Monday, October 09, 2006

Leo ni Sikukuu ya Columbus Marekani

Leo ni sikukuu ya Columbus hapa Marekani. Ni siku ya kusherekea aliyegundua Marekani, Bwana Christopher Columbus. Columbus alitua Marekani na meli zake tatu mwaka 1492. Kuna nyimbo kadhaa za kumsifia na utasikia watoto wanaimba, "Columbus sailed the Ocean blue in 1492!"

Columbus alikuwa ni mwitalia aliyepewa pesa na malkia na mfalme wa Spain kugundua nchi kadhaa duniani. Kwanza enzi hizo wazungu walidhani kuwa dunia iko fleti na ukienda mbali utaanguka na kuishia motoni. Columbus alisema dunia ni mviringo. Alivyochukua meli zake na wakawa wanaenda, wanaenda, wafanyakazi wake kwenye meli waliokuwa na hofu kubwa kuwa meli yao itafika mwisho wa dunia, wataanguka na kufa wote. Walipanga hata kumpindua Columbus na hata kumwua na kurudi huko Spain. Lakini Columbua alifanikiwa kuwatuliza na hatimaye walifika Marekani. Ukweli alligundua Marekani kwa bahati tu, maana nia yake ilikuwa afike India. Alivyofika alishangaa kuwa hauko kama alivyofikiria na ndo kajua kagundua sehemu nyingine ndo kapaita West Indies. Ukweli Columbus hakufika Marekani tunayojua leo, bali alifika visiwa vya Bahamas. Lakini alifungua mlango kwa ajili ya wazungu kuja kwa wingi huko walivyojua kuna ardhi huko upande wa pile wa bahari!

Ajabu, utadhania kuwa kulikuwa hakuna watu Marekani kabla ya Columbus kufika. Watu walikuwepo. Hao wenyeji waliteswa na kunyanyaswa na hao wazungu. Waliuliwa na kuibiwa mali zao na kufanywa watumwa. Hao wazungu waliwaletea magonjwa, kama surua, na mafua na kaswende na wenyeji walikufa kwa wingi.

Watu unaowaona Marekani leo ni mchanganyiko wa watu kutoka kila pande ya dunia. Wako wa kila rangi, kila, kabila na kila dini. Uzuri Marekani wanasema kuwa kuna 'melting pot' yaani watu wanayeyushwa na kuwa moja. Na huko serikali ya Marekani inataka kufunga milango wahamiaji waache kuja. Wanasahau kuwa hii ardhi ilinyang'anywa kutoka kwa wenyeji waliokuwepo. Maangamizi ya wenyeji wa Marekani ilikuwa ni ya hali ya juu.

Kwa kweli kuna mengi ya kusema, lakini kwangu mimi sioni kama huyo Coulumbus ni shujaa.

7 comments:

Ndabuli said...

Chemi,sijui kama wewe unasikiliza/au ni mpenzi wa miondoko ya reggae, lakini maelezo yako yanaungana kabisa na mwanamuziki wa reggae anajiita Burning spear anawimbo mmoja anamsema columbus kuwa na quote "Christopher Columbus is a damn blasted liar,He say him that he's the first one Who discovered...., I and I say that What about the Awarak indians?"

SIMON KITURURU said...

Hawa jamaa kwa kugundua mimi siwawezi. Maana hata Tanzania hata Ziwa Victoria waliligundua wao eti. Chakusikitisha ni kwamba vitabu vya historia vingi vitumikavyo vimeandikwa nao. Hivyo huendelea kufunza watu historia kwa mtazamo wao. Wewe fikiria hata wao kwa wao ulaya bado wanabishana kuhusu historia mpaka za karibuni. Juzi juzi tu hapa ndio Uswisi imegeuza historia ielwzayo kuwa ni kwanini wakati wa vita ya dunia haikuvamiwa. Historia ya mwanzo ilikuwa inadai ni kwa sababu ya jeshi lao, wakati sasa wanakiri kulikuwa na madili mengine mengi tu yakibiashara nk ambayo yalikwepesha Uswisi kuvamiwa.Sasa itafikia siku historia hizi za ugunduzi itabidi zife.

