Showing posts with label Ellen Johnson-Sirleaf. Show all posts
Showing posts with label Ellen Johnson-Sirleaf. Show all posts

Thursday, February 28, 2008

Mtindo wa 'Lishuka' mpaka Liberia!

Mammy Dresses Scarlett in Gone With the Wind
President Bush with Liberian President Ellen Johnson-Sirleaf during his recent trip to Liberia (photo courtesy of Michuzi Blog)

Aisei, kumbe watu wanausudu fesheni zetu za Bongo! Mtindo wa kutundika kitambaa begani umefika mpaka Liberia! Cheki gauni ya Rais wa Liberia Mama Ellen Johnson-Sirleaf.

TAMWA waliwahi kufanya mashindano ya National Dress ya Tanzania, miaka ya 80. Mtindo uliyoshinda ni huo wa kitambaa begani. Nadhani walisema ni fesheni ya tangu enzi za Tanganyika.

Sasa nikichambua vazi la Mama Johnson-Sirleaf, zaidi naona Kilemba chake kinaelekea kwenye asili ya mababu zao yaani watumwa waliotoka Marekani. Nimeweka picha ya Mammy hapo kuonyesha watumwa walivyokuwa wanafunga kitambaa kichwani. Mnaonaje?
Liberia ulianzishwa na watumwa walioachiwa huru Marekani na kurudishwa Afrika.

Kwa habari zaidi za kuanzishwa taifa la Liberia someni:

http://www.bbc.co.uk/worldservice/africa/features/storyofafrica/9chapter9.shtml

http://www.loc.gov/exhibits/african/afam002.html