Showing posts with label Food Label. Show all posts
Showing posts with label Food Label. Show all posts

Monday, January 04, 2010

Chakula cha Mchana

Wali mweupe, chapati, kabichi na kuku! Karibuni!

Monday, January 14, 2008

Ugonjwa wa Orthorexia


Kama uko Marekani lazima unamfahamu mtu mwenye ugonjwa wa Orthorexia.

Orthorexia ni ugonjwa ambayo unahusu chakula. Mgonjwa anapima na kuchambua kila kitu anacho kula na kunywa. Lazima kila chakula kinachoingia mdomoni mwake kiwe, 'healthy' cha kuleta afya bora.

Mfano mtu hali cereal mpaka kasoma label ya boxi na kuchambua kila kitu mle na kina calories ngapi. Hata maji ya kunywa si ajabu hataki maji ya kawaida bali anataka kunywa protein water.

Hata akienda restaurant kula lazima aombe food lable inayochambua kila kitu kwenye chakula anachoagiza. Mfano ina mafuta kiasi fulani, vitunguu, nyama, caroti, celery, spinach nk. Halafu anapima kiasi anachokula na kutupa kilichobaki.

Bongo watu tunashukuru kula ugali wetu na mchuzi, kitoweo. Hatupimi kiasi cha calories, tunaangalia shibe. Hatusemi au mchuzi umeungwa na nazi hivyo imejaa cholesterol na siwezi kula! Au nyama ina mafuta hivyo siwezi kula.
Nimegundua watu kama hao si watu wa kuwa nao karibu. Wanakuwa na hasira za karibu shauri ya kuwa na njaa! Pia watu wamekufa na huo ugonjwa, yaani wamekufa kwa njaa!
Kwa habari zaidi za Orthorexia someni: