Tuesday, February 14, 2006

Kumbuka Mpenzi Wako!

Leo ni Valentine’s Day yaani sikukuu ya Wapenzi. Ni siku ya kukumbuka wapenzi wetu. Na huko Tanzania nakumbuka tulikuwa tunakesherekea kwa kupeana kadi na zawadi ndogo ndogo. Mwanamke anaweza kukuta ana zawadi ya kanga mpya, perfume, vitambaa, nk.

Na hapa Marekani unaona watu wana haha kununua maua, machocolate, kadi, na hata chupi nyekundu na nguo za ndani zingine zenye theme ya Valentines Day. Basi bei ya maua, na hivyo vitu vimepanda kweli kweli. Yaani dozen roses leo ni zaidi ya dola mia! Hata yule mChina anayeuza maua kwenye kituo cha subway kapandishwa bei. Maua sita anauza dola thelathini, wakati juzi zilikuwa dola sita tu. Na watu wananunua kusudi wasionekane kama hawapendi wapenzi wao.

Pia, leo ni siku ya wapenzi kuonyesha mapenzi yao huko faragha yaani chumbani. Basi bidhaa za mapenzi zinauzwa kwa kasi, na hata condoms zinatolewa bure sehemu nyingi.
Watu wananunua mishumaa, mafuta, na manukato mengine, na vitu vya kufanya mapenzi iwe ya ajabu. Huko CVS na Walgreens ile sehemu ‘nyeti’ inapata biashara kweli!

Lakini nilikuwa naangalia hao wanaume wanamnunulia nani hizo zawadi. Utakuta mke kamnunulia kachocolate kidogo na kimada kamnunulia Chocolate boxi kubwa!

Basi leo nikakumbuka maongezi na wanaume kadhaa Tanzania na Marekani. Ni maongezi ya kawaida tu na wala msidhania kuwa mimi nilikuwa mpenzi wao. Utasikia mwanaume anasema mke wangu nampenda lakini zile feelings nilizokuwa napata wakati ndo yetu bado changa sisikii tena.

Niliwahi kumwuliza baba fulani, ofisa katika wizara fulani huko Tanzania kwa nini anapenda kutembea na wanawake wanaofanya kazi ofisini kwake. Nilishangaa jamaa alivyokuwa muwazi kwangu kasema “Mke wangu kachoka!” Nikamwuliza mke kachoka kwa vipi? Jamaa kasema eti matiti yake yamenyauka, kanenepa, siyo kama alivyokuwa nilivyomwoa. Nikamwuliza amebarikiwa watoto wangapi na huyo mke wake, kaniambia kuwa wana watoto sita.

Nikamkumbusha kuwa huyo mke wake ndiye mama watoto wake. Mwili wake ameutoa kama sadaka kwa ajili yake na hao watoto. Jamaa kafikiria halafu kaniambia, ni kweli, na kakumbuka kuwa alivyomwoa alikuwa mzuri kweli. Nikamshauri aende akambusu mke wake huko kwenye tumbo yake kuonyesha mapenzi na kuwa anashukuru kuwa kamzalia hao watoto.

Mwingine kaniambia kuwa eti matiti ya mke wake yamelala na yeye anapenda matiti saa sita. Anasema anapenda matiti yakimchoma kifuani akiwa anafanya mapenzi. Basi nikamwuliza kama mke wake alikuwa na matiti saa sita wakati anamwoa, kasema Ndiyo. Basi nikamkumbusha kuwa na huyo kimada wake 'spring chicken' akizaa na matiti wake yataanguka pia.

Mwingine kaniambia kuwa eti anamwona mke wake kama dada yake, hata hawezi kusimamisha hata mke wake akilala uchi kitandani! Hapo nilipigwa butwaa! Nikaona huyo kweli ana matatizo na mke wake, maana wanaume wangi wakipata nafasi ya kufanya ngono wanasimamisha bila shida! Huyo jamaa ana vimada kibao, na nadhani ana ugonjwa wa akili!

Na mwingine kaniambia kuwa anapenda kutembea na 'spring chicken' kwa vile huko chini pana bana. Nikamwambia kuwa akimzalisha mke wake kila mwaka chensi ya kuelegea huko chini ni kubwa maana uke haupati nafasi ya kurudi katika hali yake ya awali. Lakini jamani navyoona wanawake wengi pana bana ila basi tu, wanaume mnakuwa na fikra kuwa mwanamke kazaa basi tena panalegea!

Mwanaume mwingine anasema hataki kutoka na mke wake kwenye party kwa vile eti, ‘kazeeka’ au eti hajui kuvaa vizuri. Kwanza kama ni housewife ulimpa hela ya kununua nguo na viatu kusudi avae vizuri? Huko utakuta kimada katoka vizuri na nguo latest, tena kamnunulia mwanume huyo huyo. Na kama mke hana msaada huko nyumbani kweli atakuwa kachoka maana kulea watoto na kufanya house chores inachosha.

Lakini kinachoniudhi zaidi ni wanaume ambao wanasahau kutunza familia zao na badala yake wanatunza vimada au nyumba ndogo. Unakuta mke na watoto wanaishi kwa dagaa, nguo zao zimechakaa, na girlfriend anakula nyama fillet na ana nguo mpya! Wanaume mna laana kweli!

Lakini pamoja na kuwa mnasema mwanamke kachoka, na nyie wanaume mnachoka pia! Badala ya six pack mnakuwa na vitambi, full head ya nywele kichwani mnakuwa vipara, na hata huo ubarikio wenu hauwi mgumu kama ilivyokuwa awali.

Kumbukeni kuwa kila mtu atazeeka na kuonekana kuchoka. Na ule mwili uliyokuwa nayo ukiwa na miaka 20, hutakuwa nayo ukiwa na miaka 50! Lakini cha muhimu leo tuonyeshe mapenzi na heshima kwa wapenzi wetu.

3 comments:

Jeff Msangi said...

Uchambuzi mzuri sana wa siku ya wapendanao.Uliyoyasema kuhusu wanaume na jinsi wanavyozipa visogo ndoa zao,wake zao au mama watoto zao ni kweli kabisa.Pamoja ya yote,nadhani ungeweka wazi upande wa wanawake pia ingekuwa vizuri zaidi.Dunia ya sasa hususani hii ya magharibi mambo ni 50/50.Wake kwa waume wametumbukia kwenye mitego na kinaa na kukosa uaminifu.

Natamani kuona balanced analysis kwa sababu, ingawa siamini kwenye mapenzi ya siku moja tu ndani ya mwaka mzima(valentine)nadhani kwa wale wanaosheherekea siku hiyo mapenzi sio kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke tu bali kutoka pande zote mbili.Nipende, nikupende au sio?Halafu hivi kipimo cha mapenzi ni kufanya ngono tu?Kwanini bidhaa kama kondomu zipande bei siku hiyo?Je hili ndilo lililokuwa kusudio au dhamira ya waanzilishi wa siku hii kupitia kwa huyo mtakatifu Valentino??Ni wangapi wanapata maambukizi ya ukimwi siku hii kutokana na upotoshwaji wa maudhui ya siku yenyewe?

Chemi Che-Mponda said...

Jeff, Kwa kweli umeuliza maswali mazuri sana. Ni wangapi wameambukizwa Ukimwi siku hiyo, na kwa nini kondomu zinapanda bei. Yaani hapa USA wiki hiyo hakuna hata coupon ya kupata discount na kwa kweli ni ghali. Lakini watu wananunua pamaoja na ma KY jelly! Halfu zile za bure wakati mwingine siyo saizi au kavu au zina kasoro fulani. Bora mtu aweze kuchagua.

Lakini kwa wengine siku hiyo ya Valentine ndo wanapata bahati ya kuonja ngono, na wanaweza kukaa mwaka bila kufanya tena. Hasa kwa watu waliofunga ndoa miaka mingi.

Kuhusu wanawake ni kweli mambo ni 50/50 siku hizi. Wanawake nao wanaunua makadi, masharti, cologne nk kwa ajili ya wapenzi wao. Na hata siku hiyo wenyewe ndo wananunua malingerie chupi, sidiria, corset, na vitu vingine kusudi huko chumbani mambo yawe ya Valentine hasa. Fikira mambo ya vikuba Bongo.

Halafu tumesahau zile zawadi za SECRET ADMIRER!

Ndesanjo Macha said...

Umeyeyukia wapi?