Saturday, January 02, 2016

Sababu ya Mwimbaji Ommy Dimpoz Kufungwa Jela Marekani

Mwimbaji maarufu wa Bongo Flava, Ommy Dimpoz (28) alifungwa jela Marekani katika ziara yake ya hivi karibuni.  Alifungwa jela huko Minnesota. 

Si kweli kuwa alikutwa na madawa ya kulevya kama wengine walivyodai.  Tatizo, Ommy hakuwa na Visa ya kumruhusu kufanya kazi Marekani. Alitakiwa kuwa na O-1 Visa ambayo wanapewa wasanii.  Wale wafadhili wake walifanya makosa katika kumwombea Visa hasa kama walijua atafanya show kubwa kinachotangazwa sehemu nyingi na kiingilio kikubwa. Uncle Sam (Serikali ya USA) anataka hela yake (kodi).  Inaelekea alivyochelewa ndege ilifanya maswali mengi kuulizwa.

Mimi kama Msanii ninaelewa process ya kuomba Visa ya Usanii.  Zinatolewa kiasi fulani kila mwaka na nyingi zinaenda kwa wasanii kutoka Canada, Ulaya, na  nchi za Marekani ya Kusini (South America). Chache sana zinaenda kwa wasanii kutoka Afrika.  Navyoona kulikuwa na njama za kumwonea Ommy hapa USA. Nani aliwaambia hao polisi kuwa hana Visa ya Usanii na wamhoji huko uwanja wa ndege.

Pole sana Ommy  Dimpoz.


Msanii wa Bongo Flava Ommy Dimpoz


Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:


Pia unaweza kusoma maelezo ya Dimpoz  HAPA:

2 comments:

Anonymous said...

Pole zake.

Anonymous said...

Nimesoma maelezo ya Ommy. Nimesikitika kumsikia akisema kuwa eti alifurahia hiyo jela. Hakuwa na Uhuru. Pia ilibidi arudi Bongo baada ya kutolewa jela.