Trio Kaka said...

Swala la kugundua mie naona ni matumizi mabaya ya lugha. Lakini sio ni ubaya kama nikisema Trio Kaka ni Mtanzania wa kwanza kugundua Hawaii kama kweli mie ndio mtanzania wa kwanza kuigundua hata kama waHawaii walikuwepo pale.

Kwa hivo mie naona ni sawa tu kusema Kolumbasi ni mUlaya wa kwanza kuigundua Marekani, hii haimaanisha waAfirika hawakuigundua marekani kabla ya Kolumbasi.

Mabaki ya akiolojia yanaonesha kulikwa na watu wa asili ya Afirika miaka mingi kabla ya Kolumbasi Kufika Mareakani, Pia African Legends Wanasema mfalame wa ile empaya ya Asante alisha watuma watu wake waende Marekani, na wakiwa katikati ya bahari ya mbali msafara wao wa mitumbwi ulikuwmbwa na Mkondo nkali wa maji ambao uliwaua baadhi yao, kisha mfalme akaamua kumtuma kijana wake aongoze expedition hiyo na ndipo walifanikiwa ( Naona mara ya kwanza walikumbwa na msimu wa tufani ndio maana hawakufika, pia huwa nafikiria labda kuna sehemu maji ya mto yanakrosi bahari na kwa viel maji ya bahari na maji mto hayachanganyiki basi yakawazidia nguvu).

Cha kusikitisha wenzetu hawataki kukubali wabongo tulishakuja huku na kuigundua marekani kabla ya Kolumbasi, lakini ukiwaelekeza kwenye akiolojiko findings wanasema hiyo ilikuwa kabla ya kontinento drifti, yaani ile kitu iliyotokea ikaigwa dunia katika mabara ya sasa hivi yaani Ulaya afirika na marekani.

Hivi jamani kuna mtu yeyote najua historia ya jina la bara letu? hilo jina ni nani alilitoa na lilikujakujaje?

SIMON KITURURU said...

nakubaliana na Trio lakini pia tukumbuke kuwa hawa watu wakisema wamegundua wanamaanisha kuwa hata mambo yaliokuwepo hayakuwa na maana mpaka walivyo anzisha yao.Pili asilimia kubwa ya watu wao si wafikiriaji na wanabeba tu ufahari kuwa wao zaidi kwa sababu kama hizi.

zemarcopolo said...

sielewi kwa nini wanasherehekea wakati kuja kwa columbus amerika kulikuwa ni abuse to the human species kwa sababu walileta chicken pox na measles kuwauwa wenyeji wa kihindi.nadhani inabidi iwe siku ya kumlaani columbus na wenzake badala ya kumtukuza.tumesikia ufaransa imepeleka mswada bungeni kuwa yeyote atakayekataa kuwa kulikuwa na mauaji ya halaiki huko armenia mwaka 1915 atakuwa amefanya kosa la jinai.wafaransa haohao wanakumbuka pia siku ya columbus huko amerika.hii ni kutuambia maisha ya wahindi yaliyopotezwa kwa kuja kwa columbus hayana maana au?tafadhali angalieni film ya darwins nightmare jinsi haohao wa bara la ulaya wanavyopeleka zawadi ya bunduki kwa watoto wa angola na kurudi na zawadi ya zabibu kwa watoto wa ulaya.na waletaji silaha wanasema afrika hakuna vita ila tu watu wana njaa tu kwa sababu hawataki kufanya kazi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Chemi Che-Mponda said...

Cha ajabu hao Indians ambao hawakufa kwa kupigwa risasi waliwamaliza kwa kuwapa mablanketi enye smallpox! Wazungu bwana. Halafu hao red Indians wana usemi -'White man speak with forked tongue' (yaani mzungu anaongea na ulimi wa nyoka).

Aliwaletea firewater (pombe) na fire sticks (bunduki).

Trio Kaka, hata siku moja mzungu hawezi weka positives za African history kwenye curriculum ya mashule. Lakini hiyo habari ya Columbus, mungu wangu kila mtoto anamjua.

luihamu said...

leo umenena nakupa 100%.keep it up.