Showing posts with label Bongo Fleva. Show all posts
Showing posts with label Bongo Fleva. Show all posts

Saturday, January 02, 2016

Sababu ya Mwimbaji Ommy Dimpoz Kufungwa Jela Marekani

Mwimbaji maarufu wa Bongo Flava, Ommy Dimpoz (28) alifungwa jela Marekani katika ziara yake ya hivi karibuni.  Alifungwa jela huko Minnesota. 

Si kweli kuwa alikutwa na madawa ya kulevya kama wengine walivyodai.  Tatizo, Ommy hakuwa na Visa ya kumruhusu kufanya kazi Marekani. Alitakiwa kuwa na O-1 Visa ambayo wanapewa wasanii.  Wale wafadhili wake walifanya makosa katika kumwombea Visa hasa kama walijua atafanya show kubwa kinachotangazwa sehemu nyingi na kiingilio kikubwa. Uncle Sam (Serikali ya USA) anataka hela yake (kodi).  Inaelekea alivyochelewa ndege ilifanya maswali mengi kuulizwa.

Mimi kama Msanii ninaelewa process ya kuomba Visa ya Usanii.  Zinatolewa kiasi fulani kila mwaka na nyingi zinaenda kwa wasanii kutoka Canada, Ulaya, na  nchi za Marekani ya Kusini (South America). Chache sana zinaenda kwa wasanii kutoka Afrika.  Navyoona kulikuwa na njama za kumwonea Ommy hapa USA. Nani aliwaambia hao polisi kuwa hana Visa ya Usanii na wamhoji huko uwanja wa ndege.

Pole sana Ommy  Dimpoz.


Msanii wa Bongo Flava Ommy Dimpoz


Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:


Pia unaweza kusoma maelezo ya Dimpoz  HAPA:

Saturday, February 21, 2015

Bongo Fleva Staa Mez B Afariki Dunia!

Kutoka Facebook 

Msanii wa Bongo fleva  Moses Bushagama  aka. 'Mez B'  amefariki Dunia Ijumaa, February 20, mkoani Dodoma kutokana na ugonjwa wa homa ya mapafu. 

Mez B alikuwa ni mtoto wa pekee kwa mama yake kwani alizaliwa peke yake. Rest in Peace.


The Late Mez B

Friday, August 02, 2013

Rais Kikwete Afuturu na Wasanii wa Bongo Fleva Ikulu


PICHA KWA HISANI YYA IKULU
 


 Rais Kikwete akiwa akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa Filamu na  Bongofleva,Hemed Suleiman.



 Rais Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu na mmoja wa Watangazaji machachari wa Clouds FM,TV,Mbwiga Mbwiguke.





 Rais Kikwete akiwa akiwa katika picha ya pamoja na Msanii Mkongwe wa Bongofleva,Gwamaka Kaihula a.k.a King Crazy G K.



 Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa bongofleva na muigizaji wa Filamu hapa nchini,atambulikae kwa jina la kisanii Zuwena Mohamed a.k.a. Shilole.






Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii wa Bongofleva,Ally Kiba na mdogo wake Abdull Kiba.


 


Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa muziki wa Bongofleva mara baada ya kufturu.Kutoka kushoto,Snura,Keisha,Mwasiti,aliyechuchumaa ni Shilole,Dj Fetty ,Mwanahawa Abdul a.k.a Quee Doreen.





 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya pichani shoto Mwasiti Almas na kulia Zuwena Mohamed
a.k.a Shilole wakiwa sambamba na Mtangazaji wa Clouds FM,Dj Fetty wakipakua
ftari kufuatia mualiko wa Rais Kikwete kwenye viwanja vya Ikulu,jijini Dar jana.






 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a

Bongofleva wakipata ftari kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar jana kufuatia

mualiko wa Rais Kikwete.


 Rais Kikwete akisalimiana na msanii wa bongofleva,Lawrence Malima a.k.a Marlow, kulia
kwake ni Ally Kiba pamoja na Abdul Kiba na kushoto ni Mtangazaji wa East Africa
Radio, Samisango



 Rais Kikwete akisalimiana na msanii wamuziki wa kizazi kipya,Chege Chigunda na kulia kwake ni msanii wa bongofleva,Cassim Mganga,wakati wa kupata ftari jana jioni kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar.






 Rais Kikwete akiwasabahi baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya,mara baada ya
kupata ftari mapema jana jioni kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar, Rais Kikwete
aliwaalika wasanii mbalimbali kupata ftari ya pamoja Ikulu jana jioni.