Thursday, March 30, 2006

Mandisa aka Mandiva





Kama mnaangalia mashindano ya American Idol, mtaona mwaka huu kuwa kuna dada fulani anaitwa Mandisa. Huyo Mandisa ana miaka 29, ni Mmarekani Mweusi na pia ni kibonge cha dada. Pia ana matako makubwa kweli kweli.

Kwa kweli waMarekani hawapendi kuona watu wanene kwenye TV, na hasa wenye matako makubwa, lakini huyo dada amebarikiwa na sauti nzuri sana. Ana kipaji cha kuimba. Ningependa kuona anashinda na kuwa American Idol wa Season 5, lakini sidhani kama WaMarekani watampa nafasi hiyo.

Kwa msiofahamu, American Idol ni mchezo wa kuchagua mwimbaji mzuri. Mshindi anapata ‘contract’ ya kutengeza santuri, dola millioni moja, gari, na zawadi zingine tele.
Maelefu ya watu kati ya miaka 16 hadi 28, wanajaa kwenye auditions, wakiwa na ndoto ya kuchaguliwa kushiriki kwenye show. Majaji wanapita miji mingi USA wakitafuta washiriki. Halafu watu wanapunguzwa na majaji mpaka kufikia watu 24. Wakifika hapo ndo watazamaji wanapewa nafasi ya kumpigia kura mtu ambaye wanadhania anastahili kashinda.

Basi huyo Mandisa, alipoaudition mara ya kwanza mbele ya majaji na kupita kuendelea Hollywood, Simon Cowell alisema, “We’re going to need a Bigger Stage this year” Yaani watahitaji jukwaa kubwa zaidi kwa ajili ya huyo Mandisa.

Maskini Mandisa wa watu hakujua huyo Simon kasema nini, basi ikaonyeshwa kwenye National TV na dada wa watu alilia. Anasema alikuwa anatazama na marafiki zake na kwa kweli aliona kama kashfa. Baadaye baada ya kupita kuendelea akamwambia Simon kuwa amemsamehe na hata Simon mwenyewe alionekana kuwa na haya kwa alichosema.

Nimekuwa nikisikiliza redio na kusoma kwenye magazeti na Talk Shows. Anapendwa lakini watu wanasema hata pita kwa vile ni mnene. Basi kuna mzungu moja alisema eti paja moja la Mandisa ni kikubwa kuliko kiuno cha dada wa kizungu, Melissa ambaye alishatolewa wiki kadhaa ziizopita. Mara waseme hayo matako, maana wazungu hawapendi kabisa matako makubwa. Na bila kujali maneno ya watu kila wiki Dada Mandisa anatoa wimbo kali. Anaimba hasa, mpaka sauti yake inakuingia. Anapanda kwenye jukwaa anapendeza na anajiamini!

Kuona watu bado wanampenda na unene wake wengine wakamkashifu kwa kuimba wimbo wa dini wiki hii. Kwanza hiyo ‘Christian’ ni genre ya muziki kama Jazz , R& B na Classical. Wazoee! Na mbona yule mzungu Carrie Underwood ambaye alishinda mwaka jana alivyoimba wimbo wa dini kwenye show hawakusema kitu!

Kwa kweli roho inaniuma, nikifikiria kuwa huyo dada hatafika katika TOP 3 ya hayo mashindano kwa sababu ya unene. Mshindi wa zamani, Ruben Studdard alikuwa Mnene karibu paundi 400, naye alikuwa na sauti tamu kweli kama Luther Vandross. Watu wanasema, ilikuwa ‘okay’ kwa Ruben kushinda na unene wake kwa sababu ni mwanaume. Lakini eti Mandisa hawezi kupita kwa vile ni mnene na ni mwanamke. Duh, hata kwenye unene hakuna usawa.

Kama mnaangalia American Idol nawaomba umpigie kura huyo dada Mandisa.. Sauti anayo tena nzuri kuliko akina dada wote kwenye show. Matako Makubwa na unene yasiye sababu ya kukosa U-American Idol.

Na natabiri asiposhinda atakuwa Star kama akina Mo’Nique. Tutamwona kwenye commercials na sinema na concerts maana. American Idol ndo mwanzo wa kujlikana kwake.

Na baadaye nitaongea juu ya siasa za American Idol.

Kwa habari zaidi za America Idol nenda http://www.americanidol.com

9 comments:

boniphace said...

Nmatazama Mandisa, napenda sauti yake na yeye alivyo. Lakini taarifa hizi sikuwa nazo na inasikitisha sana. Kimsingi anawafunika lakini pia nilitazama namna wasanii weusi wanavyofutika kwa haraka katika onyesho hilo tangu hatua za wali sijui,ni hofu kuwa wana vipaji safi kuliko weupe, naomba unieleweshe kuhusu hilo.

Chemi Che-Mponda said...

Hi Kaka Boniface,

Kwa kweli nataka kuandika zaidi kuhusu siasa za American Idol. Kwanza wanasema kuwa mwaka huu producers wanataka Mzungu mwanaume ashinde. Mtu wao eti ni Ace. Mimi naona kama Ace anaimba vibaya, na hata hiyo sex appeal ambayo wanadai anayo sioni. Akimaliza kuimba anatamza kwenye camera, si sex appeal hiyo?

Je, umeona kuwa safari hii hakuna mwanaume mweusi katika Top 12. Yule Kijana Gedeon, alikuwa na sauti nzuri kuliko wanaume wote lakini walimtoa. Baada ya kuona Gedeon katolewa nikaamini kuwa huenda kweli kuna njama ya kufanya mzungu dume ashinde.

Na huyo Mandisa ana kipaji na bahati nzuri anapendwa kwelikweli na wengi kwa ajili ya sauti yake. Wakimtoa sasa hivi American Idol inaweza kukuosa mamilioni ya watazamaji. Hao Producers si wajinga, lakini hatashinda na watadai nikwa sababu ni mnene. Tutaona.

MK said...

Samahani ingawa haya siyo maneno yanayo endana na kichwa cha habari lakini naomba nitoe tangazo langu kuhusu blog.

TANGAZO:

Baada ya uchunguzi wa hali ya juu nimegundua jawabu la kuondoa Blogger NavBar (Sehemu ya juu kabisa ya Blog yako inayo onesha search this blog).

Hii kutokana na ya kwamba watu wengi uwa wanachukizwa na jinsi hiyo NavBar ilipo.

Jawabu la hili swali unaweza kusoma kwa kubonyeza hapa.

Kama ukipata tatizo au maswali zaidi naomba niandikie na nitakujibu asap.

Nashukuru,
©2006 MK

Imetengenezwa na kuletwa kwenu na ©2006 MK

mzee wa mshitu said...

Dada Chemi ama kwa hakika hii inasikitisha. Mimi huku Tanzania huwa nikifuatilia taratibu masuala haya kupitia televisheni local ya Channel Ten, sikuwahi kufahamu kabla kwamba kuna ubaguzi wa namna hii.

Sina uhakika kama yeyote tu anaruhusiwa kuvote, lakini kama hivyo ndivyo itabidi nijitose kwa kasi kuweza kumsaidia huyu mnene mwenzangu.

Hawa wazungu hawamaindi matako hawajui kwetu huku sisi dili, angeweza huyu mwimbaji kushinda kwa umbo lake tu. Binafsi ninamkubali.

boniphace said...

Chemi yametimia, natangaza kutotazama kabisa onyesho hili. Mgomo huu sidhani kama utamalizika mapema. Nayakimbia mashindano yanayodhalilisha watu kutokana na mitizamo ya kundi fulani. Nachukua uamuzi huu mzito lakini nitautetea katika moyo wangu. Nimedhalilishwa sana na kura hizi za kumng'oa MANDISA. Ni wazi zilikuwa na chuki na hsa uchambuzi wako unaanza kuonyesha namna haya mashindano yanavyoambatana na kupanga washindi. Kuna moja liliitwa Project run away, ambapo vita vya kumuandaa mshindi wa kike,mzungu viliambatana na kumng'oa mwafrika mapema na kisha kujenga sifa za kimama mama ili mzungu huyo amshinde Santino ambaye alikuwa creative zaidi kuliko wengine. Sasa bora nguvu hizi za kutazama mashindano haya na yale ya miss nani ambayo nilishayapinga siku nyingi katika fikra zangu, nazibakiza katika kusoma vitabu. Nitasoma bora zaidi haya magazeti Tando huenda nikafaidi weledi ulojaa huku. Sitaki tena, natangaza mgomo wangu American Idol ng'oo hamnioni kabisa tena.

Chemi Che-Mponda said...

Yaani Kaka Boniface, ungejua nilivyolia kwa hasira jana usiku! Sikuamini macho yangu kuwa Mandisa katolewa! Nilikosa raha kweli. Halafu niliingia kwenye website ya American Idol na kukuta watu hata wazungu wanalamika kuwa katolewa.

Wengine wanasema eti kwa vile kaimba wimbo wa kiKristo, wengine walisema alivaa vibaya na ni mnene mpaka kuumiza macho, yaani! Lakini sasa naamini kuwa kuna njama ya kumfanya Mzungu dume ashinde mwaka huu. Watu wanasema wanataka Ace ashinde, mbona anaimba vibaya! Na yule kijana mweusi Gedeon aliyetolewa wiki kadhaa zilizopita alikuwa na sauti nzuri kuliko wanaume wote safari hii! Na je umenoti kuwa mwaka huu, na kwa mara ya kwanza hakuna mwanaume Mweusi kwenye Top 12!

Hata mimi sasa sitaangalia! Nitaangalia shows zingine, lakini inabidi tumsupport huyo mweusi pekee aliyebaki Paris. Wazungu wanampiga vita kweli kweli eti anaringa kwa vile ana sauti nzuri.

American Idol wamepoteza watazamaji wengi!

Anonymous said...

Wow, man! Cool site!

anatrim loss weight


diet fast lose plan weight


Good Bye!

Anonymous said...

MESSAGE

Anonymous said...

panasonic digital camera software


konica minolta digital camera



kodak digital camera


casio slim digital camera