Thursday, February 28, 2008

Mtindo wa 'Lishuka' mpaka Liberia!

Mammy Dresses Scarlett in Gone With the Wind
President Bush with Liberian President Ellen Johnson-Sirleaf during his recent trip to Liberia (photo courtesy of Michuzi Blog)

Aisei, kumbe watu wanausudu fesheni zetu za Bongo! Mtindo wa kutundika kitambaa begani umefika mpaka Liberia! Cheki gauni ya Rais wa Liberia Mama Ellen Johnson-Sirleaf.

TAMWA waliwahi kufanya mashindano ya National Dress ya Tanzania, miaka ya 80. Mtindo uliyoshinda ni huo wa kitambaa begani. Nadhani walisema ni fesheni ya tangu enzi za Tanganyika.

Sasa nikichambua vazi la Mama Johnson-Sirleaf, zaidi naona Kilemba chake kinaelekea kwenye asili ya mababu zao yaani watumwa waliotoka Marekani. Nimeweka picha ya Mammy hapo kuonyesha watumwa walivyokuwa wanafunga kitambaa kichwani. Mnaonaje?
Liberia ulianzishwa na watumwa walioachiwa huru Marekani na kurudishwa Afrika.

Kwa habari zaidi za kuanzishwa taifa la Liberia someni:

http://www.bbc.co.uk/worldservice/africa/features/storyofafrica/9chapter9.shtml

http://www.loc.gov/exhibits/african/afam002.html

4 comments:

Anonymous said...

Mtindo wa kutundika vitambaa ni West Africa na nguo zao za asili. Sisi ndio tumeiga.

Anonymous said...

Sisi ndo tumeiga kweli, sio mtindo wetu!

Anonymous said...

YAANI CHEMI MIAKA YOTE UMEKAA BONGO UNASEMA KUTUNDIKA KITAMBAA BEGANI NI KITANZANIA? TYPICAL WEST AFRICAN MY FRIEND. SALMA KIKWETE KAPENDA HIYO WEST AFRICAN FASHION BASI KILA MTU KAIGA BASI UNAFIKIRI NDIYO YA KITANZANIA. LETE FASHION YA KIKWELI YA TZ KWENYE BLOG YAKO PLEASE - UTUELIMISHE.

Chemi Che-Mponda said...

Asanteni wote milotoa maelezo. Nami nimelika kwenye suala hii ya kutundika kitambaa begani. Sasa je, kuna fesheni gani original ya kiTanzania ya akina dada zaidi ya khanga?