Saturday, January 21, 2006

Kukosa Nguvu za Kiume si Mwisho wa Dunia!

Jamani, jamani, jamani, kuna jirani yangu kafa hivi majuzi. Alikuwa ni baba wa makamu, mmarekani mweusi. Alikuwa mcheshi na ilikuwa kila tukionana lazima tusalimiane. Mara ananinunulia kahawa halafu tunakaa namsimulia kuhusu Afrika. Yule baba, alionekana mzima na mwenye afya fiti kabisa. Nilibakia kushangaa kusikia kafa na si kwa ajali. Mke wake alifariki mwaka juzi, lakini miezi ya karibuni alikuwa anaonekana mwenye furaha kwa vile alipata mpenzi, dada mwenye miaka 25 hivi.

Story niliyoskia ni hivi: Kumbe jamaa alikuwa na matatizo ya moyo. Alifia kitandani akiwa kwenye shughuli ya kufanya tendo la ndoa na mpenzi wake. Tena wanasema alifariki mara alipofikia kilele cha tendo. Navyosikia ilikuwa ni ‘massive heart attack’. Kama ni massive bila shaka na utamu wa shughuli hakujua kuwa yuko hatarini. Nasikia huyo mpenzi wake alipiga sana makelele majirani walipigia simu polisi 911 kwa vile walidhania wameingiliwa na majambazi. Wanasema baba wa watu kamwangukia yule dada na kafa macho wazi.

Lakini bado nilikuwa nashangaa maana kama nilivyosema awali, jamaa alionekana kuwa na afya. Kumbe jamaa alikuwa mtumizi wa Viagra, yaani vile vidonge vya kuongeza uume, na kumpa mwanaume uweza wa kufanya tendo la ndoa. Ndugu zake wanalamika kweli, maana hakuzipata kwa prescription ya daktari, alizaiagiza kwenye mtandao (internet). Kwa kumwangalia alivyofiti nisingefikiria kuwa ana matatizo ya nguvu za kiume. Kumbe mtazame mtu, matatizo yake anayajua mwenyewe na daktari wake.

Nikawa najiuliza kama jamaa alijua ana matatizo ya moyo, kwa nini alitumia Viagra. Maana hata tangaza kwenye TV na magazeti wanaonyo kuwa kabla ya kutumia. Halafu pia wanaonya kuwa mwanaume anaweza kupofuka kama anatumia. Lakini wanaume bado wanazitumia! Na siku hizi dawa za kuongeza nguvu za kiume ziko nyingi kuna Ciallis, Levitra, Yohimbine na mengine. Hizo dawa zina side effects kama kuumwa kichwa, kuharisha, pua kuziba, macho mekundu, tumbo kuumwa na mengine mengi. Pamoja na side effects bado zina soko kubwa. Na zikipigwa marufuku nina amini kuwa watu watatajirika kwa kuzifanyia magendo.

Kwa kweli wanaume wako tayari kufa kama wakishindwa kufanya tendo la ndoa. Nashindwa kuelewa sababu. Yaani tendo la ndoa ni tamu kiasi hicho au wanahofia kuwa kwa vile hawa ‘function’ tena ndo basi si wanaume? Mtu anakuwa tayari kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya kufanya tendo la ndoa. Mwanaume anaambiwa anaweza kupofuka akitumia hiyo dawa lakini bado yuko tayari kuchukua risk. Halafu mwanaume akiitwa ‘hanithi’ yuko tayari kupigana au kuua. Sijui bila kusimamisha anajiona si mtu tena…sielewi kabisa!

Nikawa najadiili na marafiki zangu juzi na tulikubaliana kuwa wanaume wako tayari kuchukua ‘risks’ kuliko wanawake. Yaani mwanaume anaweza kufanya tendo la ndoa hata akijua kuwa kuna hatari ya mwenzake kuwa na ugonjwa wa zinaa na ataambukizwa. Bongo, walikuwa wanasema eti, ‘Ajali Kazini’! Hiyo ajali inaweza kukuua! Sijui hiyo ume ikisimama ndo basi tena, akili zote zinahamia hapo. Nauliza tena, tendo la ndoa ni tamu kiasi kwamba mko tayari kuhatarisha maisha yenu? Kukosa nguvu za kiume zi mwisho wa dunia jamani. Bado tunawahitaji!

Lakini nikirudi kwa marehemu jirani yangu, uwongo mbaya, alikuwa anatabasamu ndani ya jeneza lake!

12 comments:

Ndesanjo Macha said...

Unajua umegusa jambo fulani kubwa sana. Kutokana na malezi tunayokuzwa nayo, na kuzungukwa na mfumo dume kila upande,wanaume hukua tukitafsiri umuhimu wetu maishani kwa kutazama nguvu za kiume. Tunaamini kuwa mwanaume hasa ni yule anayeweza kufanya tendo hilo kwa muda mrefu na mara nyingi...yaani utasikia mtu anajisifu kuwa mpenzi wake hakulala kabisa maana "nilimpa vidonge sita usiku mzima." Tena mara nyingi tunafikia hatua ya kusema uongo ili tuonekana kuwa ni wanaume hasa mbele ya wenzetu.

Halafu pia tunadhani kuwa ukubwa wa uume unaashiria jinsi gani tulivyo wanaume hasa.

Ni mtazamo huu ndio unaofanya mwanaume akitaniwa au kuambiwa kuwa yuko kama mwanamke anaweza aue mtu. Tunaamini kuwa uanamke ni udhaifu na uanaume ni ushujaa fulani hivi. Na ushujaa huu tunauhusanisha na nguvu za kiume.

Tukiingia ndani kabisa kwenye saikolojia ya mwanaume na masuala ya uume na tendo la ndoa ndio unakuta majengo, kuta, mageti, viti, n.k. vikiwa vikiwa na maumbo kama vile uume. Tazama kitu kama "microphone." Hata minara kwenye nyumba za ibada. Kwa ufupi, suala la nguvu za kiume, uume, tendo la ndoa limekaa ndani ya saiki yetu kama darubini kiasi ambacho mtazamo wetu wa dunia unapitia katika darubini hiyo. Inatokea bila sisi wenyewe kujijua. Wakati mwingine tunakuwa tumeharibikiwa kabisa akili kiasi cha hata kuwa nusu-mtu. Utaona hii katika watu wanaopata furaha kwa kufanya mapenzi kwa nguvu na wanawake. Au wanaume wanavyopata furaha mwanamke anapolia (hata kama analia kwa uchungu)!

Mija Shija Sayi said...

..Hata kama analia kwa uchungu! Duh!

Lakini hebu Ndesanjo nisaidie hapa, upungufu wa nguvu za uume hutokana na nini?...Mtu huzaliwa hivyo? au hupungua baadaye kulingana na umri au ni ugonjwa?

Haya Mheshimiwa Ndesanjo.

Christian Bwaya said...

Aisee ujue sikuwa nimefikiri kukuta khabari kubwa namna hii! Hata hivyo nimevutiwa nayo sana. Hongera dada kwa mada hii nzuri.
Kuna mambo mengi huwa yanatukabili lakini (huku kwetu)ni woga kuyasema. Hili la uume ni moja wapo.
Ndesanjo na Che Mponda nisaidieni na mimi swali alilouliza Shija. Niongezzee hapo kuwa utajuaje kuwa huenda una tatizo hilo kwa kujitathimini? namaanisha ujue kinachoendelea mwilini mwako usije ukaaibika mzee mzima. Mambo mazito haya bwana.

Jeff Msangi said...

Habari ya aina yake hii.Chemi,kwa kuibua mijadala ya ndani ndani sikuwezi.Lakini kama ulivyo ukweli kwamba wanaume na nguvu zao za kiume na kama kambale na matope ndio hivyo hivyo kwa wanawake na umri wao au makunyanzi usoni.Mwambie mwanamke amezeeka au anaonekana mzee usikie majibu yake.Muangalie mwanaume akihisi nguvu za kiume hana au zimepungua anavyopata tabu.Kadunia haka bwana!

Rama Msangi said...

Dada naona umekuwa mshauri nasaha sasa.....tehe tehe teheeee

Ndesanjo Macha said...

Mija:
Sababu za kupungua nguvu hizo ni nyingi sana. Kuanzia kula ovyo, kutofanya mazoezi, hofu, umri, matatizo ya kisaikolojia, n.k. Kuna wakati pia upendo unapopungua na mvuto unapungua hivyo mwanaume anaweza kuwa kama vile ana matatizo kumbe ni kwamba havutiwi na mwenziye. Tatizo hili hutokea sana kwa mfano katika ndoa ambazo ziko njiani kuvunjika. Utaona kuwa nchi kama Marekani wanaume wengi sana wana matatizo haya ambapo mara nyingi ni kutokana na aina ya vyakula wanavyokula. Unajua sehemu kubwa ya vyakula Marekani ni sumu. Ni sumu yenye ladha nzuri sana na inayonenepesha! Madhara yake elfu kidogo.

Rashid Mkwinda said...

Dada Chemi kila wakati unakuja na mambo mapya lakini mimi nadhani si mapya kimtazamo bali kiuhalisi ingawa pia yamezoeleka katika jamii, hapa nchini Bongoilishawahi kutokea jamaa katika mikoa ya nyanda za juu kusini katika Wilaya moja mashuhuri kwa bidhaa ya ngozi za binadamu aliamua kuungiza uume wake katika jiwe ambalo alilitengeneza mithili ya uke wa mwanamke,bahati mbaya katika kuliingilia lile jiwe uume wake ulikatika na hivyo kulazwa Hospitali, Mapaparazi kama ada walimfuata Hopsitalia alikolazwa kutaka kujua sababu ya Kurisk namna hiyo,yeye alisema aliamua kufanya hivyo kwa ajili ya kuukwepa ugonjwa wa UKIMWI.
Mimi naona kuna siri kuba sana katika kufanya tendo la ngono, nndio maana watu hufikia mahala wakauana na wengine kuwekeana uhasama juu ya tendo hilo,pia nadhani jirani yako na wengine wengi hususan huku kwetu bongo hutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume kwa ajili ya aidha kuwaridhisha wenzi wao ama kuonesha umahiri wao katika tendo la ndoa.

Reggy's said...

Kama kuna nguvu za kiume, kimtazano wa kijinsia, bila shaka lazima kuna nguvu za kike pia. naomba wataalam mnisaidie zile za kike ni zipi na zikoje? lakini kwa hoja ya dada Chemi, kukosa nguvu za kiume waweza kuwa mwisho wa duania, hasa pale, wanaume wote wakizikosa. Kwani hakutakuwa na kuzaana.

MICHUZI BLOG said...

chemi umeleta nini tena hii? naungana na ndesanjo, na najaribu kumjibu da'mija. kwa uzoefu wangu, nguvu hupungua kwa (bila kujali nafasi ya namba) (i)uchovu wa kazi za ajira (ii) kuchacha (iii) kuishiwa hamu ya nyama ile-ile kila ssssssiku (iv) utovu wa ufundi wa mwanamke (v) joto/baridi lisiloepukika aidha kwa nguo kam shuka ama blanketi ama vifaa kama vile ac n.k na (vi)mwanamke aliekeketwa na asiyepandisha mzuka haraka. haya ni maoni yangu binafsi, kwa mujibu wa uzoefu wangu...

Chemi Che-Mponda said...

Michuzi,

Umenifurahisha kweli. Ama kweli una experience.

Nakubali kuwa wakati mwingine inabidi ubadilishe mazingira ya vituuz. Maana kila siku mambo yale yale unachosha. Hata inachukua muda kufikia kilele.

MzeeMzima said...

Yakhe tusidanganyane. Pale pahala ndipo panajenga nyumba eti. Kama bunduki yake hailipuki kweli, basi mwanamme huyo hawezi kuwa na nyumba; kwa hiyo atakuwa analala nje na kweli hali maisha itamuiwa magumu sana. Ni kama ndiyo mwisho wa dunia!

simon william said...

Kweli jamani mambo hayo ni nyeti si mchezo inafaa kuchukulia kwa uzito labda pendekezo ni kutumia mchanganyiko wa mdalasini na asali badala ya kutumia madawa ya kizungu ambayo yana side effects. Tukitumia God's phamarcy ambayo ni ya bure mambo yatakuwa shwari kwenye ndoa zetu kwani hakuna wa kulalamika.

It's me Simon Mnyakyu.