Showing posts with label End of Days. Show all posts
Showing posts with label End of Days. Show all posts

Sunday, May 22, 2011

Bado Tupo!

Wadau, wikiendi inaisha vizuri tu. Hatujasikia habari za tetemeko la ardhi au maafa!

Huyo mzee aliyetabiri kuwa jumamosi itakuwa mwisho wa dunia kajificha!

Friday, May 20, 2011

Kwaherini Wadau! Kesho Mei 21, 2011 ni Mwisho wa Dunia!





Wadau, inabidi niwaage! Kuna watu wanaodai kuwa kesho siku ya jumamosi, May 21, 2011 ni mwisho wa dunia! Yaani karibu kila kona unaona tangazo inayoonya kuwa kesho ni mwisho wa dunia. Sasa ni habari kuu kwenye taarifa ya habari.


Wanasema kuwa Bwana Yesu Kristo atarudi duniani kesho, na kutakuwa na tetemeko kubwa mno la ardhi itakayo anagamiza dunia nzima. Hivyo inabidi niwaage. Tutaonana huko mbele.

Habari za mwisho wa dunia zilitabiriwa na Mtume/Mchungaji Harold Camping (90) kutoka California. Aliwahi kutabiri kuwa mwaka 1994 itakuwa mwisho wa dunia.


Huo utabiri wake unawafanya wengine wahaha na wengine wanacheka. Yaani hapa kuna wanaocheka kwa kutokuamini na wengine ambao wanaamini. Leo na kesho kutakuwa na party kadhaa za kusherekea mwisho wa dunia, wengine watakuwa kwenye maombi makali usiku mzima. Kuna waliochimba mahandaki na majumba chini ya ardhi na kuzijaza na maji ya kunywa na vyakula vya makopo. Binamu yangu (upande wa mama) mwenye miaka 94, alinipigia simu na kunionya kuwa kesho ni mwisho wa dunia na hatutaonana tena.


Ila kuna jaama alinifurahisha. Kamwambia mchungaji Camping hivi: Kama kweli siku ya jumamosi, May 21, itakuwa mwisho wa dunia nitakumia dola $5,000. Kama haitakuwa mwisho wa dunia basi nitumie dola $100.


Haya wadau, kazi kwenu!

Kwa habari zaidi za mwisho wa dunia 2011 someni: