sikuamini u muwazi namna hiyo.Unajua huku Afrika kuanika mambo haya hadharani tabu sana.Si siri mie yokohama ni kivutio kwangu.Na kwa taarifa yako hapa Uganda usiombe, mimama imejazia haswa. Wanadai ni kwasababu hapa Uganda makabila mengi wanakula karanga na viazi kwa wingi.Nakwambia usiombe hapa wanayaita"BIG BUM"
Kwa ufupi, nataraji utatueleza siku za usoni ni nini sifa za uzuri wa mwanamke hapo kwa ujumla wake, hasa ukigusia umaarufu,pesa au hata elimu.

Jeff Msangi said...

Hapa sina usemi Chemi.Uliyoyasema ni kweli tupu.

Ndesanjo Macha said...

Mungu wangu! Makubwa haya...ungegusia pia kuwa mashindano kama ya "miss" Tanzania hayatilii maanani maana ya urembo katika utamaduni wetu. Dada mmoja, ambaye sasa ni marehemu, aliwahi kuja na mashindano aliyoita "miss bantu" ambayo nia yake yalikuwa ni kutukuza mtazamo wa urembo unaotokana na utamaduni wetu ambapo makalio ni sehemu muhimu ya urembo huo.

Chemi Che-Mponda said...

Ndeanjo,

Nakumbuka sana yale mashindano ya MISS BANTU! Niliifurahia sana maana ilisisitiza ule uzuri wa kimila, mguu, matako etc. Kweli hizi ma MISS WORLD nk. wana standards za kizungu, yaani mshindi lazima afanane na standard ya shepu za kizungu, na nywele za kizungu (weusi wanaiga kwa kutia weave kichwani). Aliyejaa, mwenye matako makubwa na nywele za kipilipili alie tu! Maana utaitwa ugly.

NA WEKA MTAZAMO MAKINI said...

Yaani sina cha kusema!!1Nilikuwa sijacheka siku nzima..teh teh nimecheka sasa.
Hayo mambo ni kweli..wanaume weusi wanapenda sana wanawake ambao huko nyuma kumeinuka.Nimefurahi kwa kuweza kuandika hoja kama hiyo..Mmh hata ungeniambia niblogu kwa hoja hiyo ..ningekuwa na kigugumizi cha vidole..Hongera dada Endelea kulenga masuala "sensitive"

msangimdogo said...

Naomba nianze kwa kusema HONGERA SANA. Inahitaji nguvu kidogo kuanzisha kitu hasa katika hiki hiki tunachokiita utamaduni wetu ambao watu wanaogopa kueleza ukweli, na kubakia na masononeko mengi moyoni. Ndio maana hata ndoa nyingi zinavunjika watu wakiwa wanapendana, sababu inakuwa tu kuwa mtu anashindwa kuweka mambo hadharani.

Na kisha nije kwenye hii mada sasa, hakika imenikuna, imenivuta, imenihamasisha, na imenipa nguvu ya kusema jambo ambalo muda fulani nilikuwa napata kigugumizi cha namna ya kuanza. Ni kweli kabisa kuwa huo mbarikio kwakweli ni sehemu muhimu sana ya urembo wa Mwafrika, na ndio maana tunaupenda...hivyo tuendelee kuusifia na endelea kusifia kwa nguvu zote dada.

Unajua nini? Nimekuwa nikijiuliza "Hivi Tanzania haiwezi kweli kuyafanya mashindano ya miss Batu kuwa ya kidunia?, kwani tumekosa nini? maana hii ni fursa nzuri ya kuonyesha utamaduni wetu ati...ukiwemo huo wa mibarikio ya makalio makubwa...

Matako makubwa oyeeeeeeeeeeeee

mark msaki said...

Mpendwa Chemi!

nimefurahia sana kusoma hii mambo ya matako makubwa! umeichambua kwa ufasaha na umakini, na kwa wakati huo huo kulinda fahari yetu weusi! akhsante saa! matako makubwa kwa kina dada ni bomba sana!

ninafagilia pia kuhimiza upya mashindano ya miss bantu, ila pia yaboreshwe - yaani matako iwe ni kigezo kimojawapo lakini na vingine kama vile umahiri wa kujibu maswali, kuzungusha matako wakati wa kucheza, uweusi au umaji ya kunde! kila kitu ilimradi yachukue sura ya kuyafanya yakubalike afrika na ulimwenguni kote!!!

matako makubwa oyeee!!!!

picha zenu said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Fikrathabiti said...

Dada chemi,nami pia ni miongoni mwa watu wanaohusudu wanawake wenye matako makubwa sana
Asili ni asili tu,hata kama wazungu hawaipendi.Watajiju kivyao! matako makubwa oyeeeeeeeeeeeee

Reginald S. Miruko said...

nimekuwa nikikosa mengi kwa kutokujua site yako, Chemi, kwangu mimi pia matako makubwa oyeeee!.

mark msaki said...

Sio binadamu pekee hata buibui....jamaa yangu Emmanuel Nzunda aliniletea hiki kiungo nisome nilipomwelezea kusoma habari yako kuhusu upenzi ya matako makubwa....


http://www.blackwell-synergy.com/doi/abs/10.1111/j.1095-8312.2006.00553.x

habari yenyewe ndio hii...

Female morphology, web design, and the potential for multiple mating in Nephila clavipes: do fat-bottomed girls make the spider world go round?
SHAWN E. VINCENT1* and SIMON P. LAILVAUX1

In animal species where females mate with multiple males, female mating success might be expected to covary with aspects of female morphology, such as size or shape. Spiders are especially interesting in this regard, as the females of several spider groups weave intricate webs that often accommodate multiple male spiders, all of whom are potential mates. Because web design is likely to be dependent on female size/shape, we use multivariate methods to assess the relationships among female morphology, web design, and reproductive ecology over a range of body sizes in the orb-weaving spider Nephila clavipes. Of the measured variables, only abdomen size explained a significant amount of the variation in number of males on a web, and this relationship holds even after statistically accounting for body size. Because abdomen size is an indicator of body condition in spiders, we suggest that condition is likely to be an important factor relating to potential mating success in female spiders. We found no evidence for an association between web design and number of males on a web, although our data indicate that larger females build webs that are both larger and further from the ground than those of smaller females. © 2006 The Linnean Society of London, Biological Journal of the Linnean Society, 2006, 87, 95−102.

KUMBE TUKIFUATILIA TUTAGUNDUA KUWA HATA MBUZI WAMAMAINDI WOWOWO!!! UKIAGIZIA MGUU UKAONA NI BONGE BASI JUA ALISUMBUA SANA WENZIE!! - na kama wazungu wanabisha ni kawaida yao maana wao hizi mambo za anti humane walianza siku nyingi!! si nasikia ukipata mdada wa kizungu siku hizi haelewi somo hadi uruke fensi?? ni kweli hayo chemi?

Chemi Che-Mponda said...

mark msaki,

Kwa kweli, bado nacheka kuhusu hiyo habari ya ma spider buibui.

Anonymous said...

shosti! habari hii ya matako imenigusa kunako moyo!
sio tu mimi ni mmoja wa wapenzi wa matako makubwa ila nilibahatika kushinda hiyo miss bantu,miaka kama mitatu iliyopita! nyumbani bongo daslama,
wape shosti,wape vidonge vyao!
Anna.

Anonymous said...

Mwanamke mwenye matako madogo ndio kitu, maanake unaweza kumtomba ukitumia mbinu zote. Iwe ni 'dog style' ama 'scissors' mboro huingia mpaka kwa 'cervix'. Ndoo maana sipendi matako makubwa. Nimetomba wanawake wenye matako makubwa na wale wenye matako madogo, na sasa hivi napendelea wale wenya matako madogo.

Anonymous said...

chemi wazungu wanapenda matako madogo kwa sababu ya sex....ni rahisi na wanadai wanaenjoy more, hata weusi wengine vile. matako makubwa ni mazuri machoni tu, na akiyabeba mtu mwembamba sio mnene mm!

Amu, PhD F (fuckiology) said...

Mie mkenya naishi Nairobi na nduguzanguni nawaambia hapa nairobi matako makumba ndio mtindo - yaitwa "madiaba" kwa ufupi "diabs" ama tena "rasa", "mahagga" n.k. Kama wee mwanadada huna mahagga nakuonya Kenya hukaribishwi hata kwenya foleni kwa afisi za huduma mwenye mahagga na tabasamu nzuri arukishwa laini....kisha baadaye atalipa kitu kidogo-sehemu kidogo tu ya mahagga kila weekendi. Mahagga kwa maendeleoooo!!!!!!!!!

Anonymous said...

MH!! kweli matako makubwa ni ndo utamaduni asili wa urembo wa mwanamke wa kiafrika....... lakini itategemea namatako yenyewe yapo namna gani... tukubaliane kwa muono wa kawaida tu... maana yapo majitako mengine makuuuubwaaaa!! tena sasa basi yameungana na mapaja kiasi hata hujui tako limeishia wapi na paja liko wapi... Hii bwana wala sio nzuri inakuwa kama karaha fulani hivi
Saidi Abdallah

Anonymous said...

mimi najivunia kuwa mwafrika,lakini Chemi umenitekerenya leo,nimejipata napasuka kwa kucheka {furaha } napenda uvimbe (matako ) maanake ndio urembo hapa afrika.BILA MATAKO 'RASSA' NAIROBI HAUPETI!

Anonymous said...

MIMI NI MKENYA NA NI MU HINDI LAKINI MATAKO MAKUBWA NI POA

Anonymous said...

yes you are allright, but you will excuse me beacause I pseak frensh and a feu swahili, but every yhing you can like or hate it beacause of your culture.

Anonymous said...

Ndugu zangu wa kike. Mimi asili yangu ni chotara wa kiarabu na mwafrika (Mmanyema Safi) na tangu nafugua macho naona matako makubwa tuu. Na mimi nimeowa mwanamke mwenye wowo ya heko, kwani bila ya wowo mwanamke hana heba, wala shepu. Mimi nitaendelea kupenda matako makubwa tuu.

Anonymous said...

wazungu wanapenda matako madogo kwa sababu wanattia nyuma pia, kwa hiyo itakuwa shida kuingia kama nusu ya ume inamezwa na matako

Anonymous said...

Umegonga ndipo! Wazungu hapa hawafahamu kitu kizuri kutoka kibaya, matako na matiti makubwa yatawaleeeee! Kila siku mimi husikitika kuona wanawake huku wakikula mboga utadhani hao ni ngom'be na mbuzi, hatimaye unadhani waliishi Darfur kwa muda wa mwaka moja. Hebu tuwaelimishe...

Anonymous said...

Sina la kusema maana mpaka namaliza kusoma hadithi zako, kichwa kisha kuwa mtaani nikiangalia nyuma ya kila anayepita! Tatizo ni ninyi akina chemi huko muliko. Munapata?

Mikundu Matako Makalio Manundu said...

kwa kuwa gumziwa ni matako, basi nawakaribisheni katika blogu ya matako namikundu: mikundu.blogspot.com

Anonymous said...

mimi napenda kuyaona "manyugla'au "madiggda" lakini si kuyatumia,kwa vile ukiangalia kike macho yaenda kwanza kwa sura kisha huko nyuma.hata ukimwona mwanamke kwa nyuma barabarani watakaona sura.matako juu!!!!

Francis said...

Chemi sisi watu wa Mommbasa husema MATAKO MUHIMU. lakini swali langu ni, wewe Chemi Matako yako vipi? Twaomba tafadhali picha Zima kwenye mtandao angalau tukangue. Wako Pappyg Mombasa.

taus said...

nakupongeza dada yangu kwa kuandika ukweli,mimi nipo hapa Colorado,USA.Yote uliyosema hata hapa yapo.ASANTE "Binti wa Afrika"

Anonymous said...

mi ni mbongo matako makubwa nlikuwa siyapend mpaka nilipo mfila demu mmoja aah ase hakuna raha kama kumfila manamke mwenye wowowo lainiiiii kubwaaa kama unanawaa.

Anonymous said...

zungumzeni mambo ya maedeleo si ulanisi.je mwataka kuwa kama wao.wale si sisi.wale walanisi.sisi ni sisi.

SIJAONA NASSIBU said...

matako makubwa hamna kitu tuongelee how to flood our porket